Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Tusubiri tuone lakini nafikiri na haya yatazimwa kwani tunasikia wawakilishi wa ccm wa baraza la wawakilishi wameshaitwa Dodoma hatujui safari hii watawatia nini maana wapo wazi Watangayika wasemalo wao wapo tayari kutii kama mbwa aloana chatu.
Hilo la kuitwa Dodoma kama watoto waduchu ndilo kati ya moja wasilolipenda na huko ndiko kutakako wamaliza mafisadi ,kwani hukumbuki waliitwa Butiama Kikwete akatoka anasema peke yake alipoulizwa una nini ? Akasema wataniona sasa haijulikani kama amewaonyesha au ndio kawaita kwenda kuwaonyesha.
 
JK ni paka wa ndani aliyezoea kula mabaki ya viazi na vichwa vya samaki kwahiyo kutoka kwenda kuwinda panya ni sawa na kumtuma mkeo akashike lindo kwenye ofisi ya Saccos badala yako.

Kwanini haongelei swala la Zanzibar au kulifanyia kazi hadi vita ianze? Kuna lipi la ajabu kwa sasa hadi PM wetu aliyeshuka hadhi kwa kujichanganya aseme ati Wanasheria watoe maana ya Muungano? kwani ina maana yeye siku zote alikuwa hajui maana ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Tunajua kwamba kuna matatizo ya hapa na pale..., kwani PM PindaPinda hayajui haya hadi apindishe pindishe tu mambo? Yeye ndio haswa ameruhusu haya mambo kwenda mbali maana ameruhusu mjadala na huwezi kukataza watu fulani kuongea wakati umeruhusu kundi lingine kuongea, wataongea hata kama ni chinichini halafu baadaye moto ukishakolea unatokea pande ingine.

Serikali iache kubabaika, huo ni upumbaf na ndio utatuletea balaa muda sio mrefu maana inaonekana viongozi wote ni paka wa ndani. Hakuna mwenye nguvu ya kusimama na kusema jambo sahihi ni hili. Kuna jarida moja nchini lilisema kwamba nchi imekosa kiongozi mweledi, yaani hakuna kiongozi katika nchi hii sasa anayeweza kusimama na kusema jambo la kueleweka na sisi tukamsikiliza. Nilidhani Pinda anaelewa analofanya kumbe naye ni mgonjwa wa ufisadi na anamezwa na uchafu uliopo CCM.
 
Wazanzibari wanauliza kama Zanzibar si nchi Tanganyika ilijiunga na nani ?
 
Anhaa nimemwona huyo anavyojikomba ,lakini sidhani kama hajui kuna watu wanavuka vigingi vyenye uhakika katika kesi ,kuna mawakili wanasifika kwa kuvusha wauaji ,majambazi na mambo makubwa makubwa hata haya ya vijisenti vilivyochotwa na ndivyo iliyoptokea katika kesi iliyowakabili watuhumiwa wa uhaini.
Uwakili ni fani kama ya mpira ukiujua kuucheza utashinda mechi nyingi,hivyo kesi ile ni kama mfano wa mechi anaejua kucheza ndio atakaeshinda,huyu Bwezeleni amezama katika Katiba wakati watu wapo kwenye Mkataba na Hati ya Muungano,mechi iliyochezwa pale katika kesi ilizama kwenye Katiba hivi sasa Katiba imepigwa kumbo ,pia ukiongezea uamuzi wa kesi ile uliingia katika kuihifadhi Zanzibar kama si Nchi ,na kwa vile hukumu ya uhaini inawezekana kabisa kuwa ni kukatwa shingo au kunyongwa ,watuhumiwa hawakuwa na hila ila kuzamia kule ambako roho zao zitaokoka,hivyo wakili wao alicheza kufa kupona kuwaokoa wateja wake ,huku akijua anachokidai sio cha kweli na hata kuwa kitakuwa cha kweli hakiwezi kuwa cha kweli ikiwa Mkataba na hati asili ya Muungano itatumika na kuhojiwa usahihi wake.
Wakili huyuhuyu Bwezeleni akitiliwa vijisenti ili awe mtetezi wa mkataba wa Muungano basi utaona ajabu anavyobadilika ndivyo mawakili walivyo.
So far alete mkataba au hati ambayo inaonyesha Zanzibar na Tanganyika zilifutwa ,alete hati ambayo Nchi mpya Tanzania iliomba kujiunga na Umoja wa Mataifa ikiwezekana alete makubaliano yaliopatikana kutoka kwenye mchakato wa Tanzania kuwakilishwa kwenye Umoja wa Mataifa.
So far bado atakuwa wakili wa kutetea iwe kweli au uwongo na ndio maana ya uwakili au kuna mtu hapa atupe maana ya wakili ,ili tuelewe kazi ya Bwezeleni.Kazi ikishahusiana na wateja basi ujue ni biashala.
Mawakili wanajulikana kwa ukweli kuufanya uwongo ,na uwongo kuonekana kweli ,ni watu na kazi yao ,lakini huyo hawezi kuvuka kwenye hati ya Muungano kwani ni mistari michache tu ambayo imejifunga.
Alete siku Tanganyika ilifutwa na Zanzibar nayo ilifutwa na nani alietoa ruhusa hizo ,Je wanakubalika kuyafanya mambo hayo kutokana na mujibu wa makubaliano ya Mkataba na Hati yenyewe ambayo ndio inayotambulika hadi sasa huko ulimwenguni
Tuchukulie wamekutana kibunge wamejadiliana wamekubaliana ,Je walifunga safari kwenda kuibadilisha hati katika Umoja wa Mataifa na kusema sasa hati itasomeka hivi na vile ?
Tunarejea kuwa haya mambo wamekaa mafisadi chini ya chama chao kimoja tu na kujitungia utumbo wakiona kila kitu kipo chini ya amri yao kutakuwa hakuna wa kuwahoji .Na ndivyo wanavyotuendesha WATANZANIA huku wakitupeleka puta,Lazima Tanganyika ipapatuliwe la si hivyo watakaoumizwa sio WaZanzibari peke yao bali na Watanganyika wengine waliokuwa bado wanaona Zanzibar si nchi ,kumbe wajanja wachache wa CCM ndivyo wanayojipatia mihela ya kupora kiulaini kabisa.
Ndio tukamsikia Pinda akisema anawarudishia CCM maana ndio waliotengeneza madudu yasioenunulika kwa wananchi.
Sasa tazama mwisho wa huyu mnaemwita wakili amesema ....Kama CCM ikitaka zitakuja.....! Ndio nikasema anajikomba.Watu wa aina hii waogopeni.Asubiri bakora yake kutoka kwa CUF.
 
Wazanzibari wanauliza kama Zanzibar si nchi Tanganyika ilijiunga na nani ?

