Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
kichuguu.hayo ulioyaona ni kweli kabisa na ndio hapo zanzibar ilianzisha ukurasa mpya wa chuki na ubaguzi,kwani ukirudi mwaka mmoja nyuma (disemba 1963)kabla ya mapinduzi utaona kwamba uingereza aliikabidhi zanzibar uhuru kamili ila aliowakabidhi serikali walikuwa ni wenye asili ya kiarabu
,hivyo huyo bwana john okello ambae tukimjadili sana itabidi tulete udini katika hii mada ndio akaongoza wale wenye asili ya kiafrika ili kupindua na ndio mwaka 1964 kukafanyika hayo mauwaji ambayo zaidi yalijali rangi ya mtu anavyoonekana,tukiongea ukweli ni kwamba wengi wasiokuwa na hatia yaliwaathiri mapinduzi haya na takriban kila familia iliopo leo yenye asili ya arabuni kidogo basi utaikuta iliathirika kwa namna moja au nyengine.na pia ndio maana kuna mitazamo miwili tofauti visiwani kuhusu mapinduzi haya ,kwani wapo waliyoaona ni ushujaa(washirazi) na wale walioyaona ni haramu(wahizbu).tukimuangalia huyo john okello pia tutamkuta hakuwa mzanzibari na pia kuna maneno kwamba mheshimiwa karume pia hakuwa na asili ya zanzibari(sina uhakika nayo),na huyu okello ndie aliemkabidhi karume urais ,lakini baadae ni huyo huyo karume aliempiga marufuku okello katika ardhi ya zanzibar.
hivyo utaona zanzibar ilipata uhuru wake kamili mwaka 1963(jambo ambalo wengi hawalijui) na mapinduzi ndio yakafanywa mwaka 1964.tanabahi:hawa wenye asili ya kiarabu walikuwepo zanzibar kwa karne na karne.
ombi kwa wazanzibar.
---------kama ni kosa ndio lishafanyika miaka iliopita ,watanzania wa upande wa zanzibar wasahau historia na waungane na washirikiane katika kutetea haki na maslahi ya kila mwananchi bila kujali eneo,rangi,chama,wala itikadi,.
EWE MUNGU TUONDOLEE DHULMA DUNIANI,EWE MUNGU TUONDOLEE DHULMA TANZANIA,EWE MUNGU TUONDOLEE DHULMA ZANZIBAR.AMIIN.-----penye mashirikiano hakuna lisilowezekana.ni mada nzito kuijadili ,naomba nikae pembeni.
 
Underage,
Nimemaliza kuiangalia picha. Unayosema yanapingana na ukweli wa jinsi Waarabu walivyowabagua watu weusi kwa miaka mingi kuanzia utumwani. Lakini kiujumla nilichokiona na ninachotaka kusisitiza ni uovu na dhuluma iliyoletwa na ukoloni. Nasikitika kwamba tumeanza kusahau madhara waliyotuletea wakoloni kwa karne, na leo, baada ya juhudi za akina Mandela, Nkrumah na Nyerere, walioyajua maovu hayo, kizazi cha sasa kinaanza kuwakumbatia katika mantiki ya utandawazi na uwekezaji. Wakoloni hawajabadilika. Unyonyaji haujabadikia. Kwa nini sisi kizazi hiki tubadilike tuone kuwa ni sawa tu kwa hawa tunaowaita wawekezaji kuchota maliasili zetu na kutuacha mikono mitupu? That is the question.
 
