Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
shy wee endelea tu kubwabwaja sisi tunajua nini cha kufanya and time will tell
 
Eti Third Force Theory ya Hayati Profesa Babu imeishia wapi? Can it be a solution to Zanzibar impasse? Nimewa-miss jamani
 
mie ningeomba kabla ya kuendelea nifahamishwe vyema hiyo theori maana siijui.

kisha nnaamaini nitakuwa mchangiaji mwema
 
Third Force in Zanzibar ilikuwa ni moja ya matoleo ya A. M. babu mara tu baada ya uchaguzi wa 1995 alipokuwa mgombea mwenza wa Mrema kupitia NCCR. Alikuwa anazungumzia solution ya matatizo ya Zanzibar .. ila sikupata kupitia toleo zima la machapisho yake.
Ila alizungumza ki-communist sana!
Ni vigumu ku-solve matatizo ya Zanzibar kwa itikadi za Kikomunist kama za Prof. Babu!
Mambo ya njozi... ila habari kwenye ground ni kinyume1
 
Serikali ya mseto yanukia Zanzibar
*Mazungumzo ya mwafaka yakamilika

*Uamuzi kutagazwa hivi karibuni

Na Muhibu Said

MPASUKO wa kisiasa visiwani Zanzibar huenda ukabaki kuwa historia baada ya vyama vya CCM na CUF kufikia makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo, ifikapo Agosti, mwaka huu.

Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam wiki iliyopita na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kamati za mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mpasuko wa kisiasa visiwani humo, zinadai kuwa tayari vyama hivyo vimeshatiliana saini makubaliano ya kuundwa kwa serikali hiyo.

Inadaiwa kuwa vyama hivyo vilitiliana saini makubaliano hayo siku chache kabla ya kamati hizo kukutana mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita kuendelea na mazungumzo hayo.

"Kinachofanyika Dodoma, ni kukamilisha mambo madogo madogo katika mazungumzo yaliyokuwa yamebakia ," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hizo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, wiki iliyopita alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa, kilichotarajiwa kufanywa na kamati hizo katika vikao vyake mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ni kufikia makubaliano ya mazungumzo hayo.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo (jina tunalo), uundwaji wa serikali hiyo, maarufu kama "serikali ya mseto", utatanguliwa na kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kitakachokuwa na jukumu moja la kupitisha sheria ya kuundwa kwa serikali hiyo.

Alisema kikao cha baraza hilo, kimepangwa kufanyika baada ya kikao chake cha sasa cha kujadili mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kumalizika mwezi ujao.

Mjumbe huyo alisema miongoni mwa sababu zilizofanya vyama hivyo kutiliana saini makubaliano hayo kabla ya vikao hivyo vya Dodoma, ni pamoja na mshituko alioupata Rais Jakaya Kikwete aliporejea safarini hivi karibuni.

Alisema Rais Kikwete ambaye awali aliagiza mazungumzo hayo yasizidi vikao vitano, alishituka baada ya kusikia kuwa hadi sasa bado hayajaisha.

Sababu nyingine, inadaiwa kuwa inatokana na juhudi za upande mmoja wa mazungumzo hayo kuweka sawa hali ya hewa inayodaiwa kuchafuliwa na matamshi ya Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, alipotembelea kisiwani Pemba mwezi uliopita.

Akiwa kisiwani Pemba mwezi uliopita, Makamba alikaririwa akisema kuwa aliyeshinda kihalali katika Uchaguzi Mkuu Zanzibar Oktoba 30, 2005, ni Rais Amani Abeid Karume na kwamba rais huyo hawezi kuondoka madarakani kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 na wala hakutaundwa serikali ya mseto visiwani humo kwani haiwezekani timu ya Yanga ikaichia ubingwa wake Simba.

Matamshi hayo yalizua tafrani kati ya wafuasi wa CUF wakiongozwa na baadhi ya wabunge na viongozi waandamizi wa chama hicho waliotishia kuanzisha uasi ndani ya chama endapo wajumbe wa kamati ya mazungumzo kutoka CUF wangeendelea kushiriki mazungumzo hayo, kwa madai kwamba hawaoni tena faida ya chama chao kuendelea kushiriki mazungumzo hayo.

Pia baadhi ya wafuasi wa chama hicho Zanzibar, walisambaza vipeperushi kulaani matamshi hayo ya Makamba na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati suala hilo ili kulinda amani na utulivu nchini.

Hata hivyo, hali hiyo ilizimwa baada ya Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho taifa kulaani matamshi hayo ya Makamba na kumtaka Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kutoa ufafanuzi iwapo matamshi hayo ni ya Makamba binafsi au ni msimamo wa chama hicho.

Pia Baraza Kuu liliwaomba wafuasi hao kuwa na subira na wayape nafasi mazungumzo hayo yaendelee ili kuona dhamira na malengo ya CCM katika mazungumzo hayo.

Makubaliano hayo yanatokana na mazungumzo hayo yaliyovihusisha vyama hivyo kwa lengo la kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko huo.

