Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mh. Seleli amenifurahisha sana na kunielimisha vizuri sana jambo moja... pata hii!!!

"Hakuna Rais wa Zanzibar"
kuna
"Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar"
lakini kuna
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"


Someni kwa makini hoja hii, ina hekima kubwa sana!


 
Mh. Seleli amenifurahisha sana na kunielimisha vizuri sana jambo moja... pata hii!!!

"Hakuna Rais wa Zanzibar"
kuna
"Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar"
lakini kuna
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"


Someni kwa makini hoja hii, ina hekima kubwa sana!



..hiyo hoja imejaa dhuluma! kwa watanganyika na wazenj.
 
WanaJF,

Mimi si mwanasheria lakini napenda kujifunza elimu ya uraia... kuna anayeweza kutupatia kiapo cha Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kinakuwa vipi?.
 
Dar si Lamu,

Ni katiba ndugu yangu na hata wa Zanzibar wanamuita Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

sasa kama wewe unapinga wa Zenji wenyewe wanavyomuita na walivyojitungia basi waeleze kuwa WANAJIDHULUMU!!!

JF KWELI HUTOZWI KODI KWA KUTOFIKIRI au kufikiri!!
 
Zanzibar ni ndogo kuliko Wilaya ya Kinondoni interms of Population.

Wilaya ya Tarime ni tajiri kuliko Zanzibar!

Sio iwe mkoa iwe ni Wilaya, Pemba wilaya na zanzibar wilaya kuwe na mkoa wa Tanzania visiwani.
 
Makala yangu ya Raia Mwema kesho na ya kwenye Tanzania Daima zitaweka swali hili vizuri kwa sababu kuna watu wanawachezea watu wengi; I'm in line with Selelii than most people.

Watu wakisoma Ibara ya 1 hadi ya 4 ya Katiba ya Muungano wataelewa nini kinaendelea.

Kwa kifupi:

- Serikali ya Zanzibar ipo kwa sababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema iwepo
- Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yupo kwa sababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema awepo (bila ya hivyo hakuna Rais wa Serikali hiyo)
- Baraza la Wawakilishi lipo na Mahakama ya Zanzibar ipo kwa sababu Katiba ya Muungano inasema hivyo.
- Katiba ya Zanzibar ipo kwa sababu Katiba ya Muungano inatoa nafasi hiyo.

Haiwezekani mfunge ndoa halali halafu mmoja aendelee kudai bado yuko "single" ati kwa vile ana nyumba yake na akaunti yake na bado anatumia ubini wa baba yake!
 
WanaJF,

Mimi si mwanasheria lakini napenda kujifunza elimu ya uraia... kuna anayeweza kutupatia kiapo cha Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kinakuwa vipi?.

Kwanza anaapa kulinda Katiba ya Muungano, halafu Katiba ya Zanzibar...na majukumu yake yaliyowekwa na Katiba ya Zanzibar. Jamani serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni mojawapo ya serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
2. Pinda ni Waziri Mkuu wa Tanganyika na mambo ya Muunganosio Waziri Mkuu wa Zanzibar na hilo limeshathibitishwa na serikali ya Zanzibar yenyewe.

Rais wa Jamhuri anapokuwa hayupo, na Makamu wa Rais hayupo, ni Waziri Mkuu ndiye anayekaimu urais wa Jamhuri lakini sio Rais wa Zanzibar, wala Waziri Kiongozi, sasa inakuwaje tena Waziri Mkuu wa Jamhuri asiwe juu ya hao wakuu wa Zanzibar?

Katika mikutano ya kimataifa Tanzania huwa tun wakilishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri kwa niaba ya Muungano sio kwa niaba ya bara tu, lakini tunajua better kuwa sio lazima rais wa Zanzibar anaposafiri nje awakilishe matakwa ya Muungano, kwa sababu huwa hawakilishi anyways!
 
Rais wa Jamhuri anapokuwa hayupo, na Makamu wa Rais hayupo, ni Waziri Mkuu ndiye anayekaimu urais wa Jamhuri lakini sio Rais wa Zanzibar, wala Waziri Kiongozi, sasa inakuwaje tena Waziri Mkuu wa Jamhuri asiwe juu ya hao wakuu wa Zanzibar?

