Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mauaji ya Zanzibar hayawezi kuwa sawa na ya Rwanda hata kidogo!..labda kuna mtazamo tofauti hapa, na wala sielewi ktk kipimo gani hasa! Hawa watu walikuwa chini ya Utawala wa Sultan, hiyo demokrasia ya kuvizia haiwezi kusimama kabisa kwani hata Ian Smith alifanya uchaguzi huko Zimbabwe na hata akina Botha huko South Afrika...hii ilikuwa mbinu za watawala baada ya kuona kuwa mapinduzi Afrika yamechachamaa!..mbinu ambayo haikuwa zuga waafrika.

Kwa hiyo watu waliouwawa Zanzibar wakati au baada ya mapinduzi walistahiki?

Kina Kassim Hanga, Abdallah Sadallah, Twala na wengineo hawa nao walikuwa Waarabu?
 
Jembajemba,
Utafiti gani huo?...maanake naona imekuwa nongwa hapa kijiweni..
Nafikiri wewe ndio unahitaji kusoma na kuelewa between the lines kuna kitu gani, siwezi andika gazeti hapa na wala mimi sio mwandishi. Hao ulowataja wanaweza kuwa walistahiki ama laa! kwani Mapinduzi ya silaha hayana maana hata kidogo. Inategemea walikuwa upande gani kama vile tunavyoona vita ya Iraq na Marekani!...
Mimi pamoja na yote yanayotokea huko kwa sababu naunga mkono hawa jamaa siwezi kusema hao Wamarekani wanaokufa huko wanastahiki hata kidogo!.. kosa ni kwamba wamsimama upande nisiounga mkono na heros wangu watakuwa tofauti na wa mtu yeyote anayeunga mkono Marekani ktk vita hiyo.
Na ikiwa ni swala la Okello ndio lakumaliza wewe nipe utafiti wako na unambie jinsi gani karume na ASP wamekutwa mtaani na kukabidhiwa nchi maanake hapa yaonyesha wazi unataka kunyoosha kidole tu kwa Nyerere na Okello sio Wazanzibar (Waunguja- washiraz) ambao walichoka!
kwa hiyo huu ubishi hauna nguo hata kidogo, upo uchi wa nyama na kila nitakalo sema lazima likupe kimeo..tukubali kutofutiana.
 
Mimi nina hamu ya kujua historia hii bila spin yoyote. Najua mapinduzi yale hayakufanyiuka kwa msingi wa udini kwa vile wazanzibari karibu wote ni waislamu, na hata hili la kufanyika kwa msingi wa ukabila pia silikubali kwa vile kuna waarabu waliobaki madarakani na kuna waafrika waliouwawa au kufukuzwa.

Kwa hiyo utaratibu wa mapinduzi ulikuwa na formula yake fulani ambayo ndiyo haijaeleweka sawasawa. Ila kidogo kidogo tutapata ukweli; tushirikiane kuutafuta ukweli huu kwa kuchambua kitabu hiki na historia tunayofahamu na kutumia ile link niliyottoa kule mbele bila kujali imani zetu za kidini, kisiasa au kikabila. Najua waandishi hawa ni kati ya wale walioathirika na mapinduzi yale, kwa hiyo maandishi yao yako skewed upande mmoja, hata hivyo haina maana kuwa maandiko yao yote hayana ukweli, lazima yana ukweli fulani ndani yake. Tuutafute ukweli huo.
 
Na kama kweli hawa watu wafuasi wa Hizbu walikuwa Waafrika mbona wengi wamekwenda chukua Uraia Oman miaka ya 80 wakati Sultan wa Oman alipokubali kuwapokea Wazanzibar wenye asili ya huko. Haya si ndio alokataa Idd Amin na wahindi wa Uganda! hao watutsi na Wahutu hawana nchi ya kukimbilia ni raia wa Rwanda tofauti yao ni kabila tu sio asili mbili za bara tofauti



Sasa wale waliokimbilia Uingereza baada ya machafuko ya uchaguzi wa 1995 kule zanzibar na wao pia walikuwa na asili ya Uingereza? Mbona wamekubaliwa kuishi?
 
Mimi nina hamu ya kujua historia hii bila spin yoyote. Najua mapinduzi yale hayakufanyiuka kwa msingi wa udini kwa vile wazanzibari karibu wote ni waislamu, na hata hili la kufanyika kwa msingi wa ukabila pia silikubali kwa vile kuna waarabu waliobaki madarakani na kuna waafrika waliouwawa au kufukuzwa.

