Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Gosbertgoodluck,
Chuki juu ya CCM isikufanye kuwa muongo as far as suala la Muungano! Hebu tuambie nini responce ya CHADEMA kuhusu hili? Ama kwa mimi naona CHADEMA ndio unaowauma sana Muungano huu hasa ukichukulia kauli zao baada ya Wazanzibari kuamua kuungana na pale Lissu alipoadhirika kwa kudai kuwa Zanzibar imevunja Muungano. Mbona alizungumza kwa jazba, kwa watu wasio utaka Muungano tusingetegemea responces za namna hizi!

CCM wana machafu chungu nzima na CHADEMA wameyavalia njuga lakini hili la Muungano halijawa jambo linalowakera bali ni jambo wanalolienzi!
 
Makaimati,

Hata wakati wa uhuru wa Marekani 04/07/1776 State zilizo kusini mwa USA ambazo zilikuwa zinajihusisha na shughuli za Kilimo wakati huo hazikutaka kuwa ndani ya USA, zilitaka uhuru wa kwao nje ya USA lakini zililazimishwa na watawala waliokuwepo kipindi hicho. Ndio kitu kinachoisumbua Zanzibar mpaka sasa. Nyerere alishajitanua muda mrefu na sasa mnataka kudai uhuru wenu jioni na wenzenu walishadai asubuhi. Hivi hamna mbinu nyingine za kudai nchi yenu.. tumechoka na ngonjera zenu kwenye hizi electronic media kama vipi nendeni porini mpiganie nchi kama hakijawakuta kama Kilichowapata Tamil Tagers kule Sri-Lanka, unless tuwaona mnanjaa tu kama viongozi wenu wa CUF na mkipewa pelemembe mtatulia ila bahati mbaya hamna pelemende za kuwatosha wote kwa hiyo mtapiga miayo mpaka mkome

Lingine pia fanyeni tafiti kuhusiana na society yenu.Tafitini hivi Social Cohesion ya Zanzibar iko kiwango gani kwa sasa?. Hivi Waafrica weusi na wa kiarabu wanaoleana? Tafitini je wazazi wa asili ya kiarabu wanaruhusu endapo kijana wao wa Kiume anataka owa binti mweusi? and viseversa,Tafitini wealth inanafasi gani kwenye hizo ndoa za race mbili tofauti?Fanyeni tafiti za tofauti ya kipato kati ya waafrica na waarabu na nini kifanyike. Msije mkaja chinjana baada ya kujitenga Viongozi wenu hao wanawadanganya kuwa mnakosa misaada kwa kuwa mko ndani ya muungano. Kwa maana nyingine mnataka muwe nje ya muungano ili mpate misaada.... ndo wanasaisa wenu wanawaandaa kwa mawazo tegemezi hayo.. ndio mtaendelea. Give us a break nchi inamatatizo ya uchumi na ufisadi watu wanatafuta ufumbuzi nyie mnapollute kwa maada zenu za Muungano. Tafuta mbinu zingine unless mnapiga makelele tu wakati watu tupo kutafakari hoja muhimu la kulitoa taifa kwenye umaskini na rushwa
 
Ngekewa said:
Chuki juu ya CCM isikufanye kuwa muongo as far as suala la Muungano! Hebu tuambie nini responce ya CHADEMA kuhusu hili? Ama kwa mimi naona CHADEMA ndio unaowauma sana Muungano huu hasa ukichukulia kauli zao baada ya Wazanzibari kuamua kuungana na pale Lissu alipoadhirika kwa kudai kuwa Zanzibar imevunja Muungano. Mbona alizungumza kwa jazba, kwa watu wasio utaka Muungano tusingetegemea responces za namna hizi!

CCM wana machafu chungu nzima na CHADEMA wameyavalia njuga lakini hili la Muungano halijawa jambo linalowakera bali ni jambo wanalolienzi!

Ngekewa,

..Chadema, kama walivyo CUF, wanataka muungano wa serikali 3.

..CCM sera yao ni muungano wa serikali 2, kama njia ya mpito kwenda kwenye serikali 1.

