Kwa namna moja ama nyingine ninawasiwasi na muungano huu. Hii ni kutokana na upande moja kuegemea upande mwingine kiuchumi na kisiasa.
Kwa upande wa bara ukiangalia hali halisi, inaonyesha population ya watu ni kubwa sana lakini wawakilishi ni wachache kulinganisha na zanzibar.
Mfano Bara kuna majimbo 189 = wabunge 189 @ 231216 kwa jumla ya watu 43,700,000 (takwimu ya UN 2009)
Zanzibar kuna majimbo 50 = wabunge 50 @ 20,000 kwa jumla ya watu 1,000,000
Kwa hali hii kama watanzania tukagundua kuwa wale wabunge nao wanalipwa kupitia kwenye kodi zetu, tutaomba wapunguzwe kutoka 50 mpaka watano. Na wakikataa, huo muungano ni lazima uvunjike hakuna ujanja.
Katika hili hata Dr. Slaa aliahidi kuwa angeshinda urais, lazima suala la muungano lingerudishwa mezani kujadiliwa.