Zanzibar kama wakileta fujo basi watakiona cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya Usalama wa Tanzania ni pamoja na kuona hakuna anayeleta choko choko kule visiwani, mifano ipo mingi Taiwan, Hong Kong n.k. Tanzania imetumia pesa nyingi sana kuifanya Zanzibar na mahali popote pale Tanzania kuwa hapo ilipo, waswahili walisema Usione vinaelea Vimeundwa. Hakuna kuvunja huu muungano - PERIOD!
Muungano hauvunjwi isipokuwa Utavunjika maana mafisadi wamekuwa wakiutumia kujificha ,na wale wote wanaoutetea Muungano basi ujue ndio wakubwa wa ufisadi ,kwani wale akina Kikwete na genge lake walioidai Tanganyika walikiona kilichomtoa kanga manyoya mbona wapo na wamefika kuwa Maraisi na kugawana madaraka.
Muungano huu unalindwa na watu wanaofaidika nao si mimi wala walala hoi wengine na si wa kutoka Tanganyika wala Visiwani wote wahoi bin Taaban.
CCM Zanzibar hawawezi kuuvunja Muungano hata dakika moja japo unawaona hivi sasa wao ndio wapo mstari wa mbele kusema Zanzibar ni Nchi ,wao ndio wanaojibishana na machogo wa Bara lakini hawana ubavu wa kufanya lolote.
Kitu kimoja tu kama CUF ingelikuwa madarakani kule Zanzibar basi hawa machogo wa CCM wote kila mmoja angelikuwa na adabu zake ,na kila mmoja ambae angekuwa yupo katika Serikali ya Muungano angefanya lile ambalo anatakiwa alifanye kama kiongozi wa Serikali ya Muungano na wale mafisadi kila mmoja angelikuwa ananyea debe , lakini kwenye utawala huu wa CCM tutegemee haya haya ya kujibishana tu hakuna hata moja linalokuwa.Ni kama tulivyoona pale bungeni sijui CCM huyu kasema hivi yule kasema vile ni porojo tupu hawana ukweli nasema CCM wamejaa ubabaishaji na huu au hili linalotokea sasa ambalo ni wao kwa wao ni ubabaishaji mwengine.
Chini ya Utawala wa CUF kama wangefanikiwa kupata haki yao ya kuongoza basi hizi senenesenene za Muungano zingekuwa zimeshaisha zamani na watu wanaishi katika mawasiliano mazuri tu wala kusingekuweko na majibishano na matatizo kero zote zingemalizika na kusawasishwa si zaidi ya miezi sita ,maana CUF wanawasomi waliobobea na wanajua wanachokifanya na kukijadili hawana kubadili msimamo wanachokisema na kukabiliana kwa masikilizano na kupata usuluhishi ndio hicho kinachotekelezwa.
Haya matatizo unayoyaona ni kati ya CCM Butiama na CCM kisiwa ndui wanaonyeshana misuli si umesikia jana kuna mhafizina mmoja anaitwa Shamhuna ametoa mbovu huko Unguja na kuwasemea hovyo akina Pinda na spika Sitta kuwa hawana ubavu wa kuwaziba midomo na yuko yule chokraa wa kihindi anaitwa Raza nae eti amepanda hasira anatembea Zanzibar yote kuweka mikakati ya kupambana na kauli ya Pinda ,hivyo hivi ni vita vya wenyewe kwa wenyewe kama nilivyosema wanatunishiana misuli ,kuna moja nimesikia kuwa Karume katika hili la majibishano hayumo yeye ameamua kukaa kimya kama Kikwete na hata kule Butiama ilisemekana kama yeye alikuwa tayari kuunga mkono makubaliano ya muafaka uliopatikana baina ya CCM na CUF lakini hawa akina Shamhuna na wengine ndio waliomwambia kama wewe huwezi kumkabili KIkwete basi kaa kando maana saa mbaya ,hivyo hili genge linalojibishana na bara ni genge lile lile lililomtoa kijasho Kikwete na kumuangusha na kumfanya aonekane kiongozi hovyo asie na msimamo .hivyo lile genge bado linaendelea kuisakama timu ya Kikwete ya Butiama na limesikika likisisitiza kuwa akina kaka kazi wa Kikwete wasifurukute wakijibu asubuhi wanajibiwa jioni,sasa kama utaangalia utaona pale Tambwe Hiza alipokuja na lambalamba eti anawapa Onyo wanaosema Zanzibar ni nchi ,wahafizina wa CCM kule Zenji kusikia hivyo wacha wamjie juu na sijui kama watamkaribisha tena kwenye mikutano yao maana amewapaka mavi.
Hivyo haya malumbano hayana faida kabisa ni siasa za CCM wenyewe kwa wenyewe na zaidi wanapindisha kuelekea kwengine wakati mapambano ya ufisadi yalikuwa yamepamba moto na sasa ukichunguza utaona yameshuka chati.