..msimamo na sera ya CCM kuhusu muungano uliwekwa wazi wakati wanaizika hoja ya wabunge 55 waliotaka kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.
 
Kwa maoni yangu Njelu kasaka na wale wenzake 55 ndi owaliotaka kuikoa CCM hadi kufikia kujivua ugamba amabo is too late ukweli Watanzania na Wazanzibari wanatakiwa wachukue uamuzi kama wa kule Egypt waende mahakamani kuomba court iipige marufuku CCM kwa sababu hizi hapa na hapa itakua ndio njia rahisi kupata uhuru na mageuzi ya kweli Tanzania haya yote yaliowakuta chama cha Mubarak ni sawa ya CCM kwani CCM pia imeuwa kila kona ya Tanzania na ikifikia kupigwa marufuku au kuangushwa kuna vitu vingi vya kuwafikisha mahakamani, wameuwa Watanganyika na Wazanzibari .
s
The same source told Al-Masry Al-Youm that the court has said the party, established in 1978, violated the principles that formed the cornerstone of its operations, which led to social and political corruption and undermined the rights and freedoms guaranteed by the Egyptian constitution.

The party monopolized power and sought to weaken oppositional political powers and parties, suppress freedoms and detain activists with opposing political views, and discriminate between Egyptian people, the source added.

The court said the party used governmental security bodies to crack down on its opponents.
 
@Straatkasyambe,

Straatkasyambe,

Maneno yako na 'tone' yako ukichunguza sana, utaona imejaa chuki, kejeli na dharau nyingi dhidi ya Wazanzibari na hii inanipa shaka kwamba ama huelewi kitu au hujielewi lakini zaidi unaendeshwa na hayo nilioandika hapo mwanzo na kuendekeza zaidi jazba.

Kufananisha mazingira ya Muungano wa USA na wa Zanzibar na Tanganyika ni upotofu usiomithilika na ndio maana nikasema hujielewi.

Tanganyika iliivamia Zanzibar na hilo ndilo tunalopigania kujipapatua na wala si jambo la kushangaza na wala hatutakuwa wa kwanza. Wakati wewe unasema ya USA, mbona umesahau ya USSR? Iko wapi leo wakati kuna Jamhuri huru 15 zilizotokana nayo? Iko wapi Yugoslavia? Iko wapi Senegambia? Iko UAR? Zote hizi zilikuwako, haziko tena na zimetafuta njia nyengine za kistaarabu za kushirikiana. Na zipo nchi kadhaa za kukutolea mifano lakini hizo zinakutosha nadhani.

Lugha zako za vitisho ni za kijinga kwa wakati huu. Zanzibar haitafikia hivyo na iko siku Zanzibar itakuwa huru, tena. Hatuna haja ya kuchinjana, wala kuchunana ngozi na kuua Maalbino maana Baraza letu la Wawakilishi limeshaanza kuchukua hatua madhubuti kufikia lengo.(Angalia Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya 2010)

Kuhusu mambo yetu ya ndani hayakuhusu na nini tunafanya si kazi yako kabisa. Zanzibar ilikuwa ni nchi ya amani na utulivu mpaka Nyerere alipokuja na fitna zake kwa kuichukia Zanzibar kama alivyosema hapa,


"If I could tow that island out into the middle of Indian Ocean, Id' do it."


Zanzibar imedumaa kiuchumi kwa uvamizi wenu na imekuwa tegemezi, jambo mnalolifurahia nyinyi kwa maslahi ya wakubwa wenu. unajisahau kuwa na wewe ni victim tu kama sisi.

Huu ni ukumbi huru na mada yoyote ikija tutaijafili na hata kuianzisha ikibidi. Kama wewe unaudhika, nenda Loliondo kwa Babu ukajimalize.

Zanzibar imekuwapo mwanzo kabla ya Tanganyika na hio jeuri na unga'ang'anizi wenu hauna muda kumalizika.

Zanzibar inaweza kuwepo bila ya Tanzania, Tanzania jee?

