Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Wewe acha mambo ya udaku Bwana. Baraza la wawakilishi lina pahala pake pa kukutana napo ni katika Ukumbi wa Baraza la wawakilishi. Vyenginevyo linaweza kukutana pengine katika mfumo wa Semina maalum. Sasa kama wajumbe fulani binafsi umewaona Serena acha kukipakazia hicho chombo chetu tukufu -BARAZA LA WAWAKILISHI.

Baeleze haba batu ba bara..
 
NGOJA NIJITIE UWENDAWAZIMU kwa kumuuliza...
Shy, Source?
 
taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema bunge la wawakilishi znz lilikutana ghafla kwa kificho katika hotel ya serena zanzibar jana usiku , katika mkutano huo kulikuwa na wazungu kadhaa waliokuja na magari ya kufahari lakini wakaondoka na magari ya kawaida baada ya kuona watu wameanza kuwa na wasiwasi nao haijulikani walijadili nini katika mkutano huo inawezekana ni suala la muungano na mengine yanayohusiana mafuta

Heshima mbele mkuu; tafadhali tupe source & number of participants.
 
sio baraza la wawakilishi bali ni mawaziri ndio waliokutana na hao wazungu. Na watu wengi wanahisi ni issue ya mafuta - pengine wanataka iwe ya ZNZ peke yake kama zilivyo raslimali nyingi za Bara
 
Source ni mimi mwenyewe -- haya mmeridhika

one and only SHY in bongo Tz... nimekubali
haya mwaga data maana najua lazma kuna ukoko unatafunika ukiuweka hapa mkuu
 
bunge la wawakilishi znz lilikutana ghafla kwa kificho katika hotel ya serena zanzibar jana usiku , katika mkutano huo kulikuwa na wazungu .... inawezekana walijadilisuala la muungano na mengine yanayohusiana mafuta

Katika hali ya kufikirika kwanini umefikiria wazungu kujadili muungano na mafuta?
 
Katika hali ya kufikirika kwanini umefikiria wazungu kujadili muungano na mafuta?
Lakini Wazungu walijadili Muungano pale 1964 kabla ya kufanyika mwezi wa April. Na kama mafuta wao ndio wenye kumiliki data. Sasa huo mkutano siyo issue.La msingi ni kuwa maoni ya Wazanzibari ni kubaki na mafuta yao.
 
Ulipenda kutengeneze blogu ya uwongo niweke habari hii halafu nije kuweka link hapa ndio uamini ?
 
Lakini Wazungu walijadili Muungano pale 1964 kabla ya kufanyika mwezi wa April. Na kama mafuta wao ndio wenye kumiliki data. Sasa huo mkutano siyo issue.La msingi ni kuwa maoni ya Wazanzibari ni kubaki na mafuta yao.

kama wazungu wameanza kukutana kabla ya wazanzibar! Basi wazanzibar wakikutana itakuwa mchezo wa kuigiza
 
Date::4/15/2009
Waziri Himid:
Elias Msuya

Suala la mafuta limekuwa likijadiliwa kwa muda mrefu. Hoja inayogonga vichwa vya watu ni kama mafuta hayo yanufaishe pande zote za Muungano (Bara na Visiwani) au yabaki kuwa ya visiwani Zanzibar pekee.

Hivi karibuni Waziri wa maji ,ujenzi nishati na ardhi wa Zanzibar Mansoor Yusuf Himid akilihutubia Baraza la wawakilishi alilizungumzia suala hilo. Kwa kuanza Waziri Himid anaanza kueleza jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanza uchimbaji wa mafuta hayo,

"Tangu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzuia kazi ya Utafutaji Mafuta na Gesi asilia kwa Kampuni ya Antrim ya Canada mwaka 1997 licha ya kutolewa Leseni na TPDC kwa kazi hiyo katika eneo la Zanzibar, eneo la utafiti ambalo linahusisha maeneo ya Zanzibar kama yalivyoelezewa katika Katiba ya Zanzibar 1984, Sura ya Kwanza kifungu 2.(1), kumekuwa na juhudi kadhaa za Kidiplomasia na Kisiasa katika kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Kibali cha utafiti kwa eneo la visiwa vya Zanzibar na bahari iliyozunguka visiwa hivyo kilitolewa kwa TPDC katika mwaka 1997.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,TPDC na Kampuni ya Antrim ziliingia katika mkataba wa uchimbaji (Production Sharing Agreement) tarehe 29 Januari 1997 kwa mkataba ambao ulitengenezwa na Wizara ya Nishati na Madini (SMT).

