Utengenezaji wa magari ni mojawapo ya key industries za marekani ndiyo maana kuna watu wanadai kuwa ni lazima Federal Government iingilie tatizo hilo. Suala hapa ni potential ya ku-destabilize the macroeconomics za taifa zima. Ukubwa wa hiyo impact ndiyo inayoangaliwa. Kwa mfano, ingawa makampuni makuu ya magari ya kimarekani ( uzalendo ni sehemu muhimu katika ishu nzima) yako Michigan, suppliers wa sehemu tofauti za magari wanatoka sehemu kubwa ya nchi ya Marekani. Kuangauka kwa haya makampuni bila shaka kutakuwa na knock-on effect kwenye biashara ya hawa suppliers. Makampuni haya yana dealers katika sehemu kubwa tu ya Marekani hivyo kuanguka kwake kutawa-affect na wao pia. Tusisahau kuwa Research na development inayofanywa na makampuni haya ni sehemu muhimu ya teknolojia ya Marekani hasa ukizangatia kuwa serikali ya Marekani yenyewe haijihusishi kwenye R & D bali inanunua utaalamu huo kutoka katika makampuni binafsi. Ni makampuni haya ndiyo yanayotengeneza vifaa vya kijeshi n.k.
Ni sababu kama hizi ndizo zinazofanya suala la mafuta kuwa ni la national interest. Alaska na Lousiana ingawa wanayo mafuta hawawezi kufanya maamuzi ya wapi wayachimbe bila kupata baraka za serikali kuu. Alaska wangependa kuchimba katika mbuga zake (ANWR) lakini wanazuiwa na serikali kuu. Lousiana wasingependa kuchimba katika sehemu nyeti lakini serikali kuu hivi karibuni imerahisisha kufanya hivyo! Ingawa sasa hivi mgao kutokana na royalties zinazotokana na mafuta ya Alaska ni 90% kwa Alaska na 10% kwa serikali kuu, kuna pendekezo kuwa wakiruhusiwa kuchimba kwenye ANWR, mgao huo uwe 50-50. Lakini cha msingi hapa ni kuwa ingawa sehemu kubwa ya mapato yanaenda Alaska, maamuzi makuu kuhusu mafuta yanafanywa bunge la muungano na si la jimbo. Mafuta kwa jinsi hiyo ni suala la kitaifa na si la jimbo.
Kwa vile wajibu mkuu wa serikali ni kuhakikisha usalama na integrity wa taifa lake suala la mafuta duniani kote linabaki kuwa la serikali ( au bunge) kuu na si ya sehemu ya muungano. Makubaliano ya mgawanyo wa mapato ni suala lingine lakini maamuzi ya utafutaji, matumizi n.k. ni lazima yapate baraka ya serikali au bunge la taifa zima. Zanzibar kama sehemu ya Muungano haiwezi kuachiwa hili. Ikiachiwa, uwezekano wa athari kwenye utaifa wetu ni mkubwa. Kwa mfano, nchi nyingi zina strategic reserve za mafuta ambazo ni kwa ajili ya taifa zima. Zanzibar haiwezi kuachiwa kuwa na uamuzi wa mwisho wa kuchangia au la. Uamuzi huu ni lazima ufanywe katika bunge la muungano ambamo Zanzibar ina uwakilishi tayari. Mapato kutokana na mafuta haya yatakuwa na impact kubwa katika uchumi wa taifa nzima kwa ujumla kwa hiyo ni lazima bunge la muungano lihusishwe na serikali ya muungano ipate sehemu ya mapato hayo. Maamuzi haya hayawezi kuachiwa baraza la mapinduzi ambamo serikali ya Muungano haina uwakilishi.
Wazenj wanasema hawafaidiki kutokana na madini yanayopatikana bara. Wanachosahau ni kuwa bajeti nzima ya serikali ya Muungano inapitishwa na bunge la muungano ambamo wao wana uwakilishi mkubwa. Kama wanaona wanapunjwa basi humo ndimo mwa ku-raise ishu nzima na si kwengineko.
Njia pekee ambayo Zanzibar wanaweza kuwa na milki kamili (100%) juu ya mafuta ni kujitoa kwenye Muungano. Wangali wakiwemo inabidi wakumbuke kuwa wao ni sehemu wa JMT na si taifa huru.
Mwisho, sijakuelewa ulipohusisha JWTZ na kusaini mikataba wa mafuta? Kwani kinachozungumziwa hapa ni kusaini mikataba au suala la mafuta kuwa sehemu ya masuala ya Muungano? Mandate ikishatoka kwenye bunge la Muungano, basi utekelezaji unaweza kufanywa na yeyote anayestahili. Bila shaka kama mafuta yako Zanzibar basi watekelezaji watakuwa ni wazenj. Yakiwa Mkuranga, basi watekelezaji watakuwa hao wa serikali ya Muungano.
Amandla.....[/QUOTE
Wewe Fundi , Khee!!! Fundi gani wewe. Fundi mchofu. Dawa sio kujitoa . Turekebishe mambo na tuende kwa muruwa. Long live the United Republic of Tanzania.