Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Moja ya malalamiko juu ya mfumo wa muungano wetu ni kumnyima madaraka Raisi wa Zanzibar - ambae kwa wengi wanamuona kama Maya tu wa Mkoa wa Zanzibar.

Hebu naomba tukae na tulichambue hili hapa:

Mfano "Kama Raisi wa Zanzibar angalikua na madaraka au katika mfumo huu wa Muungano ambao tunaendeleya nawo hivisasa - CUF wameipata au wameshinda uchaguzi - hii itamfanya aingie moja kwa moja ndani ya Baraza la Mawaziri kama Raisi wa Zanzibar na kushika madaraka yake yote; huku ikiwa Serikali ya Muungano imetengenezwa na CCM!"

Baraza zima la Mawaziri litakua limetengenezwa na CCM kasoro nafasi moja tu ambayo ni ya Raisi wa Zanzibar itakua imejazwa na CUF(Mfano) - hili sio jinamizi kwa wana Muungano na CCM kwakweli?

Naomba hoja zenu!
 
Kumbe huko anakotawala hakutoshi mnataka aje kutawala na bara? Si agombee tu awe rais wa Tanzania.
 
CUF wakishinda uchaguzi, halafu CCM wakashinda idadi kubwa zaidi ya wabunge, basi Rais wa Jamhuri kutoka CUF ataeua Waziri Mkuu kutoka CCM, kwa mujibu wa katiba, lakini mawaziri wangine, Katiba haisemi kwamba ni lazima watoke CCM. Kwa hiyo Rais wa CUF anaweza kuteua baraza lenye mchanganyiko. Ibara 55 (1)
 
Tatizo ni kwamba kuna utata wana maana gani wanaposema nchi? kuna state, nation, country halafu kuna swala zima la sovereignty.

Sasa mbona wanapayuka tu nchi nchi, ukifuatisha vizuri kiswahili hata unyanyembe au umasai ni nchi, kwa maana ya "an expanse of land". Watuambie wanasema nchi katika context gani?
Je Zanzibar inaweza ku sign mikataba ya kimataifa? Je Zanzibar ina sovereignty?
Bora ukamuulize Pinda aliposema Zanzibar si nchi alikusudia nini ? Ila anapata majibu kwa kila mmoja alivyofahamu ,yaani umeoa halafu mke wako anakwambia wewe si mwanamme ? Mkuu Pundit utajionaje ?
 
MUUNGANO tokea mwanzo ulikuwa ni wa kifisadi. Nyerere alimtapeli Karume na Wazanzibari na akaandika huo mkataba uitwao wa Muungano. Hakuna nchi hata moja iliyounganishwa kwa haki na nchi nyengine kwa hadaa kama za Nyerere. Lililobaki ni kwa Zanzibar kudai uhuru kutoka kwa Tanganyika iliyojibatiza jina la Tanzania. Baadaye ni kuishi kwa ujirani mwema kama mataifa huru. Itakuwa ni kosa kubwa kwa Zanzibar baada ya kuwa victimized na Tanganyika kwa miaka zaidi ya 40 irudi tena kujiunga na Mafisadi. Muungwana haumwi na nyoka mara mbili.
 
Pengo: Watanzania acheni kuchokonoa Muungano

Na Yusuph Mussa, Korogwe

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, amewataka Watanzania waache kuuchokonoa Muungano kwa kuhoji kama Zanzibar ni nchi ama la.

Alisema hayo Jumatano iliyopita wakati akizungumza na Jumuiya ya Chuo cha Tanzania College of Early Education, iliyo chini ya taasisi ya ROME mjini Korogwe,na ni sehemu ya Kanisa Katoliki alipofika kukagua shughuli za maendeleo.

Askofu Mkuu Pengo alisema kuanza kuhoji kuwa Zanzibar ni nchi ama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni dalili tosha za kuanza kuuchokonoa Muungano, jambo ambalo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere hakupenda lijadiliwe.

Wazanzibari waambiwa: Jihadharini na Pengo
WAZANZIBAR wametakiwa wachukue hadhari dhidi ya majaribio ya kutaka kuwaingiza katika balaa sambamba wakiitafakari kwa makini kauli ya Kardinali Pengo.
Aidha wametakiwa kuelewa historia ya kanisa Katoliki kuwa halijakuwa na rekodi nzuri hasa katika ukanda wa maziwa makuu pale linapojitumbukiza katika siasa.
Hayo yameelezwa na Wananchi kadhaa walioongea na gazeti hili mjini Zanzibar kufuatia kauli ya Kardinali huyo juu ya siasa za Zanzibar.
"Huko Rwanda Maaskofu wamelaumiwa kushiriki katika mauaji ya halaiki ya Wanyarwanda, huko Burundi pia wanalaumiwa, tunapowasikia leo wakizungumzia siasa zetu lazima tuhofu balaa zao, alisema bwana Hassan Mazrui.

