Jana wakati rais wenu anaongelea swala la muungano,ingawa na yeye alikuwa akijichanganya ila nilihisi nini tatizo ingawa sina uhakika kama niko sahihi,mtasema.
Kuna hofu kubwa ya wazanzibar kuipoteza nchi yao katika muungano na hili ndo tatizo.Nina wasiwasi kuna uwezekano hata Karume original alipatwa na hofu hii kipindi anatakiwa kuiunganisha zanzibar na tanganyika.Inawezekana hofu hii inasababishwa na udogo wa nchi yao ukilinganisha na ukubwa wa tanganyika wakihisi kuwa wazanzibar watakuwa hawana chao kama nchi yao itamezwa ndani ya muungano.Inawezekana hii ikawa ndo sababu ya zanzibar kuachiwa serikali yao huku tanganyika ikimezwa ndani ya muungano,hapa ndipo zikazaliwa serikali mbili na hapa ndipo palipo na tatizo.
Sasa wakati wazanzibar wana chao,watanganyika hawana cha kwao,hii ikasababisha watanganyika waifanye serikali ya muungano kuwa yakwao.Si hivyo tu bali hata wazanzibar nao wakahisi serikali ya muungano haiwahusu sana kwa kujua wanayo ya kwao.Tabu inakuja pale kiongozi wa serikali ya muungano anaposimama na kuongelea suala la muungano,kama alivyosema kikwete jana"TUNAZUNGUMZA NAO"unashindwa kuulewa wao wakina nani? wao watanganyika? wao serikali ya muungano?Hapa ni vigumu kusema wao serikali ya muungano wanaongea na wazanzibar kuhusu muungano,bali hapa alikuwa anamaanisha wao watanganyika wanaongea na wazanzibar juu ya mstakabali wa muunagano. Kwa kuwa watanganyika walikosa jinsi ya kusema sisi pindi wazanzibar wanaposema sisi,ndipo walipoamua kuiteka serikali ya muungano ikawa yao watanganyika na hapa ndipo wazanzibar wanapokosa imani na muungano kwamba unawanyonya ingawa wanashindwa kukumbuka kwamba bara hawana serikali kama wao.Hivyo moja ya suluhisho la muungano ni kuhakikisha kuwa pande zote mbili zinapewa uwezo wa kutumia neno sisi au pande zote zinyimwe uwezo huo,na wala msije kusema hakuna haja eti kwa sababu bara wenyewe hawalalamiki kwa kuwaondolea msamiati wa sisi katika muungano wao na wazanzibar.Ni kweli hawalalamiki ingawa wanautumia msamiati huo huo tena kwa vitendo.na ukijaribu kuangalia kwa makini wanao lalamika sana kuhusu muungano ni wazanzibar hata Selelii halilisema hilo kwa sababu wanahisi hawatendewi haki katika muungano.
Sasa kwanza kuna haja ya muungano kuangaliwa upya,ingawa kuna wale kama akina seif khatibu wanojifanya kutokuona haja ya suala hili.Pili hakuna jinsi suluhisho ni moja kati ya mawili haya,kuwa na serikali tatu au serikali moja,HILO LA TATU SI ZURI KWETU SOTE.