Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Among the Many books that have been written about the Zanzibar Revolution ;I suggest for those who haven't already read," The Revolution in Zanzibar" by Don Petterson is a worthwhile read.
 
Uhuni uliofanyika Janury 12, 1964( unfortunately leo "tunaadhimisha") ndio donda sugu linaloleta political instability visiwani mpaka leo.

Ndio maana kila nikisikia "mazungumzo ya muafaka" I fall off my chair laughing.....
 
Uhuni uliofanyika Janury 12, 1964( unfortunately leo "tunaadhimisha") ndio donda sugu linaloleta political instability visiwani mpaka leo.
Kamanda yale ni Mapinduzi....
Nakutakia kila la Heri katika kusherehekea siku hii adhimu
 
Na Salma Said, Zanzibar (Mwananchi)
WAKATI leo Wazanzibari wanasherehekea leo miaka 44 ya Mapinduzi, kuna baadhi ya

washiriki wa mapinduzi hayo wanajutia vitendo vilivyofanywa wakati huo.


Akizungumza kwa masikitiko jana, mshiriki mmoja ambaye hatajwi sana katika wana mapinduzi, Ali Omar Juma (Lumumba) alisema anajutia vitendo alivyofanya kila

zinapomjia fikra za mauaji ambapo nyumba zilivamiwa na kuporwa.


Mzee Lumumba ambaye hivi sasa anaishi katika maisha duni Mtoni Nje kidogo na Mji wa Zanzibar, hakutarajia kuishi maisha hayo kutokana na mchango wake mkubwa katika mapinduzi hayo.


Alisema kwamba wakati wakifanya hivyo, walikuwa na lengo na kujikomboa lakini kuna baadhi ya watu walikuwa na malengo mengine ambayo yalikwenda kinyume na utu wa ubinadamu.


Sherehe za Mapinduzi huadhimishwa kila ifikapo Januari 12 ambapo siku kama hiyo ndio Zanzibar ilipinduliwa na wazalendo na kuuangusha utawala wa kisultani uliokuwa ukiongozwa na Jamshid Bin Abdaalah.


Katika kusherehekea Mapinduzi miradi kadhaa hufunguliwa visiwani hapa ikiwemo

mashule, vituo vya afya na na barabara ambapo viongozi wa kitaifa hushiriki katika

maadhimisho hayo.


Utawala wa kisultani ulijikita kwa miaka kadhaa Zanzibar huku wazalendo wakikosa

fursa na haki za nchi yao kutokana na ubaguzi uliokuwepo ambapo baada ya kufanyika

Mapinduzi haki zote zilirudi kwa raia wa Zanzibar.


Mapinduzi hayo yaliongozwa na Jemedari Hayati Mzee Abeid Amani Karume akiongozana na wenzake ambao waliunda timu ya watu 14 iliyokuwa ikiratibu na kushughulikia mchakato wa kufanyika Mapinduzi pamoja na kundi la Umma Party ambao kwa kiasi kikubwa walifanikisha mapinduzi hayo.
 
Na Salma Said, Zanzibar (Mwananchi)

Mzee Lumumba ambaye hivi sasa anaishi katika maisha duni Mtoni Nje kidogo na Mji wa Zanzibar, hakutarajia kuishi maisha hayo kutokana na mchango wake mkubwa katika mapinduzi hayo.


Alisema kwamba wakati wakifanya hivyo, walikuwa na lengo na kujikomboa lakini kuna baadhi ya watu walikuwa na malengo mengine ambayo yalikwenda kinyume na utu wa ubinadamu.
Fainali uzeeni, mara baada ya mapindunzi wengi, walianza kuishi maisha ya anasa kubwa na kujisahau kabisa katika kuwekeza nguvu zao mara baada ya kustaafu. Sasa nguvu zimewaishia wanaanza kulia lia...!
 
Fainali uzeeni, mara baada ya mapindunzi wengi, walianza kuishi maisha ya anasa kubwa na kujisahau kabisa katika kuwekeza nguvu zao mara baada ya kustaafu. Sasa nguvu zimewaishia wanaanza kulia lia...!

wengine walisahau kuwa kuna uzee wakawa wanapigania vimwana vya kimanga.

walisahau hata dhamira za chama chao kuwa ni kuwakomboa wanyonge hasa wa kiafrika.
 
sasa alipokuja mheshimiwa shamte akaanza kuwanyofoa kwa kutaka kuwaweka wazanzibari asili na hapo ndipo hali ikazidi kuharibika.