Nyerere huyo huyo uliemsema kwenye maandishi yako, amewahi kusema,


"Ikiwa watu wa Zanzibar, bila ya kuingiliwa na watu wa nje na ikiwa wana sababu zao, wakaamua kuwa Muungano umekuwa kero kwa maisha yao, na kwamba hauna maslahi na wao sitowalazimisha kubakia na Muungano huo. Muungano huu utasita pale tu NCHI shiriki itakapoamua kujitenga"


by Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Ikiwa muasisi huyu wa huo "MUUNGANO" amesema hivi, hivyo kubwa hapa ni lipi?

Na hivi majuzi, wakati wa kujadili huu mswada wenu uliokusudia kutumaliza, muasisi mwengine, Mzee Hassan Nassor Moyo, alisema, "Bwana Sitta, its over"

Waziri wa SMZ, tena kutoka CCM yenu, Mansour Yusuf Himid nae alisema, "Its now or never"

Katika kupigania Utaifa wao Wazanzibari hawana u CCM wala u CUF ndugu yangu mrukia mada.

Huna hoja wala huna haki ya kukataza Wazanzibari wasijadili mustakabal na hatma ya nchi yao wanayoipenda, Zanzibar.

Zanzibar for Zanzibaris and we cant wait to see your backs.

Zanzibar Zindabad
 
@Straatkasyambe,
Wewe mwenyewe hujafanya utafiti wowote na wala si mdadisi.Nitakueleza hapo chini.

Huyu Makaimati kaeleza hisia zake vyema lakini kasahau nadharia moja muhimu na ya msingi kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.Ile ni aina ya crusade ambayo ili kufanikisha vita hiyo ya kidini ilitumia mianya yote..ukabila,siasa za kiwakati (ujamaa&ubepari),ubaguzi wa rangi na kila kitu.Ushahidi upo mwingi kuonesha Nyerere alikuwa mbaguzi wa rangi na mwenye chuki za kidini.Hii ndiyo injini ya kuongoza mapinduzi yale.Waislamu wa enzi zile waliomsaidia Nyerere ni kutokana na uduni wa elimu zao za uislamu.

Hizo kampeni za uongo kuhusu waarabu,waafrika au weusi na weupe waislamu wa leo wala haziwaingii.Kwanza Karume mwenyewe hakuwa nazo,aliowa waarabu wengi pamoja na mamake raisi Amani Karume aliyemaliza muda wake.Amani naye kamuoa Shadya.Mzee Jumbe na raisi mstaafu Mwinyi wakisoma huu uongo wako watakuona chizi tu.


Wakati huo muungano unafanyika wewe ulikuwa ni mkubwa uko sekondari,inasikitisha kuwa siku zote umelala hujawahi kumuona hata Jamshid aliyekuwa kibaraka wa mwisho wa muiengereza kwa jina la sultan kule Zanzibar.Ana tafauti gani na mimi kwa rangi.

Jengine ni kwamba unapozungumza watanganyika, kama kweli wewe ni mdadisi utagundua kuwa waislamu karibu wote wa Tanganyika hata wa Kigoma tunaunga mkono uhuru wa Zanzibar kwa sababu tunajuwa ni heshima ya dini yetu.Hivyo hizo peremende muda utafika zitamwagwa kila pembe lakini hakutokuwa na wa kuziokota.
 
Pindi Muungano utakapo vunjika Watanganyika tutafaidikia kuona Chama Cha Magamba au majambazi Kikifa kifo cha mende. CCM imezaliwa ili itunze Muungano sio Maslai ya Tanganyika.

CCM wamefanya Muungano ndio Mtaji wao ili waweze kuinyonya Tanganyika. Pindi tutakapo fanikiwa kuuvunja Muungano na CCM is kushne, faida moja wapo ya kuvunjika kwa Muungano ni hio hapo.

Kama bado tunauhitaji Muungano basi Katiba ya Nchi iandikwe upya na Tanganyika Izaliwe na sisi tuwe na raia wetu na ccm iuawawe.
 
