Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Vijana!
Swala hili la Zanzibar linataka turudi nyuma na kuangalia mfumo wa utawala mara tu baada ya kuundwa Tanzania. Tunaye mkongwe wetu wa siasa Mzee Kawawa ambaye bado yuko hai. Tatizo la sasa hivi ni kwamba Tanzania ina ma-rais wawili, rais Kikwete na rais Karume. Zanzibar ina mawaziri wake na wao sio manaibu-mawaziri wa muungano.
Serikali yetu ya muungano ilitakiwa kuwa na rais Kikwete, makamo wa kwanza wa rsis(First Vixe President) Karume na makamo wa pili wa rais(Second Vice President) Shein.
Kama sikosei serikali ya kwanza ya muungano ilikuwa na rais Mzee J.K.Nyerere, makamo wa kawnza wa rais Mzee Karume na makamo wa pili wa rais Mzee Kawawa.

Mgogoro huu tuutatuwe ili watoto wetu na wajukuu wetu hapo mbeleni wasipate taabu.
Kama itabidi kuuvunja muungano kwa manufaa ya watanganyika na wazanizibari basi tufanye hivyo sasa hivi kuliko kila siku kusogeza mbele maswala ya mgogoro huu.
 
Inashangaza kuona leo mtu akurupuke na atamke kuwa Zanzibar si nchi wakati Zanzibar ilikuwa nchi kabla hata Tanganyika haaijazaliwa. Hali hii sio tu inaonyesha kwa mtu kutoijua historia ya nchi yake mwenyewe, bali wakati huo huo inadhihirika kutoijua kabisa historia ya na umuhimu wa nchi ya Zanzibar katika Afrika ya Mashariki. Hali hii inathibitisha kibri kinachotokana na ukosefu wa kujua na kuheshimu mambo. Wale ndugu zetu wa Tanganyika wanaosisitiza kuwa Zanzibar si nchi wamegeuka kama matarumbeta yanayopulizwa tu na kutoa sauti na pale yanapowekwa chini sio tu hayatoi sauti bali hata kujikuna hayawezi. Uongozi wa juu wa nchi sio jambo la maskhara, kuwa na kibri peke yake hakutoshi. Kunґganґgania kutaka kuimeza Zanzibar kumewafanya ndugu zetu kujitokeza katika ngozi zao sahihi na kutupilia mbali ngozi za kondoo. Hali imebainisha kwa wengi wale waliokuwa hawajui nia ya Muungano kuamka na kujua kwamba njama za Muungano hazikuwa za kuimarisha udugu na umoja wa Bara la Afrika, bali ulikuwa na njama za kikoloni za mkubwa kuitawala na kumkandamiza mdogo.
 
Hata kura ya maoni haihitajiki ni WaZanzibari kuamua tu kama hawakuamua wao basi WaTanganyika na wao wanaweza wakaamka wakasema Muungano hatuutaki tugawane mbao.
 
Vijana!
Swala hili la Zanzibar linataka turudi nyuma na kuangalia mfumo wa utawala mara tu baada ya kuundwa Tanzania. Tunaye mkongwe wetu wa siasa Mzee Kawawa ambaye bado yuko hai. Tatizo la sasa hivi ni kwamba Tanzania ina ma-rais wawili, rais Kikwete na rais Karume. Zanzibar ina mawaziri wake na wao sio manaibu-mawaziri wa muungano.
Serikali yetu ya muungano ilitakiwa kuwa na rais Kikwete, makamo wa kwanza wa rsis(First Vixe President) Karume na makamo wa pili wa rais(Second Vice President) Shein.
Kama sikosei serikali ya kwanza ya muungano ilikuwa na rais Mzee J.K.Nyerere, makamo wa kawnza wa rais Mzee Karume na makamo wa pili wa rais Mzee Kawawa.

Mgogoro huu tuutatuwe ili watoto wetu na wajukuu wetu hapo mbeleni wasipate taabu.
Kama itabidi kuuvunja muungano kwa manufaa ya watanganyika na wazanizibari basi tufanye hivyo sasa hivi kuliko kila siku kusogeza mbele maswala ya mgogoro huu.


Wewe unataka kumuuliza Kawawa wakati Kawawa is part of the problem?

Kawawa huyu huyu aliyeitwa mjinga na rafiki yake Nyerere? But then again jitu linakupa nchi halafu unalishikia, lnaenda kufanya kazi za chama, linarudi, linakwambia nirudishie nchi yangu na wewe unalirudishia hii hapa bwana mkubwa, kwa nini lisikuone mjinga?

