Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

hio ramani ni ya zamani sana-then naamini tanganyika hawawezi kukubali kuwaachia zenji pande hizo zote-naamini hata kwa vita tutapigania ardhi yetu

Idea ilikuwa kuonyesha tu kuwa Zanzibar ilikuwapo kabla ya Tanganyika.
 
hio ramani ni ya zamani sana-then naamini tanganyika hawawezi kukubali kuwaachia zenji pande hizo zote-naamini hata kwa vita tutapigania ardhi yetu

Sasa kosa letu ni lipi kupigania Zanzibar yetu mlioikalia na mnayoikalia bila ridhaa yetu?
 
huyu aliyeleta hii ramani Unimaps.com - Tanganyika & Zanzibar, 1886 sikubaliani nayo. kama muungano ukivunjika & i pray for that nchi zitarudi kama ilivyukuwa kabla ya muungano.

binafsi mimi ni mzaliwa wa tanga tena kwetu ni vile vijiji vilivyo katika pwani ya bahari ya hindi kuelekea mombasa barabara ya horohoro ukisimama pwani ya kijiji chetu pemba unaiona ileee!... na sidhani kama tukiletewa kura ya maoni ati tangayika au znz! kamwe hatuwezi tukachaguwa znz. wazee wangu wengi wa pale kijijini wanayemfahamu ni nyerere hawana historia wala ufahamu wowote kuhusu znz.. iweje leo hii mje muwaambie kwamba wao ni wa znz! this must be JOKE!

Yaani ipigwe kura tuulizwe iwapo tunataka UHURU wetu?

Kwani tulipounganishwa tuliulizwa kama tunataka kuungana na Tanganyika?

Kwanini hamuungani na Congo yenye watu wengi, mkaing'ang'ania Zanzibar?

Zanzibar for Zanzibaris.
 
mkuu hujanaielewa... walah hakuna mtanganyika anayepigania kuungana na znz , zaidi ni serikali CCM ndiyo inayo lazimisha huu muungano. Hoja yangu ilikuwa ni kwenye ramani kwani kuna mtu alitoa hoja kwamba znz wakijitenga watadai maeneo kama hiyo ramani inavyoonyesha, na nikatoa mfano kule kwetu.. kijijini tupo karibu sana na mombasa na ukisamama pwani ya kijiji chetu pemba unaionyeshea kidole.. ilee! sasa kama wa znz bari waje wadai lile eneo ni lao pia.. ilhali ya kwamba wazee wetu pale kijijini hawajui historia / wala habari yeyote kuhusu znz,. wanayo yafahamu wao ni yale matembezi ya azimio la arusha walitembea kwa mguu toka tanga mpaka DSM. iweje leo uje uwaambie ninyi ni wa znz? hapo ndipo napinga kuhusu hiyo ramani kwamba mwambao wa pwani ya tangayika ni sehemu ya znz.

So hoja yangu ilikuwa kwenye hiyo ramani.. na asante kwa kunijulisha kwamba ilikuwa ni kuonesha tu kwamba inchi yetu ilikuwepo .. ipo.. na itakuwepo, binafsi mimi kama Mtanganyika nitafurahi mkijitenga tuje tushirikiane kama kenya & UG etcl.. Niliwahi kusema kabla sisi kama watanganyika hatupigi kelele sana sababu tunaogopa ndugu zetu mtaleta hoja tunawafukuza , hatuwapendi , "mwaonaa watanganyika wenyewe hawatutaki"

on addition - nilitembelea siku moja web ya mzalendo.net kunamtu anatumia user name ya Bosco. alikuwa akiwasema vibaya kwa kuwatukana waislamu wa tanganyika kwamba wao hawajui dini.. hawana lolote.. wameshindwa hata na mahakama ya kadhi.. mabinti zao ni wavaa suruali.. etcl alinikera kweli yule jamaa.... !! Hivi wa znz chuki yenu ndio umewaingia damuni hadi kwa waislamu wenzenu wa tangayika?!! Bwana makaimati mi nawatakia kheri! "kuvuja kwa pakacha ni nafuu kwa mchuuzi"
 
Majibu ya maswali yote yatapatikana iwapo Tanganyika Italivua Koti la Muungano.

Matatizo ya muungano huu nimefuatilia kwa kina na mijadala yake,kitu ambacho nimekiona mkanganyiko wa mambo ulianzia pale Tanganyika ilipo jufuta kimnya kimnya na kujigeuza kua Tanzania.

Hebu ndugu muuliza masuali Jaribu kujaalia kua Tanganyika ipo leo na zanzibar ipo halafu tukawa na kitu cha muungano yani Tanzania,halafu Tanganyika ikafanya mambo yake binafsi kama ilivyo Zanzibar leo,na Tanzania ikashuhulika na Mambo ya muungano tu,Je ungali jiuliza maswali hayo leo?

Na huo mfumo niliokueleza ndio mkataba wa muungano ulivyoelekeza,haukusema kabisa kua baada ya muungano Tanganyika au na pia Watu wanapaswa kufahamu kua Muungano haukua wa mambo yote bali ni baadhi tu ya mambo.

