Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Hapa kuna kichekesho sana; inaonyesha jinsi gani watu waliopewa madaraka ya kuongoza nchi hii walivyo na upeo mfupi wa kuelewa mambo. Dola na serikali ni vitu viwili tofauti kabisa. Kuwa na serikali hakumaanishi kuwa hiyo ni dola, hata wakati wa mkoloni tulikuwa na serikali yetu ikiongozwa na Gavana, lakini hatukuwa dola, bali tulikuwa sehemu ya dola ya mwingireza. Dola inaongozwa na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama tu ambaye anaweza kuipeleka nchi vitani.

Kwa mfano katika nchi ya Marekani ambayo nayo imeundwa kwa muungano wa states kadhaa; kila state ina serikali yake pamoja na mabunge yote mawili, bendera yake, mkuu wa state, na mawaziri wake. Zaidi ya hapo, kila state ina jeshi lake la polisi (State trooper) na mahakama yake mpaka mahakama kuu ya state. Mahakama kuu ya state iko chini ya mahakama kuu ya Federal, uamuzi wa mahakama kuu ya state unaweza kutenguliwa na mahakama kuu ya Federal; nadhani sote tunakumbuka kuhusu maamuzi ya mahakama za State of Florida na Federal kuhusu vote recount katika uchaguzi wa mwaka 2000 na jinsi Federal walivyo-overide maamuzi ya mahakama ya State of Florida. Mkuu wa state pia ndiye amiri jeshi mkuu wa National Guard katika state yake, lakini madaraka yake hayo yako chini ya yale ya amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi ya Marekani. Kwa hali hiyo, state hizo hazijiiti dola kwa sababu zote ziko chini ya amiri jeshi mmoja tu ambaye ni rais wa marekani.

Inawezekana kweli zanzibar ina serikali na kiongozi wa serikali pamoja na mahakama, na jeshi la KMKM lakini haina mamlaka ya kuingia vitani kwa vile mwamuzi wa mwisho kuipeleka nchi vitani ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama anayeishi pale magogoni; huyo ndiye mwenye dola; Karume hana dola kabisa. Zanzibar siyo dola. wafuasi wake wanota dola hawa; amelewa madaraka sasa anataka zaidi.

Je hii purukushani ya kudai dola ni kutaka kukana mamlaka ya Kikwete ili asiwalazimishe kukamilisha mwafaka kati ya CCM na CUF?
 
hili ccm wamelikoroga ....na sasa naona inawabidi walinywe.
when it comes to zanzibar, wazanzibari husahau chama........

suala la kitaifa na lijadiliwe kitaifa na sio kichama.
 
Kuhani what is sovereignty? katika lugha ya Kiswahili.

Hakuna!

And that is a very, very trenchant question, centrally related to this whole Zanzibar brouhaha.

Katiba ya Kiingereza inasema kuna Sovereignty moja Tanzania. Ya Kiswahili haina hilo neno. Tatizo, ile ya Kiingereza haitambuliki.

Sasa mimi japo ni mwenyeji wa mjini Dar si Mswahili mzuuuri sana wa kusema kwa mamlaka kitu chochote kuhusu Kiswahili. Ila ninachokwambia ni kile walichokisema jopo la Majaji watatu kwenye hiyo kesi hapo juu, ambao ninaamini wanajua lugha sana sana, akiwemo Jaji Mkuu A. Ramadhani (JA). Na hawa Majaji kabla ya kutoa matamko huwa wanafanya utafiti, wanapokea mpaka mapendekezo ya wasiohusika na kesi (Friends of the Court Briefs). Wakatafuta maana na asili ya hili neno mpaka kwa aliyelianzisha, mwaka 1577, Ufaransa huko, halafu wakarudi Bongo, hawakupata Kiswahili chake.

Walisema hakuna hilo neno kwenye Kiswahili. Au kwa usahihi zaidi, halijulikani.
 
