Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mwiba,

..kule UNO ZNZ na TGK walisalimisha viti vyao na kuunda kiti kimoja Tanzania.

..halafu baadaye unasikia ZNZ wanataka uanachama wa FIFA, OIC, etc etc. huoni kuna utata hapo?

..mimi nafikiri tuwe nchi moja Tanzania. mafuta, karafuu,kahawa,pamba,...viwe vyetu wote. kama hilo tunaona ni taabu basi tukubaliane kwamba Muungano umetushinda.
 
Hili suala hata mimi niliwahi kusema si suala la Lowassa na Vuai!

Hivi CCM na viongozi wake ni lini watakubaliana kuwa watanzania wana mawazo nao wanaweza kuchangia?

Kuhusu muungano ninakubaliana na wewe ni vema tuuvunje kwanza au iundwe serikali moja hata ukisoma kitabu cha Mwalimu uongozi na ... alishauri serikali moja kwa sababu alisema muundo wa muungano ni serilaki mbili kuelekea serkali moja baadaye. Lakini zanzibar cini ya CUF na CCM wenye we huko wanataka serikali tatu ili waendelee kutunyonya zaidi!!


Sawa haya ya (Lowaasa na Vuai )yakipelekwa bungeni yakapitishwa yatakuwa mabaya zaidi kuliko hata ya Nyerere na Karume . Hawa watu wa bara wataumia zaidi lakini hao hao wa bara wamekuwa kama

walinyweshwa dawa kuhuu muungano hawataki kabisa kuungolea!!!


Hapa ndipo huwa ninakubaliana na Mtikila!
Sikiliza Mkwawa acha wapeleke ila si kwamba watakuwa wamepata dawa ya muungano ila watakuwa wameongeza shida zaidi kwa huyu mgonjwa wao. Na kesho keshokutwa jambo hili litarudi kule kule back to squire one.
Kama wanataka muungano usio na mgogoro basi let all Tanzanians say whether they like this mdudu or not.
Waking'ang'ania kutuingiza huko wakati we are not ready then let them expect more troubles out of this union.
 
Mwiba,


Mwiba at least leo umekuja na rangi yako.. maneno yako hayana tofauti kabisa na Kaburu na hakika Zanzibar itaendela kuwa chini ya Bara kwa nguvu zote...
Cha ajabu ni kwamba nyie Wa-Comoro (wa kuja) wahamiaji Zanzibar ndio wenye mdomo sana nadhani ipo haja ya kuwarudisha kwanza kwenu ambako tumewafunga kamba za mbuzi.
Hivi mkuu umewahi kujitazama ktk kioo kuangalia mabichwa yenu yasiyokuwa na kisogo jinsi yalivyoishinda uzito shingo? au huwa unatazama zile pua za kiarabu ambazo hazina sifa zaidi ya kuitwa mipua!