Huyu Kawawa aliyesaidia mafisadi kufilisi benki zetu kwa kutoa pressure benki zilizokopesha maswahiba wake ziiandike mikopo hiyo kama "bad debts"?

Kawawa huyu huyu, au mwingine?
 
Iweje leo nch na dola linalotegemea misaada ya kutoka nje kwa asili mia 40-60%, lisiloweza kujimudu wenyewe litake kuitawala nchi nyengine, wakati nchi na dola lenyewe likichechemea. Kibri hichi kinatoka wapi, kwa tafsiri yangu , hakitoki kwengine ila ni kutokana na upungufu taaluma wa mambo na kutojuwa hasa nini kiini na makusudi ya Muungano au labda kuficha siri zenyewe. Ndugu zetu wengine wanajiona kama wao ni watawala na Wazanzibari kwao kuwa visonoko, hawa wanakereketesha roho. Inafaa mtu akarejea kitabu cha Amrit Wilson apate undani na makusudi ya Muungano kabla mtu hajajitutumua na kujiona bora kushinda Mzazibari
 
Inafaa ndugu zetu wanao nґganґgania kuwa Zanzibar si nchi wauchunguze kikamilifu uundaji wa Muungano kabla kukurupuka na kujitolea matamshi yasiyo na kina wala ukweli. Kwa ufupi njama za kuunda Muungano zote zina manukato ya kiharamia, tokea Alif mpaka wasalaam. Ilikuwaje kitu cha kheri na baraka kifichwe na kufanywa chini kwa chini na wajuao wa awali wawe ni watu wachache waliokaribu na kuaminiwa na Mw.Nyerere ambao wakati huo huo wawe ni wanasheria wa serikali ya Tanganyika, wakati sio tu wanasiasa wa Zanzibar kwa jumla walikuwa hawajui kitu kuhusu makusudi ya kuunda Muungano bali hata wanasheria wa Zanzibar walikuwa hawajui wala hawakushirikishwa katika maandishi, kuithamini au kuipitisha Katiba ya Muungano. Vipi Mw. Nyerere atamchukua Mzee Karume ambae hana ujuzi wa kisheria awe ndie muasisi wa Katiba hiyo bila ya Mzee huyo kuwa na utaalamu na msaada wa kisheria au wa kisiasa na kutoruhusiwa hata kuwa na wanasiasa wenziwe na wanasheria wa kumnasihi na kumtanabahisha na kumpa maarifa ya kisiasa na kisheria kuhusu jambo hilo muhimu sana kwa nchi mbili. Mzee Karume alitishwa na kudanganywa na kwa vile alikuwa anamuamini Mw. Nyerere kama kipofu kwa imani yake njema, hakuona wala kutarajia mitego aliyowekewa yeye na Wazanzibari kwa jumla. Alipokuja kutanabahi mambo yalikwisha fika kooni, hakutokeki-hakuingiliki na ndio maana siku zake za Mwisho Mzee Karume akaanza kufanya mikiki ya kutaka kujipapatua kujitoa katika Mungano.
 
Mengi sana yameandikwa kuhusu uharamia wa Katiba ya Muungano na lengo la azma ya kuyanyakuwa madaraka ya Zanzibar. Ni bahati njema kwamba sasa Wazanzibari karibu wote wameanza kuyatamka hadharani yale waliokuwa siku zote wakiyashuku na kutanabahi azma mbaya na potofu ya wale ambao wakiwaona kama ni ndugu zao. Kuna mengi ambayo Mzee Karume aliyashitukia kuhusu uundaji na lengo la Muungano, ambayo hayana kasoro ya zaidi ya kutaka kuimeza Zanzibar. Itakumbukwa jinsi Mzee Karume alipokasirishwa kwa kupitia nje ya Katiba ya Muungano, na bila ya yeye kama Makamo wa Rais wa Muungano kujulishwa, kwa kuanzishwa kwa cheo cha kuweko Waziri Mkuu ambae kwa wakati huo huo -waziri Mkuu huyo alikuwa atoke Tanganyika. Kutojulishwa, kutoshauria na kupuuzwa kwa Mzee Karume kama Makamo wa Rais na muasis wa Muungano, kulimkasirisha sana na kuzidi kumtambulisha amza halisi za Muungano. Hapo Mzee Karume alijuta kutolisikiliza Baraza la Mapanduzi na mawaidha ya wanasheria walioweka maslahi ya Zanzibar mbele. Alijuta kutolishirikisha Baraza la Mapinduzi katika kulizungumza, kulichambua na kuli- au kutolipitisha suala la Katiba ya Muungano katika Baraza. Alijuta kwa nini asiwashirikishe Wazanzibari katika uamuzi wa kujitia au kujitoa katika Muungano. Hasira zake hatimae zilimpelekea kutaka kufanya mengi, mengine ya siri na mengine ya dhahiri (soma Zanzibar Dola, Taifa na Nchi Huru). Katika jambo moja wapo la dhahiri Mzee Karume alitaka kufanya ni kuishitaki Serikali ya Muungano (yaani Mw. Nyerere) kwa kwenda kinyume na Katiba ya Muungano kwa kuanzisha Cheo cha Waziri Mkuu wa Serikali kinyume/dhidi hata na hiyo Katiba ya mabugumunya, isiyopitishwa si na serikali ya au watu wa Zanzibar. Hayo kwa bahati mbaya Mzee Karume, hakuwahi kuyatekeleza, yaliyomfika tunayajua.