Umejibu vyema! kwa sababu huu mjadala unazungumzia kitu ambacho sicho. Ulipoanza niliwahi kuuliza swali hili: Je nchi yaweza kuwa Taifa bila mipaka? Na je Taifa laweza kuwa na serikali bila nchi (mipaka)? Je Ndani ya Nchi moja (ndani mipaka) kwaweza kuwemo mataifa mawili ambayo yana serikali zake (clue: Palestina na Israeli). Je serikali ni lazima iwe na nchi ili iwe serikali kamili (clue: States government)?

Sasa utaona watu wanapoangalia maneno ya nchi, serikali, taifa, na dola they are still missing the real thing they are trying to ask and which has been answered. Sovereignty. Majimbo ya Marekani yana sifa zote za kuwa nchi, mataifa, na serikali na dola, lakini hayana kitu kimoja nacho ni sovereignty.

So, kimsingi ukiangalia hakuna hata mgogoro mkubwa isipokuwa mgogoro wa maneno tu. Mgogoro siyo kuhusu Zanzibar kuwa nchi au si nchi bali ni kama Zanzibar is a Sovereign country or not. Jibu la Mahakama ya rufaa ni kuwa Zanzibar is not a sovereign state for sovereignty iko kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Hawa wakiendelea na huu mjadala kazi rahisi tuu kuwanyamazisha..wanyimeni fungu lao la mshiko pale BOT!!!
 
... kwa sababu huu mjadala unazungumzia kitu ambacho sicho. Ulipoanza niliwahi kuuliza swali hili: Je nchi yaweza kuwa Taifa bila mipaka? Na je Taifa laweza kuwa na serikali bila nchi (mipaka)? Je Ndani ya Nchi moja (ndani mipaka) kwaweza kuwemo mataifa mawili ambayo yana serikali zake (clue: Palestina na Israeli). Je serikali ni lazima iwe na nchi ili iwe serikali kamili (clue: States government)?

Sasa utaona watu wanapoangalia maneno ya nchi, serikali, taifa, na dola they are still missing the real thing they are trying to ask and which has been answered. Sovereignty. Majimbo ya Marekani yana sifa zote za kuwa nchi, mataifa, na serikali na dola, lakini hayana kitu kimoja nacho ni sovereignty.

So, kimsingi ukiangalia hakuna hata mgogoro mkubwa isipokuwa mgogoro wa maneno tu. Mgogoro siyo kuhusu Zanzibar kuwa nchi au si nchi bali ni kama Zanzibar is a Sovereign country or not. Jibu la Mahakama ya rufaa ni kuwa Zanzibar is not a sovereign state for sovereignty iko kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Perspicacious!
 
Unajua kwa sababu wanachogombania sasa wasipoangalia wanagombania sovereignty which means, Zanzibar inataka kuwa nje ya Jamhuri kwani haiwezi kuwa sovereign ndani ya nchi nyingine. What does sovereigny means though:

Wakati Majimbo ya Marekani yanatangaza uhuru wao toka Uingereza walisema wanafanya hivyo kama nchi huru na hivyo as " Free and Independent States, they have full Power to levy War, conclude Peace, contract Alliances, establish Commerce, and to do all other Acts and Things which Independent States may of right do."

Wasipoangalia watajikuta wanagombania "Uhuru wa Zanzibar" which is to declare themselves as sovereign kitu ambacho kitakuwa kimeuua muungano.
 
SIjui kama makala hii nayo imeshajidiliwa hapa.

Muungano: Dalili wazi za kuchokana zaonekana

Mwandishi Wetu Julai 23, 2008

MUUNGANO kati ya Tanganyika na Zanzibar sasa unayumba na unaashiria kuwapo kwa hatari dhahiri ya kuvunjika kutokana na pande zote mbili kuonekana kumchoka mwenzake, Raia Mwema imebaini.

Habari za ndani ya Serikali, Chama cha Mapinduzi (CCM) na ndani ya vyama vya upinzani zinaeleza kwamba sasa wanasiasa wamechokana na wameanza kutoa matamko ya waziwazi yanayoashiria hali hiyo.




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Kwa mujibu wa habari, kauli ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba Zanzibar si nchi si ngeni kutamkwa hadharani, lakini inaelekea imeibua mjadala kwa sasa kutokana na hali ya kuchokana inayozidi kukua kati ya pande mbili za Muungano, kila upande ukiona unaonewa.

