Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Jembajemba,

Asante, nilishaisoma hiyo lakini nadhani sikuiamani na wala sukuitilia maanani kwa vile sikuweza kuingunganisha na historia sawasawa. Kwa mfano kuwa madai ya kuwa watu walitaka kupindua serikali kutokana na ugumu wa maisha nadhani haikuingia akilini mwangu kwani nanjua kuwa mauaji yale yalikuwa ya kulipiza kisasi kabisa. Yalitokea wakati nimeshakomaa na ninayakumbuka vizuri sana na jinsi kesi yenyewe ilivyoendeshwa. Yalikuwa ni mauaji ya pili ya viongozi wakuu yaliyotokea wakati wa sikukuu kuu za kikristo: Ya kwanza yalikuwa ya Dr. Kreluu yaliyotokea siku ya Krismasi ya mwaka 1971, ya pili yakawa ya Sheikh Karume yaliyotokea siku ya Ijumaa Kuu ya mwaka 1972.
 
Under_age,

Mjomba yaonyesha hata hunielewi kabisa nachozungumza. Ebu rudia mada zangu nyuma kisha jaribu kutafakari zaidi ya kunukuu!...

Kuhusu rangi yako niliuliza pale tulipokuwa tukizungumzia maswala la Mapinduzi na maafa yaliyotokea kiasi kwamba tukapoteza dira na kuwa ni swala kati ya waarabu na weusi.
Ndio sababu hasa ya kuuliza wewe rangi gani maanake tusije kuwa tunazungumza kwa rangi hapa badala ya Mapinduzi na maafa yake.

Tena nashukuru sana unaposema kwamba Zanzibar leo hii watu hawatazamani kwa rangi zao... hii ni alama kubwa sana na mafanikio ya Mapinduzi yale. Na kama umewahi nisoma mara nyingi mimi sipendi kabisa tunapo jadili kitu kwa kuzitazama nafsi zetu, rangi zetu, jinsia zetu bali hupenda kujadili issue zinazotuhusu sote kwa ujumla.

Hizo siasa za Zanzibar, huna haja ya kunitumia kama ni zinatoka Al noor maanake huzisoma na kwa bahati nzuri marafiki zangu wengi Wazanzibara na Wangazija na kwa kiasi kikubwa naiona Zanzibar kwa sura zote mbili.
Nitarudia kusema kwamba Wazanzibar siku zote wamekuwa nyuma kuelewa mbinu za CCM na mara nyingi anawapiga mabao ya penalt!.. kucheza mwacheza nyie , chenga mwawala lakini mshindi ni CCM kwa sababu mitego yote anayoiweka nyie kuingia kama ndege aloona mtama!..
Sasa nadhani turudi kwenye mada yenyewe maanake tumetoka ktk Mapinduzi na kuzungumzia haya ya leo kwa kisingizio cha Mapinduzi. Na kama utakumbuka niliwauliza swali moja! Bila mapinduzi yale unaweza kufikiria Zanzibar ya leo ingekuwaje?... wakati nchi zote zilizodai uhuru wa Bandia wakati ule zilianzisha mfumo wa Apartheid!.. Sultan ndiye aliyevikwa taji ya head of state!.. kweli hiyo Zanzibar ingekuwa tofauti na Rhodesia?.. Kama ni swala la Hizbu kuwa chama chenye weusi nilisema hata chama cha Ian Smith kilikuwa na weusi. Tanzania leo hii tuna viongozi weusi na wengi wao walikuwa against Mkoloni kwa Unyonyaji wao. Leo hii hawa wazee viongozi wetu ndio wanyonyaji wakubwa!..Hivyo basi hakuna guarantee yoyote ambayo inatuonyesha kuwa viongozi wa Hizbu wangekuwa tofauti na CCM/ASP. Hizi hadithi za kujaribu kujenga Umoja tumeziona ktk tawala zote za kiafrika na kwa bahati mbaya ndizo zimetugawa zaidi sisi wenyewe kuliko Mkoloni ambaye aliwakumbatia macheif wetu kutuweka sawa kama taifa moja la Tanganyika ama Zanzibar. Leo hii tunagawanyika ndani sisi wenyewe bila kujali rangi zetu ila mipaka iliyowekwa na Mkoloni kutumika kama ndio pindo la ardhi.

Kifupi ndugu yangu mimi siamini kiongozi yeyote yule ambaye anasimamia kundi la watu na wengine walobaki wanakaribishwa wakipenda ati nafasi yao ipo!

mkandara, nadhani jibu lililokuwa nikupe tayari jemba jemba amekupa. ila tu naongezea kwamba huwezi ukajadili mapinduzi na ukaweza kuiepuka hali ya kisiasa ya sasa zanzibar ,kwani chimbuko la mpasuko ulokuwepo sasa ni siasa inayohubiri malengo potofu ya mapinduzi.
 
ni muungano ambao kwavile upo basi tuuchukulieni tu na tuurekebishe pale panapohitajika ila kiukweli hasa basi hakuna raia wala mwananchi hata mmoja anaejua siri ya muungano huu, nakumbuka kuna vijana wa kizanzibari wale waliojitolea kumuhoji mwanasheria mkuu kuhsu waraka wa muungano na wakazungushwa zungushwa na kuachwa patupu,mpaka walitishia kuenda umoja wa mataifa ila sijui walifikia wapi? na juzi huko baraza la wawakilishi akaskika mjumbe mmoja wa baraza akisema hakuna umuhimu wa raia kuona waraka wa muungano kwani huu ni muungano halali unaotambulika umoja wa mataifa. nadhani umefika wakati kuwekwe kura ya maoni kuhusiana na muungano.kwani zogo limekuwa jingi kutoka pande zote mbili za muungano.watanganyika wanahisi zanzibar ni tegemezi ,na zanzibar wanahisi muungano umewazuilia opportunity nyingi sana kwa kuondoshewa identity yake ya kuwa independent country.alimradii ni zahma tu ,dunia hii ya leo.
 