Kama haya ndiyo mawazo yao (na yale ya kusema kuwa hakuna mzanzibari aliyewahi kuwa rais wa Muungano.), basi iko kazi. Hakuna mtu anayepinga kuwa Zanzibar haikuwa nchi kama vile ilivyokuwa kwa Tanganyika. Zote mbili zilipoteza sovereignty zao zilipojiunga na kuzikabidhi kwa Tanzania. Kwa sababu palionekana haja ya kulinda kuwepo kwa identity ya uzanzibari, Zanzibar ikabaki kama taifa na sio nchi. Mifano iko mingi ya maelewano ya namna hii:a) Great Britain ni nchi wakati Scotland,England,Wales na Northern Ireland zimebaki kuwa mataifa yenye bendera n.k. Canada hivyo hivyo. Ingawa Quebec wamepewa upendeleo lakini sio nchi. Mfano ulio karibu na sisi ni wa Finland na kisiwa cha Aland. Kina bendera, stampu n.k. lakini si nchi. Matatizo kwetu yalianza kwa kuwapa upendeleo Zanzibar kwa kujaribu kuwapa parity katika uwakilishi ingawa kwa population, uchumi ni kiduchu sana ukilinganisha na bara. Hii imewezekana kwa vile Tanganyika haipo kwa hiyo interest zake zimemezwa katika Muungano. Likifanyika ambalo mnalolidai, yaani kuundwa mseto wa nchi mbili chini ya serikali ya Muungano, hakuna kiongozi wa Tanganyika (kama alivyoasa Sumaye hivi karibuni) atakayekubali parity na Zanzibar wakati wakichangia zaidi kwenye chungu cha Tanzania! Huo utakuwa ndio mwanzo wa kuvunjika Muungano. Tusijidanganye, serikali tatu yenye kuunganisha nchi mbili zenye full sovereignty haiko sustainable. Wazanzibari wanadai hii ili waweze kuingia mikataba na jumuia za nje, hususan OIC, ambazo wanaona zitawafaa wao. Sijawahi kusikia Quebec, Catalan, British Columbia, New South Wales, California, Maharashtra n.k. zikifanya hivyo (ukiondoa Scotland na Wales kuwa wanachama wa Fifa for historic reasons!) Tusiogope kusema ukweli. Serikali tatu itafanikiwa tu ikiwa Tanganyika na Zanzibar zitapokonywa sehemu kubwa ya mamlaka na kukabidhiwa kwa serikali ya Muungano. Hili sidhani kama litakubalika kwa wenzetu.

Madai ya Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais vile vile hayana msingi. Cha kujiuliza ni kuwa katika mtindo huo ni wakati gani huyo Mheshimiwa atakuwa Rais wa Zanzibar na ni wakati gani Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano? Mshahara wake na gharama zake nyingine zitalipwa na nani? Na je hii ina maana kuwa mZanzibari akatazwe kugombea urais wa Muungano maana akishinda utawala wote utatokea upande mmoja! Na je hata kama Rais wa Muungano atatokea bara, jambo likimpata, ina maana Rais wa Zanzibar (ambaye hakupigiwa kura na sehemu kubwa ya nchi ya Tanzania) ndiye atakayerithi urais? Chogo gani atakayekubali hili? Mfumo uliokuwepo sasa ni bora kuliko ule wa awali ambao de facto ulisema Rais atatokea bara na Makamu Unguja.

Kama tunaona muundo wa Muungano wetu unamnyima haki mmoja wetu kiasi cha yeye kuona anahitaji utambulishi kama nchi, basi tukae pamoja tugawane mali na tutakiane heri. Hatutakuwa wa kwanza na wala hatutakuwa wa mwisho kufanya hivyo. Heri tuige mfano wa Czechoslovakia kuliko ule wa Yugoslavia!
 
Samahani kwa kusema hivi lakini Mkuu Mwiba si mkweli. Huo mkataba unaosema uko Umoja wa Mataifa ungekuwepo ungeishaonekana. Muungano wa nchi mbili huru hauhitaji kibali cha Umoja wa Mataifa. Hata kama tukiamua Muungano ndiyo basi, Umoja wa Mataifa utataarifiwa tu na sio kuomba baraka zao. USSR, Czechoslovakia, Yugoslavia hazikuomba. Kwa USSR, Umoja wa Mataifa ulifahamishwa tu kuwa Urusi ndiye atakayekuwa mrithi wa kiti cha USSR. Mimi naamini hizo nyaraka tumezipoteza wenyewe kama ambavyo mafaili mengi tu yanavyopotea. Kwa uzembe na si kinginecho.
 
Hayo sio mawazo yao bali hizo ni hoja zao ambazo huwezi kuzipiga teke tu kwa kuwa Tanganyika ni zaidi ya milioni 36.
Hivi kama kukabidhi ni kitu gani kilikabidhiwa ?
Hivi unakubali kuwa identity ya Zanzibar ipo ?
Hivi unakubali WaTanganyika walikubali kupoteza ID yao ?
Hivi ni nini tofauti ya Taifa na Nchi ?
Unaposema Matatizo kwetu yalianza kwa kuwapa upendeleo Zanzibar...Nyinyi mliotoa ni kina nani ?
Tanganyika haipo ipo wapi ,ni wapi imesemwa kuwa Tanganyika imefutwa ?
Usitegemee kuwa Zanzibar itahitaji kitu kutoka Tanganyika ,Zanzibar kama unaijua historia yake basi huwezi kusema hivyo,Zanzibar imeuliwa na inazidi kuuliwa kiuchumi kwani njia zake zote kuu zimebanwa.
Mbona kuna nchi za Kiarabu kila mmoja na lake na mambo yao si mabaya wala hatujasikia kuzibiana mianya ya biashara.(U.A.E) ambao mafisadi wetu wamewapa kibali cha kuvuna mali ya asili hapo mbugani.
Madai ya Raisi wa Zanzibar kuwa makamo wa raisi wa Muungano hayana msingi,sidhani kama umefikiri vilivyo ,hio ni kifungu cha mwanzo kwenye hati ya Muungano ,je mlifanikiwa kukibadilisha au mizengwe ya Utawala wa Chama kimoja ? Fundi Mchundo usijaribu kugusa wala kukarabati mambo ya Hati ya Muungano yatakupiga na chini.bora ukimbilie kwenye Katiba viraka.
Unajua unapokuja Rais au Uraisi ,kama ukiangalia nchi nyingi siku hizi zinatumia Prime Minister na raisi anakuwa kama nembo ya Taifa kama walivyo wafalme wa Ulaya.Na kwa vile nchi hizi ni za Muungano basi raisi wa Muungano hatapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi,hilo litakuwa halipo.Na nafasi yake itachukuliwa kwa kupokezana kutokana na sheria zitazotungwa na kukubalika katika Katiba mpya ya Muungano na sio Katiba hii iliyojaa ufisadi wa kiongozi kuwepo juu ya sheria, mambo ya ukiritimba yatawekwa kando na kupata katiba msumeno.
Kugawana mbao sio jambo baya lakini hilo litaiathiri Tanganyika kuliko Zanzibar kwani stability ya Tanganyika ipo mikononi mwa Zanzibar.
 