Kama ni kuitakia mema Zanzibar, haiwezi kuwa nia ya askofu alisema bw. Mazrui
Alieleza kuwa chama tawala CCM kimejiwekea tabia ya kusimamia mabadiliko ambapo moja ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kuingilia makubaliano ya Muungano. Mabadiliko ambayo yalimuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais.
"Kanisa katoliki lilikuwa wapi kukemea mabadiliko hayo yaliyovunja makubaliano ya muungano", alihoji bwana huyo.
Aidha amesema Nyerere alikaa zaidi ya miaka 20 akibadili mambo apendavyo mara kofia mbili mtu mmoja mara kofia moja tena kofia mbili, "Mbona hakuna askofu aliyehoji na kumwambia kakaa sana. Hiyo Demokrasia wameijua lini? Alihoji

Mama mmoja Safia Shaame aliyedai ni mwana CCM alisema Pengo na kanisa lake hawezi kudai anawatakia mema Wazanzibar.
Alisema muungano 1964 ulikuwa wa Mambo11 Serikali za Tanganyika na Zanzibar zilibaki na wizara zao na mambo mengine ila 11 tu ndiyo wakakubaliana yawe ya Muungano.
Ina maana kama ni Wizara 11 ndio zingekuwa za Muungano. Lakini wizara zote na watumishi wote wa serikali ya Tanganyika wakapandishwa daraja na kuwa wa Serikali ya Muungano ya Tanzania.
Matokeo yake anasema Wizara ya Maendeleo ya Jamii wanawake na watoto Tanzania ni ya muungano wakati ya Zanzibar sio ya muungano na misaada ikija inaishia kwa Marry Nagu. Hali ni hiyo hiyo kwa Wizara za kilimo, Elimu na nyinginezo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Abanwa na kumbid kuitisha kikao cha Dharura.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho ameitisha kikao cha dharura kwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la hilo kwa lengo la kuandaa utaratibu wa kuiwasilisha ndani ya baraza hilo hoja iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba Zanzibar sio nchi Juni 26 mwaka huu.
Uamuzi huo wa Spika umekuja kutokana na wajumbe wa baraza hilo kujadili mara kwa mara suala hilo huku wengine wakichukua jazba wakitaka waachiwe kuujadili kwa upana.
Sehemu kubwa ya wajumbe wa baraza hilo wakati wakichangia mjadala huo walimtaka Spika Kificho kuwaruhusu kujadili suala hilo kutokana na kuongezeka kwa matamshi ya Zanzibar sio nchi kutoka upande wa Tanzania Bara huku baadhi ya viongozi wa Tanzania Bara wakitoa vitisho vya viongozi wa Zanzibar.
Wajumbe wengi walimtupia lawama Spika kwamba lazima aruhusu suala hilo lijadiliwe na wajumbe hao kwa kwa vile wao ndio wawakilishi wa wananchi katika majimbo 50 yaliopo ndani ya baraza hilo pamoja na wajumbe wa kuteuliwa.
Wajumbe hao walimueleza Spika Kificho kwamba wao kwa nia njema bado wanampenda Spika aendelee na kazi zake katika baraza hilo lakini hawako tayari kuomuona akiwazuia kulijadilia suala hilo kwa kuwa wawakilishi hao wamekuwa wakipata wakati mgumu majimbonji mwao kwa kuhojiwa na wananchi wao waliowapigiwa kura.
Wamesema kutokana na mjadala huo kuzimwa barazani hapo wananchi mbali mbali wameonesha wasi wasi wao juu ya wawakilishi wao na kuonekana kama wawakilishi wanawasaliti wapiga kura wao.
Spika alisema kutokana na uzito wa suala hilo anakubaliana na kauli za wajumbe hao juu ya kutaka kuruhusu suala hilo lijadiliwe na wajumbe wa baraza hilo lakini kwanza lazima akutane na kamati ya uongozi ya baraza hilo.
Alisema huo ndio utaratibu wa kufanya kazi za baraza hilo na tayari ameshatoa barua kwa wajumbe wa kamati hiyo ambapo aliagiza kukutana nayo.
Alisema hoja kubwa amabyo itajadiliwa katika kikao hicho ni juu ya kauli iliyopo sasa kuwa Zanzibar ni nchi au sio nchi
Akiwataja wajumbe wa Kamati hiyo kuwa ni wenyeviti wote wa kamati za kudumu za baraza ambazo ni sita, wajumbe wa upande wa upinzani, Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Abass Juma Mhunzi, Kiongozi wa Kambi hiyo, Abubakar Khamis Bakari, na Mwakilishi wa Viti Maalumu, Najma Khalfan Juma wengine ni waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma na Iddi Pandu Hassan ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wengine Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhan Abdallah Shaaban, Spika pia aliwaalika wajumbe wengine kama waalikwa wa kikao hciho akiwemo Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna na Waziri Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha na Uchumi, Mwinyihaji Makame Mwadini.
Kikao hicho kiliendelea kujadilia suala hilo hadi sasa tano za usiku juzi ambapo jana Spika Kificho alisema atawaeleza wajumbe wa baza la wawalishi kilichojadiliwa katika kikao kamati hiyo ya uongozi.
 
Last edited by a moderator:
TAFADHALI VIONGOZI WA DINI WASIINGILIE KWA HILI KWANI KUFANYA HIVYO KUNA MADHARA MAKUBWA HASA TUKIZINGATIA MGAWANYIKO WA WATANZANIA KIDINI.
Naendelea kushauri wananchi wawaache viongozi wa dini wasiwajibu pale wanapoingia kwenye mjadala huu. Kama Watanzania waachiwe wajadili nje ya nyadhifa zao.
 
