2013
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 11,360
- 6,069
kule zanzibar asilimia 60% wamesema wanataka muungano wa mkataba, yaani hawataki serikali 3, 2, wala muungano, huku bara wasiojua kinachoendelea na pengine kutokana na uchakachuzi 61% wanataka serikali 3. swali la msingi warioba amepata wapi hayo maoni ya serikali 3?hakuna hasara, wala faida kwa muungano kuvunjika, sasa kuna umuhimu gani wa huu muungano kuwepo, Kwa faida ya nani.
leo hii baada ya kujadili katiba kwa niaba ya mtanzania maskini, katiba imekuwa no muungano mara serikali 3 na 2, Kwa manufaa ya nani, nini faida ya serikali 3 au 2 Kwa mtanzania masikini. acha muungano uvunjike kila mtu awe na serikali yake mambo yaendelee... leo hii wanasiasa wameiteka katiba, hawazungumzii tena yale ya maana kwa mtanzania masikini ila utasikia ooooh muungano, mara serikali tatu upumbavu mtupu.. TUAMKE WATANZANIA TUJIKOMBOE WENYEWE, TUSITEGEMEE KUKOMBOLEWA NAWANASIASA, TUWAKATAE ANZA SASA ULIPO GAP LA UMASIKINI NI KUBWA.
changia ili tujikomboe... tujengane kihoja na mawazo yaliotukuka.
inashangaza kuona serikali isiyo sikivu inaandaa muswada feki wa serikali tatu. Nani aliwaambia tunataka serikali tatu, inamaana maoni ya zanzibar yamewekwa kapuni.
kama moja imeshindwa tutemane. tatizo nimegundua kuna elite wachache wanalindwa. ndio maana wanang'ang'ana na serikali 3.kwa maslahi ya nani, kwa kushirikiana kitu gani, huku wakijua gharama zitaongezeka.
Tanzania bara, tuna ardhi ya kutosha, tuna maji, madini, jeshi, mvua, mifugo,n.k. kwanini tusiwaache wazenji wakale tende na halua nchini kwao.
huu muungano ni wa ku-force, nadhani kuna haja ya kuachana. i am tired. i miss tanganyika.mimi kama mtanganyika sioni cha kutegemea kutoka visiwani, kama ni ardhi wao watakuja kwetu, kama ni maeneo ya kulima watakuja bara, kama ni biashara watakuja bara.MiMi nitaenda zenji kufanya nini cha msingi?tunashea nini na hawa wazenji mpaka tuogope kuwapa chao,
mbona wao ni majasiri kudai chao sisi mbona tunazunguka mbuyu. serikali tatu za nini kwa faida ya nani. Tuache kusikiliza maneno yenye mvuto kwa wanasiasa tunaaowapenda wakati wabara tunaibiwa kwenye ardhi yetu wenyewe ambayo ingetunufaisha tukiwa wenyewe. tanganyika imekuwa shamba la bibi. BNI wbara wangapi wamewahi kuvuka bahari wakaenda zanzibar, na wananufaika na nini? wakati wao sio raia mpaka sasa hivi wakiwa kule.
tungeweza kufikiria ushirikiano wa EAC, na tukaamua kuachana na zenji na kulipa madeni yote. jamani tumechoka tindikali!!