Mh nahisi kama ni kinyume chake!!
 
Kwako Fundi
Taifa, dola au nchi haziundwi kutokana na ndoto za mtu mmoja au watu wachache. Ili taifa litambulike kama taifa kunahitajika sifa maalum za lazima na sio za kulazimishwa, kuzushwa au kubuniwa. Kwa mujib wa sifa za kimataifa Zanzibar ni nchi na taifa kamili bila ya kujali nani ana au wanabuni vyenginevyo. Nchi yenye mipaka inayotambulika kimataifa na kuwa na watu wenye sifa maalum za nchi hiyo, kwa kusema lugha inayotambulika kuwa lugha ya au za nchi, yenye utamaduni, mila na kabila au makabila ya nchi hiyo, yenye jamii halisi na makhsusan, siasa inayoifuata na uchumi wake wa kujitegemea wenyewe, inatambulika kama nchi, aidha ikiwa huru au ikiwa imetawaliwa. Yaani kama Zanzibar ilivyokuwa chini ya ukoloni wa Kiingereza (na hata ukoloni wa sasa). Nchi kama hiyo ikiwa huru inatambulika na Umoja wa Mataifa kama ni nchi na taifa huru. Bila ya haja ya kukariri zaidi Zanzibar inazo sifa zote ambazo zinahitajika ili nchi itambulike kama taifa na nchi huru , pamoja na kuwa na kiti chake katika Umoja wa Mataifa, ambacho kipo wazi tokea kuundwa kwa Muungano katika mwaka wa 1964. Natumai unafahamu maana ya kuwa kipo wazi !!!

.....................Tanzania si nchi bali ni taifa la kubuni, kama nchi ya ndotoni na sio nchi au taifa halisi kwa mujibu wa tafsiri za kimataifa zinavyotambulika. Tanzania si nchi wala dola moja, bali ni Muungano wa nchi mbili huru, mataifa mawili huru na madola mawili huru, zote mbili zilikuwa na uwakilishaji katika Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Madola. Zote mbili zikiwa na kura sawa bila ya kujali ukubwa au idadi ya wananchi wake............ hayo hapo juu ni baadhi ya madondoo ya kitabu cha Zanzibar Dola, Taifa na Nchi Huru.

Tanganyika na Zanzibar ni nchi mbili tofauti kinyume na Vietnam, China-Hong Kong na Taiwan, Korea na Ujerumani zote ziligawiwa kuambatana na vita na njama za kikoloni na kibeberu. Zanzibar haijawahi kuwa sehemu ya Tanganyika na kuunganishwa tena na sehemu ya nchi moja. Tofauti ya kugawiwa kwa lazima kwa hizo nchi nilizotaja hapo juu, Zanzibar kuambatana na mbinu za kikoloni na kibeberu ili lazimishwa katika Muungano. Huu haukuwa Muungano wa hiari baina ya watu wawili, na hata kama ungelikuwa wa khiari na nia njema, basi Zanzibar bado inatakiwa iwe na haki ya kujitoa katika huo Muungano pindi ikiona Muungano huo hauna maslahi na nchi yake na watu wake au inatakiwa kuwa na haki ya kubadilisha mfumo wa huo Muungano pindi ikiona mustakbal wa Zanzibar unaporwa . Leo Wazanzibari wanapotaka kulinda maslahi yao wanakemewa na kubwekewa, kwanini wanataka kutetea haki zao. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni mfano wa Mtawala na Mtawaliwa. Kwa hivyo ndugu zetu wa Tanganyika inabidi waelewe kwamba mtawaliwa sawa na mtumwa ana haki ya kujikombowa sio tu ikibidi bali ni wajibu wa lazima kama kufa. Vyombo vya Serikali na/au Chama tawala vinaweza kulazimisha watu wafuate na kutii fikra au sheria fulani. Wazanzibari hawawezi kulazimishwa kuamini fikra au sheria hizo za kubuni. Mzanzibari anaweza kwa muda fulani kulazimishwa kukariri kuwa Zanzibar si nchi lakini hawezi kulazimishwa kuamini na kukubali hivyo. Mzanzibari hawezi kuamini na kubururwa huku akinyoosha shingo kama n´gombe apelekwae machinjoni.

Ikiwa Mzanzibri kaweza kumtoa Mngereza mwenye nguvu mara dufu kushinda Mtanganyika hatoshindwa kumtoa mkoloni asiejitegemea binafsi. Kuna njia nyingi za mapambano ya kujikomboa, kwa mfano kuelekeza mapambano huko huko Bara na kudhoofisha kibri chao na kuna njia za kuendeleza mapambano hataa kama watazuia hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi, hata kama wakilifunga Baraza milele, jambo ambalo wameshaanza kulizungumzia.

Kulifunga Baraza la Wawakilishi ni kuwapa Wawakilishi uhuru wa kufanya kazi mitaani bega kwa bega na umma wote wa Wazanzibari, kuwatia imani Wazanzibari na kuwatayarisha kiitikadi na kimapambano. Kufyeka magugu ya Muungano na kutengeneza medani za kuirejesha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa.

Wazanzibari kukataliwa vibali vya Maandamano ni kuwazidi kuwatia mori wa kutumia mbinu kama zile za dhidi ya Muingereza za kufanya maandamano madogo madogo mengi kwa kuvaa sare za Zanzibar ni Nchi maharusini, kwenye beni, unyagoni, taarabuni, kwenye mashindano ya ngarawa, kucheza n´gombe, kwenye dhikiri n.k. Kutunga nyimbo, mashairi ya Zanzibar ni nchi. Kubandika makaratasi makutani, magarini, kwenye miti kudai uhuru na kura ya maoni. Kutawanya vidaka sauti vya "KIROBOTO" na kutunga kasseti nyengine za VIROBOTO. Kutayarisha mechi za mpira, mashindano ya baskeli kutetea maslahi ya Zanzibar ni nchi . Maandamano kama hayo hawataweza kuyazuia mradi kila siku kuna badilishwa mbinu na medani.
WaZanzibari weshakata kamba kazi kwenu waTanganyika kuwalea mafisadi mwisho watawageuza watumwa na kuwarudisha tulipotoka ,ni genge hilo epukaneni nalo ,CCM hawafai wameshapoteza dhamana ya uongozi wamebaki kuchumia matumbo yao tu,hawajali Chadema wala cha nani ,wanajiona wao tu ndio wenye hati miliki ya Tanzania ,kwa taarifa hapa tulipo ni katikati Zanzibar hiyoo na Tanganyika bado inasuasua,CCM wamekamatwa pabaya lazima waekwe pembeni kwa kuipapatua na kuwapapatua ndani ya Tanganyika waanze kukimbie kuelekea huko walikoweka vijisenti vyao sasa kama hujachukua chako mapemba ndio mbinde.. !
 
