Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

hakuna hasara, wala faida kwa muungano kuvunjika, sasa kuna umuhimu gani wa huu muungano kuwepo, Kwa faida ya nani.
leo hii baada ya kujadili katiba kwa niaba ya mtanzania maskini, katiba imekuwa no muungano mara serikali 3 na 2, Kwa manufaa ya nani, nini faida ya serikali 3 au 2 Kwa mtanzania masikini. acha muungano uvunjike kila mtu awe na serikali yake mambo yaendelee... leo hii wanasiasa wameiteka katiba, hawazungumzii tena yale ya maana kwa mtanzania masikini ila utasikia ooooh muungano, mara serikali tatu upumbavu mtupu.. TUAMKE WATANZANIA TUJIKOMBOE WENYEWE, TUSITEGEMEE KUKOMBOLEWA NAWANASIASA, TUWAKATAE ANZA SASA ULIPO GAP LA UMASIKINI NI KUBWA.

changia ili tujikomboe... tujengane kihoja na mawazo yaliotukuka.
kule zanzibar asilimia 60% wamesema wanataka muungano wa mkataba, yaani hawataki serikali 3, 2, wala muungano, huku bara wasiojua kinachoendelea na pengine kutokana na uchakachuzi 61% wanataka serikali 3. swali la msingi warioba amepata wapi hayo maoni ya serikali 3?
inashangaza kuona serikali isiyo sikivu inaandaa muswada feki wa serikali tatu. Nani aliwaambia tunataka serikali tatu, inamaana maoni ya zanzibar yamewekwa kapuni.
kama moja imeshindwa tutemane. tatizo nimegundua kuna elite wachache wanalindwa. ndio maana wanang'ang'ana na serikali 3.kwa maslahi ya nani, kwa kushirikiana kitu gani, huku wakijua gharama zitaongezeka.

Tanzania bara, tuna ardhi ya kutosha, tuna maji, madini, jeshi, mvua, mifugo,n.k. kwanini tusiwaache wazenji wakale tende na halua nchini kwao.
huu muungano ni wa ku-force, nadhani kuna haja ya kuachana. i am tired. i miss tanganyika.mimi kama mtanganyika sioni cha kutegemea kutoka visiwani, kama ni ardhi wao watakuja kwetu, kama ni maeneo ya kulima watakuja bara, kama ni biashara watakuja bara.MiMi nitaenda zenji kufanya nini cha msingi?tunashea nini na hawa wazenji mpaka tuogope kuwapa chao,
mbona wao ni majasiri kudai chao sisi mbona tunazunguka mbuyu. serikali tatu za nini kwa faida ya nani. Tuache kusikiliza maneno yenye mvuto kwa wanasiasa tunaaowapenda wakati wabara tunaibiwa kwenye ardhi yetu wenyewe ambayo ingetunufaisha tukiwa wenyewe. tanganyika imekuwa shamba la bibi. BNI wbara wangapi wamewahi kuvuka bahari wakaenda zanzibar, na wananufaika na nini? wakati wao sio raia mpaka sasa hivi wakiwa kule.

tungeweza kufikiria ushirikiano wa EAC, na tukaamua kuachana na zenji na kulipa madeni yote. jamani tumechoka tindikali!!
 
Habari wanaJF

Pamekua na mijadala mingi sana ndani na nje ya mitandao juu ya muungano. Na suala kubwa likiwa ni muundo wa serikali..

Tume ya JS Warioba imependekeza Muundo wa Serukali 3 Tena kwa hoja za kimataifa bila kumumunya maneno kwa kua anafahamu kero za muungano.

Lakini kila alipopita CCM aling'ang'ania serikali mbili bila hoja yoyote ya msingi.. na kwa kuashiria kua wana shinikizwa hakuna hata mmoja alietoa hata robo ya point alizotoa JS Warioba kutete wanacho kililia.. Hata yule Masai mtaalamu wa kulia hajaweza..

Kama kuna MwaCCM yeyote mwenye Point ya msingi ya kuitaka hii zanzibar au Serikali mbili aje atuambie na Ckukurupuka bila hoja.

Kuna nini CCM na Zanzibar...?
 