kwi kwi kwi kwi ahahahahahaha
 
Kuna mtu yeyote ambae anaweza kutoa sababu za msingi juu ya kuulinda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
Tanganyika ni Nchi iliyokuwepo zamani na Zanzibar halikadhalika lakini Zanzibar bado ipo na inaendelea ikiwa na raisi wake na mamlaka zake za ndani na baadhi ya za nje.
Katika hatua mbali mbali zinazochukuliwa ni kuulinda Muungano ,jambo ambalo sijaona sababu za viongozi wakuu wa serikali na wale wa CCM kucharuka kuwa wataulinda Muungano kwa bei yeyote ,wamefika kusema atakaehoji masuala ya Muungano huyo ni haini au adui wa Muungano.
Moja ya maazimio ya Muungano ni kufanyiwa marekebisho kwa pale ambapo panaonekana pana kasoro ,sasa hawa wanaosema kuujadili Muungano ni uhaini au uadui wamesimama katika misingi gani.
Mnapoungana haina maana kuwa ndio nchi zenu zimeyayuka kama waonavyo WaTanganyika na wamejisahau kama wao ni wazalendo wa Taifa la Tanganyika kufika kuona aibu kujitaja kuwa wao ni WaTanganyika na hata kuhoji maslahi ya wananchi wake juu ya Muungano huko ni kujidhalilisha kupita kiasi.
WaZanzibari kama visiwa vyao vilivyovidogo hawaoni taabu kuhoji maendeleo yanayopatika katika Muungano ni haki yao kwani wao ni moja kati ya nchi mbili zilizoungana,waliungana kwa kutarajia watanufaika kimaisha na katika kupata maendeleo ya kila fani,na wanapokuja kupima na kujitazama walipo wanaona hali yao iko vile vile tokea walipopata Uhuru tokea walipopindua badala ya kuenda mbele nchi yao na maendeleo yao yamekuwa hayaonekaniki wamekuwa wanarudi nyuma na hawana matumaini kama watasonga mbele na mlinganisho huu unakuja pale wanapowatazama wenzao walioungana nao ,kila wanapotazama wanaona wenzao wameendelea mji wa Daresalaamu ulivyo sasa sivyo ulivyokuwa kabla ya Muungano halikadhalika Mwanza,Arusha Tanga kote huko kumepiga hatua kubwa sana ukilinganisha na kabla ya Muungano ila Zanzibar imeota ukungu inajalizwa mabaa na makanisa wakati waumini wanaokwenda kusali kanisani hawaonekaniki.
Ukiingia kwenye majumba yanayotumiwa na Serikali ya Muungano majumba haya hayalingani hata chembe na majumba yanayotumiwa na serikali hiyo hiyo kwa upande wa Zanzibar ,Tanganyika wanatumia majumba ya kisasa na yenye kiwango cha kimataifa wakati Zanzibar bado wapo kwenye majumba yale yale yaliojengwa na Sulutani tokea enzi za mawe.
Ukija kwenye mabara bara hali ndio ile ile barabara ambazo zingeweza kujengwa zote katika kipindi kifupi tu cha mwanzo wa Muungano lakini hadi hii leo kuna watu wanaisikia tu barabara ya lami wakati Tanganyika karibu miji mikuu yake yote imetandikwa barabara za lami na wanaofanya hayo ni serikali ya Muungano kama yote haya yangeelekzwa na upande wa Zanzibar basi leo hii kusingekuwa kuna mahitaji ya barabara za lami Zanzibar kwani kilomita zake zinahesabika kwa urefu na upana hazifiki hata kilomita mia ni nusu ya hapo ,hivyo kama hii ni kero ingelikuwa imeshazimwa zamani.

Kama wanavyosema Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Tanzania ,Tanganyika kumeenezwa hospitali za mkoa na hospitali ndogondogo karibu kila wilaya na dispensary kwa baadhi ya vijijini ,Zanzibar yenye eneo dogo la mkoa kama wa Daresalaam ,Serikali ya Muungano ingelikwisha kumaliza kujenga Mahospitali na zahanati ambazo zingetoka kwenye mfuko wa Muungano na tatizo la kero la mahospitali lingekwisha kumalizwa zamani kwa Zanzibar nzima.
Ukiingia kwenye Elimu utaona vyuo vikubwa vyote vinavyotokana na mfuko wa Muungano vimejengwa bara ,Zanzibar ulikuwa mfuko huo upite na vyuo vinavyojengwa viwe vyenye kumilikiwa na Serikali ya Muungano yaani ijulikane wazi kama barabara fulani,mahospitali fulani ,mashule fulani na mambo mengine yamefanywa kupitia Serikali ya Muungano wa Tanzania ,lakini hayo hayapo wanatafuta kule wanakowekeza ufisadi na kukuimarisha ,mnawaletea TRA sijui VATI na mnakuja na mafuta ,na kodi na mapato yote yafanyiwe gawio , sasa haya tu ndio maendeleo ambayo Serikali ya Muungano imeyaona ndio yana faida na Zanzibar mengine yote hayamo. Naona Serikali ya Muungano imeitenga Zanzibar kwa visingizio vya mambo haya wanayo katika Serikali ya Zanzibar hivyo serikali ya Muungano haihitajiki kuyatazama kwa kweli naona hapo pamekosewa vibaya sana kwa hali yeyote ile Serikali ya Muungano na Mawaziri wake wanawajibika kwa maendeleo ya Zanzibar kama sehemu moja ya Jamhuri ya Tanzania na kwa mtizamo wangu huo kama mambo hayo yangekuwa yanatekelezwa basi ile miaka ya mwanzo tu ya Muungano yangemalizwa yote yaani wangeyafanya mpaka WaZanzibari wenyewe wangelisema hatuna chengine mnachoweza kutufanyia kumejaa tutakachohitaji kwenye bajeti ni vijisenti tudogo vya kufanyia ukarakabati.
Hivyo ndivyo nionavyo kusema kuulinda Muungano ni kulinda mirija ya unyonyaji na si kuisaidia Zanzibar katioka kujitatua na maisha yanayopanda kila siku waacheni wafanye na waseme wanalotaka kwani kwa hali ilivyo wanayohaki ya kusema lolote lile hata wakisema Hapa ulipofika Muungano pametosha Tanganyika chukueni nchi yenu .
 