  1. Hii documentary inasemekana imetengezwa mwaka 1966. Sijaichunguza vizuri kuona kama matukio yote mle nia ya zamani namna hiyo
  2. Mtayarishaji alikuwa na nia ya kuonyesha kuwa waafrika ni wajinga na hawana ustaarabu. Ametumia matukio yaliyotokea kweli na kuyatafsri kwa lugha yake ya white supremacy ambayo sikuipendelea kabisa.
  3. Nimekumbuka na kucheka sana jinsi Tanzania tulivyopasua vyakula na vinywaji vya kutoka Afrika ya Kusini, hasa nikiangalia jinsi tunavyowakumbatia Arika ya Kusini leo.
  4. Kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar:
    • Niliwahi kusoma kitabu cha Okello zamani sana miaka ya sabini; ansimulia kuwa yeye ndiye aliyekuwa kinara wa mapinduzi yale ila kwa vile hakuwa mwanasiasa, aliamua kumpa Karume mamlaka ya kuunda serikali halafu Karume akamgeuka.
    • Mwaka 1977 mara baada ya CCM kuzaliwa, shule yetu ilitembelewa na Brigadier Yusuf Himid aliyekuwa amehamishiwa Tabora kama kamanda wa brigade ya magharibi (wakati huo). Kwa vile naye alikuwamo katika walioendesha mapinduzi yale, tulimwomba atusimulia kuhusu mapinduzi yale. Akapiga bla bla tu na kusifia jinsi alivyoweza kuoa mwanamke wa kiarabu baada ya mapinduzi hayo!
    • Binafsi nilimwuliza Brigadier Himid swala la ushiriki wa Okello kwenye mapinduzi, akajibu kuwa Okello hakuwa ameongoza mapinduzi yale ila wao (Himid, Natepe, Karume, Kombo na ma-alwatani wa ASP) walimtumia Okello kwenda redioni na kutoa vitisho kwa vile alikuwa na sauti ya kutisha sana kutokana na kiswahili chake kuwa kibovukibovu.
    • Hii documentary inaonekana kukubaliana na account ya Okello kuwa alikuwa amefundisha jeshi kamili alilotumia kuendesha mapinduzi yale na wala siyo marungu, na mapanga kama tunavyosimuliwa miaka yote. Okello alikuwa na bunduki alizokuwa ametoa urusi.
    • Kitu ambacho nimekisikia kwa mara ya kwanza ni haya mauaji kwa vile Okello mwenyewe hakuyaandika kitabuni mwake, na vile vile Himid asingeweza kutuambia na hakuna aliyewahi kuyasimulia. Hakukuwa na tofauti kabisa na yale mauaji ya Rwanda.
    • Je Okello aliishia wapi? na Kama Okello ndiye aliyeendesha mapinduzi yale, je Karume alifanya nini? Na je mauaji ya rais Karume yalikuwa na uhusiano wowote na mauaji yaliyofanyika wakati wa mapinduzi ? - yaani kama namna ya retaliation
 
I've seen it and will be back with my comments. For those who understand Italian language will be beneficial although its a mixture as Kichuguu said.

Nitakusubiri, nina kiu ya kunyoosha knowledge yangu kuhusu mapinduzi kwa vile inaonekana kuna vitu sikufundishwa shuleni.

Underage,
Nimemaliza kuiangalia picha. Unayosema yanapingana na ukweli wa jinsi Waarabu walivyowabagua watu weusi kwa miaka mingi kuanzia utumwani. Lakini kiujumla nilichokiona na ninachotaka kusisitiza ni uovu na dhuluma iliyoletwa na ukoloni. Nasikitika kwamba tumeanza kusahau madhara waliyotuletea wakoloni kwa karne, na leo, baada ya juhudi za akina Mandela, Nkrumah na Nyerere, walioyajua maovu hayo, kizazi cha sasa kinaanza kuwakumbatia katika mantiki ya utandawazi na uwekezaji. Wakoloni hawajabadilika. Unyonyaji haujabadikia. Kwa nini sisi kizazi hiki tubadilike tuone kuwa ni sawa tu kwa hawa tunaowaita wawekezaji kuchota maliasili zetu na kutuacha mikono mitupu? That is the question.


Mimi silaumu mapinduzi kwani labda kweli yalikuwa ni ya lazima kumkombowa mwafrika. Hata hivyo kuuwawa watu wasio na hatia na kutuficha ukweli wote kuhusu mapinduzi hayo nadhani halikuwa jambo zuri.
 
Kichuguu,
Good questions. Hata mimi mara nyingi nimejiuliza Karume alikuwa na role gani katika mapinduzi yale. Hopefully siku moja tutapata jibu. Okello alifia Uganda, peniless.
 
Jasusi,Kichuguu,
.....inasemekana Iddi Amini "took care" of John Okello!!