Hicho ni kipengele kimoja tu muhimu kinachodhihirisha upotofu na upungufu wa heshima ya Zanzibar katika Katiba ya Muungano, mengi ya kificho na ya jua kali yamepenyezwa katika Katiba hiyo kwa namna hii au nyengine ndani au nje ya Katiba ya Muungano katika njama na makusudi ya kuipora Zanzibar madaraka na ujana-nchi wake............
 
"Kwa mujib wa historia ya kale ya enzi zetu, kuambatana na maandishi ya 'Perpulus of the Erythrean Sea, Claudiius Ptolemy, Edris, Chronicles of Kilwa n.k., Zanzibar (Menouthias Island) ikijulikana kama nchi iliyokuwa ikitambilika na kufanya biashara na mashariki ya kati, mashariki ya mbali zikiwemo Barahindi, uchina na Japan, pamoja na nchi kubwa kama Marekani tokea enzi za kale. Katika maandishi hayo ambayo ni kati ya maandishi ya zamani kabisa kuhusu Afrika ya Mashariki hakukutajwa nchi au taifa lilojulikana kama Tanganyika. Hadi April 28, mwaka 1885 ndio tarehe ambayo serikali ya Kijerumani ilipoamua kuzinyakua maili 60,000 za eneo la Mrima, baada ya hapo ndipo makubaliano baina ya Mngereza na Mjerumani yakafikiwa, Mngereza ikachukuwa Hegolanda kama kiunua mgongo na Mjerumani kuchua eneo la Mrima.
Unyakuaji wa Wazungu wa Bara la Afrika, ulitokea hususan baada ya Mfalme wa Ubeligiji kuitisha mkutano wa nchi zilizokuwa zikiongoza Ulaya, katika mwaka 1876, huko Brussels, Ubelgiji. Kama tunavyoona muda mrefu kabla ya hapo Zanziba tayari ilijulikana kama ni nchi wakati Tanganyika kama nchi ilikuwa bado haijazaliwa".
 
I hold no grudge against useful boldness and when it comes to writing,hell yeah we need some...just got to be useful.

You think?

I don't think so, I know so with conviction.
 
Well with this style of writing,count me out.
I'll take the message and go 'dementic' on the presentation mechanism.

I expressed my reservations about his style of writing, even wrote him.

Believe me, this is a significantly toned down version from what he had earlier on, complete with profanities like "shyt" and all. When I tell you he must be smoking or drinking something while writing I mean that.

But they say the end justifies the mean, kama inabidi kupata suba la moto na kutukana ili kufikisha ujumbe so be it, we are not in a Soviet.
 