mkandara, sikupenda niweke hii video ila imenilazimikia, ewe mola wetu naomba tuondoshee dhulma katika ardhi zetu.
hawa vijana wanateswa maskini na wala hawana chembe ya uarabu wala usultani.itikadi yao imewaponza maskini .hii ndio siasa ya zanzibar tunayokwambia hujaielewa bado ,mkandara.
http://www.youtube.com/watch?v=P1-YuxjdcvU
 
Njembajemba,

Hata sielewi umeandika kitu gani hasa!..
Katika hizo picha hapo juu ambazo ni black and white nambie hata mtu mmoja mweusi ktk picha ya kwanza!.mimi sikuona ila nimeona waarabu, hakuna aliyechanganya na Mmatumbi!
Pili, huyo Tippu Tip amehusika vipi na utawala wa Kisultan kama sii sababu ya kusema kuwa weusi ndio walikuwa watu wabaya!...
Mjomba nchi tumeisha ichukua wenyewe na nasema hivi huyo Tippu Tip alikuwa MLANGUZI (middleman) mnafiki na mshenzi aliubeba utumwa wa akili kwa roho yake. Na huyu Tippu Tip tungeweza ku deal naye kama sio nguvu ya dola ya hao ulowaweka hapo juu, Ma - King, Ma- Sultani wenye majambia kiunoni!.. Na kweli yawezekana wanatakiwa kupongezwa kwani kwa unyama wao, leo hii Zanzibar ni kisima cha Utalii!..
Mjomba, U r missing the point na kama wewe wataka kupoteza mada hii hiyo shauri yako isipokuwa nasema Mapinduzi yalikuwa halali na sisi Bara tutaendelea kuyalinda na kuyapongeza kwa Udi na Uvumba.

T tonga,
Hicho kisa hata hakina kichwa kabisa!... Sasa ulitegemea katika Mapinduzi ya silaha watu hufa bila kuwepo muuaji?.. Huyo mzee uliyemtaja pengine naye alikwisha wapoteza wazazi wake maana ke hii inaonekana kama vile ni tamthilia. Wakati akimuua baba yake na kumzini mama yake yeye huyo binti alikuwa wapi?... chini ya uvngu kama sikosei! haaa!... KIA HUA Meree!
Zanzibar ni kisiwa kidogo sana, karibu kila kisa kinajulikana na vigumu sana kuwa huyo mzee hakuweza kuuliza jina la mtoto huyo wa kike katika kumsifia. Ni ustaarabu wa Wazenj, kutoa shukran kwa majina na pengine kuulizia ubin wa mtoto hata kwa majirani.

Hizi tamthilia za Kizenj zimejaa tele na wala sintashangaa kusikia kisa hiki ambacho kingepata bei kubwa Mumbai ktk utengezaji wa sinema.
 
duh hicho kipande cha filamu kimenitoa machozi, na hapa ndipo hupata kigugumizi kushirikiana na polisi, kuna kipindi nilikuwa nikisikia polisi kapigwa hutamani angeuliwa.

na ukitazama hii na kushuhudia yaliotokea utajua kwa nini polisi pemba aliuliwa na kufukiwa, wallahi wako right.

si uongo mtu hadi nae kupata ujasiri wa kuamua liwalo na liwe si hatua ndogo.

tuombe mungu yasitokee tena, ila hii pia ni ishara nyengine inayoonyesha kuwa muungano huu una walakin iweje polisi chombo cha muungano kunyanyasa raia na serikali ya muungano kukaa kimya.


nnaamini serikali inajua fika yanayotendeka, ila kwa maslahi yao wenyewe wananyamaza kimya.


hii ni hatari maana inapalilia chuki, na kufanya hata hayo mapinduzi yawe halali kuondoka uhalali wake.


mie sikufichi zanzibar ni kwetu na sina pengine pa kukimbilia ila nikikumbuka madhila na mateso nimekuchukia sina hata hamu nako
 
Njembajemba,

Hata sielewi umeandika kitu gani hasa!..
Katika hizo picha hapo juu ambazo ni black and white nambie hata mtu mmoja mweusi ktk picha ya kwanza!.mimi sikuona ila nimeona waarabu, hakuna aliyechanganya na Mmatumbi!
Pili, huyo Tippu Tip amehusika vipi na utawala wa Kisultan kama sii sababu ya kusema kuwa weusi ndio walikuwa watu wabaya!...
Mjomba nchi tumeisha ichukua wenyewe na nasema hivi huyo Tippu Tip alikuwa MLANGUZI (middleman) mnafiki na mshenzi aliubeba utumwa wa akili kwa roho yake. Na huyu Tippu Tip tungeweza ku deal naye kama sio nguvu ya dola ya hao ulowaweka hapo juu, Ma - King, Ma- Sultani wenye majambia kiunoni!.. Na kweli yawezekana wanatakiwa kupongezwa kwani kwa unyama wao, leo hii Zanzibar ni kisima cha Utalii!..
Mjomba, U r missing the point na kama wewe wataka kupoteza mada hii hiyo shauri yako isipokuwa nasema Mapinduzi yalikuwa halali na sisi Bara tutaendelea kuyalinda na kuyapongeza kwa Udi na Uvumba.


Mkandara,

Hamujakatazwa kuyalinda Mapinduzi nyie yalindeni mpaka kiama kifike mie hainisumbui, mimi mlinzi wangu ni Mungu.


Narudia tena kusema wazanzibari ni watu waliochanganya sana rangi (kwa vile ni kisiwa)tofauti na Tanganyika. unasema picture ni black and white? sasa ulitegemea wakati ule kuwe na picture za rangi?

Hao Masultani walikuwa wakiwaoa wanawake weusi (waafrika)sasa kama kulikuwa na ubaguzi wa rangi kweli wangeliweza kuwaoa watu weusi?

Barghash.jpg
huyu nae anatofauti gani na watu wa Zanzibar? si sawa sawa na Seif Sharifu tu? au nae ni muarabu?
The third Sultan of Zanzibar (Barghash), he ruled from 1870 until 1888. His mother was a slave (who was freed upon his birth; many Zanzibar Sultans were sons of slave women).


