Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Fundi Mchundo,

..waZanzibari wamezoea vya bure hao na wanatunyonya.

..Prof.Teddy Malyamkono, pamoja na wanazuoni wenzake, wameandika kitabu kinachochambua jinsi Zanzibar inavyoishi kwa kuomba-omba Tanzania Bara.

Sikonge,

..ZNZ wana wizara yao ya fedha na kila mwaka wana bajeti ya Serikali yao.

..jaribu kutafuta hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha ZNZ utaona kwamba wanapata misaada toka nje. labda hapa tuangalie misaada inayokwenda ZNZ, tulinganishe na idadi ya watu, tuone kama wanapunjwa.

..ZNZ ina mamlaka yake ya mapato, lakini sielewi ina kazi gani tofauti na TRA.

Jokakuu:

Mbona kila state hapa mtoni ina mamlaka zake za pesa? Suala hapa ni Tanganyika kutojua kulinda maslahi yake.
 
Tatizo ni kuwa Tanganyika hai-exist kama entity. Hata huko mtoni kuna federal budget. Ndio maana watengeneza magari Detroit walienda kubembeleza Washington na sio Lansing! Ndiyo maana Paulson ana nguvu kiasi hicho.

Katika mfumo wa sasa hakuna namna ambayo Tanzania Bara inaweza kulinda maslahi yake dhidi ya Zanzibar.
 
Tanzania Bara ina zaidi ya watu 34 Millioni na Zanzibar ina watu 1 Millioni. Ukipiga hesabu utaona kuwa hakuna Tanzania Bara inachotakiwa kulinda maslahi yake dhidi ya Zanzibar.

Hizi ni kelele tu. Na hata muungano ukivunjika leo bado tunakuwa kwenye big pile of sh1t.

Muundo mzima wa uendeshaji wa serikali kuu ya Tanzania hauna ufanisi wowote.

Naona mnatoa mifano ya Majeshi ya muungano kulinda Zanzibar. Lakini wakati huohuo mnataka waliosaini mikataba ya madini kwenda kusaini mikataba ya mafuta Zanzibar. Kwa maoni yangu naona waZanzibar wasimame tu na kutoipa ruhusa serikali kuu kujiingiza kwenye uwekezaji.

Unapotoa mfano wa Detroit ni lazima ueleze ukweli vile vile kuwa viwanda vingine viko katika majimbo mengine. Na uchimbaji wa chuma huko katika majimbo mengine. Hivyo kuzorota kwa viwanda vya magari Michigan kutazorotesha shughuli za kiuchumi sehemu nyingine.

WaZanzibar wakimiliki mafuta, wataongeza shughuli za kiuchumi zilizopo Zanzibar na Tanzania bara vilevile.

Na shughuli za kiuchumi ndizo zitakazofanya watanzania kulipa kodi na kuongeza mapato ya serikali kuu.
 
Kweli wajinga ndio waliwao! tunatafuta formula ya kugawana kabla kuthibitika kwa uwepo wa mafuta yenyewe talk abt kufanya baby shower kabla mtoto kuzaliwa!

Mr Reading atakuwa kushachukua mchuzi wake na he must be laughing all the way to the bank!

Mjinga ni wewe masatu
 
Yaani kweli mnataka tugawane gesi au mapato yake? Nijuavyo mimi gesi inayochimbwa haiuzwi nje bali inatumika kuzalisha umeme ambao hata wazenj wanafaidika! Huo umeme unaosema wazenj wananunua wanauziwa kwa bei ya chini kuliko gharama za uzalishaji wakati wenzao bara kila kukicha wanapandishiwa! Pamoja na bei nafuu, hawaishi kukopa. Sasa juu ya yote hayo unataka wapelekewe mitungi ya gesi!

Mapato yote haya (ya gesi, dhahabu, utalii n.k.) yanaenda chungu kimoja kuchangia bajeti ya serikali ya Muungano. Bajeti hiyo ndiyo inayolipia wanajeshi wanaolinda uhuru wetu (pamoja na Zenj), balozi zetu zinazotuwakilisha wote n a kadhalika na kadhalika. Bajeti hiyo ndiyo inayolipia madeni ambayo serikali ya muungano inadaiwa kutokana na miradi iliyofanyika kote. Mapato hayo ndiyo yanayoenda kuisaidia serikali ya Mapinduzi wanapokosa pesa za kulipia umeme na/au kuwalipa wafanyakazi wao. Leo mnataka tufanye biashara ya kishihiri kuanza kugawana mapato ya kila kitu kinachopatikana bara.