Kwa hiyo utaratibu wa mapinduzi ulikuwa na formula yake fulani ambayo ndiyo haijaeleweka sawasawa. Ila kidogo kidogo tutapata ukweli; tushirikiane kuutafuta ukweli huu kwa kuchambua kitabu hiki na historia tunayofahamu na kutumia ile link niliyottoa kule mbele bila kujali imani zetu za kidini, kisiasa au kikabila. Najua waandishi hawa ni kati ya wale walioathirika na mapinduzi yale, kwa hiyo maandishi yao yako skewed upande mmoja, hata hivyo haina maana kuwa maandiko yao yote hayana ukweli, lazima yana ukweli fulani ndani yake. Tuutafute ukweli huo.

kwanza kabisa nnapenda kukushukuru sana mheshimiwa kichuguu kwa kutuwekea hiki kitabu, na nilitegemea kitabu hiki iwe starting point ya kuelekea kuutafuta ukweli, kwa kiasi fulani kitabu hiki kinawakilisha mawazo ya walioathirika na mapinduzi yale, sio mbaya pia kama tutapata references za upande wa pili na tukaendelea na mjadala.

hata hivyo katika mjadala mkubwa na mzito sana kwa wananchi wazanzibar ni kuhusu mapinduzi.

mimi binafsi ni mtoto niliezaliwa na pande mbili, nnasema hivi nikimaanisha upande mmoja walikuwa hizbu kindaki ndaki na hawana mchezo juu ya hilo hadi kesho. na upande wa pili ni afroshirazi kindaki ndaki hawana mchezo katika hilo.

tuutafuteni ukweli maana ninapobahatika kutembelea upande mmoja na kuanzisha hii mada hupata mambo tofauti na upande wa pili.


lakini mie nnaamini kuwa mapinduzi ni donda lililoichafua zanzibar, pili ndilo lililoengeza tofauti baina yao.

na nnapenda niseme hivi ndani ya vyama vyote vya wakati ule mlikuwa na mchanganyiko mkubwa wa watu, na tatizo sio ukabila maana zanzibar wenye makabila ni wachache sana, ukiniita mimi mshirazi siaminim kuwa ni kabila, ukiniita mtumbatu nnaamini tumbatu ni kisiwa ambacho watu hukaa, ukiniiita mhadimu pia si kabila na hivi ndivyo wazanzibari wengi walivyokuwa wakiitwa.

mfano mzuri, SH. Ali bin Muhsin alikuwa barwan yy alikuwa HIZBU, komrediu AHmed Sultan vile vile Barwan alikuwa Afroshirazi.

na wengi tu walikuwa huku na huku mfano Sh Kwacha ni mshirazi alikuwa hizbu, na Sh Thabit KOmbo mshirazi alikuwa ASP, na SH Ameir Tajo alikuwa ASP akatoka akaunda chama cha ZPPP na baadae akarudi ASP, utawakuta watu hao hao kila pahala sasa utajiuliza aliepinduliwa ni nani?

siri ya mapinduzi yale bado ni tete na tuwe wastahmilivu sana kupata ukweli huu.

ila nnaaamini serikali ya tanganyika ina mkono mkuu tu ktk mapinduzi yale.
 
kwanza kabisa nnapenda kukushukuru sana mheshimiwa kichuguu kwa kutuwekea hiki kitabu, na nilitegemea kitabu hiki iwe starting point ya kuelekea kuutafuta ukweli, kwa kiasi fulani kitabu hiki kinawakilisha mawazo ya walioathirika na mapinduzi yale, sio mbaya pia kama tutapata references za upande wa pili na tukaendelea na mjadala.

hata hivyo katika mjadala mkubwa na mzito sana kwa wananchi wazanzibar ni kuhusu mapinduzi.

mimi binafsi ni mtoto niliezaliwa na pande mbili, nnasema hivi nikimaanisha upande mmoja walikuwa hizbu kindaki ndaki na hawana mchezo juu ya hilo hadi kesho. na upande wa pili ni afroshirazi kindaki ndaki hawana mchezo katika hilo.

tuutafuteni ukweli maana ninapobahatika kutembelea upande mmoja na kuanzisha hii mada hupata mambo tofauti na upande wa pili.


lakini mie nnaamini kuwa mapinduzi ni donda lililoichafua zanzibar, pili ndilo lililoengeza tofauti baina yao.

na nnapenda niseme hivi ndani ya vyama vyote vya wakati ule mlikuwa na mchanganyiko mkubwa wa watu, na tatizo sio ukabila maana zanzibar wenye makabila ni wachache sana, ukiniita mimi mshirazi siaminim kuwa ni kabila, ukiniita mtumbatu nnaamini tumbatu ni kisiwa ambacho watu hukaa, ukiniiita mhadimu pia si kabila na hivi ndivyo wazanzibari wengi walivyokuwa wakiitwa.

mfano mzuri, SH. Ali bin Muhsin alikuwa barwan yy alikuwa HIZBU, komrediu AHmed Sultan vile vile Barwan alikuwa Afroshirazi.

na wengi tu walikuwa huku na huku mfano Sh Kwacha ni mshirazi alikuwa hizbu, na Sh Thabit KOmbo mshirazi alikuwa ASP, na SH Ameir Tajo alikuwa ASP akatoka akaunda chama cha ZPPP na baadae akarudi ASP, utawakuta watu hao hao kila pahala sasa utajiuliza aliepinduliwa ni nani?

siri ya mapinduzi yale bado ni tete na tuwe wastahmilivu sana kupata ukweli huu.

ila nnaaamini serikali ya tanganyika ina mkono mkuu tu ktk mapinduzi yale.


