Hilo wazo kuwa USA ndio walishinikiza muungano mmeitoa wapi? Au ndio mambo ya kuruhusu wageni kutuandikia historia yetu. USA miaka ya sitini halikuwa taifa lenye shobo na mambo ya watu kama ilivyo siku hizi, kusema walishinikiza muungano ni kuwapa ujiko na u nafasi ambao hawana kwenye historia yetu ya kipindi hicho
Kijana, siwezi kukulaumu. Nazungumza hili kwa uhakika mkubwa. Siyo kwa kuokoteza habari, bali kwa kuzungumza na watu waliohusika.
Yaelekea huijui vizuri historia ya nchi hii zaidi ya vile vitabu vya historia vya shule za msingi. Tulipopata uhuru, rafiki mkubwa wa Mwalimu alikuwa Rais Kenedy. Na nchi rafiki wakubwa wa Tanganyika ilikuwa US na Germany. Na Germany ilikuwa ndiye agharamie mpango wote wa maendeleo wa miaka 5.
Mashirikiano yetu mapya na Ujerumani Mashariki na kifo cha Kennedy, na sera za Rais mpya ya US, , na Germany kufuta mpango wa kugharamia mpango wa maendeleo wa miaka 5, ilimfanya Mwalimu kuchukia na kuwageukia Wajamaa, maadui wa US na Germany, kama njia ya kulipiza kisasi.
Tanganyika baada ya uhuru haikuwa na sera ya Ujamaa, ujamaa ulikuja baadaye, tuliposhindwa pa kushika.
Mwungano wa Tanganyika na Zanzibar, uliasisiwa na Marekani. Henry Kissinger ndiye aliyekutana na Mwalimu. Mwalimu wakati huo alikuwa hajawahi kukutana na Karume tangu awe Rais wa Zanzibar, na wala hakuwa na ukaribu naye. Wazanzibari walionekana kuwa karibu zaidi na Wakenya kuliko Watanganyika. Ndiyo maana karata ya kwanza ya Kissinger ilikuwa kwa Jomo Kenyatta. Alipokataa, Kissinger akamwona Mwalimu. Kisha Kissinger alenda Zanzibar kuonana na Karume akiongozana na Mzee Kaduma. Kissinger akarudi tena kwa Mwalimu kumwambia kazi amemaliza. Baada ya hapo ndipo Mwalimu akasafiri kwenda Zanzibar.
Mwalimu alikuwa rafiki mkubwa wa Rais J.F. Kennedy. Hata baada ya kifo cha Kennedy cha ghafla, kuuawa kwa risasi Nov 22, 1963, aliyemfuatia, Lyndon aliendeleza urafiki na Mwalimu, japo sera ya nje ya US ilikumbwa na misukosuko mingi. Baadaye ilipodhihirika kuwa sera ya nje ya Marekani kwa Afrika ilikuwa imebadilika kabisa, Mwalimu ikabidi aanze kuutazama Muungano kwa namna tofauti badala ya matakwa ya US. Na ndipo mambo mengine ya kuongezwa yakaanza kufikiriwa. Agenda kuu ya Muungano mwanzoni, ilikuwa ni kuipa haki Tanganyika kuwepo kijeshi Zanzibar, na kuzuia Zanzibar kuwa na sera ya nje, ambayo ilionekana kuelekea kwenye ujamaa.