Antrim kwa mujibu wa mkataba huo walitakiwa kuanza kazi za kukusanya taarifa za kitaalamu za mtetemo kwa kuhusisha eneo la kilomita 100 kisiwani Pemba, kilomita 100 kisiwani Unguja na kilomita 200 kwa eneo la baharini kwa gharama ya Dola za Kimarekani Milioni 3.5 kwa miaka miwili ya mwanzo kuanzia Aprili 2002 mpaka Aprili 2004.

Kwa kipindi cha miaka miwili mengine inayofuata kuanzia Aprili 2004 mpaka April 2006 walitakiwa wachimbe kisima cha utafiti wa mafuta kwa maeneo ya Kaskazini Pemba kwa gharama ya Dola za Kimarekani Milioni 4.

Kwa mujibu wa ramani ya eneo la utafiti huo (Antrim Block) vilihusisha Visiwa vyote vya Zanzibar na Bahari yake bila ya ridhaa na ushauri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.”

Kwa nini mafuta yalitolewa kwenye orodha ya mambo ya Muungano? Waziri Himid anasema,

"Baada ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzuia Kampuni hiyo kuanza utafiti huo kwa maeneo hayo, hatimae suala hili likawa ajenda mojawapo ya kikao cha kwanza cha kujadili kero za Muungano baina ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi.

Ndani ya Kikao hicho, msimamo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ukawa ni kuliondoa suala la Mafuta na Gesi asilia kutoka katika Orodha ya Mambo ya Muungano au kuyafanya madini yote kwa jumla kuwa ni ya Muungano.

Hata hivyo, katika vikao vilivyofuata, pande mbili hizi zikakubaliana kutafuta Mshauri Mwelekezi atakayezishauri Serikali zote mbili juu ya namna bora ya kugawana rasilimali hiyo. Kampuni ya AUPEC ya Uingereza ikashinda zabuni ya kufanya kazi hiyo.

Mshauri huyo alipewa hadidu za rejea zilizoridhiwa na pande zote mbili kama muongozo wa kukamilisha kazi hiyo, na Kampuni hiyo ilianza kazi tarehe 20 Juni 2007"

Pamoja na kumpata Mshauri huyo, bado ameonesha mapungufu kadhaa ambayo yamejitokeza katika utekelezaji wa kazi hii ya utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ndani ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, mambo ambayo zaidi yanaiathiri Zanzibar kimapato. Himid anaeleza,

"Japo kuwa TPDC (Tanzania Petroleum Development Corporation) lilianzishwa kwa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 May 1969 na Sheria ya Makampuni ya Umma ya 1969 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kurekebishwa na Sheria mpya ya mwaka 1992 inayotumika hivi sasa huko T/Bara na ambayo ilianzishwa kwa ina sura na tafsiri ya chombo cha Muungano kinachosimamia utoaji wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ushirikishwaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hususan kwa masuala yanayohusiana na mafuta na gesi asilia haupo. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawakilishwa na mjumbe mmoja tu kutoka Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi ndani ya bodi ya TPDC." anasema

Akielezea jinsi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakavyopoteza mapato kwa kuundwa kwa Taasisi mbili yaani Wizara ya Mafuta ya Muungano na TPDC, Waziri Himid anasema,

"Katika Ripoti hii Mshauri Elekezi anapendekeza kuundwa kwa Wizara itakayoshughulikia Mafuta chini ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii maana yake ni kwamba Wizara hiyo itakuwa na Makao Makuu yake Tanzania Bara kama zilivyo Wizara nyengine za Muungano.

Vyombo hivyo viwili pia ndivyo vitakavyokuwa na mamlaka ya kutoa leseni kwa makampuni mbali mbali yatakayojihusisha na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Zaidi ya hayo, suala hili la kuundwa kwa Taasisi mbili hizi na kuwa na sura ya Kimuungano zitainyima Zanzibar Mapato ya Mrahaba "Royalties" ambayo kwa mujibu wa taratibu yatatakiwa kulipwa katika taasisi inayosimamia usajili na utoaji wa leseni ambayo itakuwa ni Wizara ya Mafuta na TPDC.