Serikali ya Mapinduzi je inatoa mchango gani katika serikali ya muungano ambayo yenyewe ni sehemu? Mbona siwasikii mkizungumzia kukatiwa sehemu ya mzigo wa madeni tunayodaiwa? Au mnaamini hiyo misaada yote ilikuwa ni grants? Hiyo misaada mara nyingi ilielekezwa kwenye maeneo ambao watoaji walipendelea. Leo ndugu zako waFinn wakiamua kutusaidia kwenye sekta ya maji Lindi unataka tuwaambie hapana lazima wawekeze na Pemba? Na waNorway wakiamua kuwekeza kwenye umeme Zanzibar tuwaambie hapana lazima wakaweke na Lindi? Kweli wenzetu hampendeki!

Kama kawaida Tz Bara hupenda kuwaburuza Zanzibar, ili mradi tu kutotoa sehemu ya mgao unaostahiki kwa SMZ.

Kuhusu kuuziwa umeme kwa bei nafuu inatokana na wingi wa umeme unaonunuliwa na SMZ toka huko Bara. Kumbuka kuwa SMZ kupitia shirika lake la umeme ni wateja wa jumla wa umeme na sio wateja wa rejareja... hivyo basi bei imepangwa kwa maana hiyo na sio vyenginevyo.

Hicho chungu cha Muungano kwa kweli kina sehemu ndogo sana kwa Tanzania Visiwani, Ni wizara zilizopo kwenye Muungano ukiondoa ya Mambo ya Ndani na ya Ulinzi, zilizobaki hazina manufaa ya moja kwa moja kwa maisha ya kila siku ya Mzenj, hivyo huwa wala hazionekani kama zipo. Wananchi wanahitaji kuwa na Afya njema na wanahitaji kupata Elimu bora na mambo mengine muhimu. Haya yote hufanywa na kwa kodi chache inayokusanywa huko Zenj ambayo vilevile TRA uimega na kuipeleka huko Bara.

Ni wajibu wa Tz Bara kuheshimu makubaliano ya mgao katika misaada ambayo inalenga Tanzania na sio Tanzania Bara. Visingizio vya utoa msaada wa mishahara kwa wafanyakazi wa SMZ visiwepo kwani haukuwa ni msaada bali ni mkopo na SMZ inajitahidi kuulipa kadiri inavyoweza kukusanya mapato yake. Tena ni vizuri ukakumbuka kuwa Mkopo wa mishahara toka BOT kwenda SMZ ilikuwa ni kipindi kile ambacho Nchi wahisani walipokataa kuitambua Serikali ya Mapinduzi.

Zaidi SMZ kwa haikupaswa kutoa chochote katika serikali ya Muungano, lakini hilo likaonekana na sasa TRA wamejaa tele Zanzibar wakikusanya kodi. Kumbuka kuwa SMZ nao wana vyombo vya kukusanya kodi. Hii ina maana kuwa Mzenj hulipa kodi kubwa kuliko Mtz Bara.
 
Kibunango,

..hiyo kodi wanayokusanywa na TRA huwekwa kwenye chungu cha muungano ambacho na nyinyi mpo.

..hapa labda ungetueleza TRA inakusanya kiasi gani ZNZ, halafu ulinganishe na kile inachokusanya Tanzania bara, na baadaye ktk mgao mnapata kiasi gani.

..sina uhakika kama ZNZ inachangia TRA kiwango kikubwa kuliko mkoa kama Mwanza, au Arusha.

..kodi zinazokatwa na TRA ni tofauti na zile za Zanzibar Revenue Board. kuwepo kwa vyombo viwili vya kukusanya kodi isiwe kisingizio cha kudai ZNZ wanalipa kodi kubwa zaidi.

Zakumi,

..naungana na wewe kupendekeza kwamba ZNZ waachiwe wachimbe mafuta yao. walioweka suala hili kwenye muungano nadhani wamewaonea.

..ikiwa mafuta yatapatikana ktk eneo la bahari ambalo tuna-share basi hapo itabidi tugawane mafuta, vinginevyo kila upande uchukue kilicho chake.
 
Ile mentality ya chako chetu na changu changu inaweza kuja kuwaumiza vibaya sana baadhi ya watu wa inji hii.
 