......kutokana na historia ya Utumwa na Ubaguzi wa rangi ZNZ hivi tulitegemea Mapinduzi yangekuwa tofauti ya hicho kilichotokea?

.....How did the slaves revolt in places like Haiti?

.....sasa kama Yusuf Himidi,Abdalah Natepe,Karume...had a "limited role" ktk haya Mapinduzi does that mean they also had a no role/limited role in the killings/attrocities that took place?

.....kwanini Tanganyika walipeleka Jeshi la Polisi baada ya Mapinduzi?
 
jasusi. nakubaliana na wewe kuhusu wakoloni na ukoloni ila nadhani lugha kidogo tuliichanganya,wakati mimi nasema wazanzibar wenye asili ya kiarabu wewe umetafsiri wakoloni,nimesema wengi wa waliouliwa walikuwa sio wenye hatia kwani walikuwa ni wazanzibari wenye asili ya kiarabu na sio waarabu(nakukumbusha tena kwamba zanzibar ilipata uhuru mwaka 1963 na ikawa mwanachama wa jumuiya ya madola kabla ya mapinduzi),(sawa na watanzania wenye asili ya kiarabu unaowaona leo tanga,tabora ,dar es salam n.k.) kumbuka kwamba waarabu waliingia zanzibar tangu 1689 baada ya kuondoka wareno) hivyo utaona ni karibu karne 4 mpaka hayo mapinduzi.sipendi kutetea yeyote wala kumshutumu yeyote katika historia hii ya zanzibar ila kitu kimoja tuelewe,huyu muandaaji wa mapinduzi haya(john okello) hakuwa raia wa zanzibar wala tanganyika kwa wakati ule.masuali ya kujiuliza.
1)kwanini alishiriki kuandaa mapinduzi ya zanzibar?
2)kwanini alipigwa marufuku baadae kurejea zanzibar?
3)kwanini hata tanganyika na kenya walikataa kumpa hifadhi?
4)je baina ya kipindi uingereza kuipa uhuru zanzibar na mapinduzi ,kulikuwa na ugomvi wowote baina ya wazanzibari?
kwa uoni wangu ni kwamba kulikuwa na kitu kimepangwa na waliokuwa nje ya zanzibar, kwani tangu ulipoondoka utumwa zanzibar,zanzibar ilisifika kwa mambo kadhaa wa kadhaa ikiwemo ,mvumiliano wa kikabila,mvumiliano wa kidini,mvumiliano wa rangi, na mengineyo.
nani alikuwa nyuma ya mapinduzi ya zanzibar? jibu lipo lakini sitolitoa.
unapoijadili zanzibar elewa kwamba unajdili kisiwa ambacho kimeundwa kutokana na watu wenye asili tofauti kuhamia kwa sababu moja au nyengine wakiwemo, wabantu,wahindi,wangazija,waarabu,wareno,n.k ni tabu kuijadili zanzibar na ukampata mwenyeji halisi wa zanzibar.

hivyo unapoijadili zanzibar elewa kwamba huwezi kuepuka kuwajadili wageni.
cha msingi ni kuachana na historia na kuwa kitu kimoja kama watanzania na kutetea kila haki inayostahiki kutetewa, yaliopita si ndwele tugange yajayo.
 
jokakuu.soko la watumwa zanzibar lilifungwa mwaka 1873 na mapinduzi yalitokea mwaka 1964.sidhani kama kuna uhusiano baina ya utumwa na mapinduzi.
 
suala la mapinduzi ni suala tete, ni suala ambalo limewagawa wazanzibari kwa kiasi kikubwa sana, ni suala lilowafanya wengine wajione juuu sana juu ya wengine.

mawazo m,bali mbali yanazungumzwa kuhusu mapinduzi.

kwa mfano mapinduzi yalimuondoa mkolozi mwaraab, wengine wanaulizana mwarab yupi mkoloni aliyeondolewa pale?

bila ya kufichana wazanzibari ni mchanganyiko wa watu wanaotoka pande mbali mbali za dunia, wako watanganyika, wako wakenya wako warundi, wako wanyasa wako wahindi na wako waarab.


