Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
no no no
jamani tuombe amani tusiombe shari, jamani maisha ya watu ni bora tena sana kuliko chochote.
njia ziko nyingi za kutatua mgogoro huu, nnawaomba wazanzibari kwa itikadi zao zote wasikubali kushindwa na shetani na kuvuruga utu wao.
cha kupoteza kipo tena wazi utu wetu na nchi yetu ambayo ni fahari yetu.
wanasiasa wa pande zote angalieni suala hili msilichukulie kimzaha mzaha, mtakuja juta majuto ambayo hayataisha umri wenu wote.
nnaiona zanzibar iko kwenye huzuni, mie zanzibar ni kwetu sitopenda hata siku moja iwe kama kenya na wala uccm wangu si bora mbele ya maisha ya wazanzibari wenzetu bila ya kujali siasa zao.
viongozi wetu tunakuombeni msitunishiane vifua kaeni muyazungumze nafasi bado mnayo, jitumeni tena.
maalim seif na Mheshimiwa Makamba kaeni mtusaidie ktk hili.
jamani jamani nnajua kuna watu wanachuki na machungu ya muda mrefu wasi wasi wangu wasije wakaona wafanye kama vile walivyofanya kenya.
ule sio mfano mzuri
My dear... nimenyosha mikono yote miwili juu katika hili...
Hoja yako imezidi yangu na sipingani kabisaaa na ulichosema. Nakubali kuwa kuna section fulani ya jamii yetu ambayo inaweza kufanya chochote wakati wowote.
Katika hili basi naungana nawe kuwa Title ibadilishwe kidogo ili ifanane na content ya mtoa mada!
kwi kwi kwi.... naona debate hapa ilikuwa kati ya Bill Clinton (wewe) na Kichaka senior (mimi) mwaka 1992. Imebidi niangalie saa yangu kujua ni saa ngapi!
mwafrika wa kike, bado una point. don't give up easily. iki kichwa cha habari hakisomwi na wanacuf tu, ambao wanaweza kuhamasika na kuingia mitaani, la hasha, pia kinasomwa na JK ambaye anaweza kuangalia uzito wa jambo hili na kubadilika.
Mwanakiji hawa watu ni ndugu zetu, namna tunavyowakemea mafisadi wa uchumi wetu, ndivyo tunavyopaswa kuwakemea mafisadi wa uhuru wa zanzibar. sijaridhika kuwa sasa ni muda wa kutumia lugha nyepesi, wakati lugha hiyohiyo tuliitumia kwa ndugu zetu wa chadema kule Kiteto.
mimi sitaipigia campaign CCM kwa ajili ya kuwakandamiza CCM eti kwa sababu mimi ni mbara. sijui kama nimeenda stepi mbili zaidi ya title
Waungwana, swala hili ni tete, nashawishi tuhubiri amani siyo vita. CUF wanapaswa kufanya mapambano ya amani si vurugu, chuki nk. Nasikitika CCM wanavyolichukulia kirahisi suala la Zenj. Ni vigumu kuamini kama Kikwete ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho.
Wito wangu amani first.
Inshaalla na ianze kumwagika kwenu waliko Mabibi na Mashangazi wako.wacha damu imwagike ndio itakuwa TIBA MWAFAKA alosema MSANII JK.
Vipi yakhe sasa wewe ulitaka awe dikteta. Awazuwie wajumbe kutoka Zanzibar wasiseme, pale, maoni ya wanaowawakilisha. If peoples power fahamu tu iko pande zote. Usiione hiyo iliyoko CUF tu bali CCM-Zanzibar nako pia iko na ndiyo kubwa (the latent people's power). Ni vyema kuwasikiliza kama hawataki mseto wanataka nini na siyo kuwashurutisha (kuwalazimisha) katika jambo ambalo linagusa maslahi na maisha yao ya kila siku. Kwani solution huko ni mseto tu. Jee, hakuna njia mbadala?
mie nnaungana na mheshimiwa Cheyo, wakae kitako waangalie ni vipi watafikia suluhisho.
njia za amani ndio njia za busara, hapa pazito mie nnajua siasa kwa wazanzibari ilivyo.
kuna watu wao hawana kazi zaidi ya kufuatilia siasa.
pia kwa masikitiko yangu nnawatolea ;hawa ndugu zetu wa cuf kwa nn mlienda kuwatangazia wananchi suala lile na kuwapa matumaini mkijuwa wazi hamjafikishia mwisho ndio tuseme mlikuwa mnaweka mazingira ya kutekeleza plan b?
jueni mkiingia barabarani serikali itarudi jambo hilo kwa nguvu na hapo itakua hatari maana hofu yangu wanachama wataaamua kuwavaa wanachama wenzao na kitu hicho si cha kuomba.
vyama mnatakiwa kuweka maslahi ya taifa mbele si kutengeneza mazingira ya kuonekana mnawapenda wananchi ili mpate mtaji wa kisiasa.
muda bado tuombe mungu kikao cha mtendeni kwa watani wetu kije na hali ya amani.
historis Ya Zenj Ni Ngumu Sana....jambo Nalolijua Ni Kuwa Hakuna Zenj Bila Muungano.mpemba Kamwe Hatotawala Zanzibar,nasaema Kamwe Halitotokea....zenj Siyo Ya Wapemba Au Wana Cuf
my dear.. miye naamini katika uhuru wa maoni lakini mkiwa mmerundikana kwenye ukumbi wa sinema halafu mtu mmoja akalia "moto" watu wakaanz kukimbazana na kuuana wakigombea mlango na baadaye mtu huyo akasema nilikuwa natumia "free speech" basi free speech has lot is meaning.