Hivi sasa nipo katika moja ya nchi za kiarabu, nimefurahi kuona wao bado wanaendeleza utamaduni ambao tulikuwa nao hapo zamani Africa na sasa tunauacha. Majuzi rafiki yangu mmoja anasema alimpeleka mpwawe kwenda kuona mchumba aliyechaguliwa na wazazi, na mambo yote yamewekwa sawa. Ikanikumbusha mbali kipindi hicho nasi tulikuwa tukichaguliwa wachumba, lakini aah! mbona wazazi wetu waliishi tena vizuri tu na miaka mingi bila kuachana. Sisi leo tunajichagulia wenyewe wachumba hata mwaka bado kila mtu na lake, naamini baada ya kupewa mke/mume kikubwa kinakuwa huyu ndiye mwenzangu ktk hali zote. Muungano wetu unafanana na wanandoa waliooana kwa ridhaa ya wazazi, mzee wetu Karume na mzee wetu Nyerere waliamua kwa niaba yetu kama inavyosemwa na wengi. Lakini kama ndoa muungano ni kitu kizuri, iwe tumeungana kwa ridhaa na maoni yetu wenyewe au kuunganishwa kama ilivyo sasa. Kinachoonekana wenzetu wengi wa visiwani hawapendelei kuwa ktk huu muungano, na kila kasoro itakayoonekana wataitumia hiyo kuonyesha kuwa muungano si sawasawa. Nifahamuvyo mimi si kwamba bara hatuzioni hizi kasoro la, ila cha thamani ni kipi muungano au kasoro?. Kawaida vinapoungana vitu viwili kuzaa kimoja, vitu hivyo hupoteza asili yake na huo ndio muungano. Huwezi kuungana halafu ukawa tena bado vile vile, huo hautakuwa muungano ni ushirikiano. Hadithi hii nzima inanikumbusha nyumba ya rafiki yangu mmoja tuliyeshibana sana, kipindi alichooa alipata taabu sana. Mke kila leo kwao, nini mama kaniita, kesho kuna hili nyumbani, keshokutwa sababu hii. Alipata taabu kweli, alijaribu kutafuta msaada wa ushauri ikashindikana, na bahati mbaya ni ndoa ya kikristo akawa hana jinsi tena. Nyumba iliyumba sana, kwa sababu tu binti alijiona ana kwao. Hakuwa anajali lolote linaloweza kutokea kwa kuwa mama yupo, ikatokea bahati mbaya mama yake akafariki dunia ikawa safari za kwenda kwa mama zimekufa tena. Huwezi kuamini binti akatulia kweli, nyumba imekuwa na amani na sasa hata maendeleo yanaonekana, maana wanashirikiana. Inaonekana ndugu zetu wa Zanzibar wanaamini bado wanaye mama wa kumkimbilia, wanaamini kama si huu muungano saa hizi wangekuwa mbali, Mama angeshawasaidia. Kwa mwelekeo huu watakapotambua kuwa mama waliyefikiria kuwa yupo hayupo wamechelewa. Kilichotakiwa ni kutambua kuwa sisi ni ndugu na hawa wazee wetu hawakukosea kutuunganisha, kwani wameunganisha ndugu. Inaweza kuonekana walikuwa na sababu zao, lakini haitabadilisha undugu wetu. Hata tukiamua kuwa leo basi kila mtu ashike njia yake bado tutakuwa ndugu tu, ingewezekana kabisa kuwalazimisha viongozi wetu waweze kushuhughulikia kasoro zilizopo maana hakuna asiyeziona lakini kwanza iwepo nia. Na nia ni je tunautaka muungano au hatuutaki?, hizi sababu haziwezi kufanya muungano ukaonekana ni kitu kibaya hivi. Hebu fikiria wale waliooana kwa mapenzi ya wazazi, unafikiri hawakuti kasoro?. Inakuwa ni siri yao, kwao kikubwa ni ndoa yao na ndio maana wazee wetu zamani waliweza kuishi mpaka kifo ndio kikawatenganisha. Kasoro zipo na zitaendelea kuwepo, wala zisiwe sababu, mseme tu kwamba jamani eeh! kila mtu achukue ustaarabu wake tumempata mama wa kutusaidia kutoka kwenye huu umaskini!. Tutawaelewa tu, wala msiwe na hofu.
 
Wacha kulinganisha Zanzibar na Tanganyika kama mke na mume ,sasa nani mwanamke na nani mwanamme ?
Yaani miungano yote inaelekea kufa ila hapa mnataka misifa ,iweje upande mmoja ung'ang'anie ,huoni kama kuna pazia ambalo mafisadi wamejificha na 100% pazia hili likiondolewa utawaona watakavyotoka baru ,kuelekea walikoficha vijisenti, mimi nasema kama hujachukua chako mapema basi fanya juu chini ukwapue ili nawe ujue pa kukimbilia.
Kila siku kwenye magazeti yao wanabadili miundo mbinu,siku hizi naona wamekazania huku kwenye malumbano ya Muungano ,lakini wakiona watu wanaulizia ulizia utawaona wanaandika mabichwaa ya habari wala hayalingani na habari yenyewe ,si umesikia wamemkamata mwalimu kijijini huko masikini ya mungu hajui hata kujitetea wala hana mtandano wakumsaidi wakaandika JK afanya kweli,yaani ukiangalia wanazidi kumwangamiza Muungwana ,Pata shika ripoti ya madini sasa moto ,yaani hawajui wazibe wapi ,hawa wameshapoteza muelekeo ,kila mtu yumo kutafuta pa kuhamishia vijihela alivyokomba maana Muungano nao hauna mshiko ,Zanzibar imeshajitoa na Tanganyika ipo njiani ,lazima mafisadi sasa warudishe vyote -Warudishe Tanganyika ,Zanzibar ipo na warudishe mihela la si hivyo basi patakuwa hapaliki Tanzania.
 