Kumbe huko anakotawala hakutoshi mnataka aje kutawala na bara? Si agombee tu awe rais wa Tanzania.

na akishakugombea huo urais wa tanzania atausaidia vipi uchumi wa zanzibar ?? hatujadili nani awe rais , akiwa mbara au mvisiwani it doesn't matter ,what matter the most ni huu mfumo wa muungano ambao its more than clear kwamba una lengo la kuimaliza zanzibar in every way. com on guys , hebu naomba mmoja aje hapa atuoneshe ni vipi zanzibar inanufaika na muungano huu zaidi ya kuekewa mfumo ambao unailazimisha zanzibar iwe dependent kwa tanganyika in the so called muungano.
tulikuwa wapi tulipoungana na tanganyika? na watanganyika mmetufikisha wapi? .i like unity but not this kind of unity, u better be fair guys! make it fair and if u cant just livunjeni tugawane mbao!
nawasilisha
 
MUUNGANO tokea mwanzo ulikuwa ni wa kifisadi. Nyerere alimtapeli Karume na Wazanzibari na akaandika huo mkataba uitwao wa Muungano. Hakuna nchi hata moja iliyounganishwa kwa haki na nchi nyengine kwa hadaa kama za Nyerere. Lililobaki ni kwa Zanzibar kudai uhuru kutoka kwa Tanganyika iliyojibatiza jina la Tanzania. Baadaye ni kuishi kwa ujirani mwema kama mataifa huru. Itakuwa ni kosa kubwa kwa Zanzibar baada ya kuwa victimized na Tanganyika kwa miaka zaidi ya 40 irudi tena kujiunga na Mafisadi. Muungwana haumwi na nyoka mara mbili.
well said bro. may god bless u!
 
Kama Zanzibar si nchi, jee ni Mkoa?
George Maziku

MJADALA kuhusu hoja ya hadhi ya Zanzibar kama ni nchi au la, unazidi kupamba moto, na ni dhahiri kuwa hoja hii imewagawa Watanzania katika pande mbili. Wapo wanaoitaja Zanzibar kama nchi na dola kamili, na wapo wanaosema Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Tanzania, lakini bila kutuambia ni mkoa au wilaya ya Tanzania.

Hoja ya Zanzibar ni nchi au la ilianzia katika Bunge baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda, mara mbili kwa nyakati tofauti kusimama na kusisitiza kuwa Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Tanzania, majibu yaliyoibua mjadala na mvutano mkali kwa Watanzania wa kada mbalimbali.

Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimsingi wanaunga mkono matamshi ya Pinda huku wenzao wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanampinga. Kupitia kwa Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna, SMZ imesema: "Zanzibar itaendelea kuwa nchi hadi mwisho wa dunia…Na suala hili tuachiwe Wazanzibari wenyewe tulitolee maamuzi yetu, na huo ndio ukweli."

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wao wamegawanyika, ambapo baadhi hususan wale wanaotoka Zanzibar wanampinga Pinda huku baadhi yao hususan wanaotoka Tanganyika wakimuunga mkono.

Kwa upande wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi, wanampinga Pinda. Kwa wananchi, karibu Wazanzibari wote bila kujali tofauti zao za siasa za vyama wanampinga vikali Pinda, huku wenzao wa Tanganyika wakiwa wamegawanyika, baadhi wakimuunga mkono na wengine kumpinga.

Kwa upande wa vyama vya siasa, kama kawaida yake chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa mpiga debe wake mwenye kiherehere, Tambwe Hiza kilitoa tamko la kuunga mkono matamshi ya Pinda, huku vyama vya upinzani hususan Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kina ushawishi mkubwa visiwani Zanzibar, vikimpinga waziri mkuu.

Kwa ufupi hali ya kisiasa juu ya hoja hii ni mbaya sana, pengine kuliko ilivyowahi kutokea wakati wowote kabla. Nakubaliana na maoni ya mwanasiasa maarufu visiwani Zanzibar, Mohammed Raza kwamba upepo wa suala hili safari hii ni tofauti kabisa na mtafaruku wa siasa za Zanzibar wa mwaka 1984 uliobatizwa jina la ‘kuchafuka kwa hali ya siasa', ambao ulisuluhishwa kibabe kwa kulazimishwa kujiuzulu nyadhifa zote kwa aliyekuwa rais wa visiwa hivyo, Aboud Jumbe.

Hii inatokana na ukweli kwamba mazingira ya kisiasa nchini wakati huu ni tofauti mno na ya miaka ya 1970 na 1980. Ubabe katika kushughulikia migogoro ya kisiasa uliotumiwa na aliyekuwa rais wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM wakati huo, Baba wa Taifa hayati Julius K. Nyerere, leo hii hauwezi kufanikiwa.

Viongozi wa sasa wa serikali na CCM visiwani Zanzibar wako imara na hawawezi kutishwa wala kudhibitiwa. Na hili linathibitishwa na kauli ya Shamhuna kwamba: "Nani wa kuwadhibiti wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika suala hili? Enzi za vitisho na kutaka kudhibitiana zimepitwa na wakati…Nyakati hizi ni za uwazi na ukweli na zenye kufuata misingi ya utawala bora na demokrasia, hazipaswi kuwekewa vikwazo vya vitisho."

Misimamo thabiti na ya wazi ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi ambayo wameionyesha kuhusu suala hili wakati wa mjadala wa bajeti ya SMZ unaoendelea sasa visiwani humo ni uthibitisho mwingine wa hali halisi ya mambo. Kuna wengine walifikia hata kula kiapo barazani kuwa wapo tayari kufa kwa kutetea hadhi ya Zanzibar kuwa ni nchi na taifa huru sambamba na Tanzania!

Pamoja na ukweli kwamba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Aman Abeid Karume hajatoa kauli bayana kuelezea msimamo wake binafsi na wa serikali yake, lakini nashawishika kuamini kuwa kauli ya Shamhuna ndiyo msimamo wa Karume binafsi na SMZ kwa ujumla. Mtu anayedhani Shamhuna aliropoka na alikuwa akiwasilisha tamaa zake binafsi, atakuwa anajipotosha mwenyewe.

