Maneno matupu hayavunji mfupa ila sasa wanaanza kuchosha. Wakati taifa linakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi yanayoathiri pande zote mbili, watu wanakaa lupoteza muda kujadili tafsiri ya maneno kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili.
Hii kweli ndio Tanzania.
Hawa wanasiasa wanaoendeleza huu mjadala, wanakwepa majukumu yao kwa wananchi wao.Fanyeni kazi kusaidia taifa lipige hatua hili.
Huko visiwani, Karume na Hamad wanajua kabisa hizi zote ni kelele tupu tu, ngoja UNDP waingilie kati wawaambie hali halisi, wote watafyata tu!.
Mimi sasa nakuja na mtazamo wangu binafsi ni kwa nini nasema na kuamini kuwa zanzibar kisheria sio nchi hata kimataifa.
Navyoelewa mimi sovereignty kama alivyosema kuhani halina neno moja sahihi katika kiswahili,bali inaweza kuelezewa kuwa "ni uwezo wa kujiamulia mambo wenyewe pasipo kuingilia na mtu yeyote,uhuru huu ni absolute,kwa maana ya kuwa ni wa asilimia mia moja.Mambo yote mnayoyafanya hamuombi kibali kwa mtu wala kusema jambo fulani hatuwezi kulitungia sheri kwa kuwa faulani ndio mwenye mamlaka,mnao uwezo wa kwenda vitani wenyewe bila kuomba kibali toka kwa mtu mwingine. Hii ndio maana halisi ya sovereign.Na kulingana na international law,mataifa yote yanayotambulika kama nchi yana sovereignty.Sasa tuje katika suala la zanzibar na tanzania bara.
Ni wazi kuwa hapo kale kabla hatujawa na muungano wa mwaka 1964 tulikuwa na nchi mbili,yaani nchi ya zanzibar inayoundwa na visiwa vya pemba na unguja na nchi ya Tanganyika. Hili nadhani hakuna anayebisha.
Baada ya muungano wa mwaka 1964 nchi hizi mbili zilipoteza hadhi yake ya kuwa nchina kuunda nchi moja kubwa iitwayo Tanzania. Hii ndiyo inayojulikana na jumuiya ya kimataifa kuwa kuna nchi inaitwa Tanzania,iko afrika mashariki,upande wa mashariki inapakana na bahari ya hindi(note hawajasema upande wa mashariki inapakana na nchi ya zanzibar, la hasha) inapakana na bahari ya hindi. Hapo ina maana hii nchi inaunganisha zanzibar.
Baad ya nchi hizi mbili kupoteza hadhi yake ya kuitwa nchi automatically zilipoteza uwezo wake wa kujiamulia mambo yao kwa kuweka mambo yote chini ya muungano isipokuwa mambo machache ambayo hayakuwa kwenye mungano. Tanganika haikuishia hapo ikapoteza serrikali yake na kuifanya ile serikali ya muungano kuwa serikali yake itakayoiheshimu,wakati kwa sababu za kiutawala, zanzibar ikabakizwa na serikali yake, serikali ambayo ikapewa mamlaka yasiyo kamili na ndiyo maana ikapewa baraza la wawakilishi,rais,lakini ilipofika katika masuala ya ulinzi na usalama yote yakawa chini ya amiri jeshi mkuu ambaye ni Rais wa muungano.
Kutoka hapo zanzibar ikawa haiwezi kwenda vitani kwakuwa rais wa zanzibar si amiri jeshi mkuu,haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa bila kuwa na kibali cha rais wa muungano,haiwezi kuyatungia sheria baadhi ya mambo kwa kuwa ni ya muungano, na pia ikajiweka chini ya katiba ya muungano ambayo inaifunga hata yenyewe.Kutokana na hali hii zanzibar ikawa haina sovereignty na kama ipo sio kamili.
Hiyo ni tafsiri ya kisheria,kwa maana ya kuwa in law zanzibar is note a sovereign state. Sasa tuje in fact. In fact zanzibar na Tanganyika bado ni chi kwa kuwa ardhi za nchi hizo na watu wake bado wapo na hata mipaka yake haikuvurugwa bado ipo,ndio ksema kuwa muungano ukivunjika tayari tutapata nchi mbili yaani Tanganyika na zanzibar.Tulichonacho sasa ni nchi moja yenye serikali mbili,ambapo serikali moja ni superiorkuliko ile nyingine.Yaani serikali ya muungano is superior to that of zanzibar.Kwa maana hiyo nchi hizi mbili in fact zingefutika tu,endapo labda zingeunganishwa kwa kutumia majembe na sululu kufukia ile bahari ya hindi ili ziungane kabisa,lakini geographically kwa kuwa bado zipo ndio maana nasema in fact au physically bado zipo.
Lakini kwa kuwa sheria hutumia legal fiction?in terms of legal fiction tuna nchi moja tu ya Tanzania. Fiction hii ni sawa na ile ya ndoa inayosema mke na mme wakioana watakuwa mwili mmoja. In law and in religiuos fiction that is true but in reality teye are still two individuals.Hakuna fusion they can stil be made back to individual personalities on divorce.
Hii ndio explanation yangu.