Mazungumzo hayo yanayofanywa na kamati hizo chini ya uongozi wa makatibu wakuu wa vyama hivyo, Makamba (CCM) na Maalim Seif Shariff Hamad (CUF), yamedumu kwa zaidi ya miezi sita. Yalianza kisiwani Zanzibar Januari 16, mwaka huu.

Hata hivyo, hadi jana hakuna kiongozi yeyote wa vyama hivyo aliyekuwa tayari kuzungumzia hatima ya mazungumzo hayo.

Wiki iliyopita Lipumba alipoulizwa, alisema jukumu hilo wameachiwa makatibu wakuu wa vyama hivyo ambao kwa nyakati tofauti walikaririwa wakiahidi kutoa taarifa rasmi ya pamoja baada ya mazungumzo hayo kuisha.

Souce: www.mwananchi.co.tz (25/6/2007)

NDOTO HIZI ZA MCHANA KWEUPE HAZIKOMI!

Makamba juzi tu kawasha moto; mwaka jana CCM Zanzibar nao wakasema Serikali ya Mseto si Sera ya CCM!

Kada mpinzani hebu tumegee; serikali ya mseto ni sera ya CCM?
 
mie bado sijaamini hadi nione

maana kwa kweli kule kwetu kuna kazi kuna siasa mbili kuna siasa ya wazi na ya siri.

mie nnakwambieni zanzibar kuna siasa ya aina yake na mtu hawezi kuijua hadi awepo zanzibar na hasa katika kipindi cha uchaguzi.

lkn kama kuna jambo ambalo nitalifurahia na kuhisi hasa matunda ya muungano ni kumaliza matatizo ya zanzibar na kutufanya alau na sisi tupumue.

maana inatosha tena, nnachoka hasa kila nikifikiria tulivyo, mungu wabariki watanzania mungu wabariki wazanzibari
 
Nakuunga mkono muungwana mwenzangu lazima zanzibar tuiokoe. Tumetumiliwa sana ili tugombane wenyewe kwa wenyewe kama wapalestina, ila sasa umefika wakati tuache u-CCM na u-CUF na tujali u-Zanzibari na mila za ki-Zanzibari. Vita vyetu wazanzibari ni vya panzi na wanaoneemeka ni kunguru.

Najali ubinadamu, Allah tuondoshee dhulma duniani, Allah tuondoshee dhulma Tanzania, Allah tuondoshee dhulma Zanzibar. Na kwa nguvu za mola inshallah Zanzibar itarudi kama zamani, iwe Zanzibar njema atakae aje. Ameen
 
under_age,

ameen.

Lakini kama alivyosema Mtu - mwitu hapo juu hizi habari usiziamini mpaka tuone hilo limetokea kweli na hata baada ya kutokea hilo vile vile usiwaamini ccm 100% kwani hawa watu ni wanafik (waliyoyaficha rohoni ni mabaya kuliko wanayoyasema).

Wanaweza wakakubali kila kitu na hiyo serikali ya mseto ikaundwa lakini usije shangaa ukaona ufisadi wa ccm uko pale pale - waogope ccm kama ukoma, roho zao ni mbaya kweli kweli.
 
Waziri Mwinyi adai serikali imeondoa kero
Na Ramadhan Semtawa, Dodoma

SERIKALI imeamka na kutangaza jinsi inavyotatua kero za muungano na kuanzia sasa misafara yote ya viongozi wakuu wa Jamhuri ya Muungano, kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi katika mambo ya kimataifa itakuwa ikijumuisha viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni moja ya mafanikio saba yaliyofikiwa katika vikao vinavyoendelea kati ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na mwenzake Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamshi Vuai Nahodha.

Mpango huo unalenga kuondoa malalamiko ya Zanzibar kutoshiriki katika mambo mbalimbali ya kimataifa hivyo kuonekana kama imetengwa.

Akijibu hoja ya kambi ya upinzani juzi jioni kuhusu kero za muungano zisizokwisha, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Dk Hussein Mwinyi, alisema tatizo kubwa la kambi hiyo ni kwamba haitaki kukubali mafanikio yaliyofikiwa katika kutatua kero za muungano.

Dk Mwinyi alisema katika kipindi cha mwaka mmoja, jumla ya mambo saba yamefikiwa katika hatua nzuri ambayo ni mafanikio yanayotokana na mazungumzo kati ya Lowassa na Nahodha.

"Katika kipindi cha mwaka mmoja, kumekuwa na mafanikio katika mambo saba, moja ni kwamba sasa hivi misafara yote ya kimataifa, iwe ni shughuli za AU (Umoja wa Afrika), sasa itakuwa na viongozi wa pande zote mbili," alifafanua Dk Mwinyi.

Alisema miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama ya kupeleka umeme, uboreshaji bandari, Zanzibar itaingizwa na kuongeza kwamba kuhusu Tanzania au visiwa hivyo kujiunga na Jumuiya ya Mataifa ya Kiislam (OIC), suala hilo bado

halijaamuliwa kwani bado linafanyiwa kazi.

Dk Mwinyi alitaja eneo jingine ambalo limetokana na mazungumzo hayo kuwa ni mgawanyo wa fedha, misamaha, misaada na faida ya BoT, kwamba limefikia katika hatua nzuri na sasa ipo kamati maalumu ya pamoja Joint Finance Commission (JFC), ambayo inashughulikia jambo hilo.