Karume anapata kiburi kwa sababu aliyemuweka madarakani sio JK ni BWM. Ni dhahiri kabisa kama BWM angeruhusu matokeo ya uchaguzi ZNZ yatangazwe kama yalivyokuwa Karume angekuwa nje. Kitu kingine kinacholeta hii vurugu ni ukimya wa JK kwa Maswahiba wake waliokomba pesa pale BoT kwa gia ya kusaidia campaign wakati hela halisi iliyofika kwenye campaign ni kidogo sana. Hili limewauzi wana CCM wengi na Zanzibar ikiwepo. Pia kuoneka kwa Kikwete kuwa tayari kuwaweka CUF madarakani kama wakishinda kwa kutaka muafaka wa kudumu pia ni changamoto kwa CCM-ZNZ, na ndio maana Azimio la Butiama lilizimwa na CCM-Zanzibar. Ukimya wa kikwete umewafanya CCM kuanza kuchimbana kwani kwa muda mrefu sana wamekuwa wakiminyana katika kuila nchi na kuwafanya wajanja wachache kuendelea kuitafuna nchi kwa staili ya kudhibitiana ndani ya chama. Hapa tulipofikia sasa ni pazuri kwani inaashiria sasa nchi inapata ukombozi wa kweli wa watu kutoa au kusema kile wanachofikiri ni bora kwao hata kama kinawakwaza wajanja wachache.

Tumeshasikia kuna wakati mwingine wizi huamua kupigana risasi pale wanapotaka kuzidiana ujanja katika mgao, hiki ndicho kinachotokea sasa Tanzania kwa CCM na bado mengi yanakuja.
 
Mwiba,


Mwiba at least leo umekuja na rangi yako.. maneno yako hayana tofauti kabisa na Kaburu na hakika Zanzibar itaendela kuwa chini ya Bara kwa nguvu zote...
Cha ajabu ni kwamba nyie Wa-Comoro (wa kuja) wahamiaji Zanzibar ndio wenye mdomo sana nadhani ipo haja ya kuwarudisha kwanza kwenu ambako tumewafunga kamba za mbuzi.
Hivi mkuu umewahi kujitazama ktk kioo kuangalia mabichwa yenu yasiyokuwa na kisogo jinsi yalivyoishinda uzito shingo? au huwa unatazama zile pua za kiarabu ambazo hazina sifa zaidi ya kuitwa mipua!
Wacha Jazba ,inaonyesha umekasirika niliposema machogo,inaonyesha wewe sulubu za siasa huziwezi,unajua wakati wakampeni Salimin amour alimchokoza Seif Sharifu katika majukwaa nae kwa vile Seif ni mtaalamu wa siasa za malumbano akamwambia Salimini kuwa ameonekana baharini akifamya ugagula na moja ya lichokifanya eti alivua nguo zote na kukalia fenesi sasa weka kando hayo,mbona wengine kuitwa wapemba hawakasiriki japo hawapendi na WaZanzibari wote wanapotua bandarini dar wanaitwa wapemba na ndio hivyo hivyo wanaotoka Tanganyika nao huitwa machogo nakumbuka nilipokuwa nikisoma Ngamiani Tanga ile shule ambayo sasa inaitwa Jumuia mkabala na standi ya mabasi kwa ndani unaipata hospitali ya Ngamiani karibu na kituo cha matreni ulikuwepo wakati wa mabezo basi aliekuwa na chogo akiingia kwenye mabezo hupata tabu sana na kwa vile kwenye siasa na wanaopingana na Zanzibar wana machogo sio kosa kuwawakilisha kwa msamiati huo.