CCM ilichupia basi kwa nyuma baada kumuona Okello na kundi lake kina said Bavuai na Washoto ni wahuni na hata maneno aliokuwa akizungumza Okello ukiyasoma utagundua ni jinsi gani wasingeweza kuongoza dola. kwa hiyo ASP na UMMA party wakatake advantage.

huo ndio ukweli.

Mkuu utakuwaje ukweli wakati hata haujui CCM ilizaliwa lini?

Kama ni kweli simulizi zilizotolew humu, inatakiwa watu wa Zanzibar mumpe heshima za pekee Mwalimu Nyerere (RIP). Huyu ndiye aliyewahifadhia Sultan baada ya kukataliwa na Kenya, huyu ndiye aliyetuma askari kumbana Field Marshall na ndiye aliyewaongolea jina mizi Okello miongini mwao. Ni Mwalimu tena baada ya kuuawa kwa Karume (RIP) ndiye aliyewahifadhi wakina Babu na kuwaepusha yale yaliyowapata wakina Hanga, Mdungi na wengine. Badala ya kushinda kulaumu inabidi waangalie vyema historia yao na wawape credit wale wanaostahili! Kumbe hiyo Tanganyika ambayo hamishi kuisemea ovyo ndiyo kila wakati imekuwa kimbilio lenu wakati wa matatizo.
 
Mkuu utakuwaje ukweli wakati hata haujui CCM ilizaliwa lini?

inatakiwa watu wa Zanzibar mumpe heshima za pekee Mwalimu Nyerere (RIP).

Heshima ya Mwl. Nyerere ipo pale pale... kwa kuweza kuyatambua mapinduzi ya Zenj. Ili jina lake lisipotee barabara moja mjini Zenj imepewa jina lake...
 
Mkuu utakuwaje ukweli wakati hata haujui CCM ilizaliwa lini?

Kama ni kweli simulizi zilizotolew humu, inatakiwa watu wa Zanzibar mumpe heshima za pekee Mwalimu Nyerere (RIP). Huyu ndiye aliyewahifadhia Sultan baada ya kukataliwa na Kenya, huyu ndiye aliyetuma askari kumbana Field Marshall na ndiye aliyewaongolea jina mizi Okello miongini mwao. Ni Mwalimu tena baada ya kuuawa kwa Nyerere ndiye aliyewahifadhi wakina Babu na kuwaepusha yale yaliyowapata wakina Hanga, Mdungi na wengine. Badala ya kushinda kulaumu inabidi waangalie vyema historia yao na wawape credit wale wanaostahili! Kumbe hiyo Tanganyika ambayo hamishi kuisemea ovyo ndiyo kila wakati imekuwa kimbilio lenu wakati wa matatizo.

Usimnange mwenzio, kapitiwa tu kama ilivyokutokea wewe hapo juu!
 
Historia ya mwafrika huenda sambamba na Umaskini, kutawaliwa na fitna. Hadi hapo tutakapo jua nini thamani ya UHURU na malengo ya mapinduzi kuondoa vitu hivyo na sio kuvidumisha ndipo mwafrika ataweza ona pepo ya hapa duniani.
Besides that sisi sote manyani tu! uhuru na salama yetu ni kuishi juu ya miti.
 
Usimnange mwenzio, kapitiwa tu kama ilivyokutokea wewe hapo juu!

Asante Mkuu! Mwenyezi anajinsi ya kutuumbua sisi wenye mazoea ya kujifanya wajuaji kupita kiasi. Samahani Mtu wa Pwani kwa kukunanga(?) kama alivyosema Kithuku.
 
Mtindo:Wa MAPINDUZI !!
Umma party kwa kushirikiana na ASP

Na ASP kushirikiana na TANU

Na TANU kushirikiana na Muingereza na Mmarekani yamefanikishwa Mapinduzi!!

Umma party wamepinduliwa kwa kutumiwa ASP

Na ASP wamepinduliwa na TANU

Na TANU wamepinduliwa na Mmarekani na Muingereza na kuitwa CCM !!
Sasa kuna ishara ya Muingereza na Mmarekani kuipinduwa CCM baada ya kumaliza kazi waliopewa!!

Na ndio maana Mapinduzi yakawa DAIMA.
 
Nimesoma kwa uangalifu, makala zote hapo juu kuhusu mjadala huu. Ni lazima nikiri mimi ni mgeni katika ukumbi huu wa JF na siku shiriki, hata kwa kusoma tu, wakati suala hili lilipojadiliwa siku hizo za awali, hata hivyo, ningeomba nami nitowe mawazo yangu kama ifuatavyo.

