Mimi sijasema wanzanzibari sio watu safi, mimi sitaki muungano wa hivi hauna faida yoyote kwetu. Nilichokiongea hapo maana yake ni hii: Unapoongelea Tanzania, na wanzanzibari pia wapo ndani yake kwasababu Tanzania ni muunganiko wa Tanganyika na Zanzibar hivyo chochote cha Tanzania wanzanzibari ni chao pia ndomana wao huku wana haki zoote hata kugombea uongozi wowote ule. Unapoiongelea Zanzibar ni ya wanzanzibari tu wewe unayetoka bara huwezi kwenda kugombea uongozi Zanzibar huruhusiwi hata kumiliki ardhi hauwezi, na hata ukimiliki utamiliki kama raia wa kigeni anavyomiliki sio kama mzanzibari. Sasa huu ndo muungano gani?