MtuMwitu,

Ahsante kwa information.

Mimi nadhani sababu kubwa ya hayo yanayoitwa Mapinduzi ni uchu wa madaraka. Coz ile serikali iliyopinduliwa haikuwa serikali ya waarabu kama inavyodhaniwa, ni serikali iliyojumuisha watu mbali mbali hata Karume mwenyewe alikuwemo kwenye ile serikali (kama waziri) so akaona nafasi hiyo haitaki (yy alikuwa anataka kuwa Rais wa Zanzibar), kwa hiyo ndipo ulipopangwa huo mpango wa kuipindua serikali. Hii inadhihirisha kiasi gani alivyokuwa na uchu wa madaraka pale alipowauwa hata wasaidizi wake kina Hanga na wenzake.

Haya ndio maoni yangu
 
Jembajemba

Unaanza kuleta point ambayo huenda ikawa ni moja ya ambazo hazikuandikwa vitabuni.

Vipi umefanikiwa kupata nakala ya kitabu?
 
Jembajemba

Unaanza kuleta point ambayo huenda ikawa ni moja ya ambazo hazikuandikwa vitabuni.

Vipi umefanikiwa kupata nakala ya kitabu?

Kichunguu,

Naam nimekipata asante sana mwalimu wangu.

Mwl Kichunguu yeah hiyo nadhani ndio point muhimu iliyopelekea hayo mapinduzi (Madaraka) kwa sababu inasemekana mzee Karuma alikuwa hawataki wasomi kwa kuhofia watakuja kumuondoa katika madaraka. Anyway hayo ni mawazo tu
 
mtumwitu,mkandara,kichuguu,...
Waliotoka Hizbu kwenda ASP walikuwa wamesoma nyakati na kuona kwamba siasa za kumbagua Mwafrika kwenye nchi yake zimepitwa na wakati.

Waafrika walikuwa hawataki Sultani awe kiongozi wa aina yeyote ile ZNZ. Kitendo cha kumsimika kama kiongozi mkuu wa ZNZ ilikuwa ni kutoneka makovu ya utumwa. Mtu asiye Mwafrika hawezi kulielewa hilo.

Kuna hoja kwamba Karume alipewa Uwaziri ktk serikali iliyopinduliwa. People think that was enough. Mimi naona hilo ni tusi. Ni kama vile kumfanya Mwafrika siyo mtu kamili.

Ninasema hivyo kwasababu ASP[karume] walishinda Uchaguzi kwa wingi wa kura. Vyama vilivyokuwa vikifadhiliwa na Sultani vikaamua kuungana[kuunganisha majimbo] na kuunda serikali huko vikiiacha "solemba" ASP. That happened in two consecutive elections.

Nakubaliana na wale wanaosema kwamba issue haikuwa UARABU. Issue ilikuwa UBAGUZI dhidi ya Waafrika ndani ya nchi yao. Mapinduzi yalipofanyika, na kumuweka Mwafrika ktk stahiki yake, basi Waarabu/Machotara/Wahindi walishirikishwa ktk serikali.

Kwa hiyo MAPINDUZI yale yalikuwa na nia ya kurudisha HESHIMA YA MWAFRIKA.
 
Hao hao ASP/CCM waliokuwa wanabaguliwa nao leo hii wanarudia dhambi ile ile ya ubaguzi dhidi ya CUF. Kwa mazingira yanayojengwa hakuna uwezekano wa historia kujirudia ?
 
jembajemba,

Hao waliokwenda Oman hawakuwa wakimbizi tofauti kabisa na hao waliokwenda UK. labda jaribu kuelewa maana ya mkimbizi kwanza kisha tuwatazame hao nao wazungumzia mimi. Hawa waliondoka kwa hiari zao baada ya kuahidiwa kupewa Uraia na Sultan - Yaani wamerudi kwao!
Hao waliokimbilia UK ni Watanzania, iwe waarabu ama weusi maadam sababu ya kwenda kwao huko ni ukimbizi wa utawala wa CCM na sio wamemkimbia Sultan wa Oman - Qabus ambaye ni adui wao pia.. Kumbuka tu kwamba tunaijua hata historia ya Oman naugonvi wa hawa masultani huko kwao.
 