^^
Chama nacho ni kama binadamu, Binadamu anapofikia hatua za awali za uzee, huwa na tabia za kushikilia misimamo hata pasipo kutazama nyakati ziko wapi
^^
 
Waangalieni wazenji wawakilishi ktk bunge la jmt uchangiaji wao dhihaka! tuvunje muungano wa kutunyonya! angalia wizara ya afya, fedha,ulinzi wamepewa waunguja kwa nini?
 
hakuna hasara, wala faida kwa muungano kuvunjika, sasa kuna umuhimu gani wa huu muungano kuwepo, Kwa faida ya nani.
leo hii baada ya kujadili katiba kwa niaba ya mtanzania maskini, katiba imekuwa no muungano mara serikali 3 na 2, Kwa manufaa ya nani, nini faida ya serikali 3 au 2 Kwa mtanzania masikini. acha muungano uvunjike kila mtu awe na serikali yake mambo yaendelee... leo hii wanasiasa wameiteka katiba, hawazungumzii tena yale ya maana kwa mtanzania masikini ila utasikia ooooh muungano, mara serikali tatu upumbavu mtupu.. TUAMKE WATANZANIA TUJIKOMBOE WENYEWE, TUSITEGEMEE KUKOMBOLEWA NAWANASIASA, TUWAKATAE ANZA SASA ULIPO GAP LA UMASIKINI NI KUBWA.

changia ili tujikomboe... tujengane kihoja na mawazo yaliotukuka.

Mimi siku zote huwa nasema kwamba muungano huu ni bora uvunjike ili kila nchi ichukue 50 zake maana kila kukicha utasikia...muungano....muungano....muungano....muungano!! Mpaka kero...watu hatupumui, kila siku tukiamka tunakutana na hadithi za muungano! Utumwa huu mpaka lini?
 
Lipumba na zitto, mjue kuna leo na kesho acheni ushabiki, waungeni mkono wazenji wachukue chao.
nyinyi sio wazenji, muache kujipendekeza.muungano unaongeza umaskini nchini
 
muungano wa serikali tatu una faida kuu za kiusalama. Kubwa ni kwamba kwa hali ya kisiasa zanzibar kuna uwezekano mkubwa kutokuwa na stable government na baadae kutuletea shida bure

hata burundi na rwanda walizipiga we suvirved kenya walitwangana tukapona uganda mpaka leo konyi anazichapa tunadunda so muungano ufe wanaotaka kukaa zenji wakae na wabara wakae
 
Nilikuwa nikitafakari sana faida ya muungano na hasara zake. Pia muundo wa namna gani unatakiwa uwepo.
Jambo kubwa sana lilipo katika muungano ni swala la kiusalama la nchi zetu hizi mbili. Kwa upande wa Zanzibar ikijitenga kwenye muungano tu inaweza ikajigawa na kuwa pemba na unguja nchi tofauti. Au inaweza ikarudi kuwa koloni la waarabu tena na kuwa kisiwa cha machafuko.

Sababu zinazotajwa kero za muungano ni vema kukaa pamoja na kuwa na maridhiano.

kwa upande wa Tanganyika swala la kisalama ni pale Zanzibar itakapo jitenga kwa sababu iko na influence na ni koloni la uarabuni itakuwa katika tension ya kiusalama. Napia kutakuwa na chokocho za mipaka baharini je Zanzibar inaishia wapi na Tanganyika inaishia wapi.

upande wa muundo wa serikali ningependekeza iwe serikali moja na upande wa Zanzibar awepo governor vile vile upande wa Tanganyika awepo governor. Ambao moja kwa moja watawajibika kwa raisi.
 
Issue za kuwa na serikali mbili, tatu au zaidi ni kuvuta hisia za wananchi kujitambua kwa utaifa wao. Kuna watu wamezaliwa Zanzibar na wanaasili ya bara leo hii useme waondoke zanzibar waende wapi?
 
Issue za kuwa na serikali mbili, tatu au zaidi ni kuvuta hisia za wananchi kujitambua kwa utaifa wao. Kuna watu wamezaliwa Zanzibar na wanaasili ya bara leo hii useme waondoke zanzibar waende wapi?