Unaweza kututajia unyama ambao waliufanya hao waarabu ambao umeushinda unyama tunaofanyiwa na CCM sasa hivi baada ya kujitawala?

Mimi naona unyama waliofanya na wanaoendelea kuufanya CCM ni mbaya zaidi kuliko huo waliwahi kuufanya hiyo mijiarabu.
 
mkandara, sikupenda niweke hii video ila imenilazimikia, ewe mola wetu naomba tuondoshee dhulma katika ardhi zetu.
hawa vijana wanateswa maskini na wala hawana chembe ya uarabu wala usultani.itikadi yao imewaponza maskini .hii ndio siasa ya zanzibar tunayokwambia hujaielewa bado ,mkandara.
http://www.youtube.com/watch?v=P1-YuxjdcvU


under_age,

huo unyama unaofanywa na hao Askari polisi wa CCM humo ndani ya hiyo video ni mdogo tu kati ya dhuluma kubwa za kutoa roho zisizokuwa na hatia na wengine kubakia vilema.

Lakini kama tulivyosema huko nyuma kuwa tusahau yaliyopita na tujenge Zanzibar mpya, na hayo mengine tumueachie Mola yeye ndie atakae kwenda kuhukumu na kumpa kila mmoja haki yake.
 
Mwanzoni hata mimi nilikuwa na mtazamo huo wa kudhani kuwa watu hawa walikuwa ni waarabu. Baada ya kufuatilia historia ya na utamadunzi wa Zanzibar kwa makini sana nimegundua kuwa Zanzibari ilikuwa ni taifa la mchanganyiko sana tofauti na ilivyokuwa Zimbabwe, Afrika ya Kusini na au Marekani ya miaka hiyo. Ilikuwa ni vigumu sana kumpata mwarabu kweli visiwani pale miaka hiyo ya ukoloni, waliokuwapo ni wazanzibari waliokuwa na damu ya kiarabu. Masultani wengi waliokuwapo wakati wa ukoloni walikuwa wamechanganya wa damu mchanganyiko wa waarabu na waafrika; hawatofautiani kabisa na viongozi wetu wa kitaifa wa sasa hivi kama Dr. Salim Ahmed Salim (kipenzi kikuu cha Mwalimu), Professor Abdul Rahaman Babu (a one time friend of Mwalimu), Sheikh Seif Sharif Hamad na hata Marehemu Mzee Thabit Kombo.

Mpaka sasa sioni sababu yoyote ya msingi inayohalalisha ASP kuendesha mapinduzi yale; ule ulikuwa ujambazi na uroho wa madaraka tu.
 
Mwanzoni hata mimi nilikuwa na mtazamo huo wa kudhani kuwa watu hawa walikuwa ni waarabu. Baada ya kufuatilia historia ya na utamadunzi wa Zanzibar kwa makini sana nimegundua kuwa Zanzibari ilikuwa ni taifa la mchanganyiko sana tofauti na ilivyokuwa Zimbabwe, Afrika ya Kusini na au Marekani ya miaka hiyo. Ilikuwa ni vigumu sana kumpata mwarabu kweli visiwani pale miaka hiyo ya ukoloni, waliokuwapo ni wazanzibari waliokuwa na damu ya kiarabu. Masultani wengi waliokuwapo wakati wa ukoloni walikuwa wamechanganya wa damu mchanganyiko wa waarabu na waafrika; hawatofautiani kabisa na viongozi wetu wa kitaifa wa sasa hivi kama Dr. Salim Ahmed Salim (kipenzi kikuu cha Mwalimu), Professor Abdul Rahaman Babu (a one time friend of Mwalimu), Sheikh Seif Sharif Hamad na hata Marehemu Mzee Thabit Kombo.

Mpaka sasa sioni sababu yoyote ya msingi inayohalalisha ASP kuendesha mapinduzi yale; ule ulikuwa ujambazi na uroho wa madaraka tu.

Kichunguu,
na hata huyu rais wa sasa hivi Amani Karume mama yake ni mwenye asili ya kiarabu (Mama Fatma Karume)

Kwa hiyo masuala ya ubaguzi wa rangi Zanzibar haupo na wala haujawahi kuwepo - zanzibar kuwa kuna ubaguzi wa rangi ni uzushi tu usiokuwa na maana.

Niliwahi kusema huko nyuma kuwa yale Mapinduzi sababu yake kubwa ni uchu wa Madaraka tu wala hamna sababu nyengine, hizo sababu nyengine ni za kuhalalisha tu Mapinduzi yale period
 
Kwa vile wazanzibari wanaweza kuja bara na kufanya biashara na kulima mashamba na ambavyo wabara wanaweza kwenda zanzibar na kufanya bisahara hata na kulima mashamba au kuvua baharini, ndivyo vivyo hivyo mapato yatokanayo na madini au mafuta yangekuwa yanasambazwa pande zote za muungano.
 
hawa hasa ndio serikali ya mapinduzi wanavyoendesha nchi, wameondoa ubaguzi wa mwarab na kuleta usawa.

ona jinsi walivyowaadilifu, sasa kama uliwahi kuwapo zanzibar hutoshangaa nini kinaendelea.
MAPINDUZI DAIMA
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/7/26/habari4.php

Wawakilishi wambana Shamuhuna




na Mwandishi Wetu, Zanzibar



WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Chama cha Wananchi (CUF), wamembana Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Ali Juma Shamuhuna kwa kuvitumia vibaya vyombo vya habari vya umma dhidi ya wapinzani.

Aidha, baadhi ya wajumbe wamesema wizara yake inachangia baadhi ya waandishi wa vyombo vya serikali kuwa ombaomba kutokana kutolipwa posho zao na kupatiwa maslahi duni.

Walitoa mfano tangu kuanza kikao cha bajeti ya serikali katika mwaka wa fedha 2007/08 mwezi uliopita, mawaziri vivuli wamekuwa wakikatiwa hotuba zao katika Televisheni Zanzibar na Radio Zanzibar, mara wanaponyanyuka kwa ajili ya kuwasilisha hotuba zao.