Kile kijitabu alichotuambai Mtumwitu hiki hapa. Nimekopi zile webpages na kufanya typesetting kwa kutumia software ya kizamani kidogo iitwayo Tex.

Sikuweza kurekebisha characters za kufungua usemi, kwa hiyo utaona kuwa alama zote za kufungua usemi zinafanana na zile za kufunga usemi. Ingenichukua muda kuzitafuta zote na kuzirekebisha, nadhani msomaji ataelewa.

Kuna chapter moja haipatikani, hii ni Chapter ya 15 iliyokuwa inamhusu mwandishi mwenyewe kwa hivyo nadhani aliondoa.

Kuna chapter mbili hivi au tatu hivi nimeziungansiha na kuwa Chapter moja ya 17 nikaiita "Kuuliwa kwa Wananchi." Nimeziunganisha kwa vile zilikuwa zinaongelea jambo lilelile, mpangilio wa kitabu haukubadilika.

Kwa jumla sikubadilisha maandishi mengine yote ya mwandishi isipokuwa labda marekebisho mawili au matatu ya typos katika quote zilizokuwa zimeandikwa kwa kiingereza kwenye ukurasa wa 32.

Nimekiweka hapa kwa ajili ya kurahisisha usomaji wetu tu. Nimewasiliana na mwandishi wake kwa e-mail lakini naona hajanijibu. Pamoja na kuwa hakina copyright protection yoyote, kuna haja ya kuheshimu effort ya mwandishi original. Kwa hiyo yeyote atakayekitumia asisahau ku-acknoweldge mwandishi original na original source ya kitabu pale http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/

Mzee Kichuguu,
Ahsanse kwa kitabu- it is a very useful resource! Ndo nakisoma- so interesting!
 
JokaKuu na Mkandara,

Nimewapata sana; hata kile kijitabu kilichopo mbele yetu kinanonyesha kuwa waafrika walikuwa hawapendi Sultan kuwa mtawala wao.

Katika uchaguzi wa kwanza wa viti sita, ASP ilipata viti vitatu vya Unguja, Chama cha kiislamu kulipata kiti kimoja, na viti biwili vya Pemba vilikwenda kwa independents ambao baadaye waliungana na ASP hivyo kufanya ASP iwe na viti 5, na chama cha kiislamu kiti kimoja na HIZBU haikupata kiti. In fact kiongozi wa HIZBU alisimama dhidi ya Karume akashindwa. Halafu katika uchaguzi ambao ndio ulisababisha mapinduzi, ASP walikuwa na viti 10, ambapo ZPPP/ZNP waliunganisha viti vyao vikawa 13 na hivyo kushinda. Mambo haya yanaonyesh kuwa ASP ilikuwa inapata kura nyingi zaidi ya vyama vingine ingawa ilikuwa haipati zaidi ya nusu. Hata hivyo tunapoangalia zaidi ndani ya mapinduzi haya, kuna maswali kadhaa ambayo hayajibiwi vizuri:

(a) Je ilikuwa ni makosa kwa ZPPP/ZNP kuunganisha viti vyao? Mbona kwenye uchaguzi wa kwanza ASP iliungana na wale independents wa Pemba? Huu si ni utaratibu wa kawaida katika demokrasi ya vyama vingi?

(b) Kama mbaya alikuwa ni Sultani tu, je hakukuwa na njia nyingine ya kuondokana na utawala wa kisultani bila kuuwa raia wengine ambao hawakuwa na hatia na hawakuwa na uhusiano wowote na sultani? Je Karume ndiye aliyepanga mapinduzi yale au yalipangwa na Okello harafu Karume akawa bandwagon baada ya kupewa madaraka? Je kosa la wanachama wa ZNP na ZPPP lilikuwa ni nini kama nao walikuwa ni wananchi kama wale wanachamwa ASP?

(c) ASP kilikuwa chama cha Waafrika na Washiraz, wakati HIZBU ilikuwa ni mchanganyiko wa waarabu na waafrika na washiraz, huoni kuwa chama hiki kilikuwa na sura ya utaifa zaidi ya ASP ambayo ilikuwa imewabagua waarabu? Ikumbukwe kuwa Waarabu waliokuwa Zanzibar walikuwa ni Wazanzibari kama vile ambavyo leo tunasema kuwa Wangoni ni Watanzania ingawa tunajua kuwa walitoka Afrika ya kusini kama wazulu. Ni watu ambao mababu zao walikuwa wametoka uarabuni miaka karibu 200 iliyopita na wala walikuwa hawana ndugu tena huko uarabuni.