The Company will have to negotiate the terms of a Production Sharing Agreement (PSA) before any work can commence.
Oil seeps and surface slicks are well known on the surface of Lake Tanganyika whose South Block covers approximately 5,400 square kilometres. It forms part of the western arm of the 6,400-kilometre long East African Rift system as does Lake Albert

Hujajibu swali. Quantify it please, ni mengi in relation to what and who? Au in relation to having none? Najua kuhusu hiyo rift valley system, lakini mafuta yanayopatikana katika hiyo belt so far ni ya kubeep. Mafuta yaliyopatikana Uganda ni kiduchu mno. Gas iliyopatikana maeneo Ruvuma, nadhani ni couple hundred BCf, kitu ambacho hakitikisi masoko ya dunia wala chati za dunia.
Nimejaribu kuweka file hapa kuonyesha proven reserves, kuanzia mafuta mpaka gesi, ila nimeshindwa. Na hii ripoti ni ya BP. Hawa jamaa hawabeep (nenda website yao, search World Statistics au bonyeza BP Statistics). Personally nimedadisi katika makampuni mbalimbali na nimeona presentations sio chini ya 12 hivi karibuni, na hakuna hata anayeongelea East Africa, sana sana wanagusia Mozambique.
Na kama yangekuwepo kwa wingi, makampuni makubwa yangeshafika.

Kampuni haliwezi kufanya PSA bila ku-quantify kilichopo na return on investment. Kama mafuta yapo kirahisi hivyo, kwanini wanakimbilia brazil au north sea high temp deep water drilling? Kama wino unamwagika kwa 3% kwenye madini, we unafikiri kitu gani kitakuwa kimezuia biashara isifanyike Tanzania.

Swali ni je, wazanzibari wanajua nini??
 
Kibunango,

..hiyo kodi wanayokusanywa na TRA huwekwa kwenye chungu cha muungano ambacho na nyinyi mpo.

..hapa labda ungetueleza TRA inakusanya kiasi gani ZNZ, halafu ulinganishe na kile inachokusanya Tanzania bara, na baadaye ktk mgao mnapata kiasi gani.

..sina uhakika kama ZNZ inachangia TRA kiwango kikubwa kuliko mkoa kama Mwanza, au Arusha.

..kodi zinazokatwa na TRA ni tofauti na zile za Zanzibar Revenue Board. kuwepo kwa vyombo viwili vya kukusanya kodi isiwe kisingizio cha kudai ZNZ wanalipa kodi kubwa zaidi.

Zakumi,

..naungana na wewe kupendekeza kwamba ZNZ waachiwe wachimbe mafuta yao. walioweka suala hili kwenye muungano nadhani wamewaonea.

..ikiwa mafuta yatapatikana ktk eneo la bahari ambalo tuna-share basi hapo itabidi tugawane mafuta, vinginevyo kila upande uchukue kilicho chake.

Jokakuu:

Mara nyingi katika nchi za KiAfrika uvumbuzi wa commodities kama mafuta unaendana sana na serikali kuongeza matumizi ya miradi ya ajabu na watu kuacha kufanya.

Kwa mentality ya watanzania, mafuta yakiwa yanaingiza mapato basi wabunge wataomba kuwa na Hummers, wanafunzi vyuo vikuu watagoma kuomba ongezeko la posho. Rais atataka kuwa na Boeing yake.

Kwa upande wangu kama mafuta yanapatikana kati maeneo yaliopo Zanzibar, sioni sababu kwanini wasiachiwe.

Sio Zanzibar peke yake. Sehemu kubwa ya mapato ya madini yaliopo Mwanza, Shinyanga, Mara na mikoa mingine yabaki hukohuko na yatumike kama chachu za kuleta maendeleo.

Na hata huko Zanzibar mafuta yakipatikana Pemba, sehemu kubwa ya mapato iende Pemba.

Uchimbaji wa madini na mafuta unaleta utajiri na uharibifu wa mazingira. Waachiene wanaoharibiwa mazingira yao wachukue mshiko. Kama sehemu unayotoka haina rasimali hama ma katafute ulaji sehemu nyingine.
 
Tanzania Bara ina zaidi ya watu 34 Millioni na Zanzibar ina watu 1 Millioni. Ukipiga hesabu utaona kuwa hakuna Tanzania Bara inachotakiwa kulinda maslahi yake dhidi ya Zanzibar.

Hizi ni kelele tu. Na hata muungano ukivunjika leo bado tunakuwa kwenye big pile of sh1t.

Muundo mzima wa uendeshaji wa serikali kuu ya Tanzania hauna ufanisi wowote.

Naona mnatoa mifano ya Majeshi ya muungano kulinda Zanzibar. Lakini wakati huohuo mnataka waliosaini mikataba ya madini kwenda kusaini mikataba ya mafuta Zanzibar. Kwa maoni yangu naona waZanzibar wasimame tu na kutoipa ruhusa serikali kuu kujiingiza kwenye uwekezaji.

Unapotoa mfano wa Detroit ni lazima ueleze ukweli vile vile kuwa viwanda vingine viko katika majimbo mengine. Na uchimbaji wa chuma huko katika majimbo mengine. Hivyo kuzorota kwa viwanda vya magari Michigan kutazorotesha shughuli za kiuchumi sehemu nyingine.

WaZanzibar wakimiliki mafuta, wataongeza shughuli za kiuchumi zilizopo Zanzibar na Tanzania bara vilevile.