Hili linathibitishwa na kauli ya mwanasheria mkuu wa SMZ aliyoitoa barazani kabla ya kauli ya Shamhuna, kwamba Zanzibar ni nchi. Bila shaka mwanasheria mkuu hakutoa kauli hiyo kwa matamanio yake, bali alikuwa akiwasilisha msimamo wa mkuu wake wa kazi, Rais Karume, na uongozi mzima wa SMZ na CCM Zanzibar kwa ujumla.

Na katika kuthibitisha zaidi msimamo wa Rais Karume juu ya hoja hii ni kwamba, kwa mtu yeyote anayefuatilia siasa za Zanzibar hususan kuhusu Muungano na hadhi ya Zanzibar ndani ya Muungano, atakubaliana nami kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Karume, kumekuwepo mageuzi mengi yanayoimarisha hadhi ya Zanzibar kama nchi na taifa huru.

Ni katika kipindi hiki ambapo tumeshuhudia Zanzibar ikizindua rasmi bendera yake kama nchi na taifa huru, ambayo inapepea katika ofisi zote za umma visiwani humo, katika majengo ya Baraza la Wawakilishi na kwenye ofisi zinazotumiwa na SMZ nje ya visiwa hivyo.

Pia ni wakati huu ambapo tumeshuhudia nguvu kubwa ya SMZ ikielekezwa katika kuimarisha vikosi vya SMZ na kuvifanya vibadilike kuwa majeshi kamili ya ulinzi. Hayo yote hayafanyiki kwa bahati mbaya, bali ni mpango maalum wa kuimarisha mamlaka ya Zanzibar kama nchi na taifa huru lenye dola yake.

Kwa hiyo, bila kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar zinasema nini, viongozi na wananchi wa Zanzibar kwa ujumla wanaamini na kusimamia imani yao kwamba Zanzibar ni nchi na taifa huru. Na katika hili hakuna wa kuwatisha wala kuwadhibiti. Anayetaka kupima nguvu za upepo ajaribu kuuzuia aone atakavyosombwa na kutupwa mbali kama karatasi.

Halafu mimi nawashangaa sana hawa watu wenye kiherehere cha kusimama mbele huku mabega yakiwa juu na kunadi eti Zanzibar si nchi! Hivi lugha hii maana yake nini? Watu hawa wanataka kutueleza nini hasa? Kama Zanzibar si nchi, mbona hawatuambii hadhi yake? Ni mkoa au wilaya? Mbona hawatuambii kuhusu hadhi ya rais wa visiwa hivyo? Ni Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya?

Mimi nadhani mtu anayesema kuwa Zanzibar si nchi anajidanganya mwenyewe, wala kweli haimo ndani yake. Anajua anasema uongo na anadhani Watanzania wote ni wajinga kiasi cha kukubaliana na uongo wake. Mtu wa aina hii anadhani Watanzania wa leo ni wale wale wa miaka ya 1961 na 1980, ambao wanakubaliana na kila hoja na hawathubutu kuhoji hata kama watagundua kuwa msemaji anadanganya.

Bila kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo iko juu ya katiba zote nchini, inasema nini, Zanzibar ni nchi na taifa huru lenye dola kamili. Sisemi haya kwa matamanio binafsi na sijarukwa na akili. Nayasema haya kwa kuzingatia ukweli halisi wa mambo yalivyo na ninayo mifano kadhaa hai kuthibitisha kauli yangu.

Zanzibar ni nchi kwa sababu ina bendera yake ya taifa, ina wimbo wake wa taifa, ina mhuri wake wa taifa na ina nembo yake ya taifa. Pia Zanzibar ina majeshi yake (Vikosi vya Ulinzi vya SMZ) ambayo yapo chini ya rais wa visiwa hivyo.

Aidha, Zanzibar ni nchi kwa sababu ina mipaka yake inayotambulika na kuheshimika kimataifa.

Uthibitisho wa hili ni kwamba, kila kiongozi wa nje anapoingia hapa nchini (Tanganyika-Dar es Salaam) hupokelewa na Rais wa Tanzania (Tanganyika) na kupigiwa mizinga 21. Lakini kiongozi huyo huyo akiingia ndani ya mipaka ya Zanzibar hupokelewa na rais wa visiwa hivyo kama mkuu wa nchi na hupewa heshima ya kupigiwa mizinga 21 kama utambulisho kuwa ameingia nchi nyingine.

Hata wakati rais wa Zanzibar anapofanya ziara za kikazi nchi za nje, hupokelewa huko na wakuu au viongozi wengine waandamizi wa nchi anazotembelea, na hupewa heshima zote za mkuu wa nchi. Hutandikiwa zulia jekundu na kupewa heshima ya kukagua gwaride la kijeshi kama heshima kwake binafsi na nchi yake.

Rais wa Zanzibar huteua ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wa kuongoza Brigedi ya jeshi hilo ya Zanzibar na sharti awe Mzanzibari, na pia huteua ofisa wa Jeshi la Polisi ili kuwa kamishina wa polisi Zanzibar, na sharti awe Mzanzibari. Kwa kufanya kazi hii, anatofautiana vipi na rais wa Tanzania anyewateua mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama (CDF) na mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) akiwa amiri jeshi mkuu? Kwa kuzingatia hilo, tutakuwa tunakosea tukisema kuwa rais wa Zanzibar naye ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama visiwani Zanzibar?