Sultani alikuwa na haki ya kutawala Oman. Kimsingi alikuwa hana haki ya kuitawala Zanzibar. Alipohamishia Makao Makuu ya utawala wake kutoka Oman na kuyaleta Zanzibar, alikuwa hawatendei haki Wazanzibar. Alikuwa akitawala Zanzibar kwa nguvu na hakuwa na tofauti yoyote na Wakoloni wengine. Hata Waingereza walikabidhiwa Zanzibar na pwani yote ya Kenya na Sultan kwa ulinzi wa himaya ya Sultani na Sultani mwenyewe kwa jumla.

Kwa ajili hiyo, hoja ya kusema kuwa Sultani hakuwa na serikali wakati Mohammed Shamte akiwa Waziri Mkuu haina msingi imara. Serikali ilikuwa ya Sultani. Na wakati wote serikali ikiwa ya Sultan ni lazima tukubali kuwa Wazanzibar walikuwa bado hawajajikomboa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Baada ya kusema yote hayo hapo juu, inanibidi hapa niweke bayana kuwa siungi mkono vita au vurugu ya aina yoyote, katika kuleta mapinduzi ya kisiasa katika nchi yoyote na kwa wakati wowote ule. Na ninayalaani mauji holela ya binadamu wasio na hatia, iwe yamefanywa na ASP huko Zanzibar au CCM nchini Tanzania.

Hakuna shaka yoyote ushindi wa muungano wa ZNP na ZPPP ulishabikiwa kwa mizengwe iliyopangwa ili kudumisha utawala wa Sultani katika visiwa vya Zanzibar. Siwezi hata kidogo kushawishika vinginevyo. Mimi si mtu wa Zanzibar, lakini wakati mambo haya yakitokea kule Zanzibar, nilikuwa mtu mzima aliyesoma na akili zangu timamu. Najua, si wakati ule wala si wakati huu, unapoendelea kuwatawala watu, iwe kwa mabavu au kwa mizengwe, unakalia kuti kavu na wewe kuanguka si ajabu. ASP walikuwa na uwezo wa kusubiri au kulamikia maonevu waliofanyiwa, lakini unapoona hakuna njia nyingine ya kupata mtu haki yake, ndio mambo mabaya kama haya ya mapinduzi ya Zanzibar yanapotokea. Kwa
sababu hii, naona lawama za mauaji yale inasimama sawasawa katika mabega ya ASP na ZNP/ZPPP; pia na kwa Sultani na Waingereza.

Na kwa wote walioguswa na maafa haya, kwa namna moja au nyingine nawapa pole. Ni bahati mbaya ya matokeo ya kihistoria. Ingekuwa bora pia tusisikie kauli za kuwa eti watu wanadai kuwa "yale mapanga bado tunayo" au "kwani sisi tulipata bendera kwenye kisahani." Kauli kama hizi zinaashiria utawala wa kimabavu na kimizengwe. Matokeo yake, mwisho unakuwa ni yale yale, "anayeishi kwa upanga, hufa kwa upanga huo huo. Historia haiachi kujirudia. Tujifunze. Ukimpeleka paka ukutani, akawa hana njia ya kutokea, atakurudia akukwaruze na hata pengine akutoe macho.

Tuache siasa za visasi, "yaliyopita si ndwele, tugange yajayo."
 
Muafaka wa Zanzibar umefika hatua gani?



TULIPATWA na faraja kubwa wakati yalipoanza mazungumzo ya makatibu wakuu wa vyama vya CCM na CUF huko Zanzibar, yenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kisiasa visiwani humo.
Tulipata kuandika huko nyuma kwamba, tukiwa sehemu ya Watanzania wapenda demokrasia tulisema bayana kuhusu msimamo wetu wa kuyaunga mkono mazungumzo hayo ya heri.

Hata hivyo wakati tukisema hayo, tulieza wazi wazi kuwapo kwa wasiwasi kuhusu dhamira ya kundi dogo la wahafidhina lenye lengo la makusudi kabisa la kuyavuruga mazungumzo hayo kwa sababu wanazozijua wao.

Tulisema hivyo tukitambua kuwa kwa zaidi ya miaka 15 sasa, tangu Tanzania itangaze rasmi kuukubali mfumo wa ushindani wa vyama vingi, kumekuwa na mambo ambayo kimsingi yamekuwa yakizua maswali magumu kuhusu utayari wetu wa kuukubali mfumo huo na kuheshimu matokeo yake.

