Ndivyo Ilivyo
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 243
- 4
Sawa. Kama hili la "sovereignity. Rudia kabisa article za Muungano. Rudia Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Rudia Hotuba zile za Nyerere. Zanzibar ime-surrender part of its sovereignity to the United Republic. Lakini (pia) makubaliano ni kuwa ita-retain some aspects of her sovereignity. Jee ime-retain kweli?Zanzibar haijawahi kupewa haki sawa kivipi?
Naomba kueleweshwa maana si mjuzi sana wa mgao wa haki katika Muungano.
Maneno matupu hayavunji mfupa ila sasa wanaanza kuchosha. Wakati taifa linakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi yanayoathiri pande zote mbili, watu wanakaa lupoteza muda kujadili tafsiri ya maneno kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili.
Hii kweli ndio Tanzania.
Hawa wanasiasa wanaoendeleza huu mjadala, wanakwepa majukumu yao kwa wananchi wao.Fanyeni kazi kusaidia taifa lipige hatua hili.
Huko visiwani, Karume na Hamad wanajua kabisa hizi zote ni kelele tupu tu, ngoja UNDP waingilie kati wawaambie hali halisi, wote watafyata tu!.
Makubaliano ya Zanzibar na Tanganyika ni kuwa- Tanganyika ina-surrender full sovereignity kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (nayo inabaki kama kivuli au ni Mfu). Zanzibar ina-surrender some aspects of its socereignity. na Ina-retrain some aspects za sovereignity kwa upeo ambao itabaki kuwa Autonomous, Na pia itaendesha na kuamua mambo yake yote ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kelele za sasa ni hizi- Jee hii some aspects ya sovereignity ambayo Zanziba iko entitled kui-retain kwa mujibu wa makubalinao -inapatikana?Dola kwa maana ya sovereignty,nationa kwa maana ya taifa,government kwa maana ya serikali. Black's law dictionary inadefine sovereignty kama ifuatavyo
The supreme, absolute, and uncontrollable power by which any independent state is governed; supreme political authority; the supreme will; paramount control of the constitution and frame of government and its administration; the self-sufficient source of political power, from which all specific political powers are derived; the international independence of a state, combined with the right and power of regulating its internal affairs without foreign dictation; also a political society, or state, which is sovereign and independent.
The power to do everything in a state without accountability, --to make laws, to execute and to apply them, to impose and collect taxes and levy contributions, to make war or peace, to form treaties of alliance or of commerce with foreign nations, and the like.
Sovereignty in government is that public authority which directs or orders what is to be done by each member associated in relation to the end of the association. It is the supreme power by which any citizen is governed and is the person or body of persons in the state to whom there is politically no superior. The necessary existence of the state and that right and power which necessarily follow is "sovereignty." By "sovereignty" in its largest sense is meant supreme, absolute, uncontrollable power, the absolute right to govern. The word which by itself comes nearest to being the definition of "sovereignty" is will or volition as applied to political affairs
Kutoka hapa sasa tuone zanzibar ina fall wapi
S.M.Z. vs. Machano Khamis Ali & Others inayotajwa hapo juu inaweza kuwa haihusiki hapa, haina legal authority hapa, kwa sababu haikuwa kesi ya Kikatiba kutoka Mahakama maalum.
Nimewahi kuitumia kusema kwamba Zanzibar sio nchi kama alivyoandika A. Ramadhani (JC). Lakini inawezekana kuhusisha ile kesi na mtafaruku wa Zanzibar ni uchambuzi ambao sio well-reasoned, na ni makosa.
Maamuzi yaliyotolewa siku za nyuma Mahakamani yanakuwa ni tafsiri yenye mamlaka ya sheria, decisional law. Yanaitwa "precedents."
Lakini ili Majaji wengine waweze kufuata hizo "precedents," inabidi huo uamuzi wa nyuma uwe unahusika na swali la Kisheria la kesi iliyoko mbele yetu sasa hivi. Iwe "on point." Machano Khamis nadhani haiko "on point" hapa kwa sababu mbili.