Wazanzibari wazidi kuwaka


Na Salma Said, Zanzibar


," alisema ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi, Mzee Salim Rashid, amesema kauli ya Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna, kwamba Zanzibar ni nchi ni msimamo wa Wazanzibari wote.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Mtaa wa Vuga, Mkoa wa Mjini Magharibi, Mzee Rashid alisema, yaliyosemwa na wawakilishi na Shamhuna sio maneno yao binafsi, bali ni msimamo wa Wazanzibari kwa ujumla wao.
�Hili sio suala la Shamhuna au Serikali, ni suala la Wazanzibari wote na wawakilishi wanaosemea hilo kwenye Baraza la Wawakilishi wanawakilisha maoni ya wananchi, kwa hiyo Shamhuna hakukosea wala sio maneno yake ni maneno ya Wazanzibari wote,� alisema Mzee Rashid ambaye ana uzoefu mkubwa wa uongozi katika siasa za Tanzania.
Alisema, ipo haja ya mjadala huo kuachwa ukazungumzwa kwa upana wake badala ya kuamuliwa kwa mabavu kama ilivyofanywa awali na kuleta athari kubwa katika siasa za Tanzania.
Mzee aliwaonya wanaojaribu kuzima mjadala huo kufahamu kwamba, suala hilo ni zito na haliwezi kumalizwa kwa wepesi kwa kuwa hivi sasa, Wazanzibari wanalizungumzia na wana hamu ya kutaka kusikia kauli nzito inayotoka kwa viongozi wakuu juu ya ufumbuzi wake.
Kuhusu suala hilo kutolewa uamuzi na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Rashid alisema si sahihi kwa kuwa maamuzi yatakuwa ni ya CCM na si ya kikatiba. Alimsifu Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kuibua suala hilo sasa ambapo Wazanzibari wana hamu ya kuunganishwa.
�Jambo hili ni historia kubwa. Pinda kaondoa fitina kwani kwa zaidi ya miaka 50 Wazanzibari walikuwa wanahitaji kuunganishwa isiwezekane, lakini hili sasa limewaunganisha, Alhamdulilah,� alishukuru Mzee huyo.
Alisema Muungano si suala la CCM peke yao, bali wananchi wote wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo suala hilo haliwezi kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia Katiba ya Muungano kwa sababu lilitengenezwa katika maamuzi ya kisiasa.
Kwa mujibu wa Mzee Rashid kinachoweza kutumika kulipatia ufumbuzi suala hilo ni Hati ya Makubaliano ya Muungano badala ya Katiba ya Muungano.
Alishauri kwamba, endapo kuna haja ya kutumia sheria na Katiba katika kulitafutia ufumbuzi suala hilo, mahala panapopaswa kupelekwa suala hilo ni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (International Court Of Justice, The Hague) kwa sababu zilizoungana zilikuwa nchi mbili hivyo ni suala la kimataifa.
Akizungumzia maoni ya hivi karibuni yaliyotolewa na mwanasiasa mwenzake, Peter Kisumo, kuhusu Zanzibar, alisema Kisumo ameonyesha dharau kwa Zanzibar, kwani hakupaswa kulinganisha timu ya mpira na Zanzibar ambayo ni nchi.
�Ni dharau kubwa sana ameonyesha Kisumo kwa nchi yetu na pia amemdhalilisha hata Rais Karume, huwezi kufananisha timu ya mpira na Zanzibar, wala huwezi kufananisha wimbo wa taifa na kwaya. Si vizuri kabisa, amekosea na ni maneno ya ... si
maneno ya akiliMzee Rashid na akaongeza:
"Mimi Kisumo ni rafiki yangu kipenzi namualika awe mgeni wangu
aje Zanzibar kusikiliza maoni ya Wazanzibari juu ya suala hili linavyoendelea, hapo ndio atajua kinachoendelea hapa visiwani."
Alisema kauli ya Kisumo imetolewa kana kwamba anahutubia mkutano wa TANU Biharamulo, kwamba kinachosemwa hicho ndicho kinachotendeka, lakini wakati huu ni mwingine na mfumo wa vyama vingi ndio unaochukua nafasi ya demokrasia.
�Wapo wanaojisahau wakadhani bado kuna chama kimoja, Kisumo hana uzoefu wala ujuzi wa kuzungumzia mambo ya kimataifa au kitaifa ... maneno yake ni kama anahutubia mkutano wa TANU chini ya mfumo wa chama kimoja,� alisema na akaongeza:
�Mimi siamini kama mjadala huu unaweza kumalizwa kwa CCM kutoa tamko au kukataza viongozi wasizungumze, hapana babu, huu mjadala uendelee, wao wanadhani chama kikisema Zanzibar si nchi ndio mambo yatakwisha?�
Akizungumzia kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro, mwanasiasa huyo mkongwe alisema hana mamlaka yoyote ya Umoja huo, hivyo kauli yake haina uzito unaostahili, kwani alipaswa kuutaka mjadala huu uendelee na si kunyamazishwa na kukumbusha kwamba, Umoja wa Mataifa haujafuta kiti cha Zanzibar, kwani hakuna maombi ya Zanzibar wala Tanzania juu ya kufutwa kwa kiti hicho.
Alishauri kuitishwa kura za maoni kuhusu suala hilo na kwamba hata kama watakaoulizwa na wanaCCM wawe Wazanzibari na Wabara ili kupata uwiano wa maoni kabla ya kuamua kulipeleka suala hilo Mahakama ya Kimataifa ikitokea kura zinawiana.
Mzee Salim Rashid, ambaye amepata misukosuko kadhaa kwa kutetea masilahi ya Zanzibar, alikuwa ni Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi baada ya Zanzibar kupata uhuru, aliwahi pia kuwa Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Muungano, balozi wa nchi mbalimbali ambaye hadi kustaafu kwake mwaka 1972 alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia
 