Ushahidi wa wazi kuhusu hilo ulikuwa ukijionyesha huko Zanzibar ambako chaguzi zote tatu za vyama vingi zimekuwa zikizingirwa na mambo ya ajabu ajabu ambayo kimsingi ndiyo yamezaa mazungumo haya ya sasa na mengine kabla yake.

Pamoja na ukweli huo basi, wasomi, wanasiasa na taasisi zinazoheshimika kwa pamoja wamekuwa wakitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu namna ya kuendesha mambo visiwani humo, ambayo kwa bahati mbaya yamekuwa yakikwamishwa na viongozi walio madarakani na hususan wale wa upande wa Zanzibar.

Kwa mfano, huko nyuma, kwa zaidi ya mara moja chama hicho tawala kilionekana kikifanya mchezo wa kuigiza wa kufanya kile ambacho machoni kilikuwa kikionyesha nia njema kabisa ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la Zanzibar.

Mwaka 2001 kwa mfano, baada ya hali ya kisiasa visiwani huko kuchafuka, CCM ililazimika kukutana na viongozi wa CUF na kukaa meza moja katika vikao ambavyo vilizaa muafaka wa Oktoba mwaka huo huo.

Hata hivyo, muafaka huo ambao pamoja na mambo mengine ulipendekeza kuangaliwa kwa uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, umeendelea kupuuzwa kwa matendo na kwa maneno na viongozi wa CCM hususan wale wa upande wa Zanzibar.

Jambo la ajabu ni kwamba, hata baada ya vikao halali vya chama hicho tawala na viongozi wake wakuu kutangaza kwamba, walikuwa wameamua kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la Zanzibar, bado kumekuwa na maneno ya ajabu kutoka kwa viongozi wa pande zote yanayoiweka hali katika mazingira magumu.

Wakati maneno ya kichochezi ya baadhi ya viongozi wa CCM Zanzibar yakionekana kutokomea, ni ajabu kwamba hivi sasa si viongozi wa CCM wala wale wa CUF wanaoonekana kutoa matumaini yoyote.

Hata hivyo tukiwa sehemu ya Watanzania tunaofuatilia kwa karibu mchakato mzima wa suala hilo, tunaamini kwamba pande zote mbili zimejifunza vya kutosha kutoka Kenya, ambako mazungumzo yao ya kusaka muafaka yanatoa mwelekeo mwema katika kipindi kifupi.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya Watanzania wenzetu kwa siku kadhaa sasa kutuuliza hatua ambayo vikao vya kamati ya makatibu wakuu imefikia katika kusaka muafaka, ambao sasa unaweza kuonekana kama ni jambo ambalo halipo.

Tunachoweza kuvieleza vyama vya CCM na CUF ni kwamba, ukimya wao umeshaanza kuwatia wasiwasi wananchi wanaotaka kujua kwa hamu ni wapi yalipofikia mazungumzo ya muafaka. Ni lini basi yatahitimishwa?

tanzania daima
 
Msekwa aendeleza ngonjera za muafaka Visiwani Zanzibar
Na Muhibu Said

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mazungumzo ya kutafuta muafaka wa kisiasa kati yake na Chama cha Wananchi (CUF), yaliyoanza Januari 17, mwaka jana, bado yanaendelea.


Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, alipoulizwa na Mwananchi kuhusu hatma ya mazungumzo hayo, muda mfupi baada ya kuhudhuria kikao cha Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD), katika Ukumbi wa Mayfair, jijini Dar es Salaam jana.


"Mazungumzo bado hayajafika mwisho," alisema Msekwa na kuongeza kuwa sababu ya kuendelea kwa mazungumzo hayo ni kuwapo kwa vipengele vya ambavyo bado vinajadiliwa na wajumbe wa kamati za vyama hivyo.


Hata hivyo, alisema baadhi ya vipengele tayari vimeshajadiliwa na kufikiwa makubaliano kati ya pande hizo.


Alisema haoni kuwa ni busara mazungumzo yakaisha kama wanavyotaka baadhi ya watu bila kujadili vipengele vyote vya mazungumzo na kufikia muafaka.


Aliwashangaa wanaong'ang'aniza mazungumzo hayo yaishe haraka bila kuzingatia suala hilo na kuwataka wawape muda wajumbe wa kamati ya vyama hivyo wakamilishe mazungumzo juu ya vipengele vilivyobaki.