``Maandamano haya na mkutano wa hadhara hayana uhusiano wowote na chama chochote cha siasa au Jumuiya za kidini na shughuli hii itawashirikisha Wazanzibari kutoka Mikoa mitano ya Zanzibar,`` alisema.Kati wa wazee waliowasilisha ombi hilo kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi ni mwanaharakati machachari, Bw. Rashid Salim Adiy ambaye aliwahi kuongoza kikundi cha watu 11 waliofungua kesi Mahakama Kuu Zanzibar kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuomba kuonyeshwa hati asilia ya Muungano huo.
Hata hivyo, katika kesi hiyo, Bw. Rashid na wenzake 10 walianguka baada ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bw. Idd Pandu Hassan, kueleza kuwa Muungano huo ni halali na hati ya Muungano iko katika taasisi husika na sio katika ofisi yake.
Wajumbe wengine wa Mkoa wa Mjini Magharibi ni mzee Kadhi Zubair Juma wa Kiembesamaki, Mmanga Barua Suleiman kutoka Chukwani, Nassor Hassan Nassor Kisauni na Juma Nassor Hassan wa kijiji cha Kombeni.
Kwa upande wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, walioorodheshwa katika barua hiyo ni Haji Sheha Hamad, kutoka kijiji cha Potoa, Juma Suleiman Haji kutoka Bumbwini na Ali Omar Omar kutoka kisiwa cha Tumbatu.
Wengine ni mzee Abdulla Nadhif kutoka kijiji cha Makunduchi, Ali Simai Mwadini kutoka kijiji cha Bambi na Suleiman Mohammed Hassan Unguja Ukuu, katika mkoa wa Kuisni Unguja.
Wengine ni kutoka mikoa miwili ya Pemba, ambao ni Abdalla Rubeya Othman kijiji cha Wingwi, Ahmed Nafoo Mohammed kutoka Konde na Abdalla Mbarouk Juma kutoka Kiungoni, katika mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kusini Pemba ni Mtumwa Khatib Khamis kutoka Mtambile, Rashid Abubkar Salum kijiji cha Kilimani na Bi. Siti Shaibu kutoka Mkoa Kwa upande wa Mkoa wa Kaskazini
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Mgharibi, Bw. Bakar Khatib Shaaban, akizungumza na Nipashe mjini Zanzibar jana alisema kwamba mjadala wa Zanzibar nchi au si nchi hivi sasa umefungwa katika majukwaa ya kisiasa.
Alisema kwa vile hivi sasa suala hilo linahisia mbili kwa wananchi, ikiwemo wanaopinga na wanaokubali, polisi imeona ni bora mijadala kama hiyo isiendelezwe kwenye majukwa ya kisiasa kwa vile inaweza kuvuruga amani na utulivu.
Hilo ni ombi la tatu kuwasilishwa Polisi Zanzibar katika kipindi kisichizidi mwezi mmoja, kuomba kufanyika maandamano ya kupinga kauli ya Waziri Mkuu aliyoitoa Bungeni kuwa Zanzibar si nchi na ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano tangu kufikiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, mwaka 1964.
---------------------------------------------------
Hapa msione watu ni wajinga lakini hizi ni hatua kwa hatua ambazo zinabidi zipitiwe kuiarifu polisi ,sasa kinachopatikana hapa ni ukiukaji wa haki za binadamu ,hivyo jeshi la polisi silifikiri kuwa linawazuia watu kufanya maandamano na kuona ndio linafanya kazi ya chama vizuri ,hapana wandugu mambo sasa ni ya kimataifa ,kama polisi wangeruhusu yale maandamano ya leo Jumapili yakafanyika kwa salama na amani basi ,kidogo joto ingekuwa limeshashushwa waliotapika wametapika na siku imepita.
lakini kwa kufanya kazi za CCM polisi wamezuia hivyo rikodi inaingia katika daftari ,katiba imepingwa kwa kutowapa uhuru wananchi kupinga lile wanaloliona kwa kupitia njia za amani.
Sasa ndio kuna hilo jipya ambalo wameshasema hawashirikishi chama ni la wananchi wote wa Zanzibar kuwasakama mafisadi katika kuipapatua Tanganyika na kuivua katika koti la Muungano ,hii naweza kuweka hesabu kuwa ni hatua yao ya mwisho na kama polisi wakizidi kuendeleza kazi ya Chama basi maandamano yatakayofuata yatakuwa ya sie na mwana abebe jiwe ni all out maandamano ,haya hayatahitaji ruhusa kutoka polisi wala jeshi ni kama yale yalioyotayarishwa na CUF baada ya kupingwa kufanyika ,wataitumia Katiba hii hii ambayo CCM hawataki kuibadilisha wakidai haina haja yakubadilishwa kwa vile tu maslahi yao yatakuwa hatarini iwapo itabadilishwa ,wananchi wa Zanzibar watatoka in mass kuandamana kupinga kauli inayosheherekewa na CCM kuwa Zanzibar sio Nchi ,hapo ndipo patakaposababisha matatizo kupanda ngazi,kwa upande wangu ni bora polisi wakaachana na kutekeleza amri za chama na kuyaruhusu ili yafanyike na watu waondoe joto lao ,mambo ya kuleta kisibabu sijui kuna watu wanaunga mkono na watu wengine wanapinga hayana msingi na wala sio kwenye UTAIFA ,wasidanganye watu na habari za kuandikwa kwenye magazeti kuwa sijui Mwana Udi kasema Muungano ni mzuri na unahitaji kutiliwa mbolea lakini walipomuuliza Bwana Ubani kasema Muungano hauna maslahi yeyote na yanainyonya Zanzibar ,miandiko hii inayotokea kwenye magazeti yakiwahusisha watu tofauti wenye majina ya Kizanzibari ni uzushi usio kuwa na mshiko ni kazi ya mafisadi kutaka kugonganisha watu vichwa na polisi nayo wamekuwa wakiitumia ili kuwanyima wananchi haki yao ya kikatiba ,haya watu wa Zanzibar wameshayashitukia ,hawatozuilika kuchukua hatua ya kuweka kando amri za polisi zinatoka kwenye Chama Cha CCM na kuingia mabarabarani kwa amani kabisa ,polisi wakae wakitambua tu kuwa watu wanadai madai ya Nchi yao kuambiwa si Nchi,Raisi wao kuambiwa ni kama kocha wa Mpira na mambo kibao yamekuwa yakitupi upande wa Zanzibar nia na njama hizi za mafisadi zitazimwa bila ya wao kutegemea kwani Dunia sasa imeshaanza kutupia macho sakata hili.
 