Mwakilishi wa Muyuni, Ramadhan Nyonje Pandu (CCM), alisema wizara hiyo imekuwa haiwatendei haki wafanyakazi wake katika vyombo vya habari, kwa vile waandishi wa habari wanaofuatilia shughuli za baraza hilo hawajalipwa posho tangu Januari, mwaka huu.

Kiongozi wa upinzani katika baraza hilo, Abubakar Khamis Bakar, alisema kwamba mwenendo wa utendaji wa vyombo vya habari vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), si wa kuridhisha katika uimarishaji umoja wa kitaifa, demokrasia na misingi ya utawala bora.

Alisema kwamba yeye binafsi atakuwa mgumu kupitisha bajeti ya wizara hiyo hadi atakapopata maelezo ya kutosha juu ya sababu za vyombo hivyo vya umma kutotenda haki.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Fatma Fereji (CUF), alisema kwamba pamoja na vyombo hivyo kutakiwa katika muafaka wa CCM na CUF wa mwaka 2001 kutenda haki, hali bado haijabadilika hadi hivi sasa.

Alisema kwamba ni jambo la kushangaza kuwa, tangu kikao cha bajeti kianze, vyombo hivyo vimekuwa havionyeshi hotuba za mawaziri vivuli na hukata matangazo baada ya mawaziri wa serikali kuwasilisha bajeti zao.

Alisema kwamba waziri lazima atoe maelezo ya kutosha kwa nini vyombo hivyo vinashindwa kubadilika, hasa kwa kuzingatia waziri anayeviongoza ni miongoni mwa waliokuwa makamishana wa tume ya kusimamia muafaka huo wa CCM na CUF.

Mwakilishi wa CUF kutoka Jimbo la Mtambwe, Salim Abdallah Hamad, alisema uhuru wa vyombo vya habari bado haujapatikana Zanzibar na ndiyo maana vyombo hivyo huripoti matukio kinyume cha yalivyotokea.

Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan (CCM), aliitaka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar, iwarejeshe wafanyakazi walioondoshwa, hasa kutoka TVZ na kupelekwa katika idara nyingine.

Aidha, alisema kwamba imefika wakati Serikali ya Zanzibar ihakikishe viongozi wanawashirikisha waandishi wanapofanya ziara za nje kama anavyofanya Rais Jakaya Kikwete.

Mwakilishi huyo alisema kwamba ni jambo la kushangaza serikali imesema mwelekeo wake ni kutonunua magari ya mitumba, lakini hivi sasa wafanyakazi katika sekta ya habari wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na magari yaliyonunuliwa hivi karibuni kuharibika yakiwa yamenunuliwa katika muda mfupi.
 
duh hicho kipande cha filamu kimenitoa machozi, na hapa ndipo hupata kigugumizi kushirikiana na polisi, kuna kipindi nilikuwa nikisikia polisi kapigwa hutamani angeuliwa.

na ukitazama hii na kushuhudia yaliotokea utajua kwa nini polisi pemba aliuliwa na kufukiwa, wallahi wako right.

si uongo mtu hadi nae kupata ujasiri wa kuamua liwalo na liwe si hatua ndogo.

tuombe mungu yasitokee tena, ila hii pia ni ishara nyengine inayoonyesha kuwa muungano huu una walakin iweje polisi chombo cha muungano kunyanyasa raia na serikali ya muungano kukaa kimya.
mtumwitu,nakuunga mkono, inauma ,tena inauma ,kisha inauma kweli kweli, ila nadhani tusichoke kwani makosa yaliofanywa na waliopita basi mimi na wewe ndio wa kuyarekebisha. mpaka leo naamini kwamba wazanzibari wao kwa wao hawana chuki ila kuna chuki ambayo inapandikizwa kupitia siasa ili wenye kunufaika wanufaike kwenye maslahi yao, na amini mungu hao wanaowatumilia wazanzibari kwa ajili ya maslahi yao ni wachache sana. bado naikumbuka siku salmin walipoingia muafaka na seif sharrif! ,ndani ya wiki zile mbili za muafaka mchege basi zanzibar ilijaa nuru ,upendo,umoja,hadhi, isipokuwa kama kawaida kuna wengine hawakuipendelea hali ile na ikabidi patiwe vichokono chokono na naam walifanikiwa kwani tukakubali kurudishwa tulikotoka,.
kama mapinduzi yalikuwa ni kumuondosha sultani basi sultani keshaondoka , tena haya mateso yanini jamani?
mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.naiomba serikali ya zanzibar ikae na itafakari na ikubali umoja katika jamii na pia nawaomba wapinzani nao wapunguze ukaidi ,kwani kinachohitajika kuiokoa zanzibar sasa si chama bali ni umoja!
kama mapinduzi yalikuwa na lengo la kuondosha chuki basi tunaomba serikali ya mapinduzi ioneshe kwa vitendo ni kiasi gani inaweza kuzima chuki baina ya wazanzibari.
 
Jamani eeeeh, msitake kudanganya watu hapa. Hili somo la rangi za watu mimi sikupenda kabisa kulizungumzia ila nimelazimika kwa sababu kila napojaribu kuweka maelezo yangu sawa nyie huzidi kuuburuta Uarabu na weusi kati ya wanananchi wazawa wa Zanzibar. Swala ni Sultan ambaye ametokea kuwa mwarabu.. hata kama angekuwa mzungu ama mweusi huyu ni mgeni anayetawala nchi yetu akitokea hukoooo alikotoka!.. mambo ya South kwani Ian Smith hakuwa mzimbabwe? ama Boitha Msouth!.. hupindui mtu kwa rangi yake bali Utawala!.. na mtawala alikuwa Sultan....Period!