Na shughuli za kiuchumi ndizo zitakazofanya watanzania kulipa kodi na kuongeza mapato ya serikali kuu.

Utengenezaji wa magari ni mojawapo ya key industries za marekani ndiyo maana kuna watu wanadai kuwa ni lazima Federal Government iingilie tatizo hilo. Suala hapa ni potential ya ku-destabilize the macroeconomics za taifa zima. Ukubwa wa hiyo impact ndiyo inayoangaliwa. Kwa mfano, ingawa makampuni makuu ya magari ya kimarekani ( uzalendo ni sehemu muhimu katika ishu nzima) yako Michigan, suppliers wa sehemu tofauti za magari wanatoka sehemu kubwa ya nchi ya Marekani. Kuangauka kwa haya makampuni bila shaka kutakuwa na knock-on effect kwenye biashara ya hawa suppliers. Makampuni haya yana dealers katika sehemu kubwa tu ya Marekani hivyo kuanguka kwake kutawa-affect na wao pia. Tusisahau kuwa Research na development inayofanywa na makampuni haya ni sehemu muhimu ya teknolojia ya Marekani hasa ukizangatia kuwa serikali ya Marekani yenyewe haijihusishi kwenye R & D bali inanunua utaalamu huo kutoka katika makampuni binafsi. Ni makampuni haya ndiyo yanayotengeneza vifaa vya kijeshi n.k.

Ni sababu kama hizi ndizo zinazofanya suala la mafuta kuwa ni la national interest. Alaska na Lousiana ingawa wanayo mafuta hawawezi kufanya maamuzi ya wapi wayachimbe bila kupata baraka za serikali kuu. Alaska wangependa kuchimba katika mbuga zake (ANWR) lakini wanazuiwa na serikali kuu. Lousiana wasingependa kuchimba katika sehemu nyeti lakini serikali kuu hivi karibuni imerahisisha kufanya hivyo! Ingawa sasa hivi mgao kutokana na royalties zinazotokana na mafuta ya Alaska ni 90% kwa Alaska na 10% kwa serikali kuu, kuna pendekezo kuwa wakiruhusiwa kuchimba kwenye ANWR, mgao huo uwe 50-50. Lakini cha msingi hapa ni kuwa ingawa sehemu kubwa ya mapato yanaenda Alaska, maamuzi makuu kuhusu mafuta yanafanywa bunge la muungano na si la jimbo. Mafuta kwa jinsi hiyo ni suala la kitaifa na si la jimbo.

Kwa vile wajibu mkuu wa serikali ni kuhakikisha usalama na integrity wa taifa lake suala la mafuta duniani kote linabaki kuwa la serikali ( au bunge) kuu na si ya sehemu ya muungano. Makubaliano ya mgawanyo wa mapato ni suala lingine lakini maamuzi ya utafutaji, matumizi n.k. ni lazima yapate baraka ya serikali au bunge la taifa zima. Zanzibar kama sehemu ya Muungano haiwezi kuachiwa hili. Ikiachiwa, uwezekano wa athari kwenye utaifa wetu ni mkubwa. Kwa mfano, nchi nyingi zina strategic reserve za mafuta ambazo ni kwa ajili ya taifa zima. Zanzibar haiwezi kuachiwa kuwa na uamuzi wa mwisho wa kuchangia au la. Uamuzi huu ni lazima ufanywe katika bunge la muungano ambamo Zanzibar ina uwakilishi tayari. Mapato kutokana na mafuta haya yatakuwa na impact kubwa katika uchumi wa taifa nzima kwa ujumla kwa hiyo ni lazima bunge la muungano lihusishwe na serikali ya muungano ipate sehemu ya mapato hayo. Maamuzi haya hayawezi kuachiwa baraza la mapinduzi ambamo serikali ya Muungano haina uwakilishi.

Wazenj wanasema hawafaidiki kutokana na madini yanayopatikana bara. Wanachosahau ni kuwa bajeti nzima ya serikali ya Muungano inapitishwa na bunge la muungano ambamo wao wana uwakilishi mkubwa. Kama wanaona wanapunjwa basi humo ndimo mwa ku-raise ishu nzima na si kwengineko.

Njia pekee ambayo Zanzibar wanaweza kuwa na milki kamili (100%) juu ya mafuta ni kujitoa kwenye Muungano. Wangali wakiwemo inabidi wakumbuke kuwa wao ni sehemu wa JMT na si taifa huru.