"Machano Khamis Ali" ilikuwa ni kesi ya Uhaini. Kesi ya jinai. Swali la kisheria pale, au the "legal issue," lilikuwa ni kama jamaa walitenda haini. Ili wajibu hilo swali, ilibidi kwanza wajiulize haini ni nini. Wakakuta haini lazima itendwe dhidi ya Nchi. Kutoka hapo ikabidi wajiulize kama Zanzibar ni nchi. Wakasema sio. Lakini haya maswali ya uchambuzi wao yanaweza kuwa hayakuwa the central legal issue, na hivyo hayatusaidii kuulewa Muungano kisheria.
Isitoshe, kesi za kutafsiri Katiba zina mahakama maalum, tena sio maalum kwa maswala ya Katiba, ila ni maalum kwa masuala ya malumbano ya Kikatiba dhidi ya Zanzibar na Muungano kwa mujibu wa Ibara ya 126.
Hivyo, uamuzi wa kesi yeyote ambayo siyo ya kuhusu malumbano ya Kikatiba juu ya pande za Muungano, na wala haitoki kwenye Mahakama ya Kikatiba, na huko inakotoka haihusiani na kingine ila jinai ya Uhaini, inaweza kuwa kuwa haina nguvu ya kuwabana Majaji wa siku za mbele watakao kaa kutafsiri mgogoro wa Kikatiba. Haina mamlaka ya precedential force hapa.
Uamuzi wa Machano Ali, kesi ya jinai kuhusu Haini, inawezekana hapa haihusiki.
Unajua kwa sababu wanachogombania sasa wasipoangalia wanagombania sovereignty which means, Zanzibar inataka kuwa nje ya Jamhuri kwani haiwezi kuwa sovereign ndani ya nchi nyingine. What does sovereigny means though:
Wakati Majimbo ya Marekani yanatangaza uhuru wao toka Uingereza walisema wanafanya hivyo kama nchi huru na hivyo as " Free and Independent States, they have full Power to levy War, conclude Peace, contract Alliances, establish Commerce, and to do all other Acts and Things which Independent States may of right do."
Wasipoangalia watajikuta wanagombania "Uhuru wa Zanzibar" which is to declare themselves as sovereign kitu ambacho kitakuwa kimeuua muungano.
Kwa mujibu wa makubaliano yaliyounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar inayo Serikali yake (SMZ- na Rais Amani Karume kwa hivi sasa). Zanzibar inayo Population inayotambulika (ndio hao Wazanzibari). Inayo mipaka yake (pamoja na huu iliopo Zanzibar channel unaotenganisha Zanzibar na Dar es salaam).Kwa mujibu wa makubaliano ya Muungano inawajibika ku-retain some aspects of her sovereignity. Jee amua wewe hiyo ni Nchi au si Nchi kwa mujibu wa -montevideo- yako.Mkataba wa montevideo wenyewe unataja sifa kuu nne zifuatazo za mamlaka kuitwa nchi:-
Population, Territory, Sovereignty, Government
Je,zanzibar inavyo vitu vyote hivyo vinne?
Hivyo Ndivyo Ilivyo Bw. Ngekewa. Na Hata Nyerere anajua hivyo. Msiwe wavivu- rejeeni kusoma hotuba zake- alitetea hilo. Zanzibar ku-retain some aspects of her sovereignity .Sasa hili lina i-qualify Zanzibar kuwa NchiNAFIKIRI UNAKOSEA KUWATILIA MANENO MDOMONI WAZANZIBARI. WAO HAWAJATAKA WIZARA YA MAMBO YA NJE AMBAYO NDIO MSINGI WA KUWA SOVEREIGN STATE, WANACHOSEMA WAO NI NCHI AMBAYO SOVEREIGNTY YAKE IMECHUKULIWA NA SERIKALI YA MUUNGANO. KATIBA NI MAKUBALIANO NA WALA SI UNIVERSAL ENTITY KWA MATAIFA YOTE NA NDIO MAANA KILA TAIFA HUWA NA KATIBA YAKE.