siasa zilipoanza kushika kani miaka ya hamsini kila kundi liliingia ktk kutetea siasa zake wako waliopigania kumkomboa mzanzibari na kuondoa ukabila wakiamini kuwa zanzibar ni ya wazanzibari na wale waliokuja zanzibar kwa kutafuta rizki hawa si wazanzibari.

wako walioamini wazanzibari ni wote walio weusi na hata kaja leo maadam ni mweusi huyo ni mzanzibari na anastahiki daraja la kwanza. na hata yule aliyekuja miaka 300 na zaidi maadam ni mweupe ni mkoloni kazi ni kubwa hapo.

kila kundi linahalalisha waliopigania kwa hila mbali mbali.

ila mie nnaaamini mapinduzi ni donda ambalo imeichafua historia ya zanzibar na linaendelea kuisumbua sasa sijui kama mguu utakatwa au la.

maana hao waliopinduliwa kwa kuwa wakoloni leo wako ikulu akina aman mama yeke ni mwarab na mhindi na kina salim na wengine.


hili ni moja ya tatizo ambalo linainyima raha zanzibar na nafasi ya maendeleo
 
Hizi habari za waarabu na wazungu zote mizinguo mitupu!.. Kutawaliwa siku zote ni utumwa na ndio hao hao wanao tuita sisi leo wajinga baada ya! - All I can say is Thank you very much, lakini wasije ktk 18 zangu.

Uhuru wa Zanzibar mwaka 1963 ni sawa kabisa na Uhuru wa Ian Smith - Rhodesia au Botha south Afrika miaka hiyo hiyo! wapo wazungu na weusi waliotetea Uhuru ule kama ilivyokuwa Zanzibar na hata leo hii bado wapo watu wanaoshabikia na kudai kutambua uhuru ule.
Huyo Okello hakushiriki ktk mapinduzi ya nchi moja tu...Hii ndio ilikuwa kazi yake kama alivyokuwa Che!
Tatizo la Zanzibar wamemtazama kwa dini yake basi!..
 
Waliopinduliwa ni hawa hapa:

sultan2.jpg


Huyu alikuwa Sultan Khalifa Bin Haroub, baba yake na Sultan Jamshid bin Abdullah aliyepinduliwa. Nitatafuta picha ya Sultani Jamshid na kuiongezea hapa kesho.

sultan41.jpg


Serikali ya Shamte iliyokuwa inatawala baada ya uhuru bandia kabla ya mapinduzi. Ilikuwa ni muungano wa vyama viwili ZPPP na ZNP nadhani.

Watu hawa siwatofautishi kabisa na wanasiasa maarufu hapa nchini kama vile Abulrahman Babu, Hayati Sheikh Thabit Kombo, Balozi Salimu Ahmed Salim, na hata Maalim Seif Shariff Hamad. Naona wengine ni wabantu kabisa.

Habari zaidi soma hapa na hapa

Picha za Field Marshal Okello:

Okello%20and%20supporters%20.jpg


Nyuma yake huyo aliyenyoosha bastola nadhani ni Col. Abdallah Natepe na pembeni mwake huyo aliyeweka bastola kwenye paja nadhani ni Colonel Seif Bakari, ingawa sina uhakika. Nadhani wote wameshafariki.

Okelo alikuwa na bunduki nyingi zaidfi ya bastola zinazoonekana kwenye piocha ya juu, vile vile alikuwa na machine guns kama inavyoonekana kwenye picha za chini hapa
Okello_Guns.jpg


Okello_bren2.jpg



Picha nyingine hizi hapa:

Okelo aingia Dar kuonana na Nyerere mara tu baada ya mapinduzi

Okello3.jpg


Hapa Okello anamkabidhi Karume madaraka baada ya mapinduzi

Karume%20and%20Okello-1.jpg
 
mkandara.hayo maneno aliyoasema mtumwitu umeyafahamu vizuri lakini.siasa ya zanzibar usiisikilize redioni ni vyema ukaenda kujionea mwenyewe katika mapinduzi wako waliowauwa baba zao,kaka zao,wajomba zao n.k. je baba alikuwa mzawa tofauti na mwana? au baba anaweza kuwa mzawa na mwana akawa mkoloni? sioni kama kuna ukweli unaoelezwa kuhusu mapinduzi haya, ila kubwa ninaloliona ni kwamba yameleta athari kubwa kwa wzanzibari,na ni athari hii ndio ilioliuwa jina la zanzibar katika ulimwengu,

. ninachoomba watu wapate somo ili turekebishe tulipoharibu.ndio la msingi.
 