Binafsi naamini pia kuwa yawezekana kuitisha kura ya maoni Zanzibar ikasababisha vurugu zisizo na sababu na hata umwagaji damu usio wa lazima yoyote ile; lakini hii ni tofauti na mtu kusema "ni zamu ya Kikwete kuwaua wazanzibari".
Maneno hayo sidhani kama yana lengo la kutuamsha sisi au wanachama kufanya mauaji hayo lakini yanaweza kabisa kufanya watu wajihami kwa kufanya preemptive strike.
Visiwa vya Zanzibar vimemwaga damu ya kutosha hata kabla ya Mapinduzi, na hatuwezi kuendelea kutawala au kutawalana kwa misingi ya umwagikaji damu kwani kila damu inapomwagika kilio cha damu hiyo huenda kizazi kingine.
Lakini kuna mtego mwingine, JF ni chombo chenye nguvu sana katika kutoa habari na kupasha watu habari na kama tulivyoshuhudia mambo mengine mengi huanzia hapa; sasa itakuwaje mtu akiinukuu JF na kudai "Kikwete ana mpango wa kuua Wazanzibari" na akiulizwa umetoa wapi akasema JF? Na hapa nazungumzia watu ambao hawana muda mrefu wa kusoma internet na wanapitia kwa haraka haraka..
Kama mtu akisema "Kura ya Maoni yaweza kusababisha umwagikaji damu" nadhani laweza kuwa kweli zaidi kuliko kusema "ni zamu ya Kikwete kumwaga damu ya Wazanzibari", kwanza it is put as if it is factual; and secondly, ni kujaribu kumbebesha lawama Kikwete kwa umwagikaji damu as if ana nguvu za mbinguni. Kama kutatokea umwagikaji damu ni makosa ya jamii nzima na vyama vyote viwili vitabeba lawama (japo kwa degree tofauti)
HISTORIS YA ZENJ NI NGUMU SANA....JAMBO NALOLIJUA NI KUWA HAKUNA ZENJ BILA MUUNGANO.MPEMBA KAMWE HATOTAWALA ZANZIBAR,NASAEMA KAMWE HALITOTOKEA....ZENJ SIYO YA WAPEMBA AU WANA CUF
Chama Cha Majambazi (CCM) sio chama cha kuaminika hata kidogo, siku zote watatumia kila aina ya njia za ulaghai na udanganyifu ili waendelee kutawala. Nadhani Wazanzibar wameshavumilia vya kutosha na kuendelea kukubali huu upumbavu unaoletwa na CCM itakuwa ujinga mwingine. Sitoshangaa CCM wakiitisha hizo kura za maoni halafu wakaiba tena hizo kura na kuweka matokeo wanayotaka wao. Yaani ni usanii mtupu unaoendelea ambao uunaongozwa na Msanii Mkuu Jakaya Kikwete.
Chama Cha Majambazi (CCM) sio chama cha kuaminika hata kidogo, siku zote watatumia kila aina ya njia za ulaghai na udanganyifu ili waendelee kutawala. Nadhani Wazanzibar wameshavumilia vya kutosha na kuendelea kukubali huu upumbavu unaoletwa na CCM itakuwa ujinga mwingine. Sitoshangaa CCM wakiitisha hizo kura za maoni halafu wakaiba tena hizo kura na kuweka matokeo wanayotaka wao. Yaani ni usanii mtupu unaoendelea ambao uunaongozwa na Msanii Mkuu Jakaya Kikwete.
Tukupe kikonbe cha kahawa Mh. Mwiba unazungumza kama uko kijiweni. Tawire. Lete hoja Bwana zinazosimama katika misingi ya utawala bora, na demokrasia. Hivyo kun fa ya kun?. Wenzio wasiseme wanachoamini au kuamua. Kwa sababu eti unaweza kulalabarabarani na kusubiri polisi akukrupushe kwa bakora halafu uliye, wanionea, Hizo seram zimepitwa na wakati yakhe.Moja kwa moja nasema kama Kikwete ni Mkuu wa Majeshi,kama Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM,kama Kikwete ni Mwenyekiti wa AU na kama Kikwete ndie aliewaahidi Wazanzibar walio wengi kuwa muwafaka utatimizwa na upo karibu kumalizika basi yeye ndie mhusika mkuu kwa lolote lile litakalotokea Zanzibar ,ifahamike wazi kuwa kwa CCM hawa akina karume na genge lake hawana uwezo wa kuizuia CUF hata dakika moja na hawana ubavu wa kuzuia maamuzi ya CCM Butiama kwa kupinga kitu chochote kile zaidi ya kutomezwa au kuamriwa na kufuata ,baraka hizi za maamuzi moja kwa moja anahusika Mkuu wa Kaya na mtandao wake katika kuendeleza ukandamizaji wa haki za binadamu waishio Zanzibar.
