Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Umenukuu biblia ipi?
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Japo sasa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanaelekea miaka 60, Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
Unapohoji kuhusu muungano unafokewa, unakumbuka mambo ya Jumbe? Mimi ni haki yangu kuuliza kuhusu uhalali wa muungano. Nataka nimuenzi Mtikila kwa kudai serikali tatu. Ni kwa nini sehemu ndogo ya Zanzibar kuitwa nchi ila sehemu kubwa ya Tanganyika sio nchi?
 
Ameimega Mungu...
 
nimeamini kambona alikuwa na akili nyingi lkn mwalimu alituchuza kwenye swala la muungano.hakuona mbali.kambona apewe maua yake.
 
Nyinyi endeleeni kulinda Mapinduzi, Hali ndio hii

View attachment 2666212
 
Nyinyi endeleeni kulinda Mapinduzi, Hali ndio hii

View attachment 2666212
Jukumu la kuulinda huu muungano wetu adhimu, sio la watu fulani na kutuita nyie, ni jukumu la kila Mtanzania mzalendo wa kweli wa taifa lake.

It's very unfortunately, tuna Watanzania wenzetu ni mamluki wanatamani huu muungano wetu adhimu kuvunjika hata leo!.
Mamluki hawa watasubiri sana!.
P
 
Lakini mkuu, umeshasikia kinachosemwa na Wazanzibar? Simaanishi kila Mzanzibar, bali wale ambao wakifunua vinywa vyao sauti zao huwaamsha hata waliolala! Umeshawasikia?
 
Serkali iwe.1 ikishindikana ziwe Serkali.3
Huo ndio Muungano Adhimu!
Uvunje duka lako na mimi nivunje duka langu liwe duka.1 la Muungano!
Au nichukue ½ ya duka langu na wa ½ ya duka lako tupate duka la Muungano!
Sio duka lako ni lako na duka langu ndio la Muungano!
Hivi P hamuioni Kweli ya Kweli na kubaki kuuma uma maneno??
Mchawi nani???
 
Lakini mkuu, umeshasikia kinachosemwa na Wazanzibar? Simaanishi kila Mzanzibar, bali wale ambao wakifunua vinywa vyao sauti zao huwaamsha hata waliolala! Umeshawasikia?
Nimewasikia, wengine ni kughafilika tuu, ni wa kupuuzwa!.
P
 
Serkali iwe.1 ikishindikana ziwe Serkali.3
Huo ndio Muungano Adhimu!
Naunga mkono hoja, mimi ni Mnyerere naamini kwenye serikali moja! Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!" na hili la serikali mbili nililipinga since day 1 Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile! na hapa Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio utauvunja Muungano
Uvunje duka lako na mimi nivunje duka langu liwe duka.1 la Muungano!
Au nichukue ½ ya duka langu na wa ½ ya duka lako tupate duka la Muungano!
Sio duka lako ni lako na duka langu ndio la Muungano!
Naunga mkono hoja
Hivi P hamuioni Kweli ya Kweli na kubaki kuuma uma maneno??
Mchawi nani???
Tunaona na tumewashauri Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja
P
 
Umenena kizalendo kabisa! Atakayekejeli haitakii mema nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…