Kichuguu, UnderAge, Mkandara na wengine,
This discussion is so exposing and enlightening! Niulize swali dogo la Okello- ilikuwaje Okello- Mganda akahusika katika Mapindizi? Je aliletwa na nani? Silaha alipata wapi? Aliletwa kama Mamluki na kupewa chake baada ya Mapinduzi? Maanake hapo juu naona alikutana na Nyerere baada ya Mapinduzi- Mwalimu alikuwa na hizo habari za Mapinduzi kabla?
 
Kichuguu, UnderAge, Mkandara na wengine,
This discussion is so exposing and enlightening! Niulize swali dogo la Okello- ilikuwaje Okello- Mganda akahusika katika Mapindizi? Je aliletwa na nani? Silaha alipata wapi? Aliletwa kama Mamluki na kupewa chake baada ya Mapinduzi? Maanake hapo juu naona alikutana na Nyerere baada ya Mapinduzi- Mwalimu alikuwa na hizo habari za Mapinduzi kabla?

Hayo maswali niyouliza tayari nimepata majibu ktk links iliyotolewa! Thanks
 
Hayo maswali niyouliza tayari nimepata majibu ktk links iliyotolewa! Thanks


Kwenye kitabu chake yeye mwenywe alidai kuwa alikwenda Zanzibar kwa lengo la kuikomboa kutoka kwa wakoloni baada ya nchi zote za Afrika ya mashariki kuwa zimepata uhuru. Alitumwa akiwa ndotoni kwenda kufanya hivyo!!
 
Mkandara,Kichuguu,MzalendoHalisi,
jamani msisahau kwamba kabla ya Mapinduzi kulifanyika chaguzi 2. Katika chaguzi hizo ASP ilikuwa inashinda kwa WINGI wa KURA lakini MAJIMBO mara zote yalikuwa hayatoshi.

Sasa mara zote 2 vyama ambavyo ni PRO-ARAB vilikuwa vikiungana na kuitenga ASP ktk kuunda serikali. Katiba ya ZNZ, iliyotengenezwa na Mngereza, ilikuwa imeweka kifungu kwamba serikali itaundwa na CHAMA/VYAMA vyenye MAJIMBO mengi, siyo KURA/WAFUASI wengi.

Inasemekana pia kwamba hata hayo majimbo yalitengenezwa in such a way kwamba ASP wasingeweza kuunda serikali ktk uchaguzi wowote. Ukiangalia wingi wa kura walizopata ASP ktk uchaguzi wa pili, and the fact that they couldnt form a government, utaelewa kwanini WAAFRIKA waliamua kuchukua SILAHA.

Kwa upande mwingine nashindwa kuelewa kwanini hizi safari za kuonana na JULIASI zilikuwa haziishi? Karume alikuwa Dar muda mfupi kabla ya Mapinduzi. John Okello naye akaonana na Juliasi baada ya Mapinduzi. Tanganyika ikapeleka askari polisi baada ya Mapinduzi. WHY? WHY? WHY?

Majibu ya maswali hayo yanapaswa kutoka kwa wale waliokuwa karibu na Juliasi. Inasikitisha kwamba tumeacha wakina Mzee Mzena,Elangwa Shaidi,Mzee Kisassi,Oscar Kambona wakafariki bila kuweka bayana mambo kadhaa.

Under_Age,
Yes, soko la utumwa lilifungwa mwaka 1873, je una hakika leo hii makovu ya udhalimu ule yamepona? NEVER AGAIN. Unasahau kwamba Sultan wa ZNZ alikuwa mzao wa Mwarabu aliyewachukua Waafrika Utumwa.

Kilichopaswa kufanyika ni kufunga soko la Utumwa, na wale walioleta biashara hiyo, pamoja na vibaraka wao,kuondoka ZNZ.
 