Katika mikutano ya kimataifa Tanzania huwa tun wakilishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri kwa niaba ya Muungano sio kwa niaba ya bara tu, lakini tunajua better kuwa sio lazima rais wa Zanzibar anaposafiri nje awakilishe matakwa ya Muungano, kwa sababu huwa hawakilishi anyways!

Mkuu Field Marshal ES;

Kwanza sahihisha hakuna Rais wa Zanzibar... bali Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar!

Pili, Nakubaliana na MMK kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni Serikali ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama zilivyo serikali nyingine nyingi za tawala za mikoa.
 
Inavyoelekea, tatizo kubwa tulilonalo wengi ni kutoufahamu MUUNGANO wenyewe ukoje, majukumu ya serikali zote mbili ni yapi, itifaki ya viongozi wa serikali zote mbili imekaaje,...
Mbaya kabisa ni pale ambapo wasomi wazuri kabisa wanaonekana kutojua muungano huu ni juu ya nini!
 
Kuita Zanzibar mkoa ni kutowatendea haki. Wao ni zaidi ya mkoa lakini si nchi kamili. Hili lilipotea nchi za Tanganyika na Zanzibar zilipoungana. Tatizo lililojitokeza linafanana kidogo na lililojitokeza Canada. Quebec wamepewa haki nyingi na kutambuliwa kuwa wao kama wazungumzaji wa kifaransa wana haki ya kulindwa kikatiba. Baadhi ya wakazi wa Quebec wakaona hiyo haitoshi wakawa wanadai mambo zaidi na kutishia kuwa wasipotekelezewa watajitoa kwenye muungano wa Canada. Ilifika mahali wenzao wakachoka wakasema kama wanataka kujitoa basi waende. Ikafanyika referendum ambapo kila pande (zinazotaka uhuru kamili na zinazopinga) zikajieleza kwa wananchi wa Quebec. Wananchi hao wakatambua kuwa Quebec si lolote nje ya Canada na referendum ikashindwa!

Wenzetu wazanzibari, hasa wale wenye sauti kali, wanaamini kuwa sehemu ya bara inawashikilia kwa sababu zao za kibinafsi. Wao wamebakia kuangalia mapungufu kwa upande wao bila kuangalia kama mwenzao anafaidika vipi. Hawaoni tatizo kwa haki za mtanzania bara kuminywa akiwa zanzibar wakati wao wanakuwa sawa na mtanzania yeyote wakiwa bara. Wanadai kugawana misaada sawasawa bila kuangalia mchango wa kila upande katika bajeti ya serikali ya muungano. Na mengine mengi. Mbaya zaidi ni wao kuona mkono wa bara hata katika matatizo ya kujitakia wenyewe. Mfano, walisema bandari yao inadumizwa na bara. Wakaachiwa, wameshindwa kuiendeleza, lakini bado wanaangalia kwa kijicho bandari za Mtwara, Tanga hata Kigoma!

Pamoja na kwamba itaniumiza binafsi nadhani imefika wakati hili suala liangaliwe kwa uwazi. Hao wasiotaka muungano (tofauti na wazanzibari wanavyoamini, wako watu wengi bara walio kwenye kundi hili) wapewe uhuru kunadi sera zao kwa wananchi na hali kadhalika wale wanaotaka Muungano uendelee. Ifanywe referendum kwa pande zote mbili na kama kuna upande mmoja utakataa muungano, tukae, tugawane tulichonacho kwa amani. Muungano ubaki ikiwa utakubalika na pande zote mbili. Na kwangu mimi, muungano ulio viable ni huu tulionao sasa hivi. Zaidi ya hapo tutakuwa tunajidanganya. Hatuwezi kufanya Zanziba kuwa mkoa kwa mabavu na wala hatuwezi kuwa na serikali tatu wakati constituent states zina full sovereignty. Haiwezekani. Labda kama pande zote mbili zitapunguziwa madaraka kwa kiasi kikubwa. Kitu ambacho watakataa.

Tuige mfano wa Czechoslovakia na sio Yugoslavia.
 
Mbunge Lucas Selelii jana ametoa mtazamo wake kuwa sasa imefika wakati Wazenji waache kulalamika kama vile wao ndo wanaonewa saana katika muungano huu. Akatoa tahadhari kuwa hata Wabara wana mambo mengi ambayo wamepoteza baada ya Muungano, lakini wanavumulia kwa kuwa ndo muungano unavyokuwa ikiwa ni pamoja na kupoteza serikali ya Tanganyika. Akasema kuwa hata kiitifaki, utaratibu wa sasa unaofanywa na Znz si sahihi, lakini Wabara wako kimya tu.