(d) Swala la Babu na waarabu kadhaa kuhamia ASP bado ni tete sana na taarifa zake sijazipata sawasawa. Hata hivyo inawezekana kuwa alihamia huko si kwa mapenzi ya waafrika na washirazi, bali kwa kujua kuwa baadaye ASP ingekuja madarakani kwa vile katika chaguzi zote ilikuwa inapata kura nyingi, na yeye lengo lake lilikuwa ni madaraka. Babu amekuwa controversial sana katika historia ya nchi hii. Baada ya kuenguliwa kutoka serikali ya Nyerere kwenye reshuffle ya mwezi januari mwaka 1972 ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Mwinyi, inasemekana alishiriki katika mauaji ya Karume. Kama ni kweli alishiriki katika mauaji hayo, kuna haja ya kuhoji motive yake ya kuhamia ASP. Mpaka leo katika siasa za hapo Zanzibar, watu waliokuwa wanachama wa HIZBU wamekuwa wakichukuliwa kwa tahadhari sana ingawa sioni sababu ya kuendelea kufanya hivyo. Kati ya matatizo yanayompata Salimu katika siasa za nchi yanatokana na hiyo stigma ya kuwa aliwahi kuwa mwanachama wa HIZBU.
 
nimefurahishwa sana mchango wako, na hakika nnafurahi kwa kuwa muwazi na usieelemea upande wowote, hayo masuali ulioyauliza yanahitaji majibu maridhawa na huenda ikatusaidia sana kufikia pahala pa zuri.
 
Ndugu Kichuguu,

Nakubaliana na hoja yako unapo question solution ya tatizo la Mpinduzi ya silaha. Ni ushenzi kuuana kwa sababu ya Utawala wakati wananchi ndio wachaguzi wa serikali inayoweza kushika madaraka.

nadhani cha msingi hapa ni kuweka wazi kwamba utawala wa Hizbu ulikuwa ukiendeshwa kwa kumtunuku Sultani kama vile UK inavyomtunuku Malkia. mara nyingi naposoma historia ya Zanzibar huwa kuna vipengele vidogo vidogo huachwa nje. Vipengele ambavyo ndio sababu kubwa ya Washiraz kutokubaliana na Utawala huu wa Sultan...

Leo hii Uk inaongozwa na hao Labour lakini yanapotokea mapinduzi lengo sio kuwaondoa labour madarakani ila ni kuundoa utawala wa malkia na ndicho kilichofanyika Zanzibar.

Malengo ya mapinduzi yamekuja onekana baada ya wanachama wa Hizbu kujiunga na ASP chama tawala na ndio tunawakuta hao akina Babu, Salim, Seif Sharrif, kwa hiyo navyofikiria mimi mapinduzi yake yalikuwa kumwondoa Sultan zaidi ya uhasama wa vyama hivi. Ni kweli hizbu wamekuwa victims wa mapinduzi hayo na imekuwa taabu kwa wao kuaminika hasa baadhi yao wanapozidi kumtukuza Sultani hadi leo hii.

Ni makosa makubwa kujaribu kuburuta utawala na historia ya Sultan ktk Zanzibar ya leo na hawa wachache wanaoyafanya haya ndio wamekuwa sumu kwa viongozi wa hizbu kuweza kuthaminiwa ndani ya ASP. Mtu kama Salim kayafanya yote yenye Uzalendo lakini kuna sumu mbaya inazidi kuchochewa na baadhi ya watu wachache kama vile unavyoona Al Qaeda wanavyoupaka Uislaam. Wanaweza kuwa na kila haki ya kugombea haki zao kama raia wa nchi hiyo lakini sio kutumia jina la dini...wajinga sisi hatuwezi kutofautisha kwani maneno haya yanatoka vinywani mwao. na ndivyo ilivyo ktk swala la Zanzibar. Hawa wapinzani wengi ni raia wa Zanzibar lakini haweshi kuonyesha support ya utawala wa Sultan na kuzungumzia sifa zake kana kwamba ugonvi wao mkubwa ni kumrudisha Sultan, kutokana na kauli zao CCM anachukulia muhali na ndio maana viongozi wengi wa hizbu wanashindwa kuaminika ndani ya CCM.

Binafsi naamini kabisa kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa isipokuwa kuna siri kubwa sana ambayo imetuweka sote gizani. Mara utasikia CIA, mara Cuba wakimtumia Okello, Nyerere pia ana mkono wake na CIA hali Nyerere alikuwa Mjamaa basi ili mradi kumekuwepo na vitu fulani vimefichika.
 
Kichuguu,
1.Ukiangalia idadi ya majimbo tu huwezi kuelewa uchungu wa malalamiko ya ASP. Nakuomba uchunguze idadi ya kura walizokuwa wanapata na still never had the opportunity to form a government.