SISI TULIKUBALIANA KUWA ZANZIBAR ITAKUWEPO KAMA NCHI LAKINI ITAKASIMU MADARAKA YAKE KWA SERIKALI YA MUUNGANO and that is it.
Comparisons and qoating of others will not help us here. we have to abide to what we had agreed even if ours is a peculiar union.
Do u know the consequencies?Ukweli kisheria ni kwamba, zanzibar si nchi ila watu wanataka kulazimisha tu ili iwe nchi waseme wanataka kujitenga kwasababu zao binafsi. the issue here should not be whether Zanzibar is a state or not, it should be whether muungano uendelee au usitishwe, kwasababu kwa zanzibar kuwa nchi halina ubishi kabisa. lakini kwa mtazamo wangu, kwasababu muungano unahitaji watu wawili wakubaliane kama mmoja akikataa, unag'ang'ania wa nini? kule zenji CUF na CCM wote wanalalama kuwa zanzibar ni nchi na wote wamekuwa na mawazo ya kutaka kujitenga. sasa sisi wabara tunang'ang'ania nini wakati wenyewe hawatupendi na wala hawana hamu tena ya kuendelea kuwa ktk muungano na sisi? hata tukilazimisha, kama mioyoni mwao hawajaridhika itakuwa sio dawa, watakuja tu kuibua wakati wowote, cha maana ni kuvunja muungano huu kila mtu aanze kivyake, kwani sisi wabongo hatuwezi kuishi peke yatu bila zenji? wht do we gain from zanzibaris.....ni kuwapiga chini tu waende kivyao huko, na kuanzia siku hiyo, starting from Magomeni hadi kariakoo, wapemba na maduka yao yale wapewe masaa 24. period.
sijui Kama Makala Hii Nayo Imeshajidiliwa Hapa.
Sasa Hive Nimeanza Kuona Kama Vile Karume Ana Tamaa Sana Ya Kuitawala Zanzibar Maisha Yake Yote. Muungano Ni Kati Ya Vikwazo Vya Yeye Kutimiza Lengo Hilo, Ndiyo Maana Anatafuta Kuigawa Ccm Kwanza Halafu Aondoke Na Kipande Kimoja Cha Ccm Kutoka Kwenye Muungano.
Halafu Huyu Raza Siyo Mara Yake Ya Kwanza Kutaka Kuleta Vurugu Kwenye Muungano Huu. Miaka Ile Ya Themanini Na Tisini Alidhibitiwa Kweli Kweli. Inaelekea Wakati Huu Amepata Watu Wasioweza Kumdhibiti Kwa Hiyo Anawaendesha Atakavyo. Ubishi Wa Kusema Zanzibar Ni Nchi Au Siyo Nchi Ni Wa Kijinga Kweli Kweli. Kama Anazungumzia Nchi Kwa Maana Ya Pande La Ardhi, Hiyo Ni Sawa, Zanzibar Kama Ilivyo Tabora Ni Pande La Ardhi Kwa Hivyo Ni Nchi. Ila Kama Anazungumzia Nchi Kwa Maana Ya Taifa Au Dola, Basi Hapo Anakosea Sana Na Hapo Ndipo Anapowachanganya Wazenj. Sijui Kama Tuna Sheria Ya Dhidi Ya Upindishaji Makusudi Wa Katiba Kwa Manufaa Ya Mtu Binafsi; Inabidi Bunge Letu Liifikirie, Na Adhabu Yake Iwe Kali Sana.
Kwa mujibu wa makubaliano yaliyounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar inayo Serikali yake (SMZ- na Rais Amani Karume kwa hivi sasa). Zanzibar inayo Population inayotambulika (ndio hao Wazanzibari). Inayo mipaka yake (pamoja na huu iliopo Zanzibar channel unaotenganisha Zanzibar na Dar es salaam).Kwa mujibu wa makubaliano ya Muungano inawajibika ku-retain some aspects of her sovereignity. Jee amua wewe hiyo ni Nchi au si Nchi kwa mujibu wa -montevideo- yako.