Mwisho, sijakuelewa ulipohusisha JWTZ na kusaini mikataba wa mafuta? Kwani kinachozungumziwa hapa ni kusaini mikataba au suala la mafuta kuwa sehemu ya masuala ya Muungano? Mandate ikishatoka kwenye bunge la Muungano, basi utekelezaji unaweza kufanywa na yeyote anayestahili. Bila shaka kama mafuta yako Zanzibar basi watekelezaji watakuwa ni wazenj. Yakiwa Mkuranga, basi watekelezaji watakuwa hao wa serikali ya Muungano.

Amandla.....
 
Fundi Mchundo:

Samahani kusema kuwa mpaka sasa unabwabwaja tu. Mifano yote uliyotoa kuhusu uchumbaji wa mafuta Marekani si sahihi.

Federal Government imeweka sheria nyingi kuhusu uchimbaji wa mafuta huko Alaska, California, FL na majimbo mengine hili kulinda mazingira na sio umilikaji wa investments zenyewe.

Hapa alizungumziwi swala la mazingira. Linazungumziwa suala la investment. Ni nani amiliki investments ya uchimbaji wa mafuta.

Vilevile huko off-point. Kuna migodi mingapi ya dhahabu na hakuna ata mgodi mmoja serikali ya Tanzania inayomiliki kwa 100%. Kwa mtaji huu Zanzibar hata ikiwa nje ya muungano haiwezi kumiliki 100%. Investment yoyote inamilikiwa na wadau na wadau wana asilimia fulani za share zao.

Vilevile ni lazima turudi kwenye muundo wa Muungano wenyewe. Tumeungana katika mambo matano. Mambo ya mafuta au investments hayamo.

Kwa maoni yangu binafsi, watu mnaona kuwa upatikanaji wa mafuta utakuwa ni short cut ya maendeleo. Ukweli wa mambo ni kuwa maendeleo hayana short cut.

Nchi za Asia tiger zimefanya vizuri bila kutegemea raslimali. Na kuna nchi nyingi tu zenye rasilimali na zina maisha mabaya kupindukia.

Na ufundi wako mchundo angalia mazingira na vitu gani unaweza kuvivuna katika mazingira yako. Ni aibu kuwa na elimu na bado kuona ndoto kwa vitu vinavyopatikana sehemu nyingine wakati mazingira yako yamejaa raslimali mbalimbali za kukusaidia.
 
[/QUOTE
Wewe Fundi , Khee!!! Fundi gani wewe. Fundi mchofu. Dawa sio kujitoa . Turekebishe mambo na tuende kwa muruwa. Long live the United Republic of Tanzania.
 
Bila samahani. Kwani nikibwabwaja nisisahihishwe.

Naona sikujieleza vizuri. Serikali ya marekani haina kawaida ya kumiliki investment. Kazi hii wameiiachia sekta binafsi. Umiliki ninaozungumzia mimi ni wa broad sense, mathlani kuweka sheria kuu zinazoongoza sekta muhimu. Kwa mfano, ingawa serikali ya marekani haina hisa kwenye makampuni ya biashara, wakati wa vita baridi waliweka miongozi ku-limit ushirikiano/uhusiano wa kibiashara kati ya makampuni haya na nchi za magharibi. Uamuzi na uwezo wa kumuelekeza mwekezaji yeyote bila kumiliki unabaki wa bunge kuu (Congress) na sio serikali ya state. Regulations za Federal Government zinaongozwa na sera zinazoandaliwa na Congress. Si siri kuwa George W ( na Stevens na Sarah) angependa kuchimba mafuta katika ANWR lakini Congress ndiyo iliyozuia. Angalia kuwa natofautisha bunge na serikali kuu. Bunge haliwezi kumiliki mali kama ambavyo serikali inaweza ikitaka. Tumeyaona haya katika matatizo ya mashirika ya fedha ya hivi karibuni.

Vile vile, mapato ya serikali katika shughuli hizi mara nyingi ni kutokana na kodi, royalties na concession rights. Kumiliki si lazima. Sidhani kama serikali ya Alaska ina hisa katika makampuni yanayochimba mafuta kule. Sisi, tuliobaki na mawazo ya kijamaa, ndiyo tunaodhani kuwa ni lazima kuwa na hisa. Down side ya kuwa na hisa ni kuwa unashindwa ku-regulate maana tayari umeishaingia kitandani na mhusika!