Hapa ndio Maana wazanzibari hadi hii leo wanachojua nikua Tanzania ni Tunda la Muungano,Ndio maana wanataka kilichomo ndani ta tunda wakigawe sawa sawa.
Ama kosa lililofanywa na watanganyika wenyewe lakijiingiza ndani ya KOTI (MUUNGANO) na kujigeuza jina na kijifanya wao(Tanganyika) ndio Muungano na muungano ndio wao(Tanganyika),hili wazanzibari hatutaki kulijua tunachojua ni makubaliano yetu tu yaliomo ndani ya mkataba wa muungano.

Nikisema makubaliano ninamaana ya liokubaliwa na nchi mbili yani Tanganyika na Zanzibar sio yaliobadilishwa na Bunge la Tanganyika lililojibadilisha jina na kujiita Bunge la Muungano.

Wito wangu kwa Watanganyika waanze harakati za kuidai nchi yao kwanza halafu ndio tufikire tena kama iko haja ya kuungana au tukakutane Muungno wa Af.Mashariki.

Mkuuu umeongea vizuri sana, nahisi unatiibu akili yangu inakaa sawa hakika hicho ndicho tunachohitaji ili kuondoa utata katika suala hili!

nimependa haswa uliposema hivi ''Hebu ndugu muuliza masuali Jaribu kujaalia kua Tanganyika ipo leo na zanzibar ipo halafu tukawa na kitu cha muungano yani Tanzania,halafu Tanganyika ikafanya mambo yake binafsi kama ilivyo Zanzibar leo,na Tanzania ikashuhulika na Mambo ya muungano tu,Je ungali jiuliza maswali hayo leo? ''
 
Nilisha apa katu katu sitakubali kujiita mtanzania, mimi ni mtanganyika kwani sikushirikishwa kwenye maamuzi ya kuungana , kwa maana hiyo nawataka walete mswada wa mapitio ya muungano tujadili jinsi muungano wafaa kuwa. Kwa maana ya muungano 1+1=1 na si 1+1= 2. Kama 1+1 =2 au 1+1 =1 ni sawa bila idhini ya wananchi basi hesabu hiyo ni batili. Eti katiba ya tz na katiba ya zanzibar upuuzi mtupu. Kama ni z'bar basi ile nyingine ni tanganyika. Wendawazimu
 
Hakika hapa katika mahesabu walochemka!
 
Mkuu katika arithmetic 1+1 ni 2 lakini kwenye Constitutional Law inaweza kuwa 1 au 3.

Lakini kuwa na Serikali 1, hilo haliwezekani kabisa.

Wazanzibari hawakubali abadan

Zanzibar for Zanzibaris, Tanganyika mliiua wenyewe, mtajua la kufanya wenyewe.
 
Wazanzibari wameiandikia barua Umoja wa Mataifa na kutaka kumshitaki Mwanasheria Mkuu juu ya uhalali wa Muungano wa Unguja na Pemba. Katika barua yao, wanahoji kuwepo kwa mkataba wowote kati ya visiwa hivyo viwili-SOURCE RADIO1
 
hawaeleweki hawa
ukiwa Unguja utaambiwa CUF cha wapemba
ukiwa Pemba utaambiwa CCM ya waunguja, pia utaambiwa WAUNGUJA ni watu wa BARA mambo yaajabu ajabu
 
Nyerere kwa kweli duh! Alisema mkishaanza sisi Watanganyika na hawa Wazanzibari mtajikuta kuwa kwa Wale waZanzibari kumbe hakuna Mzanzibari bali kuna Mpemba na Muunguja. Akasema na Bara vile vile, mkishawatenga Wazanzibari mtaanza kujikuta kumbe kuna Wachagga na wapo Wasukumu. Ndipo akasema "dhambi ya ubaguzi haikomi, ikishaanza kula haikomi".

Sasa hata muungano wenyewe haujafika mwisho wameanza mambo ya Uunguja na Upemba! na Dar itakuwa ni kati ya Wapwani na Wabara?
 
Kweli maneno ya Mwalimu yanatimia. Ndugu zangu hawa wameshajiangalia ukubwa wa Ardhi yao na bara??
Hivi wameshapiga mahesabu ya miaka 1000 mpaka 5000 ijayo kama nchi yao itakuwepo tena? Kwa uchafuzi wa hali ya hewa kila siku ardhi ya ZANZIBAR inameguka na kupungua.

Muungano na sisi una faida sana kwao, security ya ARDHI!!! Sasa wanatengana wao kwa wao tena....

Siafiki kutengana no matter sijui vitu gani havieleweki,, wanasema siri ya ndoa anaijua baba na mama, pia hata siri ya kaburi anaijua maiti,,

Ila kama wakiona vipi! Wajitenge tu wao, sisi tutazidi kusema hatujaafiki, dhambi itawatafuna wao.!
Kwetu wachagga, wahaya, wanyakyusa, wahehe, wagogo, wagita, wasukuma, wanyiramba, wamasai, na makabila mengineyo yote tunapendana, tunataniana, tuanaoana NA HATUANGALII DINI WALA KABILA LA MTU! Sisi ni wazee wa upendo na furaha!