Alisema tayari waraka kwenda katika Baraza la Mawaziri la Tanzania bara umekwishaandaliwa na kuongeza kwamba ana matumaini hata Baraza la Mawaziri Zanzibar, liko katika hatua za mwisho kuandaa waraka unaohusu mapendekezo ya tume

hiyo.

Dk Mwinyi alitaja eneo jingine ambalo ni muhimu kwa uchumi wa Zanzibar ambalo limefikiwa makubaliano kwamba ni la uvuvi katika ukanda wa bahari kuu, ambapo sasa ipo mamlaka moja tu baada ya kutungwa sheria mpya ambayo sasa itavipa visiwa hivyo mgawo wa asilimia 20, bara asilimia 30 na zilizobaki kuendesha mamlaka.

Kuhusu eneo la mafuta, alisema mazungumzo hayo yamefikia hatua ya kutafuta mshauri

mtalaam kutoka katika nchi zenye umoja lakini ambazo zina mafuta, kama Uingereza, Canada na na Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE), kwani licha ya rasilimali hiyo kuwa nzuri kiuchumi lakini pia ni chanzo cha vita na mifarakano katika nchi zenye muungano.

Eneo jingine ambalo limefanikiwa ni kuhusu Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ambayo sasa itaweza kufanya kazi Zanzibar kwani awali sheria iliyounda ilikuwa haimtambui Waziri wa Utawala Bora wa visiwa hivyo.

Mafanikio mengine aliyotaja Dk Mwinyi ni miradi ya maendeleo ambayo pia inahusisha fedha za wafadhili kama Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Mpango wa Uboreshaji Kilimo (SDP) na Mpango wa Uboreshaji Elimu ya Msingi Zanzibar kama ule wa bara (MMEM).

Kuhusu eneo la kodi, alisema kinachofanyika sasa ni kuangalia jinsi ya kuweka uwiano wa viwango vya kodi kati ya pande mbili na kwamba suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na Wizara ya Fedha.

Mambo ambayo si ya muungano, alisema kinachofanyika ni kubadalisha uzoefu ambapo

sasa wizara 14 zimekuwa zikikutana kuangalia jinsi ya kuoanisha mitalaa ya shule.

Dk Mwinyi alikuwa akijibu mapigo ya kambi ya upinzani ambayo juzi mchana kupitia kwa msemeji wake, Riziki Omar Juma, ilibeza mazungumzo kati ya Lowassa na Nahodha na kusema viongozi hao hawapaswi kujifungia ndani peke yao kwani kero za muungano zinagusa wananchi wote.
 
Hivi kweli kero za Muungano zimemalizika? Je kweli kuna mafuta Zanzibar? Kama yapo mbona hatuyachimbi? Naona tutakuja gombani bure kwa ajili ya ndoto za Alinacha!!
 
mada hii ipo siku nyingi mbona MR zero ingependeza kuchangia kuliko kuduplicate mada.
just ni mtazamo tu
 
mada hii ipo siku nyingi mbona MR zero ingependeza kuchangia kuliko kuduplicate mada.
just ni mtazamo tu
 
Nilijaribu kuitafuta ile thread lakini naona iko mbali sana hivyo nikaona may be niintroduce tena. Maana nimechoka kuingia humu na kusoma ubishi kwamba JK ulikuwa wapi wakati AC anafariki.
 
Naona umeiduplicate the same story ikaipa new title halafu unanicritise. I really do not understand!!!
 
Kuna documentary moja inayokandia sana waafrika; inaitwa "Africa Addio- Farewell Africa." Documentary hii imehadithiwa katika lugha ya kigeni ambayo hata mimi sielewi ingawa baadhi ya vipande vyake viko katika kiingereza na kiswahili. Hata hivyo documentary yote ina sub-titles za kiingereza. Ingawa documentari hii inatukandia sana, mambo mengi yanayoongelewa yana ukweli wa namna fulani.

Ningependa uingalie na kama huna muda wa kutosha, basi angalia kipande kinachoanzia saa 1:00:26 hadi 1:06:00 ambacho kinahusu mapinduzi ya Zanzibar. Je ni kweli mapinduzi yale yalifanyika kama anavyodai msimuliaji?

Inapatikana hapa Google Video

Nilikuwa nimesahau kuwa siku Gavana wa mwisho (nadhani Richard Turnbull) anaondoka Tanganyika imeonyeshwa kuanzia 00:07:00 hadi 00:10:00
 
Mzee Kichuguu!
Nimeitazama hii documentary... inonekana ni ya zamani sana.. lakini dah!
Kuna kaukweli fulani ndani yake ingawa kwa kiasi kikubwa jamaa anatuona waafrika hamnazo!
kuna sehemu eti wana-supply nguo za ndani kwa wanawake wa kiafrika ili wawe kama wazungu!
???
 
I've seen it and will be back with my comments. For those who understand Italian language will be beneficial although its a mixture as Kichuguu said.
 
Back
Top Bottom