Tukija kwenye hili suala la Zanzibar na mafuta, kinachodaiwa ni kufanywa suala hili ni la Muungano na si umiliki. Sidhani kama Zanzibar wanaweza kuikataza serikali ya Muungano kununua shares katika makampuni ya mafuta yatakayokuwa yanachimba huko kama serikali hiyo itakuwa na uwezo na nia. Hilo ni suala la biashara na halina matatizo. Linalozungumziwa hapa ni suala la siasa, nani mwenye mamlaka ya kutoa maamuzi na maelekezo kuhusiana na sekta ya mafuta. Maamuzi haya yafanywe na Baraza la Mapinduzi au bunge la Muungano? Kwa mtazamo wangu, katika strategic industry kama hii ni lazima maamuzi haya yafanyika katika mamlaka ya juu katika nchi yeyote ambayo nchini kwetu ni bunge la Muungano. Kwa maneno mengine policies zote zitakazoongoza sekta hii zitoke kwenye Bunge na si Baraza la Mapinduzi. Policies hizi zitahusu masuala ya mazingira, usalama wa taifa (makampuni yapi hayaruhusiwi ku-invest n.k) na kadhalika. Masuala ya umiliki yatatokana na majadiliano na wawekezaji na serikali husika, ya JMT na Zanzibar kama itakavyokuwa kwa mgawanyo wa mapato mengine (kodi, royalties n.k.).

Nakubali kuwa niliteleza nilipotumia neno miliki kwenye sekta ya madini na pale niliposema Zanzibar hawawezi kumiliki asilimia 100 ya mafuta yatakayopatikana huko. Nilichomaanisha ( na kama ungenisoma kwa makini ungenielewa) ni kuwa sera inayoongoza uchimbaji wa madini Tanzania bara ilitungwa na Bunge la JMT. Bunge hili lina mamlaka ya kutoa miongozo ya namna gani hayo madini yatakavyokuwa exploited. Kwa bahati mbaya sidhani kama hili linafanyika bali nao kama mlivyo wenzangu wanaangalia zaidi mapato na aina, matokeo na athari ya uchimbaji huo! Zanziba ikiwa nje ya Muungano, kupitia bunge lake, itakuwa na uwezo wa kuandaa ( kwa asilimia 100) sera za kuongoza utafutaji, uchimbaji na uuzaji wa mafuta haya bila kungojea baraka za chombo kingine. Ikiwa sehemu ya Muungano, sera hizi ni lazima zibakie mikononi mwa bunge la Muungano.

Vilevile ni lazima turudi kwenye muundo wa Muungano wenyewe. Tumeungana katika mambo matano. Mambo ya mafuta au investments hayamo.

Kwa maoni yangu binafsi, watu mnaona kuwa upatikanaji wa mafuta utakuwa ni short cut ya maendeleo. Ukweli wa mambo ni kuwa maendeleo hayana short cut.

Nchi za Asia tiger zimefanya vizuri bila kutegemea raslimali. Na kuna nchi nyingi tu zenye rasilimali na zina maisha mabaya kupindukia.

Ni kweli kuwa mafuta si panacea ya matatizo yetu. Hata hivyo, mafuta ni madini yenye uwezo wa kuwa na impact kubwa mno katika uchumi na stability ya nchi yetu. Mafuta si kama rasilimali nyingine. Kulikana hili ni kujidanganya. Mifano ya nchi kama Gabon, Equatorial Guinea, Great Britain iko wazi. Hauwezi kukana mchango mkubwa wa mafuta (na gesi) katika uchumi wa nchi za Urusi, Norway , za kiarabu n.k. Uwezekano wa kuharibikiwa upo ( Nigeria, Gabon, Equatorial Guinea) na kupata neema upo (Norway, U.A.E n.k.). Katika nchi zote hizi (ukiondoa pengine U.A.E. Sijui mahusiano ya nchi zilizomo), sera ya mafuta inaandaliwa na bunge kuu.

Naheshimu sana maendeleo yaliyopatikana Singapore, Thailand, Malaysia, South Korea na sasa hivi Vietnam, Cambodia n.k. Bila shaka kuna cha kujifunza. Lakini lazima tuangalie mazingira yao. Location yao katika major trade rout kutoka Japan kwenda nchi za Magharibi. Level ya maendeleo ( kielimu n.k.) waliyokuwa nayo baada ya ukoloni. Uhusiano wao wa kitamaduni ( wachina wa Singapore na wachina wa Hong Kong n.k.). Uko sahihi kabisa, hakuna shortcut kwenye maendeleo. Hata hao unaowataja hawana majibu yote. Tujifunze, si kwa hao tu bali hata kwa jirani zetu wa Botswana na Mauritius.

Na ufundi wako mchundo angalia mazingira na vitu gani unaweza kuvivuna katika mazingira yako. Ni aibu kuwa na elimu na bado kuona ndoto kwa vitu vinavyopatikana sehemu nyingine wakati mazingira yako yamejaa raslimali mbalimbali za kukusaidia.

Aliyekuambia Fundi Mchundo, msomi nani? Zanzibar si sehemu nyingine, ni part and parcel ya Muungano. Unless wewe, msomi, unajua otherwise?