Dhambi ya ubaguzi itawaandama milele!!!!! Kwanza muunguja akimuona mmpemba pale birmingham anamkwepa!
 
Nyerere kwa kweli duh! Alisema mkishaanza sisi Watanganyika na hawa Wazanzibari mtajikuta kuwa kwa Wale waZanzibari kumbe hakuna Mzanzibari bali kuna Mpemba na Muunguja. Akasema na Bara vile vile, mkishawatenga Wazanzibari mtaanza kujikuta kumbe kuna Wachagga na wapo Wasukumu. Ndipo akasema "dhambi ya ubaguzi haikomi, ikishaanza kula haikomi".

Sasa hata muungano wenyewe haujafika mwisho wameanza mambo ya Uunguja na Upemba! na Dar itakuwa ni kati ya Wapwani na Wabara?

Mzee mwanakijiji! Imeshanitokea wakati nasoma Galanos Tanga tulikwenda kucheza na Popatrali wakawa wanaimba "wabara hao" wenyewe wa pwani..ubaguzi hupo
 
Wazanzibari wameiandikia barua Umoja wa Mataifa na kutaka kumshitaki Mwanasheria Mkuu juu ya uhalali wa Muungano wa Unguja na Pemba. Katika barua yao, wanahoji kuwepo kwa mkataba wowote kati ya visiwa hivyo viwili-SOURCE RADIO1

Endapo habari hii ni ya kweli, kwamba ipo barua ya namna hiyo, basi ninaona hizo ni siasa za kipropaganda za kuwatega wale wanaohoji muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa nguvu sasa hivi. Hilo la Wazanzibari kuanza kuhoji umoja wao, kama wao, haliwezi kuanza sasa kwa sababu wanauhitaji umoja huo ili kuhoji muungano na bara.
 
Wazanzibari wameiandikia barua Umoja wa Mataifa na kutaka kumshitaki Mwanasheria Mkuu juu ya uhalali wa Muungano wa Unguja na Pemba. Katika barua yao, wanahoji kuwepo kwa mkataba wowote kati ya visiwa hivyo viwili-SOURCE RADIO1

Hapa ipo kazi kweli kweli.

Lakini tukiitazama kwa mantiki ya Kisheria wanahaki kuuona na kupata nakala muungano wa visiwa hivyo kama upo. Lakini kama haupo basi ni lazima ukafanyika haraka sana ili kuondoa utata huo kisheria. Kwani ndani ya mkataba huo wataainisha kila kitu ikiwemo haki za kila upande katika kumiliki, maendeleo, mikopo na madeni n.k.

Wana haki kubwa sana kisheria. Hata mimi japo ni Mzanzibari kindakindaki lakini sijawahi kuona wala kusikia mkataba huo japo tunasema Zanzibar ni muungano wa visiwa viwili vya unguja na Pemba.
 
Nyerere kwa kweli duh! Alisema mkishaanza sisi Watanganyika na hawa Wazanzibari mtajikuta kuwa kwa Wale waZanzibari kumbe hakuna Mzanzibari bali kuna Mpemba na Muunguja. Akasema na Bara vile vile, mkishawatenga Wazanzibari mtaanza kujikuta kumbe kuna Wachagga na wapo Wasukumu. Ndipo akasema "dhambi ya ubaguzi haikomi, ikishaanza kula haikomi".

Sasa hata muungano wenyewe haujafika mwisho wameanza mambo ya Uunguja na Upemba! na Dar itakuwa ni kati ya Wapwani na Wabara?

Mzee Mwanakijiji umenikumbusha mbali sana,
Hata kule Kilimanjaro kuna wachaga wa aina nyingi,kuna wamachame,na wamarangu na warombo
 
Hapajawahi kuwepo na muungano wa Pemba na Unguja, visiwa hivyo na baadhi ya visiwa vingine pamoja na pwani ya Afrika Mashariki vilikuwa chini ya himaya moja, kabla ya kuanza kutenganishwa.
 
Wazanzibari wameiandikia barua Umoja wa Mataifa na kutaka kumshitaki Mwanasheria Mkuu juu ya uhalali wa Muungano wa Unguja na Pemba. Katika barua yao, wanahoji kuwepo kwa mkataba wowote kati ya visiwa hivyo viwili-SOURCE RADIO1

Hahaaaa haaaa! Baadaye wataanza kuhoji muungano kati ya Mkoa na Mkoa, kisha Wilaya na Wilaya, Tarafa na Tarafa, Shehia na Shehia, Nyumba na Nyumba na hatimaye mtu na mtu! Baada ya hapo ndio moto unawaka wakikosa majibu! Kweli dhambi ya ubaguzi ni hatari!
 
Back
Top Bottom