Tatizo sio kuvunja Muungano tatizo ni WaTanganyika nao warudishiwe Nchi yao ,kusema muungano hauvunjiki hilo siwezi kulitegemea sana kwani kwa tulivyoijua Urusi na nchi nyengine hakuna alietegemea kwamba Muungano wao utavunjika na kusambaratika kiasi wacha kuvunjika hata wilaya na mikoa nayo ilivurugika na kupatikana vinchi vidogo vidogo kama Tanga Arusha Mwanza Kigoma na kadhalika hayo ni matokeo ya matatizo ya Muungano unaoonekana hauna faida kwa upande mmoja.
Hivyo kunusuru hayoyote yasije kutokea baadae Muungano ni lazima uwepo ila Tanganyika irudi na kupata serikali mbili na ya tatu ambayo imeasisiwa na watu wawili ambao wanasemekana ndio wapigania Uhuru japo upande wa Zanzibar sivyo lakini tuchukulie hivyo.
Serikali ya Tanganyika irudi ,serikali mbili tayari zipo ,sasa tatizo mnaloogopa ni nini ? na kwa ukweli ukiangalia kwa undani hapa ndipo tutakapoweza kuwadhibiti wahujumu uchumi wakubwa wakubwa,hapa ndipo tutakapoweza kupambana na rushwa ,hapa ndipo tutakapoweza kupambana na vigogo wa biashara ya madawa ya kulevywa hapa ndipo tutakapoweza kupambana na wanaohujumu wanafunzi wa kike hapa ndipo tutakapoweza kuwadhibiti wakuu wa uhalifu hapa ndipo kila kitu kitapoanzia na kudhibitiwa lakini tusidanganyane kwenye serikali ya Muungano iliyopo ambayo inaonyesha kufadhiliwa na mafisadi wa pande zote mbili ni lazima kama kufa serikali ya Tanganyika irudi tena irudi kwa kasi na ari na kishindo juu nashangaa kwa nini suala hili hamlileti juu anaogopwa nani ? Huyu Kikwete ndie aliekuwa mstari wa mbele saa ingine nafikiri anayaachia haya mambo yapande temperature ili iwe rahisi kutekeleza ile dhana na juhudi walizokuwa nanzo kuirudisha Tanganyika.
 
Zanzibar kwanza ndio walipigia debe sana kuunganisha TANU na ASP kwa sababu walikuwa hawakohoi kule visiwani na uhuru huu ambao wanaupigia kelele wameupata baada ya CCM kuzaliwa. Ni vizuri wasome historia yao kwanza kabla ya kurukia hoja. (rejea hotuba ya Mwalimu JK Nyerere kule Visiwani wakati wa uanzishaji rasmi wa CCM).

Zanzibar kama wakileta fujo basi watakiona cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya Usalama wa Tanzania ni pamoja na kuona hakuna anayeleta choko choko kule visiwani, mifano ipo mingi Taiwan, Hong Kong n.k. Tanzania imetumia pesa nyingi sana kuifanya Zanzibar na mahali popote pale Tanzania kuwa hapo ilipo, waswahili walisema Usione vinaelea Vimeundwa. Hakuna kuvunja huu muungano - PERIOD!
 
Jambo zuri litakalofanywa na mzanzibari basi utasikia kwenye lundinga na radio mtanzania amefanya jambo zuri lakini akifanyapo mzanzibari kama kuuza unga au lolote baya utasikia mzanzibari ameleta longolongo haya mpaka lini? kama msukuma amefanya kosa utasikia mtanzania akifanya zuri ni mtanzania hivi kweli ndio muungano huu, zuri letu sote baya lao wao
 
unajuwa muungano ukileat serikali tatu basi kama mnakumbuka Sukuma land walipotaka kujitenga ndio wanayoogopa Tanganyika
 

Zanzibar kama wakileta fujo basi watakiona cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya Usalama wa Tanzania ni pamoja na kuona hakuna anayeleta choko choko kule visiwani, mifano ipo mingi Taiwan, Hong Kong n.k. Tanzania imetumia pesa nyingi sana kuifanya Zanzibar na mahali popote pale Tanzania kuwa hapo ilipo, waswahili walisema Usione vinaelea Vimeundwa. Hakuna kuvunja huu muungano - PERIOD!