Aidha, mtu akitaka kujua juu ya hadhi ya rais wa Zanzibar, basi afuatilie mpangilio wa itifaki kwa viongozi wakati wa sherehe za kumbukumbu ya mapinduzi Zanzibar. Wakati wa sherehe hizo rais wa Zanzibar huwa wa mwisho kuingia na wa kwanza kutoka eneo la tukio ambako pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huwepo. Na zaidi wakati wa sherehe hizo rais wa Zanzibar hukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama akishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kumpa rais wa Tanzania mamlaka ya kuigawa Tanzania katika mikoa na wilaya na kuteua wakuu wa mikoa na wilaya, lakini hajawahi kutekeleza mamlaka hayo kwa upande wa Zanzibar, na mgawanyo wa mikoa na wilaya uliopo sasa na wakuu wake wamewekwa na waliokuwa marais wa Zanzibar wakati huo.

Kwa hiyo, Mtanzania yeyote anayefuatilia na kufanya uchambuzi makini wa siasa za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hususan kuhusu Muungano, atakubaliana nami kuwa Zanzibar ni nchi na dola kamili. Na kimsingi hakuna wadhifa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu huyo anayedaiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano hana mamlaka hata chembe juu ya Zanzibar na wala hawezi kumwajibisha kwa namna yoyote rais wa Zanzibar kama atakataa kushirikiana naye au kumdharau.

Katika hali halisi ya mambo, kuna rais wa Tanganyika (rais wa Tanzania) na rais wa Zanzibar, ambao kwa kweli wana madaraka sawa, hakuna bosi wa mwenzake. Na kwa msingi huo ninashawishika kusema kuwa kinachodaiwa kuwa Muungano kati ya nchi hizi mbili hakipo, ila kuna mazingaombwe au kiini macho tu. Kilichopo hapa ni urafiki tu wa viongozi wanasiasa wa CCM. Siku yoyote rais wa Zanzibar anaweza kuamka na kutangaza kuitoa nchi yake katika Muungano na tusiwe na ubavu wa kumwambia wee, acha.
 
Ikumbukwe Tu Kwamba Siku Zanzibar Ni Nchi Ndiyo Siku Ambayo Maalimu Seif Anatakiwa Kwenda Jela Kwa Uhaini: Patamu Hapo.

Maana Alikwepa Ile Kesi Kwa Sababu Zanzibar Sio Nchi Au Dola. Kwa Hiyo Mara Tu Ikiwa Dola. Basi Na Yeye Ndani.
 
Sasa atafungwa na nani wakati mizengwe ikitayarishwa na vikaragosi kutoka bara.Huoni kama jamaa wote wameshituka kuwa wanagombanishwa ili mafisadi wapate kuwatawala.
Juzi chupuchupu ipigwe kura ya kutokuwa na imani na Muungano ,ila kuna jamaa nafikiri kaahidiwa Uraisi na mafisadi ndio akaweka ngumu eti mpaka october ndio hoja hiyo itafikishwa na kujadiliwa ,lakini habari za ndani za kikao kati ya CUF na CCM wote ziliwafiki kuzusha mgogoro wa Kikatiba na kuwasilisha hoja ndani ya Baraza la wawakilishi na jamaa sasa baada ya kosa kosa hiyo wamesema wamepata mwanya wa kuwashawishi wananchi wote wajiandae na october kwani mambo yanaelekea kama yalivyochokozwa.
 
Ngekewa said:
Kwa hiyo, Mtanzania yeyote anayefuatilia na kufanya uchambuzi makini wa siasa za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hususan kuhusu Muungano, atakubaliana nami kuwa Zanzibar ni nchi na dola kamili. Na kimsingi hakuna wadhifa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu huyo anayedaiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano hana mamlaka hata chembe juu ya Zanzibar na wala hawezi kumwajibisha kwa namna yoyote rais wa Zanzibar kama atakataa kushirikiana naye au kumdharau.

Endelea kutuhabarisha wewe uliye Mcha mbuzi makini wa siasa za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
 
Sasa atafungwa na nani wakati mizengwe ikitayarishwa na vikaragosi kutoka bara.Huoni kama jamaa wote wameshituka kuwa wanagombanishwa ili mafisadi wapate kuwatawala.
Juzi chupuchupu ipigwe kura ya kutokuwa na imani na Muungano ,ila kuna jamaa nafikiri kaahidiwa Uraisi na mafisadi ndio akaweka ngumu eti mpaka october ndio hoja hiyo itafikishwa na kujadiliwa ,lakini habari za ndani za kikao kati ya CUF na CCM wote ziliwafiki kuzusha mgogoro wa Kikatiba na kuwasilisha hoja ndani ya Baraza la wawakilishi na jamaa sasa baada ya kosa kosa hiyo wamesema wamepata mwanya wa kuwashawishi wananchi wote wajiandae na october kwani mambo yanaelekea kama yalivyochokozwa.
Mwiba , Umeula na Chuwa. Naona sasa unataka kukumbatia wana CCM kwa nguvu kwa kisingizio cha Muungano. Wao na ,wewe na wenzako, ni tofauti kabisa. Elewa kuwa wao (CCM -Zenj) hawatakiokuvunja Muungano wala kubadilisha Muundo wake- wanachogombania wao (CCM- Zenj) ni fair deal (ambayo ilianza kugombewa na mwenyewe muasisi Marehemu Mzee Karume). Mwiba na watu wako mnataka kuvunja Muungano. Usidanganyike hakuna CCM hata mmoja Zanzibar ambaye yuko pamoja na nyinyi CUF. CUF kaeni chonjo. CCM -Bara wanatuelewa CCM -Zanzibar - Nyie CUF mlie tu.
 