"Hivi mnadhani sisi hatujui kuongea au ni kitu gani hasa?" alisema jana Bungeni.

Akatoa hoja kuwa, anadhani sasa ama Muungano uvunjwe, jambo ambalo hata yeye halipendi, ama iundwe serikali moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mawazo haya yanashabihiana na mawazo ya G55, na hata leo Kasaka karejea maoni yao kuwa pengine sasa iundwe serikali moja tu, ili kumaliza choko choko.

Selelii akasema kuwa hata katiba ya nchi inaeleza wazi kuwa PM wa URT ndo mtendaji na kiongozi mkuu wa shughuli za URT. Katiba inaonyesha mipaka ya URT Zanzibar ikiwemo. Kwa msingi huu, Akaunga mkono kuwa ni wazenji ndo wanaotakiwa kumuomba radhi PInda na si Mwakyembe kuwaomba radhi wao.

Wote wawili wamesema kimantiki, katiba ya Zanzibar haiwezi kuwa juu ya katiba ya URT kwa sababu katiba ya Zanzibar imeundwa kwa katiba ya URT Ibara ya 102, inayotoa idhini ya kuundwa serikali ya zanzibar na katiba yake.

Sasa nadhani mjadala unaelekea kutamu. Ni dalili kuwa vuguvugu la muundo mwingine wa serikali linaibuka upya.
 
Hivi lucas ni nani katika tanzania mpaka anatoa mtizamo wake huo mtizamo wake ni kwa faida ya nani jimbo lake ? Hatuhitaji mtizamo wake kwa sasa , msimamo utakaofuatwa kwa masilahi ya wote ni ule ambao ulitolewa na waziri mkuu kwahiyo kila mtanzania awe na msimamo huo kama hana msimamo huo hana haja ya kusema chochote kuhusu muungano kwa kuwa hajui chochote wala lolote , poleni wenye misimamo na mitizamo yanu
 
Hivi lucas ni nani katika tanzania mpaka anatoa mtizamo wake huo mtizamo wake ni kwa faida ya nani jimbo lake ? Hatuhitaji mtizamo wake kwa sasa , msimamo utakaofuatwa kwa masilahi ya wote ni ule ambao ulitolewa na waziri mkuu kwahiyo kila mtanzania awe na msimamo huo kama hana msimamo huo hana haja ya kusema chochote kuhusu muungano kwa kuwa hajui chochote wala lolote , poleni wenye misimamo na mitizamo yanu

Lucas Selelii ni mwananchi na zaidi ya hapo ni mwakilishi wa wananchi bungeni na kwa hiyo ana kila haki ya kutoa maoni yake.Kama mbunge hawezi kutoa maoni yake nani ataweza?

Kusema "kila Mtanzania awe na msimamo wa Waziri Mkuu" ni collectivism ya hali ya juu, kama ni hivyo kwa nini tuna bunge basi? Si Waziri Mkuu angeamua mambo yote?

Kuna watu wanaoweza kupata courage ya kusema yasiyosemeka ambayo kila mtu anayajua, pointing out the proverbial elephant in the room, saying the emperor has no clothes while most praise his tailor.

Mr. Selelii is proving to be one of the last of this dying breed.
 
Kuanzishwe mjadala wa kitaifa hao viongozi wanaogopa nini?

kuna siri gani kama tunataka demokrasia ya kweli?

Basi tuamue kwa misingi ya sheria. Siri inayofichika ambao wengi hawaijui ni kwamba mwuungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa wa vyama viwili vya siasa TANU na ASP.

Na ahadi zilizokuwapo ni viongozi waanzilishi kurithiana katika madaraka hadi vizazi vyao ili muungano usife. Viongozi nje ya mduara huo walionekana wasaliti wataua mwuungano.Ndio maana hadi leo vizazi wa viongozi waanzilishi wanaandaliwa kushika madaraka.