2.Tatizo la muungano wa ZPPP/ZNP ni uchache wa kura na majimbo vs ASP. Nilitegemea chama kimoja wapo kiungane na chama "kilichoshinda" ili kuunda serikali. Ukiona minority parties zinaungana against majority party that is sabotage, and a recipe for conflicts/unrest.

3. On # 2 again, huoni kwamba either party ZPPP au ZNP wangeungana na ASP they would have formed a larger,more stable, and inclusive coalition? Why would they pass on such an opportunity? Mimi inanielekeza kwenye suala moja tu: MWAFRIKA NI MTU KUTAWALIWA DAIMA NA MILELE.

4.Chama cha Waafrika hakiwezi kuwa na jina Hizbu hata siku moja. Nakushauri uchunguze jina Hizbu kirefu chake na maana yake ni nini, halfu unambie kama kina mahusiano yoyote yale na utu wa Mwafrika. Hata hao kina Salim Salim waliona kuna kasoro kubwa ndani ya Hizbu ndiyo maana wakahama.

5.It is naive kulinganisha ujio wangoni tanganyika, na ule wa waarabu ZNZ. sina taarifa za wangoni kuwachukua utumwa jamii walizozikuta. ujio wa Waarabu unalinganalingana na ujio wa Mjerumani, au Mwingereza. Hawa walipaswa waondoke, au wa-submit to the NEW ORDER.

6.Mauaji ya raia wasiokuwa na hatia yameyatia doa Mapinduzi. Sidhani kama kuna yeyote anayeweza kuhalalisha mauaji yale. Lakini wakati huo huo tusijaribu kupuuza madai ya msingi kabisa ya kutambuliwa kwa utu wa Mwafrika ndani ya ZNZ.
 
Nashukuruni sana Mkandara na JokaKuu. Nakwenda mahala nitarudi tuendelee baadaye. Nina maswali na observations kadhaa.
 
JokaKuu,

Kuna mambo machache ambayo bado hatujakubalina katika hili kama ifuatavyo:

  1. Je Waarabu walikuwa ni Wazanzibar? YES. Inawezekana ni kweli historically babu zao walifanya biashara haramu ya utumwa, lakini haina maana kuwa uzao wa waarabu waliozaliwa na kukulia Zanzibar baada zaidi ya miaka mia moja tangu biashara ya utumwa iishe kuwa nao walikuwa na hatia ya kutokana na hiyo ya bishara ya utumwa. Hata marekani unaona waafgrika wanavyamchangamkia Clinton kuliko Obama ingawa historically walikuwa watumwa wa wazungu. Inafikia mambo mengine ya zamani tuseme yaliyopita si ndwele. Mbona karibu maafisa wote wa baraza la mapinduzi, akiwamo Karume mwenyewe, walikuwa wameoa waarabu?
  2. Inawezekana ni kweli kabisa kuwa ASP walikuwa wakipata kura nyingi sana kuliko HIZBU ambayo ilikuwa na waafrika na washirazi wachache sana kuliko ASP, na hasa kwa vile waafrika na washirazi walikuwa karibu asilimia themanini ya wapiga kura wote: sijapata data za kura. Hata hivyo kwa mujibu wa Katiba iliyokuwepo, uchaguzi ule ulikuwa unafuata viti siyo idadi ya kura. ASP ilikuwa imekubali mfumo ule ndiyo maana iliingia kwenye uchaguzi, sasa kupinga matokeo baada ya kupoteza uchaguzi uliofanyika kwa haki chini ya sheria siyo kukubali demokrasi. Kumbuka kuwa hata Tanzania ya leo inawezekana kabisa chama kikawa majority bungeni kwa kuwa na wabunge wengi huku kikiwa kimepata kura chache. George Bush aliingia madarakani US akiwa na kura chache kuliko Al-Gore lakini alipata vote nyingi za electral-college.
  3. Tuwe wakweli kuhusu hili la muungano wa vyama; ni utaratibu halali kabisa wa kidemokrasi na wala huwezi kuwatia hatiani eti kwa nini hawakuungana na ASP. Katika Uchaguzi ule HIZBU ilipta viti kumi, ASP nayo ilipata viti kumi wakati ZPP ilipata viti vitatu. Kibaya zaidi ni kuwa ingawa wakati huo viongozi wengi wa HIZBU walikuwa wa asili ya kiarabu, wale wa ZPPP walikuwa washiraz. ZPPP ndiyo iliyoamua kuwa iungane na HIZBU, ingeweza kuungana na ASP. Zaidi ya hayo kuna ushahidi kuwa baadhi ya viongozi wa ASP walikaribishwa kuunda serikali ya iliyoongozwa na Shamte wa ZPPP. Kwa hiyo swala la kusema ASP ilionewa katika uchaguzi ule kweli sijaliona dhahiri. Kumbuka kuwa Shamte alikuwa si Mwarabu, bali alikuwa mshiraz na alikuwa mwanachama wa ASP lakini aliondoka baada ya kushindana na Karume kuhusu strategies. Unaweza kusoma zaidi interview ya mtoto wake mwenyewe na Gazeti la IPP Guardian hapa
  4. JokaKuu, kwa mbahati mbaya sielewi maana ya jina HIZBUL-WATTAN tafadhali nifahamishe zaidi. Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka, jina hili lina maneno mawili ya kiarabu (mimi sijui kiarabu). Neno Hizbul kama linavyotumika katika "Hizbul'allah" lina maana ya jeshi au mkusanayiko wa watu, na neno wattan kama linavyotumika katika "Jamhoori Watan Party" lina maana ya Taifa. Kwa hiyo nahisi kuwa HIZBUL-WATTAN lina maana kama jeshi la kitaifa vile. Hata hivyo ukweli ni kuwa chama cha hizbu kilikuwa na waafrika weusi pia. Anayeelewa zadi anifahamishe. Nilivyosma kijitabu kile rekodi za mwandishi zinaonyesa kuwa HIZBU kilianzishwa na waafrika ila wakachaguwa waarabu kukiongoza labda kwa vile walikuwa fedha za kuweza kufanya mambo ya kisisa kama vile kwenda ulaya kwa shughuli za kichama, na nadhani pia relatively walikuwa na elimu zaidi.