Kwanza nianze na Under_age, hiyo video ni ya mwaka 2005, sidhani kama inahusiana kabisa na Mapinduzi. Ni sawa na kunionyesha video ya Mwembechai nianze kulalamikia Uhuru wa Tanganyika chini ya TANU. Ama Uhuru wa Rhodesia kwa sababu ya Mugabe kung'ang'ania kiti cha Urais huku aki watesa watu wake wale wale kama sii baba zao waliopigania Uhuru ule.
Tuwe na mtazamo nje ya kuweka visingizio! nakumbuka enzi zetu sisi tulikuwa tukilaani baba zetu kwa kutuzaa Afrika tukiona Mabaharia wakirudi na nmiguruwe (Pijo 504) pamba kali Degrese na raba. Kwa mtazamo finyu tuliyaona yale ndio maisha na maendeleo kwa sababu tulikuwa kizani. Na upumbavu mkubwa kumlaumu mzazi wako kama sii upofu wa akili... samahani jamani nazungumzia mimi na wenzangu wakati ule.
Tunachozungumzia hapa ni Mapinduzi ya Zanzibar na huwezi kunambia athari zilizopo leo zimetokana na Mapinduzi yale hali hata kabla ya Mapinduzi hawa jamaa walikuwa wakiuana. Historia inasema hivyo na muda wote mnaepa kujibu swala la Sultan kuwa head of State wakati uchaguzi umefanyika na Hizbu wameshinda. Huyu nani apewe nchi hali kutawala maanake ndio tafsiri ya head of State.. Hiyo celemonial nemdeni kwambie Waingereza maneno hayo kama watakueleweni. Sasa nakuombeni nipeni historia ya chama cha Hizbu!..kisha tutaendelea.

Jembanjemba,
Haya maswala ya rangi wala usiyaanze kutafuta sababu. Nakuomba unipe jina la mwafrika mweusi mwanaume ambaye alioa mwanamke mwarabu enzi za Sultan!..tena iwe hadharani na kusherehekewa.
Hii habari ya watu kuchanganya damu mbona ipo upande mmoja tu. Hata South Africa, Mozambique, Rhodesia, Angola na Namibia wazungu wanaume walikuwa wakiruhusiwa kuoa mwanamke mweusi lakini sio mwanaume mweusi kuoa mwanamke wa Kizungu. Hii ni historia ambayo hamuwezi kuibadilisha kamwe pamoja na kwamba kuna mchagnganyiko wa rangi ktk nchi zote hizo.
Kichuguu ndugu yangu hawa jamaa waarabu wabaguzi hakuna kama wao hata kati yao wenyewe. Jaribu kuuliza historia ya watu hawa na moja ya sifa kubwa ya Mtume Muhammad ni kuweza kuwaweka watu hawa kiti kimoja achana kabisa na mtu wa nje na hasa rangi nyeusi. Ni wabaguzi hadi leo hii tunavyozungumza hasa Saudia mjomba huwezi kuchukua mtoto wa Kiarabu kama wewe ni Mwafrika mweusi. Maanake tusiwe tunazungumza tu weusi weusi kwani wapo waarabu weusi. Na hata wale Wazanzibar waliokwenda Oman leo hii wanaitwa Wazenjibar! na wametengwa na waarabu wenye nchi kama vile wa Ethiopia wanaodai kuwa wao ni Jews wamewekwa ktk kambi kama second class citizen Utafikiria wao ni Aboliginal wa Middle east!.
kwa hiyo msitake kabisa ku bring hili swala la rangi hata kidogo! Hili ni swala zito sana ktk jamii zetu na kila mtu anajaribu kuukubali ukweli kwa njia zake. Kwani hata Bongo leo hii wapo waarabu wanachuki kubwa kuoza watoto wao wa kike kwa mtu mweusi. Ni down hill the other side, sisi weusi hatuna nongwa na mwarabu, mhindi, mzungu na kadhalika kwa sababu ya umaskini wetu wa mali na akili.
Trust me, sii warabu wala wahindi hawa jamaa wote ni wabaguzi kuliko hata mzungu inapofikia swala la ndoa. kwa hiyo mnapozungumzia wanawake sijui mwanaume gani asiyependa kuwa na kitoweo cha kila namna kwa tonge lake la Ugali ama wali.
Kama wanavyosemakisayansi:- Socket ya Umeme (female) ukutani ni moja lakini huingia kila aina ya vifaa vya moto.

Tukiachana na darasa hilo. Turudi ktk Mapinduzi. bado kabisa hamjaweza kunishawishi kuwa mapinduzi yale hayakuwa halali!... mnachokifanya ni kueleza matatizo ya leo hii kutafuta sababu za kukandya Mapinduzi.. Huu ni mfano mbaya sana ambao unalingana na kumtukana mama yako kwa kukuzaa kwa sababu leo hii unatazama maisha yako duni!. Ni mtazamo finyu ambao hauna mantiki kabisa.. mtanisamehe pamoja na kwamba nakubaliana nanyi ktk kipengele cha CCM/ASP kuwapora wananchi wake UHURU wao wa kweli ambao waliuchukua toka kwa Mkoloni - SULTAN.
Ukiniuliza kama kunahitajika Mapinduzi leo hii nitasema ndiyo lakini sintaweka lawama kwa wale walioweza kupindua serikali hii ikiwa malengo yao ni kuondoa dhulma hii... ILa hakuna guarantee ya kwamba hao watakao shika madaraka wataweza kweli KUONGOZA badala ya KUTAWALA. Na sababu kubwa ni UCHUMI wetu. Imetuuwia vigumu sisi waaafrika KUONGOZA nchi KIUCHUMI bila nguvu ya KUTAWALA!.. na kutawala ktk fasihi yetu ni UBWANA, UNYAPALA, UBWANYENYE ambao kwa muda wote wa Utumwa ndio ilikuwa dream ya mwafrika. A Wish come true!..
Hiyo ndio mirathi waliyotuachia wakoloni ukitanguliwa na Ujinga!
 
]Sasa nakuombeni nipeni historia ya chama cha Hizbu..kisha tutaendelea.