Hata kauli ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) Juma Killimbah, ya wiki iliyopita ya kuishauri Serikali ya Muungano kuukana upande unaoonekana kutoridhika na hali ya muungano, ilifurahiwa na wabunge wa Bara lakini ikiwakera sana wa Visiwani, na wote hawakuficha hisia zao hizo.

"Ingekua wakati wa Mwalimu Julius Nyerere, Killimbah angeitwa na kutakiwa kujieleza lakini hali sasa ni tete mno katika suala la Muungano na sisi tunaona sasa kama wanataka kuondoka waondoke, tumechoka na malalamiko ya kila siku na kuendelea kuwabembeleza," Mbunge mmoja kutoka Kanda ya Ziwa aliliambia Raia Mwema wiki hii Dodoma.

Mbunge mwingine kutoka Zanzibar naye alielezea kusikitishwa kwake na kauli ya Killimbah, lakini alisema, "kauli hiyo ina ujumbe mzito kwa kuwa hajakemewa wala kutakiwa kufuta usemo wake bungeni, hali inayoashiria kwamba anaungwa mkono na wengi."

Akiuliza swali bungeni wiki iliyopita, Killimbah alisema suala la utata katika Muungano halikuanza jana au mwaka 2005, na kwamba Muungano ulikuwa ni maafikiano ya pande mbili kati ya Zanzibar na Tanganyika.

" Kwa kuwa, mara zote ndani ya Bunge hili tukufu na hasa katika kipindi hiki kumeonekana upande mmoja ukionekana kulalamika sana juu ya kwamba hautendewi haki na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Je, serikali sasa ipo tayari kuukana upande ambao unaonekana kwamba hauridhiki na yale inayoyafanya Serikali ili ikawapa elimu ya kutosha na wakaondoa manung'uniko yao? " alihoji Killimbah na kushangiliwa.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muhammed Seif Khatib, alisema Serikali haiwezi kuwakana kwa sababu wana haki ya kuzungumzia juu ya maslahi ya nchi yao.

Suala hilo liliibuka tena wiki hii kwa maswali mfululizo yanayoashiria kuyumba kwa muungano likiwamo la kuhusu nishati na madini baada ya baadhi ya wabunge kutaka kujua sababu za madini kutokuwa ya Muungano lakini mafuta ambayo yanatajwa kuweza kupatikana Zanzibar kuwekwa katika masuala ya Muungano.

Hoja ya mafuta inaelezwa kuweza kuwa kiini cha malumbano yanayoendelea ndani ya Muungano, jambo ambalo upande wa Zanzibar umekuwa ukilivalia njuga waziwazi, kupingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.




Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume

Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanasema tatizo kubwa kwa sasa linaweza kuwa kwa viongozi na wanasiasa zaidi ambao wanalihusisha suala la Muungano na madaraka waliyonayo sasa ama kwa malengo ya baadaye, akitajwa wazi wazi Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuwa mmoja wa wanasiasa wanaoogopewa kwa sasa.

Karume ameelezwa kuiyumbisha CCM na serikali zake kwa muda mrefu sasa na suala la mafuta na mazungumzo kati ya chama hicho na CUF yameelezwa kukigawa chama hicho pande mbili, ile ya Zanzibar na Bara na sasa inaelezwa kwamba upande wa Zanzibar umekuwa pamoja na upinzani katika suala la Muungano.

Hata hoja binafsi zilizozuiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, zimeelezwa kulenga kupanua ufa wa Muungano kama si kuuvunja kabisa, kabla ya kuchukuliwa hatua za dharura za kudhibiti hoja hizo, moja kutoka upinzani na ingine kutoka CCM.

Mmoja wa Wazanzibari ambaye amekuwa akizungumzia sana hoja ya nchi ya Zanzibar, Mohamed Raza, ameiambia Raia Mwema kwamba watu wote Zanzibar sasa haja yao ni kuwa na serikali tatu ndani ya Muungano ili hadhi ya nchi ya Zanzibar itambulike.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete

“Hali ya hewa si nzuri, inashinda hata ya mwaka 1984, Wazanzibari wote wameungana. Nakuambia hata ungeitisha uchaguzi kesho mwana CCM atapata taabu kupiga kwa CCM, itabidi afikirie mara 10.