MJADALA kuhusu hoja ya hadhi ya Zanzibar kama ni nchi au la, unazidi kupamba moto, na ni dhahiri kuwa hoja hii imewagawa Watanzania katika pande mbili. Wapo wanaoitaja Zanzibar kama nchi na dola kamili, na wapo wanaosema Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Tanzania, lakini bila kutuambia ni mkoa au wilaya ya Tanzania.
Hoja ya Zanzibar ni nchi au la ilianzia katika Bunge baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda, mara mbili kwa nyakati tofauti kusimama na kusisitiza kuwa Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Tanzania, majibu yaliyoibua mjadala na mvutano mkali kwa Watanzania wa kada mbalimbali.
Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimsingi wanaunga mkono matamshi ya Pinda huku wenzao wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanampinga. Kupitia kwa Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna, SMZ imesema: “Zanzibar itaendelea kuwa nchi hadi mwisho wa dunia…Na suala hili tuachiwe Wazanzibari wenyewe tulitolee maamuzi yetu, na huo ndio ukweli.”
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wao wamegawanyika, ambapo baadhi hususan wale wanaotoka Zanzibar wanampinga Pinda huku baadhi yao hususan wanaotoka Tanganyika wakimuunga mkono.
Kwa upande wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi, wanampinga Pinda. Kwa wananchi, karibu Wazanzibari wote bila kujali tofauti zao za siasa za vyama wanampinga vikali Pinda, huku wenzao wa Tanganyika wakiwa wamegawanyika, baadhi wakimuunga mkono na wengine kumpinga.
Kwa upande wa vyama vya siasa, kama kawaida yake chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa mpiga debe wake mwenye kiherehere, Tambwe Hiza kilitoa tamko la kuunga mkono matamshi ya Pinda, huku vyama vya upinzani hususan Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kina ushawishi mkubwa visiwani Zanzibar, vikimpinga waziri mkuu.
Kwa ufupi hali ya kisiasa juu ya hoja hii ni mbaya sana, pengine kuliko ilivyowahi kutokea wakati wowote kabla. Nakubaliana na maoni ya mwanasiasa maarufu visiwani Zanzibar, Mohammed Raza kwamba upepo wa suala hili safari hii ni tofauti kabisa na mtafaruku wa siasa za Zanzibar wa mwaka 1984 uliobatizwa jina la ‘kuchafuka kwa hali ya siasa’, ambao ulisuluhishwa kibabe kwa kulazimishwa kujiuzulu nyadhifa zote kwa aliyekuwa rais wa visiwa hivyo, Aboud Jumbe.
Hii inatokana na ukweli kwamba mazingira ya kisiasa nchini wakati huu ni tofauti mno na ya miaka ya 1970 na 1980. Ubabe katika kushughulikia migogoro ya kisiasa uliotumiwa na aliyekuwa rais wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM wakati huo, Baba wa Taifa hayati Julius K. Nyerere, leo hii hauwezi kufanikiwa.
Viongozi wa sasa wa serikali na CCM visiwani Zanzibar wako imara na hawawezi kutishwa wala kudhibitiwa. Na hili linathibitishwa na kauli ya Shamhuna kwamba: “Nani wa kuwadhibiti wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika suala hili? Enzi za vitisho na kutaka kudhibitiana zimepitwa na wakati…Nyakati hizi ni za uwazi na ukweli na zenye kufuata misingi ya utawala bora na demokrasia, hazipaswi kuwekewa vikwazo vya vitisho.”
Misimamo thabiti na ya wazi ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi ambayo wameionyesha kuhusu suala hili wakati wa mjadala wa bajeti ya SMZ unaoendelea sasa visiwani humo ni uthibitisho mwingine wa hali halisi ya mambo. Kuna wengine walifikia hata kula kiapo barazani kuwa wapo tayari kufa kwa kutetea hadhi ya Zanzibar kuwa ni nchi na taifa huru sambamba na Tanzania!
Pamoja na ukweli kwamba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Aman Abeid Karume hajatoa kauli bayana kuelezea msimamo wake binafsi na wa serikali yake, lakini nashawishika kuamini kuwa kauli ya Shamhuna ndiyo msimamo wa Karume binafsi na SMZ kwa ujumla. Mtu anayedhani Shamhuna aliropoka na alikuwa akiwasilisha tamaa zake binafsi, atakuwa anajipotosha mwenyewe.
Hili linathibitishwa na kauli ya mwanasheria mkuu wa SMZ aliyoitoa barazani kabla ya kauli ya Shamhuna, kwamba Zanzibar ni nchi. Bila shaka mwanasheria mkuu hakutoa kauli hiyo kwa matamanio yake, bali alikuwa akiwasilisha msimamo wa mkuu wake wa kazi, Rais Karume, na uongozi mzima wa SMZ na CCM Zanzibar kwa ujumla.
Na katika kuthibitisha zaidi msimamo wa Rais Karume juu ya hoja hii ni kwamba, kwa mtu yeyote anayefuatilia siasa za Zanzibar hususan kuhusu Muungano na hadhi ya Zanzibar ndani ya Muungano, atakubaliana nami kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Karume, kumekuwepo mageuzi mengi yanayoimarisha hadhi ya Zanzibar kama nchi na taifa huru.
Ni katika kipindi hiki ambapo tumeshuhudia Zanzibar ikizindua rasmi bendera yake kama nchi na taifa huru, ambayo inapepea katika ofisi zote za umma visiwani humo, katika majengo ya Baraza la Wawakilishi na kwenye ofisi zinazotumiwa na SMZ nje ya visiwa hivyo.
Pia ni wakati huu ambapo tumeshuhudia nguvu kubwa ya SMZ ikielekezwa katika kuimarisha vikosi vya SMZ na kuvifanya vibadilike kuwa majeshi kamili ya ulinzi. Hayo yote hayafanyiki kwa bahati mbaya, bali ni mpango maalum wa kuimarisha mamlaka ya Zanzibar kama nchi na taifa huru lenye dola yake.