Hayo sio mawazo yao bali hizo ni hoja zao ambazo huwezi kuzipiga teke tu kwa kuwa Tanganyika ni zaidi ya milioni 36.
Hivi kama kukabidhi ni kitu gani kilikabidhiwa ?
Hivi unakubali kuwa identity ya Zanzibar ipo ?
Hivi unakubali WaTanganyika walikubali kupoteza ID yao ?
Hivi ni nini tofauti ya Taifa na Nchi ?
Unaposema Matatizo kwetu yalianza kwa kuwapa upendeleo Zanzibar...Nyinyi mliotoa ni kina nani ?
Tanganyika haipo ipo wapi ,ni wapi imesemwa kuwa Tanganyika imefutwa ?
Usitegemee kuwa Zanzibar itahitaji kitu kutoka Tanganyika ,Zanzibar kama unaijua historia yake basi huwezi kusema hivyo,Zanzibar imeuliwa na inazidi kuuliwa kiuchumi kwani njia zake zote kuu zimebanwa.
Mbona kuna nchi za Kiarabu kila mmoja na lake na mambo yao si mabaya wala hatujasikia kuzibiana mianya ya biashara.(U.A.E) ambao mafisadi wetu wamewapa kibali cha kuvuna mali ya asili hapo mbugani.
Madai ya Raisi wa Zanzibar kuwa makamo wa raisi wa Muungano hayana msingi,sidhani kama umefikiri vilivyo ,hio ni kifungu cha mwanzo kwenye hati ya Muungano ,je mlifanikiwa kukibadilisha au mizengwe ya Utawala wa Chama kimoja ? Fundi Mchundo usijaribu kugusa wala kukarabati mambo ya Hati ya Muungano yatakupiga na chini.bora ukimbilie kwenye Katiba viraka.
Unajua unapokuja Rais au Uraisi ,kama ukiangalia nchi nyingi siku hizi zinatumia Prime Minister na raisi anakuwa kama nembo ya Taifa kama walivyo wafalme wa Ulaya.Na kwa vile nchi hizi ni za Muungano basi raisi wa Muungano hatapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi,hilo litakuwa halipo.Na nafasi yake itachukuliwa kwa kupokezana kutokana na sheria zitazotungwa na kukubalika katika Katiba mpya ya Muungano na sio Katiba hii iliyojaa ufisadi wa kiongozi kuwepo juu ya sheria, mambo ya ukiritimba yatawekwa kando na kupata katiba msumeno.
Kugawana mbao sio jambo baya lakini hilo litaiathiri Tanganyika kuliko Zanzibar kwani stability ya Tanganyika ipo mikononi mwa Zanzibar.

Mwiba. Wewe ni shabiki na hamna jinsi ya kukufahamisha. Watu kama nyinyi ndiyo mnaochochea maandamano na vurugu lakini hamonekani mambo yanapoiva. Watanzania bara hawahitaji wazanzibari wawapiganie. Toka awali kila mkipigana, kuchinjana kimbilio lenu limekuwa bara. Sultan wenu alihifadhiwa na Nyerere wakati Kenya ilimkataa. Wakina Babu wote walipewa hifadhi na Nyerere. Nyerere na si Karume ndiye aliyedai kuwa Zanzibar ibakize identity yake. Sisi tulio bara kwa nia njema tumekubali identity ya utanzania. Hata hivyo, msidhanie hata siku moja kuwa bara watatoa machozi kama itaamuliwa kuwa kila upande uende inakojua. Kwetu sisi tofauti haitakuwa kubwa sana maana hatuna sehemu huko Zanzibar. Ni nyinyi ambao mmekuwa huru kuhamia, kuwekeza, kuoa, kulima na hata kugombea ubunge bara ndiyo mtakaoona tofauti. Ni nyinyi mtakaotakiwa kukabili tofauti zenu (mwarabu na mswahili, munguja na mpemba n.k) ndiyo mtakuwa na kazi. Kwa wengi wetu machogo tutapumua sigh of relief. Kama walivyosema wachina: kuwa mwangalifu unachomwomba mwenyezi maana anaweza akakupatia!
 
Kwako Fundi
Taifa, dola au nchi haziundwi kutokana na ndoto za mtu mmoja au watu wachache. Ili taifa litambulike kama taifa kunahitajika sifa maalum za lazima na sio za kulazimishwa, kuzushwa au kubuniwa. Kwa mujib wa sifa za kimataifa Zanzibar ni nchi na taifa kamili bila ya kujali nani ana au wanabuni vyenginevyo. Nchi yenye mipaka inayotambulika kimataifa na kuwa na watu wenye sifa maalum za nchi hiyo, kwa kusema lugha inayotambulika kuwa lugha ya au za nchi, yenye utamaduni, mila na kabila au makabila ya nchi hiyo, yenye jamii halisi na makhsusan, siasa inayoifuata na uchumi wake wa kujitegemea wenyewe, inatambulika kama nchi, aidha ikiwa huru au ikiwa imetawaliwa. Yaani kama Zanzibar ilivyokuwa chini ya ukoloni wa Kiingereza (na hata ukoloni wa sasa). Nchi kama hiyo ikiwa huru inatambulika na Umoja wa Mataifa kama ni nchi na taifa huru. Bila ya haja ya kukariri zaidi Zanzibar inazo sifa zote ambazo zinahitajika ili nchi itambulike kama taifa na nchi huru , pamoja na kuwa na kiti chake katika Umoja wa Mataifa, ambacho kipo wazi tokea kuundwa kwa Muungano katika mwaka wa 1964. Natumai unafahamu maana ya kuwa kipo wazi !!!

.....................Tanzania si nchi bali ni taifa la kubuni, kama nchi ya ndotoni na sio nchi au taifa halisi kwa mujibu wa tafsiri za kimataifa zinavyotambulika. Tanzania si nchi wala dola moja, bali ni Muungano wa nchi mbili huru, mataifa mawili huru na madola mawili huru, zote mbili zilikuwa na uwakilishaji katika Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Madola. Zote mbili zikiwa na kura sawa bila ya kujali ukubwa au idadi ya wananchi wake............ hayo hapo juu ni baadhi ya madondoo ya kitabu cha Zanzibar Dola, Taifa na Nchi Huru.

Tanganyika na Zanzibar ni nchi mbili tofauti kinyume na Vietnam, China-Hong Kong na Taiwan, Korea na Ujerumani zote ziligawiwa kuambatana na vita na njama za kikoloni na kibeberu. Zanzibar haijawahi kuwa sehemu ya Tanganyika na kuunganishwa tena na sehemu ya nchi moja. Tofauti ya kugawiwa kwa lazima kwa hizo nchi nilizotaja hapo juu, Zanzibar kuambatana na mbinu za kikoloni na kibeberu ili lazimishwa katika Muungano. Huu haukuwa Muungano wa hiari baina ya watu wawili, na hata kama ungelikuwa wa khiari na nia njema, basi Zanzibar bado inatakiwa iwe na haki ya kujitoa katika huo Muungano pindi ikiona Muungano huo hauna maslahi na nchi yake na watu wake au inatakiwa kuwa na haki ya kubadilisha mfumo wa huo Muungano pindi ikiona mustakbal wa Zanzibar unaporwa . Leo Wazanzibari wanapotaka kulinda maslahi yao wanakemewa na kubwekewa, kwanini wanataka kutetea haki zao. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni mfano wa Mtawala na Mtawaliwa. Kwa hivyo ndugu zetu wa Tanganyika inabidi waelewe kwamba mtawaliwa sawa na mtumwa ana haki ya kujikombowa sio tu ikibidi bali ni wajibu wa lazima kama kufa. Vyombo vya Serikali na/au Chama tawala vinaweza kulazimisha watu wafuate na kutii fikra au sheria fulani. Wazanzibari hawawezi kulazimishwa kuamini fikra au sheria hizo za kubuni. Mzanzibari anaweza kwa muda fulani kulazimishwa kukariri kuwa Zanzibar si nchi lakini hawezi kulazimishwa kuamini na kukubali hivyo. Mzanzibari hawezi kuamini na kubururwa huku akinyoosha shingo kama n´gombe apelekwae machinjoni.