Wewe Fundi , Khee!!! Fundi gani wewe. Fundi mchofu. Dawa sio kujitoa . Turekebishe mambo na tuende kwa muruwa. Long live the United Republic of Tanzania.

Mimi ni mchovu kweli! Anayetaka kujitoa nani? Sasa kama hayo mambo hayarekebishiki,au kama hamna nia ya kuyarekebisha, kwa nini tuendelee na Muungano? Kusema Long Live URT hakusaidii. Ni lazima pawe na nia thabiti na kuukubali Muungano kwa dhati. Kukubali huku ni pamoja na kukubali ku-sacrifice. Bila hiki tunajidanganya tu na ku-postpone the inevitable!

Naona, nimebwabwaja vya kutosha
 
Je umewahi kusikiliza hotuba hii ya Nyerere hapa kwa Nukta77? Anazungumzia jambo hili la Uzanzibari na Utanganyika. Bofya hapa
 
Utengenezaji wa magari ni mojawapo ya key industries za marekani ndiyo maana kuna watu wanadai kuwa ni lazima Federal Government iingilie tatizo hilo. Suala hapa ni potential ya ku-destabilize the macroeconomics za taifa zima. Ukubwa wa hiyo impact ndiyo inayoangaliwa. Kwa mfano, ingawa makampuni makuu ya magari ya kimarekani ( uzalendo ni sehemu muhimu katika ishu nzima) yako Michigan, suppliers wa sehemu tofauti za magari wanatoka sehemu kubwa ya nchi ya Marekani. Kuangauka kwa haya makampuni bila shaka kutakuwa na knock-on effect kwenye biashara ya hawa suppliers. Makampuni haya yana dealers katika sehemu kubwa tu ya Marekani hivyo kuanguka kwake kutawa-affect na wao pia. Tusisahau kuwa Research na development inayofanywa na makampuni haya ni sehemu muhimu ya teknolojia ya Marekani hasa ukizangatia kuwa serikali ya Marekani yenyewe haijihusishi kwenye R & D bali inanunua utaalamu huo kutoka katika makampuni binafsi. Ni makampuni haya ndiyo yanayotengeneza vifaa vya kijeshi n.k.

Ni sababu kama hizi ndizo zinazofanya suala la mafuta kuwa ni la national interest. Alaska na Lousiana ingawa wanayo mafuta hawawezi kufanya maamuzi ya wapi wayachimbe bila kupata baraka za serikali kuu. Alaska wangependa kuchimba katika mbuga zake (ANWR) lakini wanazuiwa na serikali kuu. Lousiana wasingependa kuchimba katika sehemu nyeti lakini serikali kuu hivi karibuni imerahisisha kufanya hivyo! Ingawa sasa hivi mgao kutokana na royalties zinazotokana na mafuta ya Alaska ni 90% kwa Alaska na 10% kwa serikali kuu, kuna pendekezo kuwa wakiruhusiwa kuchimba kwenye ANWR, mgao huo uwe 50-50. Lakini cha msingi hapa ni kuwa ingawa sehemu kubwa ya mapato yanaenda Alaska, maamuzi makuu kuhusu mafuta yanafanywa bunge la muungano na si la jimbo. Mafuta kwa jinsi hiyo ni suala la kitaifa na si la jimbo.

Kwa vile wajibu mkuu wa serikali ni kuhakikisha usalama na integrity wa taifa lake suala la mafuta duniani kote linabaki kuwa la serikali ( au bunge) kuu na si ya sehemu ya muungano. Makubaliano ya mgawanyo wa mapato ni suala lingine lakini maamuzi ya utafutaji, matumizi n.k. ni lazima yapate baraka ya serikali au bunge la taifa zima. Zanzibar kama sehemu ya Muungano haiwezi kuachiwa hili. Ikiachiwa, uwezekano wa athari kwenye utaifa wetu ni mkubwa. Kwa mfano, nchi nyingi zina strategic reserve za mafuta ambazo ni kwa ajili ya taifa zima. Zanzibar haiwezi kuachiwa kuwa na uamuzi wa mwisho wa kuchangia au la. Uamuzi huu ni lazima ufanywe katika bunge la muungano ambamo Zanzibar ina uwakilishi tayari. Mapato kutokana na mafuta haya yatakuwa na impact kubwa katika uchumi wa taifa nzima kwa ujumla kwa hiyo ni lazima bunge la muungano lihusishwe na serikali ya muungano ipate sehemu ya mapato hayo. Maamuzi haya hayawezi kuachiwa baraza la mapinduzi ambamo serikali ya Muungano haina uwakilishi.

Wazenj wanasema hawafaidiki kutokana na madini yanayopatikana bara. Wanachosahau ni kuwa bajeti nzima ya serikali ya Muungano inapitishwa na bunge la muungano ambamo wao wana uwakilishi mkubwa. Kama wanaona wanapunjwa basi humo ndimo mwa ku-raise ishu nzima na si kwengineko.