CCM wameshasaturate hamna namna watakayo weza rudi just is the matter of time tu kwa wao kukabali kushindwa issue ya msingi sisi kama wanaharakati tujipange na ajenda za msingi na tuweze kuzitetea kwa dhati.

Faida za kuvunja muungano ni nyingi sana kwa sasa kuliko hasara kwa maoni yangu tungeuvunja muungano wa sasa kwanza tuweze kuconcrete kwenye mambo ya msingi sana kama la katiba mpya tume huru ya uchaguzi ,east african community, uchumi wetu , kuhakisha watawala wanaelewa kwamba wameshasaturate so wa step down kistaarabu wengine waje wajenge nchi.

Muungano kwa sasa ni kero kubwa kwa kweli tuvunje tuondoe tofauti kwa kuwa sisi wote ni waungwana itakapo kuwa kuna haja ya kuungana tutafanya hivyo tena ila kwa sasa say no kwa muungano usio na tija.
 
mhhhh .sijui kama wapemba walio jenga huku bara na biashara zao itakuwaje, pili umeme,vyakula nk vinatoka bara,tukiwakatia itakuwaje?wale kule hawana jeshi na hawa viongozi walio huku watafanyaje? itabidi pia zanzibar ife kuwe na pemba na unguja sijui dr shein wa pemba atakuwa rais wa wapi na unguja atatawala nani.ni ngumu lakini kuvunja muungano wkt CCM inamuandaa DR Mwinyi kugombea 2015.hbr ndio hiyo.
 
Siutaki muungano usio na tija kama huu,lakini napingana na mleta hoja ktk point kwamba muungano uvunjike au usivunje ,ccm itakufa kifo kibaya na hii ni ndani ya miezi48 ijayo. Si bara si visiwani ccm imekwisha!
 
Kwa kadiri siku zinavyokwenda, suala moja kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar linajidhihilisha. Kwamba wenzetu wa Zanzibar hawatambui Serikali ya Muungano wa Tanzania kama serikali yao, wanaichukulia kama serikali ya Tanganyika.

Kwa msimamo huo, basi hawamtambui hata Rais wa jamhuri ya muungano kama Rais wao, halikadhalika mawaziri wa muungano, mwanasheria mkuu na hata bunge la jamhuri ya muhungano. Kwao viongozi hao na vyombo hivyo ni kwa ajiri ya Tanzania bara au Tanganyika (kama wao wanavyoita)

Nasema hivi kutokana na ushahidi wa kimazingira unaoendelea kujidhihilisha. Malalamiko yaliyoibuka zaidi upande wa Zanzibar kuhusu muswada wa marejeo ya katiba ya jamhuri, yalikuwa kwamba wao (Zanzibar) hawakushirikishwa! Kibaya zaidi hata viongozi wa serikali ya mapinduzi nao wana mtazamo huo!

Hii haijalishi, ubaya wa muswada wenyewe. Kama tatizo hili tunaliacha hivi hivi, ipo siku Rais wa jamhuri atafanya jambo kwa niaba ya taifa, wazanzibari wajitoe kwamba wao hawahusiki! Kwa kuwa si Rais wao.

Hata kama katiba inaruhusu kushirikishwa kipekee kwa Zanzibar katika baadhi ya mambo, haina maana kwamba kila jambo washirikishwe maana kuwepo kwa viongozi wa muungano tayari wameshirikishwa.

Kwa nini washirikishwe kuandaa muswada wa katiba kama wanavyotaka? waliona nani ameshirikishwa!? Kama Wanyambo kule Karagwe na Wafipa huko Sumbawanga hawalalamiki kutoshirikishwa kwa kuwa wanaamini viongozi walioshiriki kundaa muswada huo ni Viongozi wao, Wapemba wa Waunguja hawana hoja ya kutaka kushirikishwa kipekee!

Maana Rais au serikali ya jamhuri ya muungano inapotekeleza wajibu wake, ni kwa ajili ya watanzania wote (wazanzibari na wa-bara) na wala si kwa niaba ya Tanganyika pekee.


