Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

muarobaini wa matatizo yote haya ni katiba tu.watangulizi waliitengeneza hiyo katiba kwa ajili ya kulinda maslahi yao na pia inawezekana mazingira ya wakati ule yaliwalazimu wafanye vile lkn kwa sasa hakuna njia nyingine zaidi ya kuwa na katiba mpya na sielewi kwa nn mamlaka zinaogopa kuwa na katiba mpya wakati majirani zetu wamezibadilisha katiba zao mara kibao.katiba tulionao inatubagua na pia inatoa mamlaka makubwa kwa watawala.

Katiba ya wapi Na huu ni uvamizi uliopewa Jina la muungano ?
 
Ni bora huu Muungano wetu ukavunjika halafu tukawa nchi jirani zenye kupendana kuliko maelezo,ila hivi tulivyo inakuwa kama hatuelewani.
Tugawane mbao kisha kila mtu ajenge mtumbwi wake.
Tatizo wabara hawajiamini kujitawala,wanahisi watagawika ,Zanzibar imekuwa kama hirizi.
Sasa unafikiri Zenj ikienda,ndio Bara itakuwa moja?
Nje ya muungano(hata sasa hv),hakuna bara,Kuna sukuma gang,Wapiga deal Chaga,Wahaya,Uislam na ukristo.
Ukaskazini na ukanda ya ziwa.
Yaani sijuhi kwanini watu wanakuwa na vichwa vigumu,Bara na Zenj,haziwezi kutengana Wala kutenganishwa,huu muungano ni kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya TZ,sio kwa ajiri ya kuwaridhisha wananchi.whether you like it or not,Zenj,or Tanganyika no one is going anywhere.
Ni Sawa na china umwambie Hongkong,au Taiwan ni nchi kamili na sio sehemu ya china.
Au Catalonia sio sehemu ya Spain.
Kwa maslahi mapana ya TZ,this union is here to stay,ukitaka kila kitu uwaulize wananchi,wachaga watakuambia Bora wajitenge wawe Nchi,na Lindi na Mtwara hivyo hivyo.
 
Yaani sijuhi kwanini watu wanakuwa na vichwa vigumu,Bara na Zenj,haziwezi kutengana Wala kutenganishwa,huu muungano ni kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya TZ,sio kwa ajiri ya kuwaridhisha wananchi.
Ukisikia uzalendo wa kweli wa nchi yako ndio huu!. Muungano upo na utaendelea kuwepo kwa maslahi mapana ya JMT.
whether you like it or not,Zenj,or Tanganyika no one is going anywhere.
Ni Sawa na china umwambie Hongkong,au Taiwan ni nchi kamili na sio sehemu ya china.
Au Catalonia sio sehemu ya Spain.
Kwa maslahi mapana ya TZ,this union is here to stay,
Hiki ndicho nilichosema, the union is there to stay forever na tutaulinda kwa gharama yoyote!.
P
 
Hakuna muungano wa milele hapa duniani.
Muungano wetu ni muungano wa pekee na wa aina yake duniani, hakuna muungano mwingine wowote kama huu muungano wetu. Miungano mingine yote ni miungano ya mikataba, kwenye kila mkataba lazima kuwepo na kipengele cha kuvunjika kwa mkataba, lakini huu muungano wetu adhimu, sio mkataba, it's not a contract, ni muungano wa makubaliano, agreement. Zile Articles of Union sio contract ni agreement, hazina kipengele cha kuvunja muungano, hivyo muungano wetu ni muungano for life!. Ni muungano wa milele!.
Hili nimeliandikia kabisa makala
P
 
Tunaposema Muungano wetu adhimu tutaulinda kwa gharama yoyote, we mean it, and it's forever!.
P


Is it bound by divine laws ??!!----- kama Muungano umeletwa na watu basi ni watu hao hao au watu wengine wanaweza kuuvunja, nchi tu zinapanganyika sembuse Muungano wa nchi !!!??
 
Ulikuwa kwa manufaa ya Nyerere na Karume.Kwa maana Karume aliogopa sultan kurudi Znz.Nyerere aliwaogopa Waraabu pia kuilinda znz isiwe ngome ya kuipigia bara.
Vyote hivi havina uhalisia kwa zama hizi.
 
Ukivunjika wazenji wote tunawatimua tuone nani atapata hasara

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Kutimuana hovyohovyo haiwezekaniki. Kuna sheria za kimataifa zinalinda.

Kitakachofanyika ni makubaliano fulani. Rejea Sudan na Sudan Kusini baada ya kuvunjika. Wapo Wasudan weusi kutoka Sudan Kusini wao waliamua kusalia Sudan na kuwa raia wa huko.

Hata huku kama muungano utavunjika, basi kutakuwa na kipindi cha mpito cha kuweka mambo sawa, mfano miaka 3.

Rejea tena, Uingereza na Brexit

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wanashindwa kutafakari huu muungano, waulize huo wa EAC itakuwaje? Nchi hii inaongozwa na vilaza yaani hawafahamu 1+1=2 or more.

Huu Si muungano ni uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar, mwaka 1964 Nyerere aliivamia Zanzibar na kumkamata Waziri Mkuu wake Muhammed Shamte na baraza lake la mawaziri waliochaguliwa na wananchi kidemokrasia na kuwafunga kwenye jela Za Tanganyika kabla huo uvamizi haujapewa jina la muungano wa Tanzania
 
Huu Si muungano ni uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar, mwaka 1964 Nyerere aliivamia Zanzibar na kumkamata Waziri Mkuu wake Muhammed Shamte na baraza lake la mawaziri waliochaguliwa na wananchi kidemokrasia na kuwafunga kwenye jela Za Tanganyika kabla huo uvamizi haujapewa jina la muungano wa Tanzania
Be serious kidogo. Yaani uvamizi udumu kwa zaidi ya miaka 60 na dunia inaangalia tu! Hainishawishi.
 
Back
Top Bottom