Mkandara,Kichuguu,MzalendoHalisi,
jamani msisahau kwamba kabla ya Mapinduzi kulifanyika chaguzi 2. Katika chaguzi hizo ASP ilikuwa inashinda kwa WINGI wa KURA lakini MAJIMBO mara zote yalikuwa hayatoshi.

Sasa mara zote 2 vyama ambavyo ni PRO-ARAB vilikuwa vikiungana na kuitenga ASP ktk kuunda serikali. Katiba ya ZNZ, iliyotengenezwa na Mngereza, ilikuwa imeweka kifungu kwamba serikali itaundwa na CHAMA/VYAMA vyenye MAJIMBO mengi, siyo KURA/WAFUASI wengi.

Inasemekana pia kwamba hata hayo majimbo yalitengenezwa in such a way kwamba ASP wasingeweza kuunda serikali ktk uchaguzi wowote. Ukiangalia wingi wa kura walizopata ASP ktk uchaguzi wa pili, and the fact that they couldnt form a government, utaelewa kwanini WAAFRIKA waliamua kuchukua SILAHA.

Kwa upande mwingine nashindwa kuelewa kwanini hizi safari za kuonana na JULIASI zilikuwa haziishi? Karume alikuwa Dar muda mfupi kabla ya Mapinduzi. John Okello naye akaonana na Juliasi baada ya Mapinduzi. Tanganyika ikapeleka askari polisi baada ya Mapinduzi. WHY? WHY? WHY?

Majibu ya maswali hayo yanapaswa kutoka kwa wale waliokuwa karibu na Juliasi. Inasikitisha kwamba tumeacha wakina Mzee Mzena,Elangwa Shaidi,Mzee Kisassi,Oscar Kambona wakafariki bila kuweka bayana mambo kadhaa.

Under_Age,
Yes, soko la utumwa lilifungwa mwaka 1873, je una hakika leo hii makovu ya udhalimu ule yamepona? NEVER AGAIN. Unasahau kwamba Sultan wa ZNZ alikuwa mzao wa Mwarabu aliyewachukua Waafrika Utumwa.

Kilichopaswa kufanyika ni kufunga soko la Utumwa, na wale walioleta biashara hiyo, pamoja na vibaraka wao,kuondoka ZNZ.


Nashukuru sana kwa maelezo. Hiyo historia ya uchaguzi ninaifahamu sana kwa vile tulifundishwa shuleni. Ila hakuna aliyewahi kunifahamisha jinsi majimbo hayo yalivyokuwa yamegwanywa, na jinsi gani yalivyokuwa yanaikoseha ASP ushindi.

Kuna makala ya Mjengwa ambayo nayo inauliza baadhi ya maswali kama haya haya tena kwa undani zaidi na kutoa taarifa zinazozidi kuchanganya; unaweza kuisoma kwenye blogu yake hapa. Zaidi ya kuulizia role ya Okello katika mapinduzi yale, swali zuri zaidi ni kuwa, je kama waliopinduliwa walikuwa watu wenye asili ya "kiarabu" tu, ilikuwaje akina Abdulrahman Babu (ambaye alikuwa ZNP (HIZBU) ambayo ilikuwa imeunda coalition na ZPPP kuunda serikali) na wengineo kama Ali Sultan Issa, Kulatein, Ali Mahfoudh na Salim Ahmed walipewaje madaraka nao walikuwa na asili ya "kirabu?" Babu naye alikuwa hakosi kukutana na Nyerere kiasi kuwa hata siku ya mapinduzi alikuwa Dar kuonana na Nyerere, alikwenda kwa mtumbwi wa kasia.
Babu-copy.jpg

Kutokana na viongozi wa mapinduzi kuwa karibu sana na Nyerere, je ni sahihi kuhisi kuwa Nyerere ndiye alikuwa background force ya mapinduzi yale huku aki-organize kwa kuwapa silaha kuwapelekea polisi mara tu baada ya mapinduzi, na kuwasaidia kuunda umoja wa watu aliokuwa akiwapenda tu?


Jembajemba, hizo links ulizoonyesha hapo ndizo hizo hizo zilizoko kwenye post yangu ile yenye picha nyingi pale mbele.
 
Back
Top Bottom