Kwa mfano, hata kama Rais kikwete na mwanasheria wake mkuu na wataalamu wa sheria waliokaa kuandaa muswada ya marejeo ya katiba, hawakushirikisha serikali ya mapinduzi (wazanzibari), tatizo li wapi! Kwa maana hawa ndiyo true representative wa watanzania wote toka pande mbili za muungano.

Kwani walipokuwa wanampigia Rais kura walimchagua akawe Rais wa Tanganyika, kwa nini hawakuhoji, na kuwaachia wakurya na wamakonde wajichagulie Rais wanayemtaka! kama wao walivyofanya kwa kumchagua Rais wa bara za la mapinduri.

Pamoja na mapungufu ya kiuongozi waliyonayo viongozi wetu wanapaswa wawe na ushujaa wa kuweka msimamo hususani kuhusiana na chokochoko hizi za muungano, vinginevyo muungano utabaki pambo tu na sifa mbele ya mataifa wakati, hakuna muungano kwa maana ya muungano.

Vinginevyo nifahamishwe vizuri kisheria, kikatiba na ahata kimantiki, mipaka ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na vyombo vyake, kwa nini inapotenda haichukuliwi ni kwa ajili ya wananchi wa Zanzibar na bara- Tanganyika.

Tatizo pengine linaweza kuwa kutokuwepo serikali ya bara (napata ukakasi kutumia Tanganyika maana jina hilo lilikufa mwaka 1964, vinginevyo nikumbushwe vinginevyo) na kwa kuwa serikali na vyombo vya muungano ndivyo vinafanya kazi za sehemeu ya bara pamona na muungano, basi wenzetu wa Zanzibar wanashindwa kuelewa ni wakakti gain, Rais kikwete kwa mfano, anafanya kazi kama Rais wa muungano au wa bara, maana bara hawana Rais.

Hili ndilo linaipa nguvu hoja ya wanaopinga maoni ya serikali kwamba muungano usiwe sehemu ya mijadala wakati wa mapitio ya katiba. Vinginevyo siku wa-tanganyika watakapoingiwa wazimu kama wa wenzao, hapatakalika maana kimantiki nao wnaweza kuwa na malalamiko!

Kwa mfano, pale panapohitaji kushirikisha pande mbili za muungano, uwiano wa wawakilishi ukoje, idadi inayotoka visiwani inawiana na idadi inayotoka bara, kwa viwango vyovyote vile, kama ukubwa wa jiografia na hata kiuchumi, ukiacha kisiasa.

Wanaweza kuhoji kuna haja ya kuwa na idadi iliyopo sasa ya wabunge toka visiwani, ikilinganishwa na ukubwa wa maeneo wanayowakilisha ukilinganisha na majimbo ya bara, kwa kuzingatia gharama za kuwaudumia wabunge hao.

Au kuhoji, wanachokuwa wanafanya bungeni pale, mabo yasiyohusu muungano yanapojadiliwa bungeni. Kuna haja ya wabunge wa Zanzibar kupiga kura kuhusiana na jambo lisilohusu muungano, kwa mfano sheria ambayo haifanyi kazi Zanzibar, kwanini wasikae majumbani kwao na kutakiwa kuhudhuria pale masuala ya muungano yanapojadiliwa!

Ilipohojiwa kwa nini wazanzibari wanaajiriwa na kupewa fursa katika vyombo ambavyo si vya muungano, kama jeshi la kujenga taifa (JKT) wakati wasukuma na wafipa hawawezi kupata ajira katika jeshi kama hilo upande wa pili wa muungano (JKU), serikali ilijibu kwamba, JKU ni ya Zanzibar kama lilivyo baraza la mapinduzi na kwamba wazazibari wanaajiriwa JKT na kuwa na haki ya kumiliki ardhi Kariakoo na hata Kigoma kwa kuwa ni Watanzania!

