Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
shy wee endelea tu kubwabwaja sisi tunajua nini cha kufanya and time will tell
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Serikali ya mseto yanukia Zanzibar
*Mazungumzo ya mwafaka yakamilika
*Uamuzi kutagazwa hivi karibuni
Na Muhibu Said
MPASUKO wa kisiasa visiwani Zanzibar huenda ukabaki kuwa historia baada ya vyama vya CCM na CUF kufikia makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo, ifikapo Agosti, mwaka huu.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam wiki iliyopita na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kamati za mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mpasuko wa kisiasa visiwani humo, zinadai kuwa tayari vyama hivyo vimeshatiliana saini makubaliano ya kuundwa kwa serikali hiyo.
Inadaiwa kuwa vyama hivyo vilitiliana saini makubaliano hayo siku chache kabla ya kamati hizo kukutana mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita kuendelea na mazungumzo hayo.
"Kinachofanyika Dodoma, ni kukamilisha mambo madogo madogo katika mazungumzo yaliyokuwa yamebakia ," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hizo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, wiki iliyopita alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa, kilichotarajiwa kufanywa na kamati hizo katika vikao vyake mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ni kufikia makubaliano ya mazungumzo hayo.
Kwa mujibu wa mjumbe huyo (jina tunalo), uundwaji wa serikali hiyo, maarufu kama "serikali ya mseto", utatanguliwa na kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kitakachokuwa na jukumu moja la kupitisha sheria ya kuundwa kwa serikali hiyo.
Alisema kikao cha baraza hilo, kimepangwa kufanyika baada ya kikao chake cha sasa cha kujadili mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kumalizika mwezi ujao.
Mjumbe huyo alisema miongoni mwa sababu zilizofanya vyama hivyo kutiliana saini makubaliano hayo kabla ya vikao hivyo vya Dodoma, ni pamoja na mshituko alioupata Rais Jakaya Kikwete aliporejea safarini hivi karibuni.
Alisema Rais Kikwete ambaye awali aliagiza mazungumzo hayo yasizidi vikao vitano, alishituka baada ya kusikia kuwa hadi sasa bado hayajaisha.
Sababu nyingine, inadaiwa kuwa inatokana na juhudi za upande mmoja wa mazungumzo hayo kuweka sawa hali ya hewa inayodaiwa kuchafuliwa na matamshi ya Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, alipotembelea kisiwani Pemba mwezi uliopita.
Akiwa kisiwani Pemba mwezi uliopita, Makamba alikaririwa akisema kuwa aliyeshinda kihalali katika Uchaguzi Mkuu Zanzibar Oktoba 30, 2005, ni Rais Amani Abeid Karume na kwamba rais huyo hawezi kuondoka madarakani kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 na wala hakutaundwa serikali ya mseto visiwani humo kwani haiwezekani timu ya Yanga ikaichia ubingwa wake Simba.
Matamshi hayo yalizua tafrani kati ya wafuasi wa CUF wakiongozwa na baadhi ya wabunge na viongozi waandamizi wa chama hicho waliotishia kuanzisha uasi ndani ya chama endapo wajumbe wa kamati ya mazungumzo kutoka CUF wangeendelea kushiriki mazungumzo hayo, kwa madai kwamba hawaoni tena faida ya chama chao kuendelea kushiriki mazungumzo hayo.
Pia baadhi ya wafuasi wa chama hicho Zanzibar, walisambaza vipeperushi kulaani matamshi hayo ya Makamba na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati suala hilo ili kulinda amani na utulivu nchini.
Hata hivyo, hali hiyo ilizimwa baada ya Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho taifa kulaani matamshi hayo ya Makamba na kumtaka Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kutoa ufafanuzi iwapo matamshi hayo ni ya Makamba binafsi au ni msimamo wa chama hicho.
Pia Baraza Kuu liliwaomba wafuasi hao kuwa na subira na wayape nafasi mazungumzo hayo yaendelee ili kuona dhamira na malengo ya CCM katika mazungumzo hayo.
Makubaliano hayo yanatokana na mazungumzo hayo yaliyovihusisha vyama hivyo kwa lengo la kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko huo.
Mazungumzo hayo yanayofanywa na kamati hizo chini ya uongozi wa makatibu wakuu wa vyama hivyo, Makamba (CCM) na Maalim Seif Shariff Hamad (CUF), yamedumu kwa zaidi ya miezi sita. Yalianza kisiwani Zanzibar Januari 16, mwaka huu.
Hata hivyo, hadi jana hakuna kiongozi yeyote wa vyama hivyo aliyekuwa tayari kuzungumzia hatima ya mazungumzo hayo.
Wiki iliyopita Lipumba alipoulizwa, alisema jukumu hilo wameachiwa makatibu wakuu wa vyama hivyo ambao kwa nyakati tofauti walikaririwa wakiahidi kutoa taarifa rasmi ya pamoja baada ya mazungumzo hayo kuisha.
mie bado sijaamini hadi nione
maana kwa kweli kule kwetu kuna kazi kuna siasa mbili kuna siasa ya wazi na ya siri.
mie nnakwambieni zanzibar kuna siasa ya aina yake na mtu hawezi kuijua hadi awepo zanzibar na hasa katika kipindi cha uchaguzi.
lkn kama kuna jambo ambalo nitalifurahia na kuhisi hasa matunda ya muungano ni kumaliza matatizo ya zanzibar na kutufanya alau na sisi tupumue.
maana inatosha tena, nnachoka hasa kila nikifikiria tulivyo, mungu wabariki watanzania mungu wabariki wazanzibari
Nakuunga mkono muungwana mwenzangu lazima zanzibar tuiokoe. Tumetumiliwa sana ili tugombane wenyewe kwa wenyewe kama wapalestina, ila sasa umefika wakati tuache u-CCM na u-CUF na tujali u-Zanzibari na mila za ki-Zanzibari. Vita vyetu wazanzibari ni vya panzi na wanaoneemeka ni kunguru.
Najali ubinadamu, Allah tuondoshee dhulma duniani, Allah tuondoshee dhulma Tanzania, Allah tuondoshee dhulma Zanzibar. Na kwa nguvu za mola inshallah Zanzibar itarudi kama zamani, iwe Zanzibar njema atakae aje. Ameen