“ Unasema Zanzibar si nchi, sasa huo Muungano Tanganyika iliingia na nani? Halafu mwaka 2010 watakuja kusema wanapiga kampeni kwa uchaguzi wa Rais, Rais wa nchi gani kama Zanzibar si nchi,” alihoji Raza.

Kwa mujibu wa Raza, salama ya Muungano katika mazingira ya leo ni kuwa na serikali tatu: ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano ili kila upande wa Muungano ujisikie vyema.

“ Kwanza mbona tayari kuna serikali tatu? Hayo yanayozungumzwa kuhusu kero za Muungano si sawa na kuweka serikali nyingine, mkizungmzia jinsi ya kuchangia kwenye Muungano si mnazungumzia Bara na Visiwani kuchangia Muungano,” alieleza Raza.

Lakini Raza, ambaye mara nyingi huzungumza kile ambacho viongozi wa Zanzibar wanakiamini lakini ambacho hawawezi kukisema wazi, alisema dawa ya malumbano ya Muungano ni kuwatumia wastaafu kutafuta muafaka.

“Tunao kina Mzee Kawawa (Rashidi) Mzee Mwinyi (Ali Hassan), Mzee Msekwa (Pius), Mzee Msuya, (Cleopa) Mzee Mkapa (Benjamin), Mzee Moyo (Nassoro), Mzee Salmin (Dk Salmin Amour) na kina Mzee Warioba (Joseph), hawa wanaweza kumaliza matatizo haya ya Muungano, wana hekima, hili si suala la kutuvunjia heshima ambayo tumeijenga,” alisema.


Source: Raia Mwema

Sasa hive nimeanza kuona kama vile Karume ana tamaa sana ya kuitawala Zanzibar maisha yake yote. Muungano ni kati ya vikwazo vya yeye kutimiza lengo hilo, ndiyo maana anatafuta kuigawa CCM kwanza halafu aondoke na kipande kimoja cha CCM kutoka kwenye Muungano.

Halafu huyu Raza siyo mara yake ya kwanza kutaka kuleta vurugu kwenye Muungano huu. Miaka ile ya themanini na tisini alidhibitiwa kweli kweli. Inaelekea wakati huu amepata watu wasioweza kumdhibiti kwa hiyo anawaendesha atakavyo. Ubishi wa kusema Zanzibar ni nchi au siyo nchi ni wa kijinga kweli kweli. Kama anazungumzia nchi kwa maana ya pande la ardhi, hiyo ni sawa, Zanzibar kama ilivyo Tabora ni pande la ardhi kwa hivyo ni nchi. Ila kama anazungumzia nchi kwa maana ya taifa au dola, basi hapo anakosea sana na hapo ndipo anapowachanganya wazenj. Sijui kama tuna sheria ya dhidi ya upindishaji makusudi wa katiba kwa manufaa ya mtu binafsi; inabidi bunge letu liifikirie, na adhabu yake iwe kali sana.
 
Last edited by a moderator:
Yote inaonesha udhaifu mkubwa wa Kikwete na wasaidizi wake kuweza kusimama na kuzungumza suala hili. Hili ndilo lililotokea Comoro kwa na namna fulani. Wakati Bakari anachezea muungano walimpuuzia hadi pale alipojitangaza kuwa ni nchi huru.

Karume anachezea hivyo hivyo, na kwa vile sasa hivi CUF na CCM zanzibar wanamsimamo mmoja siwezi kushangaa kama wakiamua kutangaza uhuru CCM na CUF watakuwa pamoja. Ni udhaifu mkubwa sana kwa Kikwete kama Rais wa Muungano.
 
Yote inaonesha udhaifu mkubwa wa Kikwete na wasaidizi wake kuweza kusimama na kuzungumza suala hili. Hili ndilo lililotokea Comoro kwa na namna fulani. Wakati Bakari anachezea muungano walimpuuzia hadi pale alipojitangaza kuwa ni nchi huru.