Kama hivyo ndivyo, nionavyo mimi na kwa mantiki ya majibu ya serikali kuhusu fursa wanazopewa wazanzibar katika pande zote mbili za muungano kwa kuwa ni watanzania - bila kujali kama wenzano hawapati fursa adimu kama hizo visiwani, basi hata pale maamuzi au hatua zinapochuliwa na uongozi wa taifa (Tanzania) wachukulie kwamba wamewakilishwa sawa na wenzao wa Tanganyika maana wanaofanya maamuzi hayo ni viongozi wa atanzania na wala si wa watanganyika pekee.
 
Kwanza wabunge wa CCM toka Zanzibar watatoweka. Bara watapoteza Miji karibu yote na kubaki Vijiji vya wasio elimu
 
theophilius,

Mkuu.

Kwa kuandika post hii, Tayari umegundua kuwa Muungano ni changa la macho.

Mambo mawili nimeyasoma katika post yako.

Kwamba Zanzibar hawahitajiki kushirikishwa.
Kwamba Zanzibar ni kama Karagwe.

Mawazo yangu.
Moja historia ya Muungano huijui vyema...Tanganyika na Zanzibar hawakuunganisha kila kitu. Na kama ni hivyo kila sehemu ilibakisha mamlaka yake kwa mambo yasiyo ya Muungano.

Utata unakuwa hausawazishiki pale inapokuwa rais wa muungano, pia ni rais wa Tanganyika. Mgongano wa kimaslahi unajitokeza inapokuja issue ya kuipunguzia mamlaka na hadhi Zanzibar.

Mkuu, Unasema Tanganyika ilikufa, hapa pia inaonekana hujaipitia hati ya Muungano.TANGANYIKA haikufa wala haikuuliwa iliwekwa chini ya mwevuli wa Muungano.(kubebwa)

Kosa jengine nililoliona ni kuwa Unaifananisha Zanzibar na Karagwe na Sumbawanga....kweli Zanzibar ni sehemu kama Sumbawanga lakini Zanzibar ina hadhi ambayo Karagwe haina. Zanzibar iliungana na Tanganyika kama nchi. Je lini Karagwe au Sumbawanga zilikuwa nchi? Tukisawazisha kosa hili tutaitazama Zanzibar kama Mbia wa Muungano na sio kama sehemu tu kama Karagwe , Arusha au Sumbawanga.

Mkuu...Hii katiba iliyopo sio sheria kuu ya Jamhuri ya Muungano au Muungano wenyewe. Kuna sheria iliyo juu ya Katiba nayo ni the articles of Union. Kama katiba inataja kitu ambacho ni kinyume na hati hii maana yake hiyo kitu si halali.

Kwa bahati mbaya wengi tunaoandika hizi issue za Muungano tunatawaliwa na ushabiki. Jaribu kuuangalia Muungano wa Tanzania ukiwa si Mtanzania , ndio hapo utaona madudu yake.

Pitia hizi.
Articles.znz+Tngk[1]

http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27
 
Nonda,

nimekupata mkuu, ila bado nina tatizo, nalo ni je rais, na uongozi wa serikali ya muungano si jambo la muungano! kama jibu ni ndiyo, kwa nini wanapotekeleza wajibu wao inachukuliwa si kwa niaba ya wazanzibari, mpaka washirikishwe, na kama jibu ni hapana kwa nini wanapiga kura kumchagua raisi? nauliza hivyo kama layman wa constitutional law, japo natambua kwamba kutojua vifungu haitoshi kutokufanya uchambue mambo kimantiki.

uzuri umekubali kwamba muungano una matatizo, kama mimi ninavyoamini ndiyo maana napata shida ku-digest haya ninayojadili
 
Wana JF, nakwazika na saa zingine nasikia kupata wehu na mambo kadhaa ya Jamuhuri yetu ya Muungano. Naomba mnisaidie majibu au kutoa hoja na mwelekeo katika haya yafuatayo:
1. Tangayika na Zanzibar (nchi mbili) ziliungana na kutengeneza nchi mbili, Tanzania na Zanzaibarhii inawezekanaje??? marais wawili?? Katiba Mbili? tena kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar iliyofanyiwa marekebisho mwaka jana, Zanzibar ni nchi huru yenye mipaka yake?

