Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Ukiangalia sababu zilizofanya kuundwa kwa JMT wakati huo na hali ilivyo sasa,
ukiangalia kufa kwa vita baridi kati ya mataifa makubwa (ubepari vs ujamaa),
Ukiangalia utandawazi ambao umefanya dunia kuwa kama kijiji,
ukiangalia mahitaji ya kuundwa mikoa mikubwa ya kiuchumi ya kikanda kama vile EAC, SADEC utaona kuwa kuna haja ya kuacha wazanzibar wabaki kama nchi ili waweze kujiunga na hizo jumuiya bila vikwazo. Kuendelea kuwalazimisha kubaki ndani ya Muungano ni kuwanyima haki yao ya kushiriki kwa uhuru katika kuunda hizo Jumuiya. Dalili zote zinaonyesha kuwa wangependa wawe huru zaidi.Hayo ni mawazo yangu kutokana na hali ninavyoiona.Hii yote nasema kwa nia njema kabisa Naombe mchango wenu wanajamvi
 
manenge,

Muungano katika Muundo uliopo sasa ni bomu linalosubiri kulipuka.
The sooner we solve this "Kero" the better!

Ni vyema turudishe nchi zetu za awali kama zilivyokuwa. Tanganyika na Zanzibar.

Tunaweza kuweka "special relation" agreement baina yetu kutokana na uhusiano wa karibu wa muda mrefu.
na kila nchi itaacha kuwa na visingizio vya kunyonywa au kuhujumiwa na Muungano. Wananchi wataweza kupambana moja kwa moja na "wachawi",viongozi wabovu wao.

Viongozi wa Tanganyika na Zanzibar wamejificha nyuma ya pazia la Muungano kwa muda mrefu huku wakitugawia umaskini wakati wao wanajineemesha na familia zao.

Wananchi tumeachwa kuingia katika malumbano ya Muungano yasio na tija nasi. Tunatukanana, tunakejeliana ,kubezana na kukebehiana huku "fisadis" wanavuna shamba la bibi.
wake up guys!
 
Kwa mtu ambaye ni mkweli muungano ni kama haupo. Inasubiriwa tu kutamkwa rasmi kuwa Zanzibar ni Jamhuri
 
Huwezi hata siku moja,kuona mfanya biashara anafunga duka lake wakati anapata faida,,,,,haingiii akilini....

Hatanganyika siku zote katika amini zao wanaamini zanzibar tunafaidika sana katika muungano kutona na uchache wetu na visiwa vyetu na udogo wake,lakini huwezi amini,haipati hata senti moja kutoka katika muungano,kwa mfano faida ambayo inangia katika muungano. nin

International relation

Hapa tunawakilishwa kama tanzania,kuna pesa huingia kwa jina la tanzania ,lakini zanzibar haipati hata seinti tano,tunasikia tu inapokea 4.6 asimilia lakini sijasikia hata siku moja imepokea asimilia hiyo,mtalii yoyote kutona njee analipa 100 dola katika balozi ya tanzania,jee kwa mwaka wananigia watalii wangapi ? NA WAKISHALIPA HAPO wakija zanzibar hawalipi tena,jee kuna faida gani sisi ? pia mikopo kutoka njee,misaada kutoka njee,kieleimu kushirikiana na watu wa njee,hata kibiashara, haya nio tunayokakota wazanzbari,kiuchumi pia.

Ni vigumu kuwa kiuchumi kama huan international relation,na sisi hatuna,hatuna kiti katika umoja wa mataifa,wala hatuna mabaolozi,haya ni mambo ambayo yanayofanya tuwe karibu na nambazo zilizo endelea kuwa na uchirikiana katika kusaidiana kujenga nchi na uchumi na kuwawezesha wananchi.

Wazanzbari ndio wanapata hasara zaidi kwani sisi ni taifa sio mkoa,hamuwezi kutuchukulia kama ni mkowa,wazanzbari ndio wanao athirika zaidi,sitokueleza sana nimekueleza hasara moja tu hapo,

Nakuomba sikiliza hapo nitakuwekea link kongamano la katiba ambalo linaelezea hasara za muungano,kuwa na time,take your time kuangalia.

Video:Muungano ni kero twachelea ni ukoloni mweusi! | MZALENDO.NET
 
MUWAZA:Barua ya Wazi kwa Wajumbe wa BLW | MZALENDO.NET


bendera1.jpg

Wananchi, wazalendo, wapenda amani, maendeleo na utaifa wa nchi yetu ya Zanzibar
 
Si muondoke tubaki na tanganyika yetu, mbona mnatufanya kana kwamba bila nyie hatuwezi ishi? kumbuka mko 1067800 kati yamilioni arobaini. We have nothing to lose!
 
Kwa heshima na taadhima nimeombwa na sahib yangu ambae yeye ni Mzanzibari kuleta hii post kwenu na mie nimetimiza wajibu wangu katika hili.

Na Mohammed Ghassany,

Hata baada ya karibuni nusu karne ya Muungano, bado masuala ya uhalali, usahihi na ulazima wa Muungano wenyewe ni mambo yanayopata ufuasi mkubwa Zanzibar. Hali ni tafauti kabisa na upande wa pili wa Muungano huu, Tanganyika, ambako si watu wengi ambao hata wanauhisi Muungano wenyewe.

Hoja yangu ni kuwa, Wazanzibari na Watanganyika wana malezi tafauti kuhusiana na sura na dhati ya Muungano huu. Ambapo Watanganyika wanauangalia huu kuwa ni wa serikali moja, Wazanzibari wanauangalia kuwa ni wa shirikisho la serikali tatu (au, angalau, ulitakiwa uwe hivyo). Ambapo Watanganyika hawashughuliki sana kuuwazia, maana si sehemu ya maisha yao, Wazanzibari wanalala wakiamka nao mawazoni, maana wanaamini una athari kubwa kwa maisha yao. Unaweza kufahamu kwa nini Watanganyika hawashughuliki nao sana, kwa kuwa tayari wametengenezwa kuuamini, kinyume na Wazanzibari ambao wametengenezwa kuushuku.

Unaweza usiambiwe haya moja kwa moja au neno kwa neno, lakini tabia, matendo na maono ya watu ndiyo yanayosomeka hivyo. Kwa mfano, si rahisi kumkuta Mtanganyika anajiita kwa jina hilo, maana kwa wengi wao Tanganyika imeshapotea. Hata wewe ukimuita hivyo katika muktadha wa Muungano, atakuchukulia kuwa u mbaguzi tu.
Lakini kila mara utamkuta Mzanzibari akijiita na akijinasibisha kwa Uzanzibari wake; na kama kuna orodha ya mambo kumi yanayowagusa Wazanzibari wote kwa pamoja, la hisia zao kwa Uzanzibari na dhidi ya Muungano litakuwa namba moja, kabla ya dini, vyama, na au uzawa wao.

Huu ni uamuzi wa kimapinduzi kwa pande zote mbili za Muungano. Kwa Tanganyika ni wa kimapinduzi kwa kuwa umeweza kupindua fikra za karibuni vichwa milioni 40 na kuvifanya viamini kitu kimoja tu. Utanzania.
Kwa Zanzibar ni wa kimapinduzi kwa kuwa vichwa milioni moja tu, ambavyo vinafanya chini ya asilimia 3 tu ya Watanzania wote na vinakaa chini ya asilimia moja tu ya ardhi yote ya Jamhuri ya Muungano, vimeweza kuhimili kubakia na hisia za kutokuridhika kwa miaka 47 ya Muungano huu. Lazima tukiri kwamba ni ujasiri tu ndio unaomuwezesha mwanaadamu kuweza kukaa na fundo la moyo kwa miaka mingi kama hii, akiendelea kuridhika na kutokuridhika kwake!

Hili la Wazanzibari kuendelea kuishi ndani ya Muungano wakiridhika na kutokuridhika kwao, ndilo wengine wanalolichukulia kimakosa kwamba linamaanisha kuwa Muungano huu ni halali na unatakiwa! Kwa maoni yangu, hiyo ni tafsiri potofu, lakini inaakisi ukweli unaoufanya Muungano uendelee kuwapo kwa karibuni nusu karne sasa.
Vyenginevyo, tunapaswa kukiri kuwa kuna kutokuridhika kwa upande wa Zanzibar; na kwa kuwa Zanzibar ni sehemu moja kuu ya Muungano huu, basi hisia zake hazipaswi kupuuzwa tena. Kukiri ukweli huu ndiko kutakakotusaidia kuyageuza mateso yetu kuwa faraja. Kwa nini na kwa vipi?

Kwanza, kutayaendeleza mapinduzi ya kweli ya Zanzibar kwa kuyapa maana katika maisha ya kila siku na ya kila mmoja wetu. Kwa dhati yake, mapinduzi ni matokeo ya kutokuridhika, ambako huletwa na mgogoro kati ya njia ambazo watu wanaouona ukweli na njia ambazo wangelipenda ukweli huo uwe.

Pili, Zanzibar inauona ukweli kuwa Muungano huu, katika hali uliyo, ni tatizo kwake na, sasa, ni moja kati ya mawili: ama uwe sehemu ya utatuzi wa tatizo lenyewe au usiwepo kabisa. Kwa kutumia maneno ya mwanasiasa mmoja kijana wa Zanzibar, ni ama Muungano wa kuhishimiana au basi.

Huko hakuwezekani ila kwa mapinduzi; na hayo si mapinduzi ya mapanga na marungu, wala bunduki na mizinga, bali ni ya fikra na ya mkakati, ambayo yanatakiwa yapitie hatua tano zifuatazo:

i. Kujitayarisha kwa ajili ya mapinduzi

ii. Kuporomoka kwa mfumo mkongwe

iii. Kuharibika kwa mahusiano makongwe

iv. Kujenga mahusiano mapya

v. Kuuimarisha mfumo mpya

Ama kwa kujijua au kutojijua, tayari tumeshapita kipindi cha kwanza cha matayarisho kwa ajili ya mapinduzi, ambacho kilitawaliwa na woga wa wananchi na mateso kutoka kwa watawala. Hicho kilikuwa ni kipindi ambacho, ingawa palikuwa na kiwango kikubwa cha kutokuridhika na jinsi Muungano huu unavyoikandamiza Zanzibar, si Wazanzibari wengi waliokuwa na uthubutu wa kusema kutokuridhika huko. Bali hata wale wachache waliothubutu, walisemea vibuyuni, ambako ama walichokisema kilimalizwa huko huko au wenyewe walimalizwa kwa njia zao za kumalizana. Silazimiki kuwataja kwa majina wala kuitaja mikasa ya aina hiyo kwenye historia ya miongo miwili ya kwanza ya Muungano (1964 1984) kuhalalisha hoja hii.

Sasa tulipo, kwa maoni yangu, ni katika hatua ya pili ya mapinduzi, ambapo mfumo mkongwe wa Muungano usio na maslahi kwa Zanzibar unaelekea kuporomoka. Kawaida kipindi hichi ni matokeo ya kupotea kwa uongozi ndani ya kundi la watawala, ambapo mgawanyiko wa makundi humfanya kila mmoja kutenda kivyake.

Mara nyingi hatua hii haifikiwi mpaka ajitokeze kiongozi anayejiona kuwa mwanamageuzi kutaka kuunusuru mfumo mkongwe; na akafeli. Turgot na Necker walijaribu kuunusuru ufalme wa Ufaransa kabla ya mwaka 1798 na Stolpyin akafanya jaribio kama hilo nchini Urusi kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, lakini wote walishindwa.

Huwa ni wakati ambapo, kutokana na mtikisiko wake, mfumo mkongwe huwa kama tayari umeshakufa kitambo, lakini kwa kuwa watu wanaothubutu kuyathibitisha mauti yake hawajatokea, basi mfumo huo huendelea kuwepo tu ukiishi kwa upepo. Kikwetu tunaiita hali hii ya kuwa maiti-kwenenda. Muungano huu sasa ni maiti-kwenenda!

Huu ni mfano wa kile kisa cha mauti ya Nabii Suleiman (A.S), ambaye hata baada ya kuwa alifariki siku nyingi akiwa amekaa kwenye kiti chake cha ufalme, lakini raia wake, wakiwamo wanyama, wanaadamu na majini, waliendelea kuamini kuwa mfalme wao amekaa kitini akiwasimamia. Ni hadi mchwa walipokuja kuila fimbo yake, ambayo alikuwa ameegemea, ndipo wakatanabahi kuwa kitambo kirefu Suleiman hawakuwa naye tena.

Historia ya Ufaransa inathibitisha hivyo pia. Kuna watu waliojuwa kuwa awamu ya tatu ya serikali ya nchi hiyo ilishakufa tangu mwaka 1934, lakini maziko yake yalikuja kufanywa mwaka 1940. Miaka sita baadaye!

Wazo ninalojaribu kuliwasilisha hapa ni kuwa: kuna siku yale yale matakwa ya Wazanzibari, kama yalivyoelezwa kupitia Ripoti za Tume za Jaji Nyalali na Jaji Kisanga, ndiyo yatakayoongoza mahusiano baina ya Tanganyika na Zanzibar (yawe na jina lolote lile: Muungano, Shirikisho, Umoja, Ushirikiano, n.k) na wala sio Katiba ya Muungano iliyopo sasa wala hiyo inayoambiwa kuwa itaandikwa upya baada ya uchaguzi wa 2015. Na viashiria vya utabiri huo vimeanza kujengeka kitambo.

Leo tunazungumzia Muungano ambapo Zanzibar ina bendera yake, ina wimbo wake wa taifa, ina vikosi vyake vya ulinzi mbali ya katiba, bunge na rais wake mwenye madaraka zaidi kuliko miaka kumi nyuma. Tunazungumzia Muungano ambapo utambulisho wa Uzanzibari umeshindwa kuuliwa na kuzikwa hata baada ya nusu karne nzima. Huu, hapana shaka, si Muungano ambao mmoja wa waasisi wake, Mwalimu Julius Nyerere wa Tanganyika, aliuwazia.

Kwa mujibu wa maneno na matendo yake, Nyerere alipendelea sana kuona kuwa, haraka iwezekanavyo, raia wa pande zote mbili wanajitambulisha kwa Utanzania wao tu, kiumbe chake. Hii ni kwa kuwa, Nyerere, kama walivyo Watanganyika wengine wengi, alipuuzia sana hisia za uzalendo wa Kizanzibari. Hata hivyo, kuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuwa muasisi mwengine, Mzee Abeid Karume wa Zanzibar, aliiwazia Zanzibar yake vyengine na vikubwa zaidi ya haya.

Changamoto iliyo mbele yetu kwa sasa ni ukweli kwamba hatua za tatu, nne na tano zinakuja kwa kasi na, yumkini, hatuna matayarisho mazuri kuzikabili. Kwa mfano, hatua ya tatu, ambayo ni ya kuharibika kwa mahusiano makongwe, kwa mintarafu ya kuharibika kwa muundo wa sasa wa Muungano, ina matatizo yake.

Mojawapo ni kwamba, wenye maslahi na mahusiano haya hivi sasa, wanajitahidi kutumia nguvu zao za ziada kuzuia yasiharibike. Na ingawa, kutokana na matakwa ya kiwakati hawataweza kuzuia chochote, lakini, kama tusemavyo kikwetu buyu likigwa, hugwa na vishindovye. Maana yake ni kuwa, mti mkubwa kama mbuyu unapoanguka, unakuwa na vishindo vikubwa pia: husababisha maafa kwa pale unapongokea, ambapo huweza kuchimbika shimo kubwa litakalochukua muda kufukilika, na kule unakoangukia, ambako nako huweza kuelemea nyumba au wapita njia na kuwajeruhi, kama si kuwatoa roho zao kabisa! Muungano huu ni mbuyu mkubwa, lakini mkongwe na, hivyo, dhaifu kwenye mizizi yake!

Ulimwengu una mifano mingi kama hii. Kuna wa Indonesia na Timori ya Mashariki, wa Morocco na Sahara ya Magharibi, wa China na Macao au na Hong Kong. Mwengine mumekuwa na mafanikio, na mwengine bado mapambano yanaendelea. Muongo uliopita ulianza kushuhudia mahusiano makongwe baina ya Syria na Lebanon yakianza kuharibika. Na Lebanon ndiyo iliyoonekana kulipia gharama za kipindi hiki, pale wanaharakati walio mstari wa mbele kusaidia maharibiko hayo, walipoanza kukabiliwa na vitendo vya kigaidi vinavyoaminika kusimamiwa na kuongozwa na Syria ndani ya ardhi ya Lebanon. Haitakuwa ajabu hata kidogo kwa Zanzibar kukumbwa na hayo hayo, japo kwa staili na matukio mengine.

Lakini hakuna sababu ya kutishika wala kuvunjika moyo kwa sababu mbili: kwanza, lolote litakalotokea kwa mwanaharakati wa Kizanzibari, ikiwa ni kwa ajili ya imani ya nchi yake, basi halina majuto. Pili, kipindi hiki kinapoanza tu, hutanguliwa haraka sana na kipindi cha ujenzi wa mahusiano mapya, ambacho nitakifananisha na ujenzi wa nyumba mpya juu ya kongwe, ambao ni maarufu kwa jamii za watu masikini kama Zanzibar.
Katika mazingira haya, mwenye nyumba huendelea kujenga nyumba mpya, huku yeye akiwemo ndani. Anachofanya ni kuvunja kiambaza kimoja kwanza na kusimamisha kipya mahala pa kilichovunjwa, kabla hajakwenda katika kiambaza chengine.

Ingawa huweza kuchukua muda mrefu kwa nyumba kukamilika, kutegemea na uwezo wa kifedha, kiufundi na mazingira ya ujenzi; lakini ni staili ya ujenzi ambayo ina faida moja kubwa: hakuna wakati ambapo mwenye nyumba analazimika kulala nje, hata kama katika kipindi cha ujenzi wake, huwa hakai katika makaazi mazuri sana.

Hapo ndipo, kwa maoni yangu, Muungano huu unapoelekea. Unaingia kwenye kuvunjika na kuundika kwa wakati mmoja. Tunakwenda katika kipindi ambacho hatutasema kuwa hatuna Muungano moja kwa moja, lakini pia hatutakuwa na Muungano huu uliopo sasa.

Mwisho tutaingia kwenye kuimarisha mahusiano mapya tutakayoyajenga; maana ukweli ni kwamba Zanzibar, Tanganyika na mataifa mengine ya jirani, yataendelea kuwa katika mahusiano ya ukaribu, udugu na ujirani mwema daima na dawamu. Huu ni uhusiano wa zaidi ya milenia mbili na hauwezi kupuuzwa wala kuvunjwa. Lakini tafauti na sasa, mahusiano yajayo kwa sababu ya mapinduzi haya, yatakuwa na sura nyengine na matakwa mengine. Kuna ambao tunataka mahusiano hayo yawe kama yale ya mataifa yaliyo kwenye Umoja wa Ulaya (EU) au Baraza la Ushirikiano wa Nchi za Ghuba (GCC).

Hata hivyo, lazima tuzinduke Wazanzibari. Kwamba jambo pekee linaloweza kutufikisha hapo ni moja tu, nalo ni mkono mmoja kuyashikilia mapinduzi yetu na mwengine kuishikilia Zanzibar yetu, ambayo imeelezewa vyema kwenye Mabadiliko ya Kumi ya Katiba yaliyofanywa na Baraza la Wawakilishi mwaka jana. Tuiamini, tuitetee, tuilinde na tuisimamie Katiba yetu hii, maana ndani yake muna kila aina ya fursa na silaha ya kufanikisha mapinduzi yetu.

Source:
Miaka 47 ya Muungano, Zanzibar na Mapinduzi mapya « Zanzibar Daima
 
mtumbwi ni chombo muhimu huko zenji ila ni gogo la kuachwa shambani litafunwe na mchwa huku tabora.....so siasa za zenji kwangu ni gogo
 
Nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakiongea mabaya kuhusu Muungano. Bahati mbaya au nzuri watu wengi hawaoni umuhimu wa muungano. Binafsi ninajiuliza, ikiwa muungano utavunjika; watu wa unguja na wapemba walioko bara na wale waTanganyika walioko Zanzibar, watapendelea kwenda upande upi wa uliokuwa muungano? Sipati picha...
 
Suala zuri kabisa. Sisi wazanzibari tunakwetu tutarudi na nyinyi watanganyika muna kwenu murudi. Sasa, kwa kuwa kuna demokrasia, watu wataamu wanapotaka kuishi. Sisi wazanzibari hatuwafukuzi binaadamu kuishi zanzibar. Hatuna chuki na raia. Matatizo yetu ni kuburuzwa na watawala. Wananchi hawatuletei matatizo yoyote bali muungano na viongozi wake ndio tatizo.
 
kwanini ukimbie? Baki hapo hapo ulipo uendelee na maisha yako!
 
Nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakiongea mabaya kuhusu Muungano. Bahati mbaya au nzuri watu wengi hawaoni umuhimu wa muungano. Binafsi ninajiuliza, ikiwa muungano utavunjika; watu wa unguja na wapemba walioko bara na wale waTanganyika walioko Zanzibar, watapendelea kwenda upande upi wa uliokuwa muungano? Sipati picha...

Ndugu yangu, si afadhali ya hao WATANGANYIKA na WAZANZIBAR wananchi zao ambazo ni TANGANYIKA na ZANZIBAR na Sisi WATANZANIA je? Ambao ni ZAO kati ya mtz na mznzbr,TUTAKWENDA WAPI?
 
kwani sasa hivi unaishi wapi?. Muungano ukivunjika utaishi na baba na mama. Kwani kuna vita baina yetu?. Hakuna vita, kitu kilioko ni kujikomboa na uongo ulio dumu miaka 47. Kunakosa kudai haki yako?. wewe unakubaliwa kuishi utakapo wala muungano ukivunjika haimaanishi ndio mwisho wa ulimwengu. Kwa walala hoi kama sisi, tunateseka kama kawaida. Tunachapa kazi na hakuna lolote.
 
Na uvunjike tu maana wanzenji wanaonewa sana na wanafanywa mambumbumbu! kama ukivunjika si watawapa visa muishi huko. Mie mtanzania kwetu nitaishi na nitaaenda matembezi nchi ya nje zenji kwenda kula tende na kunywa ghahawa!
 
Au ndiyo maana walisema Muungano usiguswe kwenye mjadala wa Katiba. Ili kuondoa hii sintofahamu ni bora iwe nchi moja na hapo hakutakuwepo na haja ya watanzania kurudi pande ile au hii.....!
 
sheikh-farid1-564x272.jpg


Na Salma Said,


MKUTANO wa kutoa maoni kuhusu mswaada wa uundwaji wa kamisheni ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umevunjika hapa rasimu za mswaada huo kuchanwachanwa katika mkutano huo.

Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed akiongea katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa shule ya Haile Sellasie ndio aliyechana mswaada huo na kufuatiwa na watu wengine kuchana nyaraka hizo kwa madai kwamba hauna maslahi ya wazanzibari na kwamba suala hilo halijazingatia hadhi ya Zanzibar hivyo hauna faida kwa wananchi.

Mkutano huo ulipangwa kumalizika saa nane mchana lakini ilipofika saa saba Sheikh Farid alisema hakuna haja ya kuendelea na mkutano huo huku badhi ya wananchi wakiwataka wananchi wengine kundoka katika mkutano huo kwa kuwa hakuna faida a kujadili kitu ambacho haina faida kwao.

Awali akiochangia mjadala huo Sheikh Farid alisema alijaribu kufutalia mchakati mzima wa rasimu hiyo ya katiba lakini inaonesha kwamba kuna taratibu nyingi hazikufuatwa na hivyo hakuna sababu ya kuendelea kuujadili kwa kuwa hauna maana.

"Hapa tumesikia kelele nyingi sana kwa hivyo ilikuwa inatosha tutawanyike kabisa, tunakwenda katika kujadili marekebisho ya katiba ya Tanzania lakini swali jee katiba ya Tanganyika mnao? Jee hapa huo muungano uko wapi? Kipi cha kutangulizwa? Kwanza kafanyeni katiba ya Tanganyika kwanza" alisema huku akishangiriwa na wananchi.

Sheikh Farid alisema ngea katika akiwataka wananchi kutawanyika kujadili katiba kwa wadau mbali mbali umevunjika kufuatia sheikh Farid Hadi Ahmed kuchana rasimu ya katiba iliyowasilishwa kwa wadau mbali hapo katika ukumbi wa Shule ya Haile Sellasie ambapo awali mkutano huo ulipangwa kumalizika saa 8:00 kamili mchana lakini ulilazimika kukatishwa baada ya kuchanwa na watu wote kutawanyika katika ukumbi huo majira ya saa 7 mchana.

"Mswaada kwao sisi hatuna shida ya kutungiwa mswaada basi tunasema hatutaki kuvundwa vundwa….huu mswaada mnautaka ….mnasubiri nini chengine mkitaka muone kivitendo kwamba hatuutaki basi ndio hivi" alisema Sheikh Farid huku akichana chana mswaada huo.

Akichangia kwa ufupi mswaada huo Farid amesema lazima maamuzi ya wananchi yachukuliwe na suala la kuheshimu mawazo yao ni suala la lazima hivyo hakuna sababu ya kuwalazimisha kitu wasichokitaka.

"Natoa wasia wangu kwa serikali ya mapinduzi na serikali ya umoja wa kitaifa tunataka kura ya maoni tuulizwe muungano tunautaka au hatuutaki" alisema huku akipigiwa makofi kwamba muungano huo hatuutaki" alisema.

Akichangia katika mjadala huo baadhi ya wananachi walisema wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakidharauliwa sana hivyo hakuna sababu ya kuendelea kudharauliwa.

Walisema walisema zama za udikteta umekwisha na kama serikali inaogopa basi wananchi wapo tayari na hawataki kuingiliwa.

Mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria ya bunge la jamhuri ya muungano Jadi Simai Jadi wa jimbo la Mkwajuni Zanzibar alitamka katika mkutano huo kwamba hakuwezi kuenelea tena na mkutano huo kutokana na hali ya usalama kutisha ndipo wananchi wakaanza kushuka nazi na kuondoka taratibu bila ya fujo lakini walikuwa wakiimba kwa nyimbo ya kuukataa muungano.

"'Wadau mliohudhuria mkutano huu wa kujadili rasimu ya katiba hapa ndio mwisho wa mkutano huu…hali ya usalama inatia mashaka"'alisema Jadi.

Kufuatia tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria alitangaza kwamba hapo ndiyo mwisho wa kikao hicho.

Kufuatia tukio hilo baadhi ya wananchi waliohudhria mkutano huo nao walichukuwa uamuzi wa kuchana mswada huo na hivyo hali ya usalama kuwa tete katika kipindi hicho.

Katika mjadala huo walikuwepo viongozi waandamizi akiwemo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Samuel Sitta pamoja na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa kwanza wa rais Muungano Samia Suluhu Hassan.

Akiongea katika mjadala huo Mzee Nassor Moyo ambaye alikuwa waziri wa sheria wakati muungano uliopoundwa alisema yeye amekuwa shahidi wa makubaliano hayo kati ya Zanzibar na Tanganyika.

"Nilikuwa waziri wa sheria wakati huo mambo haya ni 11 lakini hivi sasa yameongezeka naambiwa yamefikia mpaka 30 haya yote yaliongezwa na wenzetu bara ….na kwa yale yalioengezwa na watu wa unguja Jumbe alifukuzwa kazi sasa spirit ile ile ya Jumbe ipo maana sisi wengine tuhai hatujafa na pia wapo wanaunga mkono na yeye mwenyewe jumbe hajafa yuhai" alisema Mzee Moyo huku akionesha nakala ya makubaliano hayo ya muungano.

Alisema mambo waliokuwa wameafikiana Nyerere na Mzee Karume wakati huo yameweza kuheshimiwa na viongozi wengine kulingana na wakati lakini kwa sasa vijana hawawezi kupangiwa mambo kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo sas vijana wanahitaji kurekebisha na kuwepo muundo wanaoutaka wao jambo ambalo alisema lazima serikali iwasikilize wananchi.

"Tusiwazuwie vijana hawa kufanya muungano wanaoutaka wao wenyewe, mimi na karume na jumbe tumeufikisha hapa …na haiwezekani kama tumeshaufikisha hapa halafu tuendelee hivi hivi bila ya wao vijana kuwaachia wenyewe wanavyotaka kuuendeleza lazima tukubali kuwapa fursa waseme wenyewe wanataka muungano wa iana gani …tusiwazuwia wenyewe …sisi yetu tumeshwikwisha" alisema Mzee Moyo.

Mzee moyo alisikitishwa na tabia ya kuambiwa kwamba suala la muungano zilijadiliwe jambo ambalo amesema iwapo halitazungumzwa kutakuwa hakuna jembo jengine la kulijadilia zaidi ya muungano kwa kuwa ndio kubwa kwa Zanzibar.

"Mnatwambia tusizungumze suala la muungano mnataka tuzungumze nini hapa wakati hilo ndio jambo la msingi….mnataka tuzungumze nini …hili ndio jambo tutakalolizuingumza" alisema huku akisisitiza kwamba kosa walilolifanya wakati huo hivi sasa lisirudiwe tena kwa kuwa vijana wa sasa wamesoma na sio wajinga kama wao ambapo haifai kupuuzwa vijana hao.

Akizungumza katika mjadala huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari alisema utaratibu uliotumiwa sio na serikali haikushirikishwa katika uandaaji wa rasimu hiyo na serikali ya muungano haifajafan ya uungwana hata kidogo.

Alisema licha ya kuwa hawajashirikishwa lakini serikali ya Zanzibar kupitia mwanasheria mkuu wake aliandika barua kupeleka serikali ya muungano lakini hakujibiwa angaua kwamba barua yao imepokelewa lakini pia walipeleka mapendekezo yao 14 lakini jambo la kusikitisha ni mambo mawili tu ndio yalioingizwa katika rasimu hiyo na badala yake kuongezwa mambo mengine manane kinyume na makubaliano.
 
Haya, Huu ndio msimamo wa Wazanzibari. Muungano hatuutaki. Kura ya maoni kuhusu muungano ndio tunasubiri. Sisi wazanzibari tuna KATIBA yetu. Hatuna haja ya katiba feki kutoka kwa SITTA. Kutawaliwa basi tumetosheka. Mashekhe wetu, wanasiasa na wananchi wazanzibar wamekwisha tamka wazi kabisa , "HATUNA HAJA YA MUUNGANO". Jamani lazima mulifahamu hili vinginevo tutapeana shida sana. Mwaka huu, ZANZIBAR KUMEKUCHA.
 
Muda wa kupelekeshwa kama kondoo apelekwae machinjioni umekwisha heko Zenji na CCM watakiona cha moto kwa mtindo huu...Kwanini hawakwenda kukodi watoto huko wajaze watu wa kuwazomea kwenye kutoa maoni? Kwa maoni yangu nashauri maono ya watanzania wasikilizwe na Kikwete na mafisadi wenziwe waende kidogo likizo ili jambo hili lifanikiwe bila hivyo...ile amani ya uhuru wa bendera itatoweka dakika sifuri
 
Wale wanaishi karibu na nyumba au maduka ya wapemba nawaonea wivu sana maana muda si mrefu zali litawaangukia.Anzeni kabisa kagawana nyumba zao kwani muungano ukifa tu lazima tuwarudishe kwao.
 
Back
Top Bottom