Karume anachezea hivyo hivyo, na kwa vile sasa hivi CUF na CCM zanzibar wanamsimamo mmoja siwezi kushangaa kama wakiamua kutangaza uhuru CCM na CUF watakuwa pamoja. Ni udhaifu mkubwa sana kwa Kikwete kama Rais wa Muungano.

Hiyo niliyowekea rangi ndiyo yenye uzito kabisa. Ninaloona hapa ni kwamba Karume anamdharau Kikwete. Halafu Kikwete mwenyewe anajua hilo ila analinyamazia badala ya kuonyesha kuwa yeye ndiye bosi. Ndiyo maana amehsindwa kusimamia mazungumzo ya mwafaka kama alivyokuwa ameahidi. Aliwaza kusimamia ya kenya lakini siyo ya Zanzibar.
 
Unajua kwa sababu wanachogombania sasa wasipoangalia wanagombania sovereignty which means, Zanzibar inataka kuwa nje ya Jamhuri kwani haiwezi kuwa sovereign ndani ya nchi nyingine. What does sovereigny means though:

Wakati Majimbo ya Marekani yanatangaza uhuru wao toka Uingereza walisema wanafanya hivyo kama nchi huru na hivyo as " Free and Independent States, they have full Power to levy War, conclude Peace, contract Alliances, establish Commerce, and to do all other Acts and Things which Independent States may of right do."

Wasipoangalia watajikuta wanagombania "Uhuru wa Zanzibar" which is to declare themselves as sovereign kitu ambacho kitakuwa kimeuua muungano.

Lakini unajua nini, I don't blame them.

Simlaumu mtu yeyote asiyeelewa, au anaejikuta anasema vitu vinavyodhoofisha Muungano. Kwa sababu siku zote tulikuwa tumefungwa mdomo kuhusu details zake.

Sitaki kiubua mengine hapa, Mwkjj, lakini inawezekana tatizo lilikuwa kwa waasisi wetu. Watu walioomba details za hivi vitu toka zamani walifungwa. Wa kina Maalim Seif, na kina Jumbe kufukuzwa kazi. Hizi details zilikuwa zinaitwa "nyaraka." Nilikuwa katoto ka shule wakati ule tunasikia Jumbe kawa fired, halafu baadae Seif kakamatwa na "nyaraka." Scary word! Come to find out the word means nothing but "document," a "letter."

Ninaposema sitaki kuibua mengine Mwnkjj unanielewa, and I really mean it, kwamba sitaki kuwalaumu moja kwa moja hawa Waasisi kwa sababu inawezekana wakati ule wa "ka nchi kachanga," kama mmoja wao alivyokuwa anapenda kukaita, inawezekana ile ficha ficha na kamata kamata ilikuwa ndio njia walioijua kutuepusha na yaliyowakuta wenzetu wengi miaka ile baada ya Uhuru. Kwa hiyo nawapa benefit of the doubt kubwa wale waasisi. Walivyofanya labda ilikuwa ni baraka, lakini vinaelezea kwa nini hivi vitu vinakuja ku unravel leo.

Martin King alisema "ukweli unaofukiwa ardhini utachipuka tena." Huwezi kuuzika. Sasa utawandawazi umekuja, watu wa Baraza la Wawakilishi wanajisikia huru kurusha maneno across the sea, Pinda usituyeyushe. Pinda mlaumu kwa gaffes zake za kila leo, lakini hapa alikuwa right on the money. Kakitoa right out of the Katiba, Ibara ya Kwanza: "Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano." Kwa sababu hii mijadala ilipigwa marufuku, watu hawakuwahi kuvisikia hadharani vitu alivyosema Pinda Bungeni. Kama unavyomjua Pinda tena, "anawesha" kama anavyojua yeye. Watu wanashtuka, wanawaka. Can't blame them.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ashawahi kushuhudia mbele ya Mahakama kwamba hajawahi kuuona mkataba wa Muungano. Inasemekana haupo. Lakini tunajua ulikuwepo. Kuna picha moja black and white inaonyesha Wakuu wanasaini Muungano. Lakini ukiuliza nakala zimeenda wapi, Haini! Jamani, labda mmoja ya kwake ilipotea baharini akiwa njiani kurudi kwao. Haya nakala ya huyo mwingine iko wapi, Haini! Jamani, wote walipewa copy? Haini! Nimemuua nani, umeulizia "nyaraka"!