Muungano hauvunjwi isipokuwa Utavunjika maana mafisadi wamekuwa wakiutumia kujificha ,na wale wote wanaoutetea Muungano basi ujue ndio wakubwa wa ufisadi ,kwani wale akina Kikwete na genge lake walioidai Tanganyika walikiona kilichomtoa kanga manyoya mbona wapo na wamefika kuwa Maraisi na kugawana madaraka.
Muungano huu unalindwa na watu wanaofaidika nao si mimi wala walala hoi wengine na si wa kutoka Tanganyika wala Visiwani wote wahoi bin Taaban.
CCM Zanzibar hawawezi kuuvunja Muungano hata dakika moja japo unawaona hivi sasa wao ndio wapo mstari wa mbele kusema Zanzibar ni Nchi ,wao ndio wanaojibishana na machogo wa Bara lakini hawana ubavu wa kufanya lolote.
Kitu kimoja tu kama CUF ingelikuwa madarakani kule Zanzibar basi hawa machogo wa CCM wote kila mmoja angelikuwa na adabu zake ,na kila mmoja ambae angekuwa yupo katika Serikali ya Muungano angefanya lile ambalo anatakiwa alifanye kama kiongozi wa Serikali ya Muungano na wale mafisadi kila mmoja angelikuwa ananyea debe , lakini kwenye utawala huu wa CCM tutegemee haya haya ya kujibishana tu hakuna hata moja linalokuwa.Ni kama tulivyoona pale bungeni sijui CCM huyu kasema hivi yule kasema vile ni porojo tupu hawana ukweli nasema CCM wamejaa ubabaishaji na huu au hili linalotokea sasa ambalo ni wao kwa wao ni ubabaishaji mwengine.
Chini ya Utawala wa CUF kama wangefanikiwa kupata haki yao ya kuongoza basi hizi senenesenene za Muungano zingekuwa zimeshaisha zamani na watu wanaishi katika mawasiliano mazuri tu wala kusingekuweko na majibishano na matatizo kero zote zingemalizika na kusawasishwa si zaidi ya miezi sita ,maana CUF wanawasomi waliobobea na wanajua wanachokifanya na kukijadili hawana kubadili msimamo wanachokisema na kukabiliana kwa masikilizano na kupata usuluhishi ndio hicho kinachotekelezwa.
Haya matatizo unayoyaona ni kati ya CCM Butiama na CCM kisiwa ndui wanaonyeshana misuli si umesikia jana kuna mhafizina mmoja anaitwa Shamhuna ametoa mbovu huko Unguja na kuwasemea hovyo akina Pinda na spika Sitta kuwa hawana ubavu wa kuwaziba midomo na yuko yule chokraa wa kihindi anaitwa Raza nae eti amepanda hasira anatembea Zanzibar yote kuweka mikakati ya kupambana na kauli ya Pinda ,hivyo hivi ni vita vya wenyewe kwa wenyewe kama nilivyosema wanatunishiana misuli ,kuna moja nimesikia kuwa Karume katika hili la majibishano hayumo yeye ameamua kukaa kimya kama Kikwete na hata kule Butiama ilisemekana kama yeye alikuwa tayari kuunga mkono makubaliano ya muafaka uliopatikana baina ya CCM na CUF lakini hawa akina Shamhuna na wengine ndio waliomwambia kama wewe huwezi kumkabili KIkwete basi kaa kando maana saa mbaya ,hivyo hili genge linalojibishana na bara ni genge lile lile lililomtoa kijasho Kikwete na kumuangusha na kumfanya aonekane kiongozi hovyo asie na msimamo .hivyo lile genge bado linaendelea kuisakama timu ya Kikwete ya Butiama na limesikika likisisitiza kuwa akina kaka kazi wa Kikwete wasifurukute wakijibu asubuhi wanajibiwa jioni,sasa kama utaangalia utaona pale Tambwe Hiza alipokuja na lambalamba eti anawapa Onyo wanaosema Zanzibar ni nchi ,wahafizina wa CCM kule Zenji kusikia hivyo wacha wamjie juu na sijui kama watamkaribisha tena kwenye mikutano yao maana amewapaka mavi.
Hivyo haya malumbano hayana faida kabisa ni siasa za CCM wenyewe kwa wenyewe na zaidi wanapindisha kuelekea kwengine wakati mapambano ya ufisadi yalikuwa yamepamba moto na sasa ukichunguza utaona yameshuka chati.
 
Mwiba,
Wacha Jazba ,inaonyesha umekasirika niliposema machogo,inaonyesha wewe sulubu za siasa huziwezi,unajua wakati wakampeni Salimin amour alimchokoza Seif Sharifu katika majukwaa nae kwa vile Seif ni mtaalamu wa siasa za malumbano akamwambia Salimini kuwa ameonekana baharini akifamya ugagula na moja ya lichokifanya eti alivua nguo zote na kukalia fenesi sasa weka kando hayo,mbona wengine kuitwa wapemba hawakasiriki japo hawapendi na WaZanzibari wote wanapotua bandarini dar wanaitwa wapemba na ndio hivyo hivyo wanaotoka Tanganyika nao huitwa machogo nakumbuka nilipokuwa nikisoma Ngamiani Tanga ile shule ambayo sasa inaitwa Jumuia mkabala na standi ya mabasi kwa ndani unaipata hospitali ya Ngamiani karibu na kituo cha matreni ulikuwepo wakati wa mabezo basi aliekuwa na chogo akiingia kwenye mabezo hupata tabu sana na kwa vile kwenye siasa na wanaopingana na Zanzibar wana machogo sio kosa kuwawakilisha kwa msamiati huo.
Mkuu sina jazba isipokuwa unapouchonga jua wengine pia twaweza, hakuna jazba hapa hata kidogo Uhuni hujibiwa kwa uhuni. Umetuita machogo kama neno la kutuona sisi tupo chini yaani binadamu waliokuwa na kasoro ya kimwili. Hii haisemi mtu mmoja wala kundi dogo la watu ila tusi lenu kubwa kwa Watanzania wote wa bara. Ttatizo la msemo huu metokana na watu wa kuja Wa Comoro ambao tumewapatia hifadhi Bara na Visiwani bila shukran mnaanza kuleta za kuleta kama Makaburu. Tutawafanyia kikweli maanake mnajiingiza sana ktk siasa za Tanzania wakati hamna hata nchi.. Ombeni tuwarudisheni Comoro hilo litakuwa wazo zuri sana..
Matusi ya nguoni tunayaweza sana mkuu!
 