Jembanjemba,
Haya maswala ya rangi wala usiyaanze kutafuta sababu. Nakuomba unipe jina la mwafrika mweusi mwanaume ambaye alioa mwanamke mwarabu enzi za Sultan!..tena iwe hadharani na kusherehekewa.
Hii habari ya watu kuchanganya damu mbona ipo upande mmoja tu. Hata South Africa, Mozambique, Rhodesia, Angola na Namibia wazungu wanaume walikuwa wakiruhusiwa kuoa mwanamke mweusi lakini sio mwanaume mweusi kuoa mwanamke wa Kizungu. Hii ni historia ambayo hamuwezi kuibadilisha kamwe pamoja na kwamba kuna mchagnganyiko wa rangi ktk nchi zote hizo.
Kichuguu ndugu yangu hawa jamaa waarabu wabaguzi hakuna kama wao hata kati yao wenyewe. Jaribu kuuliza historia ya watu hawa na moja ya sifa kubwa ya Mtume Muhammad ni kuweza kuwaweka watu hawa kiti kimoja achana kabisa na mtu wa nje na hasa rangi nyeusi. Ni wabaguzi hadi leo hii tunavyozungumza hasa Saudia mjomba huwezi kuchukua mtoto wa Kiarabu kama wewe ni Mwafrika mweusi. Maanake tusiwe tunazungumza tu weusi weusi kwani wapo waarabu weusi. Na hata wale Wazanzibar waliokwenda Oman leo hii wanaitwa Wazenjibar! na wametengwa na waarabu wenye nchi kama vile wa Ethiopia wanaodai kuwa wao ni Jews wamewekwa ktk kambi kama second class citizen Utafikiria wao ni Aboliginal wa Middle east!.
kwa hiyo msitake kabisa ku bring hili swala la rangi hata kidogo! Hili ni swala zito sana ktk jamii zetu na kila mtu anajaribu kuukubali ukweli kwa njia zake. Kwani hata Bongo leo hii wapo waarabu wanachuki kubwa kuoza watoto wao wa kike kwa mtu mweusi. Ni down hill the other side, sisi weusi hatuna nongwa na mwarabu, mhindi, mzungu na kadhalika kwa sababu ya umaskini wetu wa mali na akili.
Trust me, sii warabu wala wahindi hawa jamaa wote ni wabaguzi kuliko hata mzungu inapofikia swala la ndoa. kwa hiyo mnapozungumzia wanawake sijui mwanaume gani asiyependa kuwa na kitoweo cha kila namna kwa tonge lake la Ugali ama wali.
Kama wanavyosemakisayansi:- Socket ya Umeme (female) ukutani ni moja lakini huingia kila aina ya vifaa vya moto.

Mkandara,

Historia ya chama cha HIZBU unaweza kuipata katika kile kijitabu alichokileta Mwl Kichunguu.

Hata nikikutajia huyo mtu mweusi alieoa mwanamke wa kiarabu utaamini? wakati wewe hujawahi kuishi Zanzibar na wala huwajui wananchi wa Zanzibar, si utasema nakudangaya?

Mzee Mkandara usiifanishe Zanzibar na South Africa au Zimbabwe, kwa sababu Zanzibar zaidi ya asilimia 95% ni waislamu na uslamu unakataza watu kubaguana kwa rangi, kama ulivyosema kuwa Mtume Muhammad (SAW) ndie aliyekuja kuwaweka watu pamoja na kuachana na tofauti za rangi. Nakubali kuwa inawezekana baadhi yao (waarabu) walikuwa wanawabagua watu weusi kwa rangi yao lakini sio kugeneralize kuwa waarabu wote ni wabaguzi wa rangi, kwani hata hao weusi inawezekana wapo ambao wanawabagua waarabu kwa rangi yao.

Mimi naamini Mapinduzi yale hayakuwa halali kwa sababu hayakuwa na lengo la kumuundosha sultani bali wale jamaa walikuwa na uchu wa madaraka tu, usultani ilikuwa ni kudanganya umma tu ili wafikie lengo lao.

Tusidanganyane bwana, mambo yote yanayotokea sasa hivi (mpasuko wa kisiasa zanzibar) ni reflection ya Mapinduzi ya mwaka 64. Na inaonyesha kazi ya kuziba ufa huo itachukua muda mrefu kwa sababu CCM bado fikra za Mapinduzi zimo kwenye akili zao, Seif Khatibu anathibitisha hayo:

Naye Waziri Khatib katika makala yake ya hivi karibuni, iliyochapishwa katika safu maarufu ya "Kipanga", inayochapishwa na gazeti la Mzalendo kila Jumapili, alisema muafaka pekee wa kweli ni ule uliofikiwa mwaka 1964 na kwamba, muafaka mwingine wowote utakaosainiwa baadaye utakuwa ni feki
. source:http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=717