Mkandara,

  1. Jambo kubwa nililokubaliana nawe kabisa ni hili la kuhusu usultani. Kuwa mapinduzi yalikuwa dhidi ya sultani zaidi ya uhasama wa vyama, lakini historia imekuwa inasisitiza kuwa mapinduzi yalisababishwa na ASP kudhulumiwa kwenye uchaguzi, Jambo ambalo hakuna aliyeprove. Isingekuwa uongozi mbovu wa Karume ndani ya ASP, uchaguzi ule wa 1963 ungechukuliwa na ASP kwa vile ushindi uliamuliwa na viti vilivyochukuliwa na Shamte ambaye alikuwa ametokea ASP.
  2. Mtoto wa Shamte ambaye alikuwa ASP tangu wakati huo alitoa jawabu kama lako kwenye gazeti na IPP Guardian hapa kuwa mapinduzi yalikuwa dhidi ya sultani zaidi ya mfarakano wa vyama. Tatizo linalokuja hapa ni maelezo ya kwa nini Viongozi wa ZNP kama akina Muhsin waliuwawa, Sheikh Shamte mwenyewe aliponea chupuchupu kuuwawa lakini aliwekwa kizuizini kwa miaka 15, sasa kama mapinduzi yalikuwa dhidi ya Sultani kwa nini Sheikh Shamte ambaye wala hakuwa mwarabu alitiwa ndani?
  3. Ukiangalia ile picha ya G-14 la Okelo lililoendesha mapinduzi yale ukalinganisha na picha za wanasiasa wengine waliokuwapo wakati ule, unaweza pata picha ya kuonyesha kuwa jamaa wale walikuwa wahuni tuu wasiokuwa na kazi wala shughuli za maana ila walikuwa wafuasi wa ASP. Ndiyo maana ninakuwa na shaka na kuhusika kwa Karume katika maandalizi ya mapinduzi yale. Inanipa picha kama vile yalifanywa na wahuni wasiojua wanafanya nini halafu wakamkabidhi Karume nchi naye akafurahi. Sikubaliani na dhana kuwa yalipangwa kwa msaada wa Nyerere kwani yalikuwa rudimentary sana. Hata hivyo ni wazi kuwa Nyerere, kama Karume waliyaunga mkono baada ya kuona "mahasidi" wao wametolewa madarakani.

Sasa baada ya miaka 40, mnaonaje kama serikali ya mapinduzi ingejitokeza mbele na kuwaomba radhi wale wote waliodhuriwa na mapinduzi yale kwa namna yoyote na kama kuna namna ya kuwalipa fidia za namna fulani kama kifuta machozi, basi wawalipe. Mauaji yale yalikuwa ni aibu sana na kwa bahati mbaya serikali ya mapinduzi imekuwa inarudiarudia kuuwa wananchi kama ilivyotokea mwak 2002 kule Pemba.

Jambo jingine, sijui kama mnaelewa kuwa mapinduzi ya Zanzibar ndiyo yalikuwa ya kwanza ya kuondoa serikali madarakani kwa kutumia nguvu katika bara lote la Afrika? yale ya Ghana na ya Nigeria yalifuatia mwaka 1966.
 
