Imekuwa ni jadi na utamaduni kufurahia sikukuu hii na kuwaenzi waasisi wa Muungano wetu Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid Karume kwa matamasha, gwaride na shangwe kebekebe.
Lakini imekuwa ni dhambi, tena yenye sumu kali kwa mtu yeyote kuhoji au kutaka kuuchambua Muungano huu.
Lengo langu si kuuliza historia au kudadisi uhalali wa Muungano wa Tanzania bali ni faida zake na manufaa yake kutokana na mfumo wa Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, mamlaka zilizoko kama vile Mahakama, Bunge, Baraza la Wawakilishi na ni vitu gani ambavyo ni kwa ajili ya Muungano na vipi si kwa ajili ya Muungano.
Je, kwa nini tuliweka vipengele fulani viwe masuala ya muungano na vingine visiwe?
Je, Muungano huu una maana gani ikiwa vipengele ilivyoko vinakingana na azma kuu ya kuunda Taifa lenye nguvu na umoja?
Je, Wananchi wa Tanzania, wananufaika vipi na Muungano huu na wanaathirika vipi kutokana na Muungano huu na mfumo wake?
Je, kuna haja ya kuupitia Muungano na ama kupangua vipengele fulani au kuunganisha kila kitu na kuwa na sura moja bila kutofautisha ya hili la Watanganyika au Watanzania Bara na lile ni la Wazanzibari?
BAADHI YA MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU KUHUSU MADA HII
---
---
---
---
---
---
---
ZAIDI UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
= > Lipo wapi tatizo kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Tafakari!
= > Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na Muungano wa Siria na Ejibti walioungana 1958
= > Waliohoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wafikia hatua gani?