Awali, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ambaye ni Kiongozi wa Kamati ya Mazungumzo hayo kutoka chama hicho, alikataa kuzungumzia suala hilo.


"No comment (sina la kusema)," alisema Maalim Seif alipotakiwa na Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo kuzungumzia suala hilo ukumbini hapo jana.


Mazungumzo ya muafaka yalianza Januari 17, 2007 kwa kikao cha kwanza kilicho wakutanisha makatibu wakuu wa vyama hivyo na mchakato wa mazungumzo ukaanza.


Mausla yaliyojadiliwa ni pamoja na uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 30, 2005 na taathira zake, usawa na haki katika kuendesha siasa, masuala ya utawala ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, njia za kuimarisha mazingira ya maelewano ya kisiasa na uendeshaji wa uchaguzi huru na wa haki Zanzibar, na utaratibu wa kutekeleza programu ya utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa katika mazungumzo haya.

?

Kwa mujibu wa Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, mambo ambayo yameshajadiliwa na kufikiwa hatua nzuri.


Mapema, Mwenyekiti wa TCD Cheyo alisema TCD inawapongeza wabunge kwa kazi nzuri waliyoifanya kwenye mkutano wa kumi wa Bunge uliopita katika kupambana na ufisadi wa fedha za umma.


Cheyo ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha UDP na Mbunge wa Bariadi Mashariki, alisema sekretarieti vya TCD imeagiza kuwa vikao hicho vifanyike katika ngazi mbalimbali nchini.


Alisema uongozi wa TCD umeamua nafasi ya Mwenyekiti wake, iendelee kushikiliwa naye na ile ya Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo utashikiliwa na Msekwa katika kipindi cha mwaka mmoja.


Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge, akiwamo Msekwa, Maalim Seif (CUF), Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Cheyo na wajumbe wao.

mwananchi
 
"Mazungumzo bado hayajafika mwisho," alisema Msekwa na kuongeza kuwa sababu ya kuendelea kwa mazungumzo hayo ni kuwapo kwa vipengele vya ambavyo bado vinajadiliwa na wajumbe wa kamati za vyama hivyo.
 
Mwanasheria Mkuu amchambua Lowassa

2008-03-03 08:41:37
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bw. Idd Pandu Hassan, amesema Bw. Edward Lowassa hastahili kuitwa Waziri Mkuu Mstaafu kwa vile hakufikisha kipindi cha miaka mitano, ambapo angestahili kuitwa mstaafu.

Aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Nipashe juu ya nafasi ya wastaafu wanaoondoka kwa sababu mbali mbali, ikiwemo tuhuma za ubadhirifu.

Mwanasheria Mkuu alisema kwa mujibu wa sheria za viongozi wastaafu hutakiwa kutumikia serikali kwa miaka mitano na sio chini ya hapo, ili uweze kunufaika na mafao yote ya wastaafu.

Bw. Pandu alisema sheria hiyo haina tofauti na ile ya watumishi serikalini, kwa vile huwezi kuitwa mstaafu hadi ufike umri wa miaka 55 hadi 60 na hapo ndipo pia unastahili kulipwa mafao yako.

``Huwezi kumwita Bw. Lowassa kuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu au Waziri Mkuu aliyefukuzwa kwa vile alijiuzulu mwenyewe na hasa unaweza kumwita `aliyekuwa Waziri Mkuu`, basi,`` alisema.

Hata hivyo, alisema mtu anaweza kumuitwa waziri mkuu mstafu kwa lugha ya kisiasa tu ili kuendeleza umoja na mshikamano, kama ilivyotokea kwa viongozi wengine waliondoka madarakani kwa matatizo.

Alisema wapo viongozi wanaoitwa wastaafu katika lugha ya kisiasa, lakini hawana sifa za kuitwa hivyo na kutoa mfano wa aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Bw. Seif Sharif Hamad.

Alisema Bw. Hamad hana sifa ya kuitwa Waziri Kiongozi Mstaafu kwa vile hakutumikia kipindi cha miaka mitano, lakini amekuwa akinufaika na kulipwa mafao yake baada ya kufikiwa muafaka wa mwaka 2001, ili kujenga umoja na mshikamano.

Alisema viongozi wengine wamekuwa wakiitwa wastaafu kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano katika taifa, kama vile Mzee Aboud Jumbe Mwinyi na Mzee Ramadhan Haji Faki ambaye aliwahi kuwa Waziri Kiongozi.