Can't blame the masses here.

Details za Muungano zilifichwa.
 
Kuhani, nyaraka za Muungano zipo na zinajulikana (ukisoma ile hukumu ya Mahakama ya Rufaa wana nukuu toka humo kwa urahisi tu). Si kweli kwamba nyaraka hazikupatikana ila ugumu wa kupatikana kwa watu wa kawaida. Wasomi walikuwa nazo na wengine wanazo. Tatizo ambalo naliona hata leo hii ni kuwa pamoja na kisingizio cha zamani cha usalama, teknolojia n.k sijaona sababu kwanini kwa mfano:

a. Hadi leo hii kwa upande wangu sijaiona Katiba ya Zanzibar online!
b. Articles za Muungano zipo hata hapa JF (you need to search for a liitle bit) lakini nani anaweza kuwa nazo kule kijijini?
 
Mimi nadhani, ule mkutano wa CCM wa kujadili ripoti ya muafaka wa CCM na CUF ndo ulitia chumvi katika kidonda hiki cha mapungufu ya muungano,watu nadhani waliondoka na vinyongo pale, wakajipanga kutetemeshana, bahati mbaya sasa wanatetemeshana katika "a very sensitive issue" ya muungano.it is so pity
 
Unajua tumechoshwa kweli na haya ya muungano nonesense, hivi hawa watu watachoka lini na huu ujinga wa muungano na kuhamia makao makuu Dodoma,

Yaani mimi I am sick na hivi vitu viwili ambavyo kwa kweli ni waste of time and money kwa taifa letu!
 
Unajua tumechoshwa kweli na haya ya muungano nonesense, hivi hawa watu watachoka lini na huu ujinga wa muungano na kuhamia makao makuu Dodoma,

Yaani mimi I am sick na hivi vitu viwili ambavyo kwa kweli ni waste of time and money kwa taifa letu!

Spot on! Kama namna gani vp tuitishe referendum nchi nzima tujue moja mbivu au mbichi
 
Ninavyomwona Shamhuna anafanya kazi ya kupunguza nguvu na ushawishi wa Maalim Seif kwa kusema exactly kile ambacho Seif anataka kukipandia na kujiongezea UMAARUFU feki kwa Wazanzibari wa kawaida. Hili linafanyika sana hata huku bara kwa kuwatangulia akina Mh. Zito, Dr. Slaa, Mh.Mbowe,...
 
Kama Znz ni nchi basi wale waliokuwa kwenye ile kesi ya uhaini hawana budi kurejeshwa jela.

Kwa nini kipindi kile walikubaliana na hukumu kuwa znz sio nchi na sasa hao hao ndio wapo mstari wa mbele kusema kuwa ni nchi ?
 
Huu muungano katika mfumo wake, ni moja ya matatizo tuliyorithishwa na Nyerere pasipo ridhaa yetu.
 
Yaani zanzibar mawaziri kama wabunge vile,yaani nao huuliza au kuunga mkono hoja badala ya wao kuwa ndio wenye majibu. Hivi hukumu mbili za mahakama kuhusu suala hilo hawajaziona bado?
Yaone tu wewe Bw. Augustoons. Hizo ndio, (kasheshe za watu kama kina Shamhuna (the opportunist). Hajitambui - ni nini role yake- kama Naibu Waziri Kiongozi. Vikao vya Wakubwa si vipo (SMZ na SMT) ? Ya nini yeye kuuunga msururu wa wawakilishi na wabunge wa kawaida kukurupuka kulisemea hilo, kama si kufukuzia umaarufu kwa wananchi (wapiga kura)?
 
Back
Top Bottom