Inaposemwa Kikwete ,ikiwa leo wazanzibari wataingia barabarani amri ya piga uwa itatoka kwa Mkuu wa majeshi kama ilivyotoka kwa Mkapa alipokwenda kuwaua waPemba 2001,na kutoa wakimbizi ambao hadi hii leo wengine wapo kenya na Somalia.
Hivyo alietoa amri ni Kikwete ,kuna maraisi wengi tu wanashitakiwa baada ya kutokea mauaji ,anytime Mkapa anaweza kushitakiwa na hili limo katika agenda za waPemba wanaoomba ni huyu jamaa asije akajifia na mapema lakini wakipata nafasi tu basi Mkapa atapandishwa kizimbani ,hilo alijue popote alipo ,akumbuke tu waliouwa wakati waHitler basi tunasikia wakipandishwa kwenye kitalu na kujibu mashitaka.
Huyu Kikwete ndie alieandika waraka rasmi kuwaomba CUF wasijitoe katika mazungumzo ,je aliogopa kitu gani au ni lipi lilomfanya aandike barua ile kwa haraka ,sasa ikiwa ni muislamu moja kwa moja ataingia katika kundi la wanafiki maana ametoa ahadi na hakuitimiza na wala hajasikika kutoa kauli ,tusubiri hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi.
Wazanzibari wanasema weka jeshi na polisi kando uwawachie wao na CCM aonekane nani mwanamme.
Kwa vile Chama cha CCM kimeukataa muafaka inambidi Makamba ajiuzulu na kwa kuongezea jamaa wanasubiri kauli rasmi ya CCM ili waanze vituko ,halafu chama chenyewe ni CUF fujo wanaliweza bila ya shaka yeyote ,maana sasa wameshaamini kama ustarabu hauna mshiko ,tena sio Zanzibar tu safari hii ni Tanzania nzima ukichanganya na uhuni wa ufisadi basi ndio lazima watu watajua kama embe ni tunda.Na sikilizeni Zanzibar sasa wanasema nini wamishageuza kura ya maoni ya vyama wanasema kura ya maoni Muungano na sio hapa watauvunja Muungano kupitia umoja wa Mataifa hayo ni mazungumzo yalioanza mitaani ,jamani hili kundi la Karume linajulikana kama la wahifidhina halina wafuasi kabisa wasiwadanganye huko na kusema wana watu ,hamna kitu wandugu kama mnavyowaandama mafisadi kuwa ni kundi fulani basi na huko Zenji nako hili ni kundi lenye mfano wa hao mafisadi.Ikiwa huwezi kuagiza simenti mpaka upitie kwa mke wa Karume ,nani wa kuwahoji ,viwanja na ardhi wanagaiana wana familia tu mapande kwa mapande nani wa kuwahoji zanzibar ni visiwa vidogo tu,watu wote wameshawachoka ,wala Kikwete asijidanganye kwa kuona kuwaweka watu hawa kutampa suport ya kupita uchaguzi wa 2010 ,kama alivyofanya mbinu za yeye kupita na wengine watapita huko huko ,na mtaona CCM Zanzibar ni wale wale tokea miaka hiyo ila huku Tanganyika kila mmoja anakuja na timu yake ,hivyo hakuna lisilo kuwa na mwisho unaweza mwisho ukawa mtamu au mchungu.Kama kutatokea fujo Zanzibar basi wa kulaumiwa ni Mh.Kikwete hilo halina rangi ni jeupe pepe.
Mchezo hapa ni kuitisha uchaguzi mwezi wa kumi mwaka 2009. Matokeo yatakuwa kura za hapana kwa serikali ya mseto 52% na za kukubali serikali ya mseto 47%, zilizoharibika 1%. Baada ya hapo CUF wataanza kuandamana kupinga matokeo, kesi itafunguliwa mahamakani, na mahakama itaahidi kutoa uamuzi mwezi wa tano mwaka 2010, wakati huo ccm watakuwa wameanza kupitisha mtu wa kugombea uraisi wa Zanzibar 2010 na kampeni zitaanza na mambo yote yatakuwa kama ilivyokuwa 1995, 2001, na 2005 na process yote itaanza all over again!
Hivyo wewe hujui kuwa Zanzibar ni Taifa . Fanya reference ya hizo definition ulizopewa hapo. Zabzibar ni Tafa Bwana lililokuwa chini ya himaya ya usultani na British Protectorate. Mapinduzi ya 1964 yalifanyika katika Taifa la Zanzibar ambalo lilijitwalia uhuru wake. Na hilo Taifa likaungana na Taifa jengine la Tanzania-halisi kuunda Taifa moja kubwa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Haya mambo nashukuru kuwa wanasomeshwa watoto wetu. Haya nimenukuu katika vitabu vyake vya skuli ya Msingi.