Kichuguu na wengine,
Sasa huu Upemba na Uzanzibari wa sasa na mpasuko- unasababishawa na Unguja kuonekana ASP na Pemba HIZBU hadi leo? Je hii ndo inafanya Serikali ya Mseto inakuwa vigumu?
Kuna mengi yalifichwa ndo yanaanza kujulikana- kuna haja watu Viswani kujadili kwa uwazi zaidi kitaifa over huu mpasuko- na pengine kuwa na Truth and Reconciliation ili wote wasameheane (including mwandishi wa hiki kitabu).
Muufaka wa CUF na CCM is one step- ila tatito ni pana zaidi.
Wana JF mimi nimefunguka sana macho kutokana na hizi discussion na hiki kitabu- nlifundiswa na Dr. Muya haya mambo hapo UDSM siku za nyuma- ila haikuwa kwa kina kiasi hiki!
 
JokaKuu,

[*]JokaKuu, kwa mbahati mbaya sielewi maana ya jina HIZBUL-WATTAN tafadhali nifahamishe zaidi. Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka, jina hili lina maneno mawili ya kiarabu (mimi sijui kiarabu). Neno Hizbul kama linavyotumika katika "Hizbul'allah" lina maana ya jeshi au mkusanayiko wa watu, na neno wattan kama linavyotumika katika "Jamhoori Watan Party" lina maana ya Taifa. Kwa hiyo nahisi kuwa HIZBUL-WATTAN lina maana kama jeshi la kitaifa vile. Hata hivyo ukweli ni kuwa chama cha hizbu kilikuwa na waafrika weusi pia. Anayeelewa zadi anifahamishe. Nilivyosma kijitabu kile rekodi za mwandishi zinaonyesa kuwa HIZBU kilianzishwa na waafrika ila wakachaguwa waarabu kukiongoza labda kwa vile walikuwa fedha za kuweza kufanya mambo ya kisisa kama vile kwenda ulaya kwa shughuli za kichama, na nadhani pia relatively walikuwa na elimu zaidi.
[/LIST]

nitajitahidi kuweka wazi maana ya neno hili la hizbu alwatwani zenjibar.


kiswahili cha zanzibar na hasa wakati ule kiliathiriwa zaidi na kiarabu, na mara nyingi watu wa kisiwa kile walikuwa katika maongezi yao huchanganya zaidi baina ya kiswahili na kiarabu, sawa na leo kuona baadhi ya miji yetu kuchanganya kiswahili na kiingereza.

mfano utasikia nnmpeleka mtoto madrasa ikimaanisha nnampeleka mtoto shule.

wizara ya ya ziraa maana yake wizara ya kilimo, na hadi leo bado athari hizo zipo, kwa mfano kule kwetu zanzibar ktk kipindi hiki kuna wizara inaitwa wizara ya elimu na mafunzo ya amali neno amali ni la lugha ya kiarabu likimaanisha vitendo au kazi za mikono.

sasa rurudi kwenye neno letu, hizbu kama ulivyosema lina maana ya army, lakini kwa nyongeza lina maana ya movement, party

mfano hizbollah( hizb maana yake party na allah maana yake god) kwa hiyo maana kamili itakuwa Party of God pia yaweza kuitwa Army of God (for ref: www.yeshuatyisrael.com/Powerpoint/Hezbullah.ppt

mfano mwengine ni chama cha HAMMAS cha wapelistina hiki urefu wake Hizbu Almuqqawamat Al-islamiyy
nacho kina maana hizbu ni movement, na almuqawamat Resistance na Al- islammiy iko wazi sasa utaona wanakiita Islamic Resistance Movement hapa imetumika kama movement.

na hata kule Sudan chama kinachoongoza nchi kinaitwa Almuutamar hizbu alwattwan ikiwa na maana almuutammar ni congress, na hizbu party na wattan ni National utapata kinaitwa ni National Congress Party.

turudi kwenye alwattaniy, zanzibar hadi kesho neno hjili tunalitumia kumaanisha utaifa au mzawa, japo sasa kuna harakati za kuliondoa na kutumia mzanzibari halisi lakini ukitaka kusema mimi ni mzawa kindaki ndaki unasema mimi ni muwattin , yule alwattwan.

sasa nnataka kusema kuwa chama cha hizbu urefu wake hasa ni hizbu alwatwani zenjibar na maana yake ni Zanzibar National Party (ZNP). watu kwa ufupi wakawa wanakiita Hizbu na hii ndio maana yake.

na kuitwa Hizbu haimaanishi kuwa waliokuwa hizbu ni waarab tu, hata kwenye quraan neno hili limetumika na wazanzibar wengi ni waislam na wameathiriwa na lugha ya kiarabu ktk matumizi yao.

nnategemea nitakuwa nimejaribu kufafanua maana ya hizbu na any comment zinakaribishwa
 
Back
Top Bottom