Sasa hapa kuna kazi kweli kweli
 
mkandara, kuna sehemu uliniandikia kunambia kwamba inaonekana sikuelewi na ni kweli kabisa ni tabu kukuelewa kwani maongezi yako yameelemea kwenye uoni wa siasa lakini maongezi yangu yameegemea kwenye uhalisi wa mambo.pia katika maongezi yako unafuata kile kinachoongelewa na wengi duniani bila ya kuchunguza kutoka kwa wahusika,pia kosa lako jengine ni kushindwa kumuelezea mzawa kwa dira ya utaifa na badili yake unamuelezea kwa dira ya bara(continent) na rangi,na jengine ni pale unaposhindwa kukaa neutral katika kuyajadili haya mapinduzi,na namna unavyolazimisha ubaguzi ambao unashindwa kuutolea ushahidi,na la mwisho ni pale unaposhindwa kukubali kwamba zanzibar ni kisiwa chenye asili ya mchanganyiko wa wageni. kijana wa miaka 15 wa zanzibar ukimuuliza kwamba mpasuko wa siasa wa zanzibar umesababishwa na nini? basi atakujibu kwamba mapinduzi yamechangia sana,awe cuf au ccm.nashangaa pale unapoukiuka ukweli ambao mpaka serikali inatamka hadharani kwamba serikali haiwezi kutolewa kirahisi kwani ni ya kimapinduzi, tena unataka ushahidi gani?
acha hayo sasa turudi kwenye mapinduzi yenyewe.utakumbuka kwamba wengi walikuunga mkono kuhusu kuondoshwa kwa sultani lakini wakakupinga kuhusu malengo ya mapinduzi.hakuna atakaekubishia kwamba wazanzibari wenye asili ya kiarabu walikuwa ni watu na hawa waliopo madarakani sasa pia ni watu ,hivyo wana mazuri yao na mabaya yao ila la kujiuliza je kulikuwa na umuhimu wa mapinduzi? kama ukijibu ndio ina maana na sasa kuna umuhimu wa mapinduzi kwani dhambi iliosingiziwa wakati wa mapinduzi ndio dhambi tunayoiona sasa ,tafauti ni kwamba mapinduzi tunahadithiwa lakini haya ya sasa tunayaona kwa macho yetu.ila ninachokwambia ni kwamba zanzibar kwa miaka ya alfu tisa mia na sitini hakukuwa na ubaguzi wa rangi wala wa nywele, ni siasa iliokuwa na lengo mbali na lililotangaziwa kwa wananchi. na ndio ukikumbuka ni pale nilipokwambia kwamba mapinduzi yale hata kusingekuwa na sultani basi yangetokea, mapinduzi hayapangwi siku 33 tusidanganyane. kulikuwa na lengo zamaniii sana ila lengo hilo lilikuwa limefungiwa ndani ya briefcase ya mtu. ni nani? ingia porini ,tafuta walioshiriki na kuathirika katika mapinduzi watakupa clue. mie simoooo ,mie nahimiza umoja tu kwasasa.kwa upande wangu naweka "the end" kwenye mada hii ila nitaendelea kuisoma nijifunze mengi na zaidi kwa wenye kuchangia ,
ni mdogo wenu underage
 
Jembajemba,

Ndugu yangu weee lini utaweza kufahamu kwamba Usultan hauwezi kuwa ndio Uislaam hata Kidogo.. Na haiwezekani kabisa kwamba waislaam wa Zanzibar wote ni Ibadhi, dhehebu la huyo Sultan.
Jembajemba, Kuishi Zanzibar sio kufahamu yote, sijawahi kuishi South Africa ama Rhodesia lakini najua kulikuwepo na Apartheid!...Nimekutajia nchi zote hizo za kiarabu ikiwa ni pamoja na Oman wote ni wabaguzi kishenzi.. Na kwa sababu huna mtu yeyote mweusi aliwahi kuoa kwa mwarabu wakati wa Sultan ndio maana unachemsha! Huna story hapa mjomba na nakuhakikishia kama angekuwepo historia ingeweza kuweka kumbukumbu hiyo!... Hiyo ingekuwa historia kubwa kwa nchi zilizotawaliwa!
hakuna mwarabu, mzungu wa mhindi miaka ya 60 alikubali kuona binti yake akiolewa na mtu mweusi!.. Hii ni kweli ambayo huwezi kuibadilisha na hata leo hii ni wasichana wachache wa kiarabu waliokubali kukosa radhi za wazazi wao kuolewa na mweusi tena basi huyo mwarabu labda mwarabu Koko!..

Under_age,
hapana ndugu yangu wewe ndio unasukumwa na uzawa wak badala ya kutazam ninihasa lilikuwa lengo la Mapinduzi. Huyu kijana wa kmiaka 15 ambaye atasema ni kwasabu ya Mapinduzi ndio dhahiri inaonyesha kwamba mnatembeza propaganda nyingi sana dhidi ya Mapinduzi kwani huyu kijana hana kumbukubmu yoyote ya Utawala wa Sultan.
Mna wa brain wash vijana kuweza kuamini historia mnazoziandika nyinyi wenyewe kwa vidole vyenu.
Nimewauliza maswala mawili na Ombi moja.. tuweke hapa kila mtu anaesoma hapa apate kuona. Tusiweke habari za mimi nikasome ktk kitabu cha Kichuguu!.. Jibuni maswali yangu kwa hoja zenu na sio kunifanya mimi hoja yenyewe. Kila mara wee Mkandara hujui hiki wala kile nambie unachokifahamu wewe!..Haya maswala ya mchanganyiko nimesema hata huko Msumbiji na Angola kuna mchanganyiko tena mkubwa zaidi ya Zanzibar lakini wote wanafahamu kuwa Mreno alikuwa MKOLONI! wanaweza kuziona tofauti za kutawaliwa na kujitawala hata kama jua halija pungua ukali.
Na bahati mbaya ni wewe unayeshindwa kutengenisha Utawala na hisia zako za Uzanzibar kiasi kwamba umeshindwa kumtazama Sultan kama ni Mtawala mgeni toka Oman. Nimesema hata Ian Smith alikuwa/analo ganda la Zimbabwe, wareno na Makaburu wote koo zao zipo huko South zaidi ya karne 6, lakini hii haihusiani kabisa na Kutawaliwa na falme ya nje!..
Kwa hiyo tunapozungumzia Zanzibar hatuzungumzii rangi zao, haya ni maneno mmeyaleta nyie!. Waarabu kwa kwanza kuingia Zanzibar ni Persian, Wahindi wabarush, Wa Yemen hao wote hawahusiani kabisa na Utawala wa Sultan!..Na hawana uasili kabisa na Oman na pengine hesabu ya watu wenye asili ya Ki- Oman sio kubwa hata kidogo. Hivyo basi aliyepinduliwa ni Sulatn wa Oman na sio mwananchi mwenye asili ya Oman, Yemen ama Burush!..

Tunachozungumzia hapa ni MAPINDUZI na mapinduzi siku zote ni chimbuko la Kisiasa sio uhalisi wa mambo!.. kwani ktk uhalisi wakoloni wangeweza dai kila haki chini ya Utawala wao. Mbona South Afrika leo wameweza ishi wazungu na weusi chini ya Uongozi wa wananchi wenyewe na sio Utawala bandia wa wageni.. je hapa hakuna uhalisi ila ni siasa?
Swali la kwanza, Kwa nini Sultan alipewa kuwa Mtawala wa nchi ambayo imefanya uchaguzi na Hizbu kashinda!.
Pili, Ikiwa tawala zote za Mkoloni waliojipatia Uhuru bandia waliweza kuweka sheria za Apartheid. nini tofauti ya Utawala wa Sultan na huo wa hao Makaburu.