Mambo yote haya yamesababishwa na ujinga wa raia wetu. Kama Raia wangefahamu kuwa nchi yetu inahitaji kiongozi madhubuti sana, wangejizuia kumchagua kiongozi legelege huyu Kikwete, na yote haya yasingekuwapo. Kihitoria tumeshuhudia kuwa kila mara kukitokea ulegelege kwenye uongozi wa kitaifa huwa tunapata misukosiko mingi ya kugawa taifa letu ama kidini au kwa kutumia huu muungano. Kwa bahati nzuri miaka ya nyuma kulikuwa na Baba wa Taifa Nyerere aliyekuwa akikemea mambo hayo. Kwa sasa hivi mtu pekee anayeweza kuyakemea ni Rais Mwinyi tu, hata hivyo sijui kama kweli mzee Mwinyi ataamka na kuchukua nafasi hiyo ya Mlezi wa Taifa.

Kikwete hana moral authority ya kukemea mabaya ya aina yoyote hata yale ambayo ni mepesi kama wizi wa fedha za umma. Ukiongezea kuwa vile vile mtu huyu ni intellectually light weight, mchanganyiko huo ni sumu sana ambayo inamfanya asiweze kabisa kufanya surgical operation juu ya swala hili la muungano ambalo liko juu sana ya uwezo wake. Laiti tungekuwa na SAS, huenda maneno kama haya yasingekuwapo.

Mzee Mwinyi, tafadhali sana amka ukemee kansa hii inayolinyemelea taifa letu. Pamoja na kuwa nachukizwa sana na muungano kwa vile umekuwa unawapendelea watu wa zanzibar kutita kiasi ukilinganisha wa wale wa bara, bado siafiki kuuvunja baada ya kuwa nao kwa zaidi ya miaka 40; raia wetu zaidi ya asilimia 60 wamezaliwa chini ya Muungano huo. Nadhani kosa kubwa lililofanyioka baada ya Muungano ni kuendelea kusimika nguzo za kutengana kwa kuendelea kuwapo kwa serikali ya Zanzibar pekee. Najua kuwa kulikuwa na sababu za maana kufanya hivyo ila ukweli ni kuwa sababu za aina hiyo ndizo zinazotuyumbisha leo hii. Ni afadhali tangu mwanzo tungeunda serikali moja tu kwa nchi nzima na kama kulikuwa na haja ya kuwalinda wazazibar wasimezwe, ni afadhali kungewekwa vifungu vya katiba vinavyowahakikishia protection hiyo badala ya kuwaacha na serikali ambayo leo hii inajiita dola. Kwa zanzibar kujiita dola ni kwamba ina uwezo wa kuamarisha majeshi yake kupigana vita dhidi ya dola ya Muungano ambayo kwa mawazo yao inachukuliwa kuwa ni Tanzania Bara. Hiki ni kichekesho kweli kweli, lakini kinahitaji mtu wa busara kukikabili, ndiyo maana ninadhani kuwa kwa mazingira ya sasa mtu pekee wa kuweza kufanya hivyo ni Rais Mwinyi peke yake.
 
This is the price which our country is paying for allowing some people to be our leaders because of the stolen money. SAS hakuwa na hela ya kuwapa wajumbe wa Mkutano mkuu CCM na ndiye aliyekuwa anatakiwa awe kiongozi wa Tanzania ambaye angerudisha heshima ya IKULU yetu. Sasa watumie tena hela kuzima mjadala wa kuvunja muungano kwa ama kuwapa vyeo baadhi ya wabunge wanaopigia kelele kuwa mawaziri au kuwafungulia accounts offshore. G55 ilizimwa na Mwinyi kwenye hoja ya Tanganyika kwa kuwapatia vyeo baadhi ya vinara wake.