Ikiwa Mzanzibri kaweza kumtoa Mngereza mwenye nguvu mara dufu kushinda Mtanganyika hatoshindwa kumtoa mkoloni asiejitegemea binafsi. Kuna njia nyingi za mapambano ya kujikomboa, kwa mfano kuelekeza mapambano huko huko Bara na kudhoofisha kibri chao na kuna njia za kuendeleza mapambano hataa kama watazuia hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi, hata kama wakilifunga Baraza milele, jambo ambalo wameshaanza kulizungumzia.

Kulifunga Baraza la Wawakilishi ni kuwapa Wawakilishi uhuru wa kufanya kazi mitaani bega kwa bega na umma wote wa Wazanzibari, kuwatia imani Wazanzibari na kuwatayarisha kiitikadi na kimapambano. Kufyeka magugu ya Muungano na kutengeneza medani za kuirejesha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa.

Wazanzibari kukataliwa vibali vya Maandamano ni kuwazidi kuwatia mori wa kutumia mbinu kama zile za dhidi ya Muingereza za kufanya maandamano madogo madogo mengi kwa kuvaa sare za Zanzibar ni Nchi maharusini, kwenye beni, unyagoni, taarabuni, kwenye mashindano ya ngarawa, kucheza n´gombe, kwenye dhikiri n.k. Kutunga nyimbo, mashairi ya Zanzibar ni nchi. Kubandika makaratasi makutani, magarini, kwenye miti kudai uhuru na kura ya maoni. Kutawanya vidaka sauti vya "KIROBOTO" na kutunga kasseti nyengine za VIROBOTO. Kutayarisha mechi za mpira, mashindano ya baskeli kutetea maslahi ya Zanzibar ni nchi . Maandamano kama hayo hawataweza kuyazuia mradi kila siku kuna badilishwa mbinu na medani.
WaZanzibari weshakata kamba kazi kwenu waTanganyika kuwalea mafisadi mwisho watawageuza watumwa na kuwarudisha tulipotoka ,ni genge hilo epukaneni nalo ,CCM hawafai wameshapoteza dhamana ya uongozi wamebaki kuchumia matumbo yao tu,hawajali Chadema wala cha nani ,wanajiona wao tu ndio wenye hati miliki ya Tanzania ,kwa taarifa hapa tulipo ni katikati Zanzibar hiyoo na Tanganyika bado inasuasua,CCM wamekamatwa pabaya lazima waekwe pembeni kwa kuipapatua na kuwapapatua ndani ya Tanganyika waanze kukimbie kuelekea huko walikoweka vijisenti vyao sasa kama hujachukua chako mapemba ndio mbinde.. !

Unajua unapokuja Rais au Uraisi ,kama ukiangalia nchi nyingi siku hizi zinatumia Prime Minister na raisi anakuwa kama nembo ya Taifa kama walivyo wafalme wa Ulaya.Na kwa vile nchi hizi ni za Muungano basi raisi wa Muungano hatapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi,hilo litakuwa halipo.Na nafasi yake itachukuliwa kwa kupokezana kutokana na sheria zitazotungwa na kukubalika katika Katiba mpya ya Muungano na sio Katiba hii iliyojaa ufisadi wa kiongozi kuwepo juu ya sheria, mambo ya ukiritimba yatawekwa kando na kupata katiba msumeno.

Haujui unachozungumza. Nchini India kuna jimbo linaitwa West Bengal. Hili jimbo lina Chief Minister wake na serikali yake. Lina lugha yake, kibengali, ambayo ni tofauti na kihindi. Kwa muda mrefu limekuwa likitawaliwa na chama cha kikomunisti tofauti na nchi ya India. Kina mipaka yake na wananchi wake wanajitambua (identify) kama wabengali. Lakini hata siku moja hautasikia wakijiita nchi. Wakiwa nje wao ni raia wa India na si West Bengal.

Uchumi wa jimbo la California ungeifanya kama ingekuwa nchi kuwa moja ya nchi tajiri sana duniani. Lina mtawala wake, Gavana Arnold. Lina identity yake ( watu wa California wanajiona tofauti na watu wa Arkansas n.k). Lina sheria zake ambazo ni tofauti na za nchi ya marekani. Zina mahakama zake, polisi wake n.k. Lakini nako hautasikia mtu anajitambulisha ni raia wa California. Uraia ni wa nchi ya marekani, full stop. Kwa mantiki hiyo hawawezi kuingia mikataba na nchi nyingine au kujiunga na Umoja wa Mataifa au kuwa na mabalozi wake n.k.

Soverignty mnayoidai kwa kigezo cha kuwa nchi ni hiyo ya kuwapa mamlaka ya kutambuliwa kuwa mtofauti na nchi ya Tanzania. Kwa hali hiyo muweze kuingia mikataba na nchi nyingine, kujiunga na jumuia mnazotaka, kuwa na ubalozi na hatimae, ndiyo, uwezo wa kutangaza vita dhidi ya nchi nyingine. Hivi vyote ndivyo vinavyotofautisha utaifa na nchi na si hizo cultural issues ulizozingumzia. Kama alivyosema mwingine, mkipewa yote hayo basi hautakuwa muungano bali ushirikiano.

Kwa nini tumlipe na kumpa vibwagizo vyote Rais ambaye hana manufaa yeyote kwetu? Kama Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na full sovereignty, huyo Rais wa Tanzania atakuwa wa nini? Nchi zenye ceremonial President ni nchi ambazo the federal government ina nguvu. Nchi kama India, inajulikana wazi ni nani mwenye mamlaka kati ya prime Minister na Chief Ministers wa states. Prime Minister wa Great Britain ana nguvu kuliko viongozi wa serikali za Wales, Scotland na Northern Ireland. Mfumo wa kupokezana uongozi walijaribu Yugoslavia na wote tunajua hatma yake. Ukweli ni kuwa either tuwe na Muungano wenye strong federal government au kila mmoja achukue hamsini zake.
 
Mfanyabiashara mashuhuri Z'bar achochea ufa wa Muungano
Na Salma Said, Zanzibar

MFANYABIASHARA mashuhuri Zanzibar, Mohammed Raza, amewashauri Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka visiwani hapa, warudi makwao kwa vile hawaiwakilishi nchi.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Jeshi la Polisi visiwani hapa kupiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), yaliyotarajiwa kufanyika jana.