Hakuna anayewalazimisha kuondoka. Mbona kuna watu wamezaliwa Kenya, Uganda etc na wana asili ya bara wanapeta tu? Muungano wa kijamii upo tu hata Zanzibar ikiwa nchi huru watu tutaendelea kuwapo tu.
 
Hakuna anayewalazimisha kuondoka. Mbona kuna watu wamezaliwa Kenya, Uganda etc na wana asili ya bara wanapeta tu? Muungano wa kijamii upo tu hata Zanzibar ikiwa nchi huru watu tutaendelea kuwapo tu.
pointi yako ni nini sasa hapa?
 
pointi yako ni nini sasa hapa?

Pointi yangu ni kuwa, mtu asiweke hofu mbele kwa kigezo cha kufukuzana toka sehemu moja ya nchi kwenda sehemu nyingine ya nchi. Nina maana huyu bwana ameona uwezekano upo wa watu kudai kila upande wa muungano uwe nchi huru kama jinsi kila upande ulivijitafutia uhuru bila kumshirikisha mwenzie
 
Hivi madhara yake unayajua au umeamua kuongea tu. Mtu kama bakhresa kawekeza makumi ya miaka leo hii umfukuze!! Tanganyika hivi negative effect unazifikiria au bora liende tu?
 
Hivi madhara yake unayajua au umeamua kuongea tu. Mtu kama bakhresa kawekeza makumi ya miaka leo hii umfukuze!! Tanganyika hivi negative effect unazifikiria au bora liende tu?

We una idea za kukaririshwa. Unadhani kuna waKenya wangapi wamewekeza Tanzania na mpaka sasa hivi hawana tatizo? Uwekezaji wa Bakhresa unahitajika sana na tutatangaza fursa zaidi si kwa waZanzibar tu, hata waCanada UK etc. Tumia na akili zako
 
Hujui unachoongea. Hivi fursa ya muwekezaji na raia ziko sawa. Vipi kuhusu ardhi wanayo miliki? Au unajibu hoja bila kutazama mapana. Na kuhusu bakhresa ni mfano acha kukariri.
 
Hivi madhara yake unayajua au umeamua kuongea tu. Mtu kama bakhresa kawekeza makumi ya miaka leo hii umfukuze!! Tanganyika hivi negative effect unazifikiria au bora liende tu?

Mbona amewekeza Msumbiji?Au kuna muungano na Msumbiji ?
Hakuna mtu atakayemfukuza mzanzibar kama atakua yuko bara.Wasiwasi wa kuvunjika kwa Muungano wanao wazbr kwa sababu ya hulka yao ya ubaguzi.Ardhi ya Zanzibar ni ya kwao wenyewe lakini ardhi ya Tanganyika ni ya Muungano..Muungano ni Tanganyika. Ni ukweli kwamba ujinga wa watanganyika ndio mtaji wa watawala na Wazenj kupora raslimali za Tanganyka.
 
Znz hatuwez kuiachia serkal tatu maana yake n kuachia znz sis hatufaidiki lolote na znz zaid ya kiusalama,position ya znz n mbaya sn kwa tanganyika, serkal inajua yote lkn n bora kuliko hili la kiusalama,na ndo mana kuna kamb jeshi yetu kule
 
Hujui unachoongea. Hivi fursa ya muwekezaji na raia ziko sawa. Vipi kuhusu ardhi wanayo miliki? Au unajibu hoja bila kutazama mapana. Na kuhusu bakhresa ni mfano acha kukariri.

We una hofu gani? Bakhresa ni mfanyabiashara wa kimataifa hana tatizo kama mawazo yako yalivyo. Nikurejeshe kwenye post yako kuu. Hivi Zanzibar ni koloni la waarabu wa wapi? Qatar, UAE, Yemen au nini. Ndo mana nakwambia umekaririshwa na hujui ulisemalo. Leo hii bado unaongelea kutawaliwa na Taifa lingine. We mtupu kweli
 
Mbona unakomalia Bakhresa au akili zako ndio mwisho wake. Nakuomba utoe hoja ya msingi kuhusu wale wanaomiliki ardhi na ni watu wa kawaida kabisa je mtataifisha ardhi yao au mtawapa fidia warudi kwao?
 
Back
Top Bottom