Wakorofi kamw Shamhuna ni kumlundikia madaraka ili anyamaze na kujiridhisha uzao wake kamwe hautapata tena baraka za uongozi. Huo ni mfano wa kiini cha matatizo ya mwuungano. Hivyo wanaodai zanzibar ni nchi ni riski za kisiasa za kutaka madaraka zaidi maana waona kuwa miaka nenda rudi vizazi vya havita nufaika na uongozi mkubwa watabaki walewale waanzilishi wa mwuungano.

Kimsingi anayedai zanzibar ni nchi haswa akiwa mwana CCM basi huyo ni mnafiki wa chama chake hicho kwa kuwa nadani ya Chama cha CCM kuna taratibu zake za kufuata na haswa ukiwa kiongozi. Haiingii akilini kiongozi mkubwa wa Chama kutoa madai mazito hadharani. Wapeni urais kama watapiga kelele za zanzibar ni nchi maana sheria wanazifahamu fika. Kwa mtazamo wangu ni kuwa wanasiasa wa zanzibar wanaona kuwa serikali ya zanzibar inaendeshwa kiswahiba na kurithiana wao kwa wao hivyo wamechoka.

Sasa wafanyeje ni kuanzisha migogoro ya kisiasa watambulike pamoja na famili zao kama ilivyo kwa wengine. Lakini kwa umbumbumbu wetu ili kulindana hakuna anayeweza kusema waziwazi. Hivyo mimi naita unafiki wa kisiasa.
 
Rais wa Jamhuri anapokuwa hayupo, na Makamu wa Rais hayupo, ni Waziri Mkuu ndiye anayekaimu urais wa Jamhuri lakini sio Rais wa Zanzibar, wala Waziri Kiongozi, sasa inakuwaje tena Waziri Mkuu wa Jamhuri asiwe juu ya hao wakuu wa Zanzibar?

Katika mikutano ya kimataifa Tanzania huwa tun wakilishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri kwa niaba ya Muungano sio kwa niaba ya bara tu, lakini tunajua better kuwa sio lazima rais wa Zanzibar anaposafiri nje awakilishe matakwa ya Muungano, kwa sababu huwa hawakilishi anyways!

FIELD MARSHAL, Mbona unatudanganya. Akiwa Makamo hayupo madaraka huenda kwa Aidha Spika Wa Bunge au Jaji Mkuu na sio Waziri Mkuu.
 
Globarch hakuna haja ya mijadala - na anayetaka kuanzia mijadala atakuwa amevunja sheria waziri mkuu alishatoa tamko la serikali watanzania wote wafuate hilo asiyekubali basi yeye haitakii mazuri nchi hii , ni kama muasi na fisadi wa kisiasa na mwaka 2010 atakokoma
 
Kumbe hata sheria ya taifa letu huijui, kwamba huwezi kuwa waziri katika serikali ya bara wla visiwani, bila kuwa mbunge either wa kuchaguliwa na wananchi au rais, either wa bara au visiwani?

Shamuhuna ni mbunge, ndio maana akawa waziri, kwa hiyo mahali muafakapa ye kutoa kero zake on mungano ni kwenye bunge la jamhuri ambako ana haki kisheria ya kuingia kama mbunge an waziri na hasa Deputy Waziri Kiongozi,

Kwenda kuongelea kero zake za muungano, kwenye Baraza la Wa Wakilishi ambako wabunge wa bara hawako mandated kuhudhuria kisheria ni tabia mufilisi ambayo ndio hasa tunayoikataa hapa.

Unajua Mkuu inabidi suala ulijuwe ndipo ulitolee maelezo. Hivyo hujui kuwa Zanzibar kuna Wabunge na hawa hawachaguliwi kuwa Mawaziri wa SMZ na Wawakilishi ambao ndio wanaochaguliwa kuwa Mawaziri wa SMZ. Ni vitu viwili kabisa Bunge na Baraza la Wawakilishi na ni vitu viwili tofauti pia Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar. Hebu nifanye niwe mwalimu wako kwa masuala ya Zanzibar.
 
Kuita Zanzibar mkoa ni kutowatendea haki. Wao ni zaidi ya mkoa lakini si nchi kamili. Hili lilipotea nchi za Tanganyika na Zanzibar zilipoungana. .

Mzee nipe sababu kubwa tatu kwanini Unguja na pemba sio mikoa, sio za kikatiba nataka.

Angalia idadi ya watu
Uchumi
Eneo


Asante
 
Back
Top Bottom