Raza alisema pia, wafanyakazi wote wa taasisi za Muungano wanaoiwakilisha Zanzibar katika serikali ya Muungano, wanapaswa kurudi nyumbani kwa vile visiwa hivyo siyo nchi.

Licha ya Raza kuwataka Wabunge wa Zanzibar kurejea kwao kwa hoja kuwa wanaiwakilisha Zanzibar, ukweli ni kuwa, Wabunge kutoka Zanzibar na Tanzania Bara huingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwakilisha majimbo yao.

Vile vile, kauli ya Raza ya kuwataka wafanyakazi wa taasisi za Muungano wanaoiwakilisha Zanzibar kurejea kwao haina ukweli wowote kwa kuwa hakuna wafanyakazi wanaotoka Zanzibar kuiwakilisha katika Muungano.

"Wabunge wote wa Zanzibar warudi makwao. Wasiende Dodoma. Kwa sababu hawawakilishi nchi pamoja na wafanyakazi wote wa taasisi za Muungano warudi kufanya kazi kwao hadi hapo itakapojulikana moja wapo kama ni nchi au si nchi,” alisema Raza, ambaye ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumzia kauli kwamba, wanaozungumzia Zanzibar ni nchi kuwa ni wahaini, Raza alisema Wazanzibari wote kwa sasa ni wahaini na wataendelea kuwa hivyo hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.

“Tunaambiwa Zanzibar siyo nchi. Je, mwaka 1964 Wazanzibari tuliuzwa kwa Watanganyika?” alihoji na kuongeza: “Tuambiwe basi kama tuliuzwa kwao.”

Raza, ambaye aliwahi kuwa Mashuhuri kwa Michezo wa Rais wa awamu ya tano Zanzibar, Dk Salmin Amour Juma, alisema kuitwa wahaini hakuwezi kuua mjadala huo kwani Wazanzibari wana machungu ya tangu kusainiwa kwa mkataba wa Muungano na waasisi wawili, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, ambao wote wameshafariki.

“Sisi Wazanzibari sote ni wahaini, nikiwamo mimi na tutaendelea kuwa wahaini kwa kusema Zanzibar ni nchi. Sote wahaini ndio na hilo tumethibitishiwa na Baraza la Wawakilishi kwamba, Zanzibar ni nchi na hakuna kitakachobadilisha hilo,” alisema.

Alidai, kuwa vikao vilivyofanyika kuidhinisha kwamba Zanzibar si nchi, havikuwa halali kwa kuwa havikupata ridhaa ya Wazanzibari.

“Vikao hivyo vilivyoidhinisha sio halali kwa sababu havikupata theluthi tatu ya Wazanzibari. Katiba lazima ipatikane kwa theluthi tatu ya Wazanzibari. Kwanza, hakuna mkataba ulioondosha Zanzibar kuwa nchi, hakuna makubaliano hayo, hakuna,” alisisitiza Raza.

Alisema Katiba ilivunjwa wakati wa kupitisha mabadiliko, ambayo yalimwondolea madaraka Rais wa Zanzibar asiwe Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa mabadiliko hayo hayajapata ridhaa ya Wazanzibari inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Alisema, wakati umefika kwa Wazanzibari kudai hati ya makubaliano ya Muungano ili kujua ukweli wa mambo, ambayo yameanza kutokota jikoni hivi sasa sambamba na kutaka kura ya maoni juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Alisema, makubaliano ya Muungano hayakuwa sehemu kubwa iibane sehemu ndogo wala Muungano haukuwa kwa mmoja mume na mwingine mke, bali ulikuwa kati ya nchi mbili zilizo huru zenye kujitawala, tena kwa muda maalumu na siyo milele.

“Hatukuungana kama mke na mume wala kama mkubwa na mdogo. Tumeungana nchi mbili huru na zenye kujitawala. Hatukuungana kama nchi hii ina watu wengi hii kidogo ahhh hapana,” alisema na kuongeza:

“Kama ni hivyo, basi tuachieni Wazanzibari tujitegemee kwa njia nzuri, tusije tukapigana mizinga, tusigombane. Tuachieni Zanzibar. Kwa nini mnatung'ang'ania?" alihoji Raza, ambaye katika siku za karibuni amelivalia njuga suala la Muungano bila kutumia vikao rasmi vya chama chake.

Alidai kuwa, umefika wakati kwa suala hilo kujadliwa na kupatiwa ufumbuzi wa haraka na hakuna suala la kudhibitiwa watu na kukemewa na lazima demokrasia ipewe nafasi yake.

“Matusi yamekuwa mazito mno. Mara tunaambiwa wimbo wetu wa taifa kama kwaya, mara rais wetu kama rais wa timu ya mpira, mara bendera kama ya

simba..ahhh! Tuheshimiane. Mambo ya kutukanwa hatutaki. Maneno yanayojitokeza hivi sasa, ni matusi kwa Wazanzibari wenzetu. Wajifunze lugha ya kusema na sio matusi,” alisema kwa hasira.

Raza, alisema mjadala kuhusu suala hilo, umekuja siku mbaya, ambayo CCM inateremka kilima, ambacho karibuni wananchi wataingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, ambao hautakuwa na Ilani wala sera kwa kuwa suala hilo litakuwa limewagawa wanachama, akiwamo yeye.

Aliwataka polisi kuacha kuingilia siasa, badala yake wafanye kazi zao za kulinda raia na mali zao, ikiwa ni pamoja na kuwapa haki Wazanzibari kufanya maandamano yao kwa amani, kwani hiyo ndio njia pekee ya kufikisha ujumbe kwa viongozi wao waliowachagua kwa kura.

Alipoulizwa kama wako tayari kupokea ushauri wa Raza, Mbunge wa Ziwani, Ali Said Salim (CUF), alisema hawawezi kurudi kwa vile wanachokiwakilisha bungeni, ni Zanzibar.

Hata hivyo, Salim, ambaye pia ni Naibu Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema kisiasa Zanzibar, ni nchi, lakini kikatiba ya Jamhuri ya Muungano, si nchi.

"Kama Zanzibar siyo nchi, Rais anawakilisha kitu gani? Hatuwezi kurudi kwa sababu tunawakilisha Zanzibar," alisema Salim.

Alisema anamshangaa Raza kuibuka leo wakati alipokuwa Mshauri wa Rais wa Zanzibar, aliridhia marekebisho ya Katiba, ambayo yalimwondolea madaraka Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, licha ya wapinzani kupinga suala hilo kwa nguvu zao zote.

Tuma maoni kwa Mhariri
 
Si unaona uwezo wake wa kuchambua mambo ulivyo mdogo? Yeye anadhani Wabunge wanaotoka Zanzibar wanaiwakilisha "nchi" yao kwenye Bunge la Muungano!
 
Back
Top Bottom