Kwa hiyo, bila kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar zinasema nini, viongozi na wananchi wa Zanzibar kwa ujumla wanaamini na kusimamia imani yao kwamba Zanzibar ni nchi na taifa huru. Na katika hili hakuna wa kuwatisha wala kuwadhibiti. Anayetaka kupima nguvu za upepo ajaribu kuuzuia aone atakavyosombwa na kutupwa mbali kama karatasi.
Halafu mimi nawashangaa sana hawa watu wenye kiherehere cha kusimama mbele huku mabega yakiwa juu na kunadi eti Zanzibar si nchi! Hivi lugha hii maana yake nini? Watu hawa wanataka kutueleza nini hasa? Kama Zanzibar si nchi, mbona hawatuambii hadhi yake? Ni mkoa au wilaya? Mbona hawatuambii kuhusu hadhi ya rais wa visiwa hivyo? Ni Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya?
Mimi nadhani mtu anayesema kuwa Zanzibar si nchi anajidanganya mwenyewe, wala kweli haimo ndani yake. Anajua anasema uongo na anadhani Watanzania wote ni wajinga kiasi cha kukubaliana na uongo wake. Mtu wa aina hii anadhani Watanzania wa leo ni wale wale wa miaka ya 1961 na 1980, ambao wanakubaliana na kila hoja na hawathubutu kuhoji hata kama watagundua kuwa msemaji anadanganya.
Bila kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo iko juu ya katiba zote nchini, inasema nini, Zanzibar ni nchi na taifa huru lenye dola kamili. Sisemi haya kwa matamanio binafsi na sijarukwa na akili. Nayasema haya kwa kuzingatia ukweli halisi wa mambo yalivyo na ninayo mifano kadhaa hai kuthibitisha kauli yangu.
Zanzibar ni nchi kwa sababu ina bendera yake ya taifa, ina wimbo wake wa taifa, ina mhuri wake wa taifa na ina nembo yake ya taifa. Pia Zanzibar ina majeshi yake (Vikosi vya Ulinzi vya SMZ) ambayo yapo chini ya rais wa visiwa hivyo.
Aidha, Zanzibar ni nchi kwa sababu ina mipaka yake inayotambulika na kuheshimika kimataifa.
Uthibitisho wa hili ni kwamba, kila kiongozi wa nje anapoingia hapa nchini (Tanganyika-Dar es Salaam) hupokelewa na Rais wa Tanzania (Tanganyika) na kupigiwa mizinga 21. Lakini kiongozi huyo huyo akiingia ndani ya mipaka ya Zanzibar hupokelewa na rais wa visiwa hivyo kama mkuu wa nchi na hupewa heshima ya kupigiwa mizinga 21 kama utambulisho kuwa ameingia nchi nyingine.
Hata wakati rais wa Zanzibar anapofanya ziara za kikazi nchi za nje, hupokelewa huko na wakuu au viongozi wengine waandamizi wa nchi anazotembelea, na hupewa heshima zote za mkuu wa nchi. Hutandikiwa zulia jekundu na kupewa heshima ya kukagua gwaride la kijeshi kama heshima kwake binafsi na nchi yake.
Rais wa Zanzibar huteua ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wa kuongoza Brigedi ya jeshi hilo ya Zanzibar na sharti awe Mzanzibari, na pia huteua ofisa wa Jeshi la Polisi ili kuwa kamishina wa polisi Zanzibar, na sharti awe Mzanzibari. Kwa kufanya kazi hii, anatofautiana vipi na rais wa Tanzania anyewateua mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama (CDF) na mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) akiwa amiri jeshi mkuu? Kwa kuzingatia hilo, tutakuwa tunakosea tukisema kuwa rais wa Zanzibar naye ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama visiwani Zanzibar?
Aidha, mtu akitaka kujua juu ya hadhi ya rais wa Zanzibar, basi afuatilie mpangilio wa itifaki kwa viongozi wakati wa sherehe za kumbukumbu ya mapinduzi Zanzibar. Wakati wa sherehe hizo rais wa Zanzibar huwa wa mwisho kuingia na wa kwanza kutoka eneo la tukio ambako pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huwepo. Na zaidi wakati wa sherehe hizo rais wa Zanzibar hukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama akishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kumpa rais wa Tanzania mamlaka ya kuigawa Tanzania katika mikoa na wilaya na kuteua wakuu wa mikoa na wilaya, lakini hajawahi kutekeleza mamlaka hayo kwa upande wa Zanzibar, na mgawanyo wa mikoa na wilaya uliopo sasa na wakuu wake wamewekwa na waliokuwa marais wa Zanzibar wakati huo.
Kwa hiyo, Mtanzania yeyote anayefuatilia na kufanya uchambuzi makini wa siasa za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hususan kuhusu Muungano, atakubaliana nami kuwa Zanzibar ni nchi na dola kamili. Na kimsingi hakuna wadhifa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu huyo anayedaiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano hana mamlaka hata chembe juu ya Zanzibar na wala hawezi kumwajibisha kwa namna yoyote rais wa Zanzibar kama atakataa kushirikiana naye au kumdharau.
Katika hali halisi ya mambo, kuna rais wa Tanganyika (rais wa Tanzania) na rais wa Zanzibar, ambao kwa kweli wana madaraka sawa, hakuna bosi wa mwenzake. Na kwa msingi huo ninashawishika kusema kuwa kinachodaiwa kuwa Muungano kati ya nchi hizi mbili hakipo, ila kuna mazingaombwe au kiini macho tu. Kilichopo hapa ni urafiki tu wa viongozi wanasiasa wa CCM. Siku yoyote rais wa Zanzibar anaweza kuamka na kutangaza kuitoa nchi yake katika Muungano na tusiwe na ubavu wa kumwambia wee, acha.