Bw. Pandu alisema viongozi hao hawakuondoka kwa utaratibu wa kustaafu, lakini kwa kuzingatia umoja na mshikamano wa taifa ndio maana wanaitwa viongozi wastaafu na kulipwa mafao yao kama kawaida.

Hata hivyo, alisema Bw. Lowassa atabakia kama kiongozi aliyejiuzulu mwenyewe kwa vile Bunge halikupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Bw. Hamad alifukuzwa katika CCM kutokana na kwenda kinyume na maadili ya chama, chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Aidha, Rais Mstaafu, Bw. Jumbe alijiuzulu yeye na Waziri Kiongozi wake kutokana na kilichoitwa machafuko ya kisiasa Zanzibar.

Tangu Bw. Lowassa atangaze kujiuzulu kumekuwepo mjadala mkubwa juu ya kuendelea kuitwa Waziri Mkuu Mstaafu, au Waziri Mkuu wa zamani.

Bw. Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli alijiuzulu kutokana na kashfa ya kampuni iliyopewa zabuni ya umeme wa dharura, Richmond.

Wakati huo huo, Simon Mhina anaripoti kwamba Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augustine Mrema amemshauri aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, aachane na CCM na atafute chama kingine.

Akizungumza na Nipashe ofisini wake jijini Dar es Salaam Mwanasiasa huyo alisema kama kweli Bw. Lowassa anasema kutoka moyoni mwake kwamba ameonewa na hahusiki na ufisadi, basi awatose CCM.

``Inaonekana kwamba Lowassa hakutaka kujiuzulu, kwa mujibu wa kauli zake ndani na nje ya bunge anaonyesha wazi kwamba amedhalilishwa ameonewa, inaonekana huyu bwana anayo agenda na siri nzito moyoni. Mimi sio Mungu sijui ukweli halisi, lakini atauthibitishia ulimwengu kwamba hana kosa, iwapo ataachana na chama kilichomsingizia,`` alisema Bw. Mrema.

Kiongozi huyo alikuwa anazungumzia hatua ya Bw. Lowassa kutangaza rasmi kwamba ameufunga majadala wa yeye kujiuzulu baada ya kuamua kuwajibika kutokana na kuhusishwa na kashfa ya Richmond.

Alisema kama kweli Lowassa akiwa Waziri mkuu wanchi anadhani kasingiziwa, basi nchi inayo matatizo makubwa.

Bw. Mrema alimuonya Bw. Lowassa asifikiri kwamba yaliyomfika yatawatoka wananchi vichwani na kusahau.

``Nimesikia watu wakisema huu sio mwisho wa Lowassa. Mimi nasema alichofanya hakitasahaulika, kwa hiyo njia ya kujisafisha sio kuzungumza mitaani achukue hatua ya kuonyesha kukerwa na kusingiziwa huko, yaani kuihama CCM, kama kweli anasingiziwa,`` alisema.

Alisema iwapo atakihama CCM atapata uwanja wa kutoboa siri zote za chuki zilizojengeka katika serikali.

``Lowassa ndani ya CCM ajihesabu amekwisha, amejizolea sifa mbaya sana, na bila kuchukua uamuzi wa kijasiri ataingia kaburini na lawama,`` alisema.

Alipoulizwa kwamba atakuwa tayari kumpokea Bw. Lowassa ndani ya TLP, Bw. Mrema alisema iwapo ataamua kujiunga atahojiwa kwanza.

``Akija kwetu tutamhoji kiundani, maana kupitia kwake tutafanikiwa kuwabaini mafisadi wengi zaidi, na kama atakuwa tayari kuwataja na mahali wanapoweka pesa zao, tutamsamehe, huu ndio mkakati wangu, hata nilipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani majambazi ambao walikuwa wanasalimu amri na kurejesha silaha, nilikuwa nawasamehe, halafu nawatumia kuwafichua wenzao waliojificha. Mtindo huu nataka kuutumia pia kwa Lowassa,`` alisema Bw. Mrema.

Alisema licha ya kwamba amelaumiwa vya kutosha, Bw. Lowassa anaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa lawama hizo, iwapo atawasaidia watanzania kuwafichua mafisadi ndani ya serikali.

Alisema ni ukweli ulio wazi kwamba kuna mambo mengi yanayofanana na Richmond, ambayo bila shaka Bw. Lowassa anayafahamu na hawezi kulipua bomu akiwa bado ndani ya CCM.

SOURCE: NIPASHE

Hiyo kauli (bold) ya Mrema imeniacha sina mbavu...lakini ni kweli,kuna umuhimu wa kutumia panya kunasa panya wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom