Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Wale wanaishi karibu na nyumba au maduka ya wapemba nawaonea wivu sana maana muda si mrefu zali litawaangukia.Anzeni kabisa kagawana nyumba zao kwani muungano ukifa tu lazima tuwarudishe kwao.

Duu domo kubwa kula kwa jirani? Utakufa mdomo wazi kwa vya bure!
 
hata sisi wa bara hatuutaki muungano.. hongera kwa znz kwa kuliona hilo
 
Munaota ndoto mbaya sana. Watangayika mume wa "understimate" wazanzibari. Sisi tuna historia yetu wala hatuna wasiwasi muungano kuvunjika kwani hilo ndio jambo tulilokusudia. Hatuna haja ya muungano wala malumbano. Sisi tuna haja ya taifa letu huru. Ukoloni wa miaka 47 ufike kikomo. Kwa kuwa ni majirani tuashirikiana na tutakuwa pamoja katika east africa community musiwe na wasiwasi. Maamuzi yetu kujitenga ni vizuri zaidi kwa tanganyika. Sisi tuko "self sufficient" musiwe na wasiwasi eti wazanzibari watalala njaa. La hasha, tunaweza kumudu yetu bila wasiwasi. Zanzibar imeshindwa kujiendeleza sabau ni muungano. Basi tena na uvunjike.
 
Hii concept ya muungano na madhumuni yake CCM yenyewe imeharibu na sasa tutaona kama itabaki wakati huu wa katiba. Uwezekano mkubwa ni kifo na kaburi la ccm vinakwenda kuja sambamba na swala la muungano.
1. Kwanini tunataka muungano?
2. Hizi nchi zinachangia nini katika huu muungano?
3. Muundo wa uongozi kitaifa?
4. Katiba itengenezwe kwa misngi ipi?
 
Wanaotamani maduka na nyumba za wapemba tutawaachia.mnafikiri sisi tunaona raha kukaa huku?siku ukivunjika muungano tutafanya sherehe kubwa maana kikwazo cha maendeleo yetu kitakuwa kimeondoka.bora tuanze maisha upya kuliko muungano huu wa mashaka.
 
Kwa siasa za dunia ya leo muungano wetu ni muhimu sana, kinachotakiwa ni kuuimarisha kwa kuondoa kero zote.Nchi zote zilizoendelea zinatafuta namna ya kuungana na nchi nyingine ili kukuza nguvu za kijeshi na kiuchumi.Nchi ndogondogo na maskini katika dunia ya leo bila muungano zitaishia kuwa watumwa wa nchi za magharibi.

Kwa hiyo tuuimarishe muungano wetu na kuhakikisha tunaweka misingi imara ya nchi za afrika mashariki kuungana ili ku-survive katika dunia ya leo.Kwa taarifa yako nchi za magharibi zinaposikia nchi za afrika zinaungana wanaogopa sana kwa kuwa wanajua tutakuwa na nguvu na kuwa tishio kwao, na wanaposikia tunatengana wanafurahi sana , na wapo tayari hata kugharimia utengano huo kwa kuwa wanajua hiyo ni nafuu kwao.

Walisheherekea sudani kusini kujitenga, ila sasa hawana raha baada ya habari kuwa sudan kusini inakusudia kujiunga na jumuiya ya afrika mashariki, na baadaye east african federation.
 
Wazanzibar wanapiga kelele kuhusu Muungano ila wao wananufaika zaidi kuliko watanganyika..wanapata % flani ya kodi za bara kwa ajili ya shughuli zao za ki maendeleo..zanzibar kuna barabara ya lami inaitwa benjamin willium mkapa,alijenga mkapa..nashindwa kuelewa wanataka nini?labda wanadanganywa na mataifa ya nje
 
Wanaotamani maduka na nyumba za wapemba tutawaachia.mnafikiri sisi tunaona raha kukaa huku?siku ukivunjika muungano tutafanya sherehe kubwa maana kikwazo cha maendeleo yetu kitakuwa kimeondoka.bora tuanze maisha upya kuliko muungano huu wa mashaka.

Muda c muda,mtaanza upemba na uunguja,au mwajifanya mmesahau mlivyokuwa mnawanyanyasa wapemba? By the way wacha uvunjike 2 maana mmechukua ardhi mpaka Mbalali..na mnavyozaana mtatosha zenji kweli?
 
shekhe mbona waja juu... mbona watanganyika tunawaunga mkono kwa hili... usihofu sharif lianzisheni.. watanganyika tutamilizia nakumbuka kama niliwahi kusoma kipindi cha nyuma kwenye web ya mzalendo.. sikumbuki ni comment ama makala.. kwamba pemba na unguja wanataka kujitenga yaani mmoja wao anaona anaonewa..! so baada ya kuvunja huu muungano.. mjitayarishe kugawana visiwa vile wenyewe kwa wenyewe

Haya ni ya kawaidatu! Nasikia kuna mpango wa kuzuia Rais wa Tanganyika asitoke upande fulani jee hili unalizungumziaje?
 
Wazanzibar wanapiga kelele kuhusu Muungano ila wao wananufaika zaidi kuliko watanganyika..wanapata % flani ya kodi za bara kwa ajili ya shughuli zao za ki maendeleo..zanzibar kuna barabara ya lami inaitwa benjamin willium mkapa,alijenga mkapa..nashindwa kuelewa wanataka nini?labda wanadanganywa na mataifa ya nje

Tehee hee Hivyo Mandela aliijenga ile barabara ya Dar ndio ikaitwa jina lake? Sawa tuko tayari kukosa hiyo % (0) inayotoka kwenu.
 
Muda c muda,mtaanza upemba na uunguja,au mwajifanya mmesahau mlivyokuwa mnawanyanyasa wapemba? By the way wacha uvunjike 2 maana mmechukua ardhi mpaka Mbalali..na mnavyozaana mtatosha zenji kweli?

Ugomvi wa ndugu unauvalia suti? Kama mgawannyiko kwa kugombana basi Tanganyika ingekwishakuwa vipand vipande kwani tunawasikia kila siku mnauwana kikabila.
 
hata sisi wa bara hatuutaki muungano.. hongera kwa znz kwa kuliona hilo

Bara ndiyo itanufaika mkivunja muungano tunawabeba mno, bara inapata nini toka huko? muungano ukivunjika bara itabata dola kibao kwa kuwauzia chakula, umeme, vibali vya kuishi na kufanya kazi vya wapemba maelfu kwa maelfu, pia itabidi warudishe arhi yetu maana sheria haitawaruhusu tena. Hayo mawazo ya wengine eti muungano ukivunjika watapata misaada mingi, misaada badala ya kujitegemea? hao watoa misaada kwani hawachoki, kama misaada ingekuwa dili Karume asingeleta mapinduzi. Fanyeni kazi msitafute mchawi.
 
Ugomvi wa ndugu unauvalia suti? Kama mgawannyiko kwa kugombana basi Tanganyika ingekwishakuwa vipand vipande kwani tunawasikia kila siku mnauwana kikabila.

Ngekewa, mimi ni Mtanganyika wa kila kitu na ardhi kwetu mmeichukua sana huku Tanganyika tofauti na sisi Watanganyika tumeshindwa kuchukua kipande chochote cha ardh huko kwenu,tena waambie Maalim seif na wenzake wauze makazi yao huku Tanganyika kabla ha2jachukua kwa nguvu,crap!
 
Bara ndiyo itanufaika mkivunja muungano tunawabeba mno, bara inapata nini toka huko? muungano ukivunjika bara itabata dola kibao kwa kuwauzia chakula, umeme, vibali vya kuishi na kufanya kazi vya wapemba maelfu kwa maelfu, pia itabidi warudishe arhi yetu maana sheria haitawaruhusu tena. Hayo mawazo ya wengine eti muungano ukivunjika watapata misaada mingi, misaada badala ya kujitegemea? hao watoa misaada kwani hawachoki, kama misaada ingekuwa dili Karume asingeleta mapinduzi. Fanyeni kazi msitafute mchawi.
Hewalla bwana, nyie mnaofanya kazi naona hata Japani ilikumbwa na majanga mnachekelea waliposema watatoa msaada mara mbili.
Usijidanganye kijana Zanzibar ilishaishi bila ya kununua chochote kutoka huko na iliendelea kwani ilikuwa huru! Uhuru ndio msingi wa uzalishaji mali. Na hizo mali unazodai mtazipata kutoka kwa Wazanzibari mliwagaia au walifanyakazi kuzalisha? Kama mlishindwa kuzalisha na huku ukijisifu kuwa nyinyi ni wafasnyakazi huoni kuwa Wazanzibari hapo watakapoamuwa kufanyakazi basi mtarejea kazi zenu za umanamba( safari hii sio Tanga bali Pemba)
 
Ngekewa,mimi ni mtanganyika wa kila k2 na ardhi kwe2 mmeichukua sana huku Tanganyika tofauti na cc watanganyika 2meshndwa kuchukua kipande chochote cha ardh huko kwenu,tena waambie Maalim seif na wenzake wauze makazi yao huku Tanganyika kabla ha2jachukua kwa nguvu,crap!

Naam tumechukuwa ardhi na kukujengeeni majumba huku mkijitamba kuwa nyie ndio mnaofanyakazi. Unachosema isije ikawa ukatafsiri kejeli nitakapokwambia kuwa ni kweli kuwa Wazanzibari ndio waliowaosha macho nyie. wao ndio waliojenga magorofa pale Kariako, wao kwa kuchukua bidhaa kutoka Zanzibar ndio waliobadilisha maisha ya watu huko na mengi chungu nzima! Hata hivyo nafikiri muwe na shukurani kwani kama unavyosema huu muungano ukivunjika hao Wapemba hawatobeba maduka, mabsi ,majumba na ardhi waliochukua. Laiti kama wakoloni wangefanya waliofanya Wapemba basi ingekuwa jambo la maana.
 
Ngekewa unachonga sana,kwa hakika kumbuka nyie mnazaliana kwa wingi,my take mtatosha kweli maana mmezaliana kwa wingi huku kwe2 Tanganyika.
 
Kwanini wasiwape nchi yao? kuna nini Zanzibar nyuma ya pazia? mtoto alilia wembe mpe, akijikata atajifunza.
 
Ndugu yangu, si afadhali ya hao WATANGANYIKA na WAZANZIBAR wananchi zao ambazo ni TANGANYIKA na ZANZIBAR na Sisi WATANZANIA je? Ambao ni ZAO kati ya mtz na mznzbr,TUTAKWENDA WAPI?

Inategemea na sheria za nchi,ikiwa baba ni mzenji basi unahaki ya kuenda kwa baba,kama mama mzenji mama yako anaweza kukuombea ukawa ni mzanzibari,lakini tutaweka sheria ambazo hazitoleta athari kwa wale waliochanganya damu mbili ya visiwani na bara,ila kuna haki utazikosa ikiwa sio mzaliwa hasa hapa zanzbar,kama kugombea urais,

Lakini nitawaambia kitu kimoja,udugu utakuwepo pale pale,utengano ni nchi tu,tufahamu hilo,mie muungano ukivunjika nakuja bara kuna mtoto mmoja nimeshaposa singida wa kiarabu nasubiri amalize shule tu nije kuowa.
 
Back
Top Bottom