source; Tanzania Daima.
 
Zenj si chochote.
Wanajikanyaga tuuuuuuuuuu
O.K jitoeni haraka kwenye MUUNGANO muone matunda yake.
Hata ivo hakuna M-Tanganyika anaewahitaji.
Mwambie na huyo presido wenu atangaze kujitoa,la sivo fungeni midomo yenu,tumechoka na Vijineno venu.
 
Inauma lakini imejionesha wazi kwamba Zanzibar inachukuliwa kama sehemu ya Tanzania (mkoa) na wala si nchi kamili. Hapa kuna kitu kikubwa sana kinafichwa. Wazanzibari tumedanganywa kwa zaidi ya miaka 40 kwamba Zanzibar ni nchi kumbe kiundani inajulikana Zanzibar ni mkoa kama vile ilivyo Tanga, Mbeya nk.

Sasa kwanini tumekuwa na Raisi wetu, Baraza letu la mapinduzi muda wote huo?. Kwanini hatukuelezwa hayo mapema ili tukajua hatima yetu?.

Ndugu zangu Wazanzibari hakuna sababu ya kumchukia Mizengwe Pinda kwa kutoa ukweli. Huyu amekuwa ndani ya serikali (Ikulu) zaidi ya miaka 40 hivyo anajua ukweli uliofichwa, inabidi tumshukuru kwa kutupa ukweli wa hali halisi.

Sasa inabidi tuamke na kuanza kudai Serikali yetu na uhuru wetu kwani Zanzibar ni nchi kamili na wala si mkoa. Kama lengo la muungano lilikuwa kuifanya Zenj mkoa basi tuuvunje mara moja.
 
Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, si Mkoa ,wilaya ,Shina ,Kata au Mtungi. Ni sehemu ya Jamhuri iliyoko Mashariki ambayo ndani yake imo Mikoa na wilaya kama zilivyo sehemu zingine za Jamhuri ya Tanzania kwa Kaskazini na Kusini bila ya kuiacha sehemu ya Magharibi.
Kabla ya Muungano sehemu hii ya Mashariki mwa Tanzania ilikuwa ni Nchi kamili yenye mamlaka sawa na Tanganyika ambazo kwa pamoja ziliunganishwa na kupatika eneo ambalo litakuwa linajulikana kama Tanzania au Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tan Tanganyika , Zan Zanzibar ia=invidual artist)
 
mmmhh, haya maneno ni ya ugomvi ugomvi tu au uchambuzi?

Ni katika kipindi hiki ambapo tumeshuhudia Zanzibar ikizindua rasmi bendera yake kama nchi na taifa huru, ambayo inapepea katika ofisi zote za umma visiwani humo, katika majengo ya Baraza la Wawakilishi na kwenye ofisi zinazotumiwa na SMZ nje ya visiwa hivyo.

Kwa hiyo, bila kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar zinasema nini, viongozi na wananchi wa Zanzibar kwa ujumla wanaamini na kusimamia imani yao kwamba Zanzibar ni nchi na taifa huru.

Bila kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo iko juu ya katiba zote nchini, inasema nini, Zanzibar ni nchi na taifa huru lenye dola kamili. Sisemi haya kwa matamanio binafsi na sijarukwa na akili. Nayasema haya kwa kuzingatia ukweli halisi wa mambo yalivyo na ninayo mifano kadhaa hai kuthibitisha kauli yangu.

Zanzibar ni nchi kwa sababu ina bendera yake ya taifa, ina wimbo wake wa taifa, ina mhuri wake wa taifa na ina nembo yake ya taifa. Pia Zanzibar ina majeshi yake (Vikosi vya Ulinzi vya SMZ) ambayo yapo chini ya rais wa visiwa hivyo.

Rais wa Zanzibar huteua ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wa kuongoza Brigedi ya jeshi hilo ya Zanzibar na sharti awe Mzanzibari, na pia huteua ofisa wa Jeshi la Polisi ili kuwa kamishina wa polisi Zanzibar, na sharti awe Mzanzibari. Kwa kufanya kazi hii, anatofautiana vipi na rais wa Tanzania anyewateua mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama (CDF) na mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) akiwa amiri jeshi mkuu? Kwa kuzingatia hilo, tutakuwa tunakosea tukisema kuwa rais wa Zanzibar naye ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama visiwani Zanzibar?

Huyu mheshimiwa na hoja yake ya jeshi, hivi anajua kwamba JWTZ ni Moja chini ya Wizara ya Ulinzi na JKT?, na kwamba Wizara ya Mambo ya ndani ni moja? ulinganifu wake ndo umeniacha hoi. Sidhani kama yuko serious.

Sasa soma huyu:

"I ask myself: If Zanzibar was a sovereign state, then how would questioners be elected into the Union parliament? Does this suggest these people are so naive as to think that they can sit in any parliament outside Zanzibar, say--in the Comorian, Malawian, Kenyan, Ugandan, Ethiopian parliaments--as and when they wish?"
 
Back
Top Bottom