Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mimi naona kuwa

Mapinduzi yalifofanyika Zanzibar tarehe 12 Januari hayakuwa halali na hayakuwa na ulazima wowote, ila kwa vile yalishatokea hatuwezi kuyafuta. Ni wakati wa serikali kuja mbele na kuwaomba radhi wazanzibar wote waliodhuriwa na mapinduzi yale bila kujali rangi zao. Halafu iwaombe wasahau yaliyopita ili tusonge mbele. Serikali inafanya makosa sana kuchukulia kuwa mapinduzi hayo yalikuwa ya haki; inawezekana ndiyo maana uhasama umeendelea kuwapo baina ya waZanzibari hadi leo kwa vile serikali haijakiri kuwa ilifanya makosa.
Halafu serikali Zanzibar iache kujiita serikali ya mapinduzi badala yake iwe serikali ya Zanzibar.

Historia ya mapinduzi ya Zanzibar inafaa kuandika upya.

Siku ya Uhuru wa Zanzibar kutoka Uingereza isizikwe.

Pascal Mayalla p
 
Wakiwa wanahamia Tanganyika wanajiita watanzania sababu huku kuna ardhi na fursa za kutosha.
Wakienda visiwani sisi ni watu wa nchi nyingine. Nani hapo anajidanganya mwenyewe? Hakuna kitu kibaya kama kuidanganya nafsi yako mwenyewe 😂😂😂😂😂
 
Halafu serikali Zanzibar iache kujiita serikali ya mapinduzi badala yake iwe serikali ya Zanzibar.

Historia ya mapinduzi ya Zanzibar inafaa kuandika upya.

Siku ya Uhuru wa Zanzibar kutoka Uingereza isizikwe.

Pascal Mayalla p
Kuna jamaa anaitwa "Aman Thani Fairooz" alikuwa na webpages kwenye mojawapo ya platforms za mwanzoni mwa internet iliyojulikana kama FortuneCity.com. Aliweka pages hizo mwaka 1995 lakini mwaka huo 2007 mimi nilizi-typeset kwa kutumia LaTex kama kijitabu hiki nilichoweka hapa mwaka huo huo kwenye thread hii lakini nimeshindwa kuipata post hiyo. Nasikia baadaye kuna mtu mwingine alikitafsiri kwa kiingereza na kukiuza Amazon.
 

Attachments

Back
Top Bottom