Mwisho naweka Ombi langu tena. Itoeni hadharani historia ya chama cha Hizbu!..

Tusizungushe, mkiniuliza swali najibu lakini nyie mnapinda kushoto na kulia maadam mnajaribu kuepuka Ukweli na hiyo mnayodai halisi ya mambo!
 
KUASISIWA HIZBUL-WATTAN (ZANZIBARNATIONALIST PARTY)

Wakati Sheikh Ali Muhsin akiwemo katika safari zake huko nchi za Ulaya,huko nyumbani walichomoza wananchi wengine waliokuwa nao na ghera na mapenzi ya nchi yao. (wote, isipokuwa mmoja tu kati yao - Sheikh Abdalla Mahmoud - walikuwa si Waarabu) Wananchi hao walikutana kuzingatia na kutafakari juu ya kupo-tea kwa nchi yao kutokana na mbinu za mkoloni za kuwagawa wananchi kwa kutumia asili za makabila yao. Wananchi hao waliibuka na amuo la kuanzisha Umoja wa Wananchi wa Unguja na Pemba. Umoja ambao kila raia wa Zanzibar atastahiki kuwemo bila ya kujali asili ya kabila yake wala Imani ya Dini yake, la umuhimu ni URAIA wake.

Hichikilikuwa ndio chama cha kwanza na pekee katika nchi kuasisiwa kwa kufua-tia misingi ya Uwananchi. Wananchi waasisi hao walikuwa ni, Sheikh Vuai Kiteweo, Sheikh Miraj Shaalab, Maalim Zaid Mbarouk, Maalim Maksud Fikirini, Maalim Mwandoa Khamis, Maalim Wazir Ali bin Maalim, Sheikh Haji Hussain Ahmed, Sheikh Othman Soud, Sheikh Abdulla Mahmoud Kombo (wa Makunduchi), Sheikh Ramadhan Tosir (Ramadhan Madafu), Maalim Hija (wa Ndijani), Sheikh Ame, Sheikh Abdulla Mali, Sheikh Haji
Kombo (wa Kiboje), Sheikh Abdalla Mahmoud na wenziwe wachache. Kwahivyo wale wenye kusema na kutangaza kuwa Hizbu (ZNP) iliasisiwa na Waarabu au kilikuwa chama cha Waarabu, hapana shaka wanakosea, amma kwa ku-tokujuwa ukweli ulivyo au wana-sema hivyo kwa makusudio ya kutafuta maslaha yao. Uk-weli na hakika ilivyo ni kuwa Hizbu haikuasisiwa na Waarabu wala hakijapata kuwa Chama chaWaarabu. Na kama Hizbu kinge-likuwa ni Chama cha Waarabu, basi kisingeweza kupata ushindi katika ch-aguzi zilizofanyika za (One Man One Vote) kwani idadi ya hao wenyekuitwa Waarabu nchini ilikuwa ndogo; kwahivyo idadi yao hiyo haingaliwezesha kukipa (hicho kisemwacho ni chama chao) voti za ushindi. Madai hayo ni miongoni mwa maneno na mbinu za ku¯tinisha na kuwagawa wananchi kwa kuuwogopa umoja wao. Hapana shaka zimetungwa na wakoloni na kuimbwa na vibaraka vyao, kwa maslahi yao. Mabwana hao tuliowataja hapo juu wakiwa ndio waasisi wa Chama cha Hizbul-Wattan, wao ndio waliy-omuendea Sheikh Ali Muhsin nyumbani kwake baada ya kurejea kutoka sa-
farini na kumueleza kukhusu kuasisi kwa chama chao na nini dhamiri zilizo wapelekea kuasisi chama hicho. Baada ya kumueleza, walimtaka na yeyeawaunge mkono kwa kujiunga katika chama. Sheikh Ali Muhsin alipoona kuwa hayo wayatakayo wananchi wenzake ndio hayo hayo ayatakayo na kuyapigia mbio daima basi, hapo hapo aliamua kujiunga na kushirikiana nao. Baada yakujiunga, waasisi hao walimtaka Sheikh Ali Muhsin aanze
kuzungumza na nduguze wenye asili za Kiarabu - bali na kila anaefahamiananae - ili wajiunge na wananchi wen-ziwao. Sheikh Ali aliupokea na kuanza kuutekeleza ujumbe huo. Miongoni mwa wa mwan-zo (kati ya hao wenye
kuitwa Waarabu) kujiunga na Umoja huo ni, Sheikh Badr Muhammed Bar-wani, Sheikh Ahmed Seif Kharusi, Sheikh Amour Zahor Ismaily, Sheikh Ali Ahmed Riyamy . Sheikh Nassor bin Isa Ismaily na Sheikh Ahmed Khalfan.Naamani haikuchukuwa muda ila nao walijiunga.

Hiyo ni historia fupi ya chama cha HIZBU.

Mkandara kwani ni nani aliyempa Sultani uhead of state? naomba unieleweshe
 
Mama Zanzibar!

Date: 15 Feb 2003

Umezaa na kulea, wengi mno auladi
Kubagua hukujua, ndani ya mwako fuadi
Huku kiwakumbatia, kuwalinda na hasidi
Baraka kiwamwagia, kuwafanya mashadidi
Siku mpya kingia, kukuta kwenye jihadi
Sio jua si mvua, lokukata juhudi
Mengi mevumilia, wewe kweli ni shahidi
Mabungo tukijilia, hakika tulifaidi
Wengi tumekukimbia, Tumehajiri biladi
Dunia tumeenea, Tumezivuka hududi
Si kwamba twapendelea, twakimbia ufisadi
Ni lini tutarejea, Ajuwae ni wadudi


Said Paul
 
Back
Top Bottom