Waulize wasomi wenzio hao wanasheria. Ukivunja Muungano. Hilo suala linakuwa in-dispute. Mali zake zote zinapelekwa kwa msuluhishi. Kwa hivyo elewa hata ile Ofisi ya Katibu Kata kule Kijijini kwenu ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukianza na Tanganyika yako Unaanza Alifu kwa Ujiti. Zanzibar wana system yao kule. Very Healthy- ina kila kitu Watakachofanya ni kujaliza tu Mambo ya Nje. Wana Vikosi vya SMZ. Huku wakati JWTZ na Polisi na Magereza tunavunja. Tanganyika itabidi uandikishe na uanzishe la kwako. Can u bear the consequencies?- Rejea Hotuba ya Nyerere wakati anawakanya G55 kudai Tanganyika yao.Tuvunje bwana, kwani muungano una faida gani kama sio lawama na chuki tu kati yetu na hawa wanaoitwa wazanzibari? watu wenyewe hatufaidiki nao halafu tunajikomba kwao, kwani tumekosa nini? you think we need them more than they need us, or they would need us more than we need them? tupilia mbali huko bwana.
yote Inaonesha Udhaifu Mkubwa Wa Kikwete Na Wasaidizi Wake Kuweza Kusimama Na Kuzungumza Suala Hili. Hili Ndilo Lililotokea Comoro Kwa Na Namna Fulani. Wakati Bakari Anachezea Muungano Walimpuuzia Hadi Pale Alipojitangaza Kuwa Ni Nchi Huru.
Karume Anachezea Hivyo Hivyo, Na Kwa Vile Sasa Hivi Cuf Na Ccm Zanzibar Wanamsimamo Mmoja Siwezi Kushangaa Kama Wakiamua Kutangaza Uhuru Ccm Na Cuf Watakuwa Pamoja. Ni Udhaifu Mkubwa Sana Kwa Kikwete Kama Rais Wa Muungano.
Waulize wasomi wenzio hao wanasheria. Ukivunja Muungano. Hilo suala linakuwa in-dispute. Mali zake zote zinapelekwa kwa msuluhishi. Kwa hivyo elewa hata ile Ofisi ya Katibu Kata kule Kijijini kwenu ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukianza na Tanganyika yako Unaanza Alifu kwa Ujiti. Zanzibar wana system yao kule. Very Healthy- ina kila kitu Watakachofanya ni kujaliza tu Mambo ya Nje. Wana Vikosi vya SMZ. Huku wakati JWTZ na Polisi na Magereza tunavunja. Tanganyika itabidi uandikishe na uanzishe la kwako. Can u bear the consequencies?- Rejea Hotuba ya Nyerere wakati anawakanya G55 kudai Tanganyika yao.
Nadhani kama ulivyoisema hapo awali labda main issue iwe je,hizo some aspects of sovereignty walizoretain je wana full exercise? bado sio nchi kwa kuwa haina full sovereignty.Mamlaka ya RAIS wa zanzibar hayatofautiani na ya kandoro pale Dar kwani rais wa zanzibar anazo wizara wakati kwa kandoro zinaitwa idara,kandoro ana some aspects of sovereignty akiwa mkoani kwake dar ahali ambayo hata karume ndio ilivyo,mambo mengine hadi asubiri mkuu wa kaya.Kandoro mwenyewe anaweza kuamru jeshi la polisi mkoani kwake kufanya chochote linachoweza kufanya ila hawezi kuamuru JWTZ vivyo hivyo karume hawezi kuamuru JWTZ haya nadhani ndio yanayoleta huu utata.
Karume Ni Rais Wa Zanzibar Na Kwa Hili Wote Wanamsapoti Leo Unampaka Ujinga Na Uhaini Wa Kumfananisha Na Muhaini Wa Commoro
Ni Sawa Na Kusema Wazanzibari Wote Ni Wahaini(si Wanamsapoti)?