Muungano ni kitu muhimu sana lakini uwe muungano wa kweli watu waujadili na kuja na suluhu itakayoridhiwa na WATANZANIA wa pande zote na sio issue ya kigenge cha wachache wanaojiita CCM. Hoja nzito kama hii AGENDA irudishwe kwa wananchi.

Tatizo linalotokea leo ni result of RISK AVOIDANCE tendancy ya Viongozi wa Tanzania kila mmoja hataki kuliongea kwa kuhofia Muungano kuvunjikia kwake. Tusipoziba ufa tutajenga ukuta. Tusipouongelea muungano leo huko tuendako tutakosa nafasi ya kuuongelea na itabaki kuwa majuto baada ya kuvunjika.
 
This is the price which our country is paying for allowing some people to be our leaders because of the stolen money. SAS hakuwa na hela ya kuwapa wajumbe wa Mkutano mkuu CCM na ndiye aliyekuwa anatakiwa awe kiongozi wa Tanzania ambaye angerudisha heshima ya IKULU yetu. Sasa watumie tena hela kuzima mjadala wa kuvunja muungano kwa ama kuwapa vyeo baadhi ya wabunge wanaopigia kelele kuwa mawaziri au kuwafungulia accounts offshore. G55 ilizimwa na Mwinyi kwenye hoja ya Tanganyika kwa kuwapatia vyeo baadhi ya vinara wake.

Muungano ni kitu muhimu sana lakini uwe muungano wa kweli watu waujadili na kuja na suluhu itakayoridhiwa na WATANZANIA wa pande zote na sio issue ya kigenge cha wachache wanaojiita CCM. Hoja nzito kama hii AGENDA irudishwe kwa wananchi.

Tatizo linalotokea leo ni result of RISK AVOIDANCE tendancy ya Viongozi wa Tanzania kila mmoja hataki kuliongea kwa kuhofia Muungano kuvunjikia kwake. Tusipoziba ufa tutajenga ukuta. Tusipouongelea muungano leo huko tuendako tutakosa nafasi ya kuuongelea na itabaki kuwa majuto baada ya kuvunjika.

Naungana nawe asilimia 100%, ila siamini kuwa kama mjadala ukirudishwa kwa wananchi jibu pekee litakuwa ni kuvunjika kwa muungano. Mimi naamini utapatikana muungano bora na unaoelezeka, sio huu wa sasa. Kuna ufa mkubwa ktk muungano, jibu sio kufunika magunia ili usionekane. Jibu ni kuzungumza, pande zote mbili zitoe maoni zingependa iwe vipi. Tatizo hapa ni itapatikanaje hiyo fursa ya watu kuujadili huu muungano?
 
Nimevumilia vya kutosha nikidhani kama kuna mtu anayekerwa na fumbuzi wa matatizo ya muungano yaliyotolea kwenye kikao cha pamoja kati ya Mh. Lowassa na Mh. Nahodha.
Kitu kinachonitisha ni kwamba yale mambo waliowaamulia wananchi yatapelekwa bungeni october kwa ajili ya "constitutional reforms".
Kwa upande wangu sikubaliana na ufumbuzi waliofikia kwa 100%
Check this out:
1) mineral and oil exploration be co-opted into the national debate on the future of the political federation.
-debate is good but mineral and oil exploration should not be political.

2)Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) should have an equal number of representatives from either side.
-Equal number kwa vigezo gani? Idadi ya watu? Tuelezene mlivyokuja na hiyo soultion equal number of people.

3)consultant on the distribution of wealth generated through mining and oil extraction be hired to advise the Union government on how it can be shared equitably.
-Please kama ni hivyo na huo muungano hatuutaki. For what?

4)It was decided that 50 per cent of the income would be used to finance the operations of the authority and the other 50 per cent be distributed on the basis of 60 per cent for the Mainland and 40 per cent for Zanzibar.
-Hivi hizo hesabu mnafanyaje? How did you come up with 60%, ardhi, watu,?????

Najua watanzania hawataki kuongelea muungano wakiogopa mizimu ya Mwalimu. Kwa upande wangu kuna mambo mawili tu hapa ambayo yanaweza kuleta ufumbuzi wa kudumu kwanza kuuvunja muungana na Zanzibar ikawa nchi kama ilivyo Kenya na tutaendelea kushirikian nao kama tunavyoshirikiana na Kenya, au Zanzibar uwe mkoa. zanzibar kuna watu wasiozidi 3 mil wakati mkoa wa Dar tu una watu 4 mil. Hapo utajiuliza ni kivitu tugawane nusu kwa nusu?
Kama watu hamtaki kuongela hili sual basi mwezi October linaengia kwenye katiba.