Inashangaza kuona leo mtu akurupuke na atamke kuwa Zanzibar si nchi wakati Zanzibar ilikuwa nchi kabla hata Tanganyika haaijazaliwa. Hali hii sio tu inaonyesha kwa mtu kutoijua historia ya nchi yake mwenyewe, bali wakati huo huo inadhihirika kutoijua kabisa historia ya na umuhimu wa nchi ya Zanzibar katika Afrika ya Mashariki. Hali hii inathibitisha kibri kinachotokana na ukosefu wa kujua na kuheshimu mambo. Wale ndugu zetu wa Tanganyika wanaosisitiza kuwa Zanzibar si nchi wamegeuka kama matarumbeta yanayopulizwa tu na kutoa sauti na pale yanapowekwa chini sio tu hayatoi sauti bali hata kujikuna hayawezi. Uongozi wa juu wa nchi sio jambo la maskhara, kuwa na kibri peke yake hakutoshi. Kunґganґgania kutaka kuimeza Zanzibar kumewafanya ndugu zetu kujitokeza katika ngozi zao sahihi na kutupilia mbali ngozi za kondoo. Hali imebainisha kwa wengi wale waliokuwa hawajui nia ya Muungano kuamka na kujua kwamba njama za Muungano hazikuwa za kuimarisha udugu na umoja wa Bara la Afrika, bali ulikuwa na njama za kikoloni za mkubwa kuitawala na kumkandamiza mdogo.
Bwana mwiba kumbe una mambo wakati mwengine . Kama haya ni ya kweli. Hee usinchekshe!!!!!.
 
Hata kura ya maoni haihitajiki ni WaZanzibari kuamua tu kama hawakuamua wao basi WaTanganyika na wao wanaweza wakaamka wakasema Muungano hatuutaki tugawane mbao.


I think this is the beginning of the end of muungano (forced marriage),why did it take so long!!
 
Mbona mpaka hapa sijasikia kauli ya kiongozi wa nchi yenu yule anaitwa Dr nani vile? Yeye kakaa kimya sasa wanaosema ni loud speaker yake?
 
Tatizo ni kwamba kuna utata wana maana gani wanaposema nchi? kuna state, nation, country halafu kuna swala zima la sovereignty.

Sasa mbona wanapayuka tu nchi nchi, ukifuatisha vizuri kiswahili hata unyanyembe au umasai ni nchi, kwa maana ya "an expanse of land". Watuambie wanasema nchi katika context gani?

Je Zanzibar inaweza ku sign mikataba ya kimataifa? Je Zanzibar ina sovereignty?
 
Jamani tuna watu wamesoma sheria na wanajua kutafisri, hivi ili nchi iitwe nchi inatakiwa kuwa na vitu gani, au na kigoma nao waseme kuwa nao ni nchi na kagera nao wasemem nao ni nchi kwa kuwa nao wana viongozi wao ambao hawatambuliki nje ya nchi kama raisi wa zanzibar.
 
Zanzibar kwa sasa wanataka kuwa sovereign state, jambo ambalo haliweaekani bila kuivunja serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachoinguzwa hapa kwa mlango wa nyuma ni kuvunjwa kwa muungano na sijingine. Ni wazi wakisema hivyo kwa uwazi watashtakiwa kuwa ni wahaini!!! Moto unaowaka Zanzibar sasa hivi ni mkubwa kuliko unavyoongelewa. It is just a tip of the iceberg. Hoja hii itakapokamilika itafuata uhalali wa uwepo wa baraza la Mapinduzi katika mazingira ya demokrasia ya vyama vingi. Viongozi wakuu kama huyo katibu wa kwanza wa BM ajue anaingia kwenye boti bila kujua liendako!!!
Itakuwa jambo jema sasa tuweze kujiuliza umuhimu wa muungano katika mazingira tuliyonayo sasa. Labda kulikuwa na sababu za msingi na dharura zilizoharakisha kuundwa kwa muungao wakati ule, je bado zinaprevail? Tusione ajabu au aibu kuuvunja muungano wetu, kwani hatutakuwa wa kwanza. Pengine kuvunjika huko kutatufanya tuwe karibu zaidi kama ilivyo Czch republic na wenzao Slovakia.
 
Back
Top Bottom