Njia pekee ambayo Zanzibar wanaweza kuwa na milki kamili (100%) juu ya mafuta ni kujitoa kwenye Muungano. Wangali wakiwemo inabidi wakumbuke kuwa wao ni sehemu wa JMT na si taifa huru.

Mwisho, sijakuelewa ulipohusisha JWTZ na kusaini mikataba wa mafuta? Kwani kinachozungumziwa hapa ni kusaini mikataba au suala la mafuta kuwa sehemu ya masuala ya Muungano? Mandate ikishatoka kwenye bunge la Muungano, basi utekelezaji unaweza kufanywa na yeyote anayestahili. Bila shaka kama mafuta yako Zanzibar basi watekelezaji watakuwa ni wazenj. Yakiwa Mkuranga, basi watekelezaji watakuwa hao wa serikali ya Muungano.

Amandla.....
Ndugu yangu Fundi unaongea kama mtaalamu. Na mimi ukiwa Intellectual nakufamahu vizuri. Lakini kwa ndugu zangu wa kawaida hawafahamu ukisema mafuta yao mgawane, na almasi zenu -Wabara ziwe zenu. Hili jambo linahitaji ufafanuzi sana. Wataalamu nafikiri tushirikiane kuwafahamisha watu wetu.
 
Hehhehehheh, Hata wapeleke ripoti kwa Kissinger, mafuta ya zanzibar hayachimbiki. Bei ya nafuta imeanguka tena. Hizi ni ndoto za ma CCM, kibao kinawazunguka. waste of time.
 
Bei ya mafuta haijaanguka ila imeshushwa ili watu wapumue ni tactic zilizomiminwa katika hali ya uchumi , inayoendelea hivi sasa ndio pakasemwa kama una fedha ni wakati mzuri wa kununua na kuhifadhi,huu ndio wakati wa kununua na kuhifadhi ,ila endelea kubana matumizi.
 
Federal Government imeweka sheria nyingi kuhusu uchimbaji wa mafuta huko Alaska, California, FL na majimbo mengine hili kulinda mazingira na sio umilikaji wa investments zenyewe.

Hapa alizungumziwi swala la mazingira. Linazungumziwa suala la investment. Ni nani amiliki investments ya uchimbaji wa mafuta.

Federal Government (serikali ya George W) ingependa sana kuchimba mafuta yaliyopo kwenye ANWR. Na hata serikali ya jimbo la Alaska. Na hata aliyekuwa seneta wa Alaska. Ni Congress ndiyo inayotia ngumu. Chama cha Republicans kimeshindwa kuwavuta watu wakutosha kupitisha sheria ya kuruhusu uchimbaji huo.

Mjadala kuhusu uchimbaji wa mafuta katika sehemu nyeti hauhusu mazingira tuu bali zaidi ni security issue. Security, in the sense ya kuondoa kuwa tegemezi kwa mafuta yatokayo nje. Wanao-support uchimbaji katika sehemu hizo wanadai kuwa kuwa na secure source ya mafuta ina trump mambo ya mazingira. Wanaopinga, wanadai kuwa hayo mafuta yatakayopatikana yatapunguza kwa kiasi kidogo sana utegemezi kwa mafuta kutoka nje. Wao wanasisitiza kuwa badala ya kuchimba huko ni kutafuta njia mbadala na kuongeza efficiency ya vyombo vinavyotumia mafuta.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana nasisitiza kuwa taifa haliwezi kuachia maamuzi ya mwisho kuhusu mafuta yanayopatikana ndani ya mpaka wake yaamuliwe na sehemu moja tu ya Muungano. Maamuzi ni lazima yafanywe na bunge la muungano. Kudai kuwa mbona Zanzibar haifaidiki na gesi ni upuuzi maana hakuna serikali wala bunge la Tanzania Bara. Waziri kivuli wa wizara ya Nishati na Madini ni mbunge wa Mkanyageni (CUF) Mh. Mohamed Habib Juma Mayaa. Huyu ndiye anajukumu la kuangalia na kukosoa inapobidi jinsi serikali tawala ya JMT inavyoendesha shughuli zake katika sekta hii!

Sekta ya mafuta na gesi ni sekta sensitive mno na haziwezi kuwa nje ya Muungano. Au tuseme kwa vile sekta ya viwanda haimo katika masuala ya muungano basi Zanzibar wanaweza kujiamulia kujenga viwanda vya silaha kutosholeza soko la DRC bila kupata kibali cha Bunge la Muungano?

Tusijidanganye. Mafuta si Tanzanite au pamba.
 
Back
Top Bottom