Akieleza athari ambazo Zanzibar itazipata kutokana na kutopata kodi za mapato, kwa kutoshirikishi kikamilifu kwenye usimamizi wa mafuta hayo, Himid anasema,

"Kodi ya Mapato inayolipwa na Watu Binafsi na Mashirika ni suala la Muungano na linasimamiwa na Sheria ya kodi ya Mapato ya mwaka 2004. Kwa hali ya sasa hivi kwa mujibu wa Sheria hii, Mapato yanayotokana na kodi ya Mapato kwa upande mmoja wa Muungano yanapokusanywa huwa yanabakia katika sehemu ile ya Muungano .

Hivi sasa, kwa upande wa Mashirika kodi ya mapato kwa kampuni husika huwa inalipwa pale kampuni iliposajiliwa na yalipo Makao Makuu yake.

Kutokana na Mapendekezo ya Mshauri Elekezi ya kuundwa kwa Wizara ya Mafuta na TPDC kupewa mamlaka ya kusajili, kutoa leseni na usimamizi wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, Kampuni zote za uchimbaji wa mafuta zitasajiliwa na vyombo hivyo viwili na mapato yote ya kodi ya mapato kwa makampuni italipwa Tanzania Bara na hivyo kutokuchangia chochote katika Mfuko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kodi nyengine ya Mapato ambayo itakosekana kwa upande wa Zanzibar ikiwa Makampuni yatakuwa yanapewa leseni na kusajiliwa Tanzania Bara ni Kodi ya ufundi stadi (SDL) ambayo huwa inalipwa kila mwezi kwa mujibu wa asilimia ya mishahara ya wafanyakazi. Mfano wa Taasisi hizo ni BOT, JWTZ, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa" anasema.

Akieleza jinsi suala la mafuta lilivyoingizwa kwenye katiba, Waziri himid anasema,

"Suala la mafuta liliingizwa katika Katiba mwaka 1984 baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Sheria ya Mafuta ya mwaka 1980 inayosimamia Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia.

Hata hivyo ikumbukwe kwamba katika Mkataba wa muda wa Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar 1964, haikuhusisha kabisa suala la mafuta katika vipengele kumi na moja vya kushirikiana vya makubaliano hayo kama ifuatavyo:-

Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Serikali na vilivyotajwa kuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mambo ya Nchi za Nje, Ulinzi, Polisi, Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na Biashara ya Nje, Utumishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na Idara ya forodha, Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa Anga, Posta na simu.

Ni dhahiri kuwa suala la Mafuta na Gesi Asilia halikuwemo kabisa katika makubaliano ya Muungano ya mwanzo (matters within the first schedule to the Union Constitution)." anasema Waziri Himid.

Tuma maoni kwa Mhariri
 
kama wazungu wameanza kukutana kabla ya wazanzibar! Basi wazanzibar wakikutana itakuwa mchezo wa kuigiza
Mbona hueleweki? Hivi unataka kueleza nini?Hiyo story ya SHY anajua mwenyewe shy, Nilichojaribu kukutanabahisha ni maoni tu ya Wazanzibari. Hayo wanazungumza hivi sasa katika kila kona.
 
Ukiangalia hizi Articles of Union hapa chini, suala la mafuta halikuwa sehemu ya Mambo ya Muungano. Lakini katiba iliweka utaratibu wa kuingiza mambo ya muungano na mengine kuyaondoa kwa kuridhiwa na pande zote. Hivyo, tujadili:

-Utaratibu ulifuatwa kuingiza mafuta kuwa suala la muungano? Kama jibu ni ndio, kwa nini malalamiko sasa? Kama jibu ni hapana, kwanini?
-Je, kuna mambo gani mengine ambayo hayakuwepo katika mambo ya awali ambayo yameongezwa baadaye? je, mambo hayo yanafaida gani kwamba pande zote mbili? Nani ananufaika zaidi? Kwanini hayo nayo hayajadiliwi kuondolowe sambamba na hilo la mafuta?