2.Tanganyika iko wapi katika Muungano au Watanganyika (kama sehemu mojawapo ya muungano) tunatambulika au kuji-identify wapi katika Muungano?

3. Je kipi ni sahihi kutamka au kutambulika kati Tanganyika na Tanzania bara??

4. Najua kwenye hesabu inawezekana 1 + 1 = 2 lakini huwezi kuunganisha nchi mbili ukapata nchi mbili, hapa si hakuna muungano??? Au sisi ni shirikisho?

5. Katika kuandika katiba, katiba ya WAZANZIBAR iliandikwa na wao wenyewe tena na referendum yao wenyewe bila kuhusishwa Tanzania bara. Sasa sisi wa bara tunapotaka kuandika katiba kwanini iwe ndio katiba ya Muungano pia???

6. Watanganyika tuna haki gani katika muungano kuandika katiba yetu wenyewe kwanza (inayotuhusu sisi na watu wetu hao zaidi ya Million 40) kabla ya waZanzibari kuhusishwa??? NAONA TANGANYIKA TUNAINGILIWA NA KUNYIMWA HAKI YA KUTAMBULIKA (KAMA SEHEMU MOJAWAPO YA MUUNGANO) KULIKO HATA MNAVYOFIKIRIA?

7.Kwanini ya ZANZIBARI yawahusu ZANZIBARI TU na ya Hayatuhusu WABARA,wakati ya BARA yawahusu WANZANZIBARI??? au ndio mambo ya chako changu, changu changu??

8. Inakuaje Rais wa Muungano ndio rais wa Bara (Tanganyika - ambayo haipo) tena ni Rais wa Zanzibar pia?? hapohapo eti Wazanzibar Wana Rais wao tena????

9. Inakuaje Tanzania ndio Tanganyika pia???? yaani hata sijui nauliza nini nahisi naanza kuchanganyikiwa???

10. Kama sisi ni muungano kwanini Wazanzibar wampigie kura Rais Wetu (wa bara) na sisi hatumpigii kura kumchagua Rais wao (zenji)????? Huu ni muungano wa aina gani huu???? muungano nusu (partial) au????

11. Hivi sasa naambiwa KATIBA YA ZANZIBAR NI KINYUME NA KATIBA MAMA YA MUUNGANO na ETI pia kutokana na marekebisho ya KATIBA YA ZANZIBAR ya Mwaka jana HUU MUSWADA wetu wa katiba ni batili HIYO PIA ni kwa mujibu wa KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO kwa kuwa haujahusisha Baraza la wawakilishi la Zanzibar na Rais na Mwanasheria wau sijui......Hapa nahisi haya mambo yanazunguka katika duara la kizungu zungu (in cycles) na yaani inakua ni kama ile ishu ya nani alianza kati ya kuku na yai na ndipo hunifanya nijione kama akili yangu imefika mwisho wa kufikiria...which is which jamani????

12. Haya yote ya muungano ambayo na Zanzibar inahusika yananichanganya akili sana naweza kuchanganyikiwa mwenzenu! Je sisi (Tanzania Bara) tunaweza kutumia utaratibu gani utakao tuwezesha kuandika katiba yetu wenyewe kwanza kabla na waZanzibar kuhusika?

13. Nashindwa hata kuendelea sijui hata niulize nini, yaani sijui????

14. Wakati hapo hapo kuna ANGALIZO hili hapa chini (alilolisema Nyerere) nalinukuu...
"....On april 26, 1964, two independent African states surrendered their sovereignty to one New country - the United Republic of Tanzania......"

......naona kwa mujibu wa marekebisho ya katiba (ya Zanzibar - 2010) Zanzibar washajichululia 'SOVEREIGNTY' yao Sisi Bara tunasubiri nini????

15. Yaani hata sijui, hivi naruhusiwa kujadili muungano au siruhusiwi???...

Msaada wenu jamani!......
 
Back
Top Bottom