Bro nina wasiwasi na IQ yako. Waswahili wanasema ukubwa wa pua si wingi wa makamasi. Ivyo unafikiri ukubwa na idadi ya nchi ndiyo inayoamuwa status ya nchi? Hebu fikiria mabwana zetu tunaowaomba misaada kama Japan, Sweeden, Denmark na nyenginezo zina ukubwa gani na hizo ni nchi sio sisis tulio mkiani.
Fikira hivi za ubora na uchoyo hazitajenga bali kubomoa. Nchi ni kama binaadamu tumeumbwa na mungu kwa hivyo kuishi na jirani au ndugu yako huku ukijifikiria wewe tu ni tatizo. samahani lakini nafikiri kuna ka kigenes fulani cha nje ya Tanzania hapo.
 
Mzee Mkandara,
Mimi naamini hakuna kitu kitachotutengenisha kati yenu na Zanzibar kijamii, sisi ni wamoja na tunashirikiana vizuri sana kijamii. Muungano wa kiuchumi na kisiasa unaturudisha nyuma sana kimaendeleo. Ni kitu ambacho hakiingii akilini kwa nini Zanzibar iwe na serikali yake ndani yamuungano wakati Dar es Salaam ambayo wakati wake ni mara mbili ya wakazi wa visiwani na bado wanataka wachukua 40% for what. Kama hawataki Zanzibar uwe mkoa basi muungano wa kisisa na uchumi ufe, ni gharama kubwa kwa serikali ya Muungano.

HABARI NDO HIYO|
Hayo yaliyozungumzwa hapa ni mapendekezo na angalieni namna mnavyoreact. Sasa kama nyie mgekuwa Wazanzibari wakati hamna uhuru wa kujiendeleza kiuchumi na kunyanyaswa eti hamna rasilimali (resourses) na wenzenu wanazo na kutumia kwa faida yao na kwa bahati nzuri mnaokota mafuta na hapo yule aliyeakitanuwa sasa anakuja na kudai kile chako kiwe chenu pamoja HALI INGEKUWAJE? hebu jaribuni kutafakari hilo na kulitolea jibu.
 
Sasa ni wakati muwafaka wa kuutoa waraka wa Tume ya Nyalali kwenye madroo na kufanyiwa kazi .
yaani Kikwete ana zana kibao za kutatua jambo hili.
Muungwana utafutewaraka huo na kuufanyia kazi .
Unajua sasa hivi kuna maneno kule Zanzibar yanazungumzwa hata na watoto wadogo wanasema tumewashika pabaya machogo yaani wanasema hii ni saa ukombozi kama ilivyokuwa wameshikwa pabaya mafisadi ni saa ya ukombozi kwa WaTanganyika na vilevile ni saa ya Ukombozi kwa WaZanzibari ila katika kukulu kakala zenu msije mkaisahau Pemba wanaweza wakafanya maandamano mpaka United Nation kwenyewe.
 
Muungwana ni vitendo, huyo mnayemuita Muungwana anafanana na matendo yake?

Huyu jamaa ni mtu mzuri sana na amejaa imani ni mtu mwema tu kiasi hapendi kuona mtu anateseka ,ndio ukaona ameshindwa kuwashukulia hatua mafisadi.
Huwa anajitahidi kutaka kuweka maisha ya Mtanzania yawe ya grade ya pili na jitihada zake zimekuwa zinakumbana na mitihani mingi lakini nia ya Mheshimiwa Kikwete sio mbaya kwa WaTanzania anataka kumridhisha kila mmoja wetu.
 
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema mazoezi ya kijeshi yanayoshirikisha askari wa vikosi vyake; Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo (Magereza), Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Zimamoto hayahusiani na malumbano yaliopo kuhusu Zanzibar kuwa ni Nchi au si nchi, badala yake imesema huo ni mpango uliopangwa hivi sasa kwa kuviweka vikosi vyake katika hali ya ukakamavu badala ya kukaa na kupiga domo.Waziri alikuwa akijibu suala aliloulizwa kuwa mazoezi hayo yamekuja baada ya kauli kuwa Zanzibar haina dola na serikali yake haina nchi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga, hatua hii ina lengo la kuwaimarisha askari hao kupambana na magendo na biashara ya madawa ya kulevya yaliyojitokeza mara kwa mara katika visiwa hivyo kuzunguka mipaka yake.
 
Back
Top Bottom