Asha




THE ARTICLES OF UNION

between

THE REPUBLIC OF TANGANYIKA AND THE PEOPLES' REPUBLIC OF ZANZIBAR

WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar being mindful of the long association of the peoples of these lands and of their ties of kinship and amity, and being desirous of furthering that associatio! n and strengthening of these ties and of furthering the unity of African peoples have met and considered the union of the Republic of Tanganyika with the Peoples Republic of Zanzibar:

AND WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples'Republic of Zanzibar are desirous that the two Republics shall be united in one Sovereign Republic in accordance with the Articles hereinafter contained:-

It is therefore AGREED between the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar as follows: -

(i) The Republic of Tanganyika and the Peoples' Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.

(ii) During the period from the commencement of the union until the Constituent Assembly provided for in Article (vii) shall have met and adopted a Constitution for the united Republic (hereinafter referred to as the interim period) the united Republic

(i! ii) to (vi).

shall be governed in accordance with the provisions of Articles

(iii) During the interim period the Constitution of the united Republic shall be the Constitution of Tanganyika so modified as to provide for-

(a) a separate legislature and executive in and for Zanzibar from time to time constituted in accordance with the existing law of Zanzibar and having exclusive authority within Zanzibar for matters other than those reserved to the Parliament and Executive of the united Republic;

(b) the offices of two Vice-Presidents one of whom (being. a person normally resident in Zanzibar) shall be the head of the aforesaid executive in and for Zanzibar and shall be the principal assistant of the President of the United Republic in the discharge of his executive functions in relation to Zanzibar;

(c) the representation of Zanzibar in the Parliament of the United Republic;

(d) such other matters! as may be expedient or desirable to give effect to the united Republic and to these Articles.

(iv) There shall reserved to the Parliament and Executive of the united Republic the following matters-

(a) The Constitution and Government of the united Republic.

(b) External Affairs.

(c) Defence.

(d) Police.

(e) Emergency Powers.

(f) Citizenship.

(g) Immigration.

(h) External Trade and Borrowing.

(i) The Public Service of the united Republic.

(j) Income Tax, Corporation Tax, Customs and Excise.

(k) Harbours, Civil Aviation, Posts and Telegraphs.

And the said Parliament and Executive shall have exclusive authority in such matters throughout and for the purposes of the united Republic and in addition exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika.

(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject-

(a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

(b) to such provision as may be made by order of the President of the united Republic for the extension to Zanzibar of any law relating to any of the matters set out in Article (iv), and the revocation of any corresponding law of Zanzibar;

(c) to such amendments as may be expedient or desirable to give effect to the union and to these Articles.

(v) (a) The first President of the united Republic shall be Mwalimu Julius K. Nyerere and he shall carry on the Government of the united Republic in accordance with the provisions of these Articles and with the assistance of the Vice-Presidents aforesaid and of such other ministers and officers as he may appoint from Tanganyika and Zanzibar and their respective public services.

(b) The first Vice-President from Zanzibar to be appointed in accordance with the modifications provid! ed for in Article (iii) shall be Sheikh Abeid Karume.

(vii) The President of the united Republic: in agreement with the Vice-President who is head of the Executive in Zanzibar shall-

(a) Appoint a Commission to make proposals for a Constitution for the united Republic.

(b) Summon a Constituent Assembly composed of Representatives from Tanganyika and from Zanzibar in such numbers as they may determine to meet within one year of the commencement of the union for the purpose of considering the proposals of the Commission aforesaid and to adopt a Constitution for the united Republic.

(viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

IN WITNESS WHERE Julius K. Nyerere, the President of the Republic of Tanganyika, and Abeid Karume the President of the Peoples' Republic of Zanzibar have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April, 1964.

Passed in the National Assembly on the twenty-fifth day of April, 1964.
 
Suala la mafuta linazungumzika. Na linahitaji mazungumzo ya kina na tafakuri ya ndani. Tumeshasikia jazba (maoni mbali mbali-lakini yote ni yenye mantiki) nafikiri ni vyema ukafanywa machakato wa dharura hivi sasa kulizungumzia suala hili.
 
Article za Muungano siyo Msahafu. Hivyo hatuwezi kubaki na zile zile tu walizopeana Nyerere na Karume. Na tulizajidili sasa kulingana na mazingira yetu Tuzipunguze na tuziongeze. Mazingira yanaashiria kuwa mafuta hayatakiwi kuwa katika Muungano.
 
Back
Top Bottom