Kwa kadiri siku zinavyokwenda, suala moja kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar linajidhihilisha. Kwamba wenzetu wa Zanzibar hawatambui Serikali ya Muungano wa Tanzania kama serikali yao, wanaichukulia kama serikali ya Tanganyika.
Kwa msimamo huo, basi hawamtambui hata Rais wa jamhuri ya muungano kama Rais wao, halikadhalika mawaziri wa muungano, mwanasheria mkuu na hata bunge la jamhuri ya muhungano. Kwao viongozi hao na vyombo hivyo ni kwa ajiri ya Tanzania bara au Tanganyika (kama wao wanavyoita)
Nasema hivi kutokana na ushahidi wa kimazingira unaoendelea kujidhihilisha. Malalamiko yaliyoibuka zaidi upande wa Zanzibar kuhusu muswada wa marejeo ya katiba ya jamhuri, yalikuwa kwamba wao (Zanzibar) hawakushirikishwa! Kibaya zaidi hata viongozi wa serikali ya mapinduzi nao wana mtazamo huo!
Hii haijalishi, ubaya wa muswada wenyewe. Kama tatizo hili tunaliacha hivi hivi, ipo siku Rais wa jamhuri atafanya jambo kwa niaba ya taifa, wazanzibari wajitoe kwamba wao hawahusiki! Kwa kuwa si Rais wao.
Hata kama katiba inaruhusu kushirikishwa kipekee kwa Zanzibar katika baadhi ya mambo, haina maana kwamba kila jambo washirikishwe maana kuwepo kwa viongozi wa muungano tayari wameshirikishwa.
Kwa nini washirikishwe kuandaa muswada wa katiba kama wanavyotaka? waliona nani ameshirikishwa!? Kama Wanyambo kule Karagwe na Wafipa huko Sumbawanga hawalalamiki kutoshirikishwa kwa kuwa wanaamini viongozi walioshiriki kundaa muswada huo ni Viongozi wao, Wapemba wa Waunguja hawana hoja ya kutaka kushirikishwa kipekee!
Maana Rais au serikali ya jamhuri ya muungano inapotekeleza wajibu wake, ni kwa ajili ya watanzania wote (wazanzibari na wa-bara) na wala si kwa niaba ya Tanganyika pekee.
Kwa mfano, hata kama Rais kikwete na mwanasheria wake mkuu na wataalamu wa sheria waliokaa kuandaa muswada ya marejeo ya katiba, hawakushirikisha serikali ya mapinduzi (wazanzibari), tatizo li wapi! Kwa maana hawa ndiyo true representative wa watanzania wote toka pande mbili za muungano.
Kwani walipokuwa wanampigia Rais kura walimchagua akawe Rais wa Tanganyika, kwa nini hawakuhoji, na kuwaachia wakurya na wamakonde wajichagulie Rais wanayemtaka! kama wao walivyofanya kwa kumchagua Rais wa bara za la mapinduri.
Pamoja na mapungufu ya kiuongozi waliyonayo viongozi wetu wanapaswa wawe na ushujaa wa kuweka msimamo hususani kuhusiana na chokochoko hizi za muungano, vinginevyo muungano utabaki pambo tu na sifa mbele ya mataifa wakati, hakuna muungano kwa maana ya muungano.
Vinginevyo nifahamishwe vizuri kisheria, kikatiba na ahata kimantiki, mipaka ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na vyombo vyake, kwa nini inapotenda haichukuliwi ni kwa ajili ya wananchi wa Zanzibar na bara- Tanganyika.
Tatizo pengine linaweza kuwa kutokuwepo serikali ya bara (napata ukakasi kutumia Tanganyika maana jina hilo lilikufa mwaka 1964, vinginevyo nikumbushwe vinginevyo) na kwa kuwa serikali na vyombo vya muungano ndivyo vinafanya kazi za sehemeu ya bara pamona na muungano, basi wenzetu wa Zanzibar wanashindwa kuelewa ni wakakti gain, Rais kikwete kwa mfano, anafanya kazi kama Rais wa muungano au wa bara, maana bara hawana Rais.
Hili ndilo linaipa nguvu hoja ya wanaopinga maoni ya serikali kwamba muungano usiwe sehemu ya mijadala wakati wa mapitio ya katiba. Vinginevyo siku wa-tanganyika watakapoingiwa wazimu kama wa wenzao, hapatakalika maana kimantiki nao wnaweza kuwa na malalamiko!
Kwa mfano, pale panapohitaji kushirikisha pande mbili za muungano, uwiano wa wawakilishi ukoje, idadi inayotoka visiwani inawiana na idadi inayotoka bara, kwa viwango vyovyote vile, kama ukubwa wa jiografia na hata kiuchumi, ukiacha kisiasa.
Wanaweza kuhoji kuna haja ya kuwa na idadi iliyopo sasa ya wabunge toka visiwani, ikilinganishwa na ukubwa wa maeneo wanayowakilisha ukilinganisha na majimbo ya bara, kwa kuzingatia gharama za kuwaudumia wabunge hao.
Au kuhoji, wanachokuwa wanafanya bungeni pale, mabo yasiyohusu muungano yanapojadiliwa bungeni. Kuna haja ya wabunge wa Zanzibar kupiga kura kuhusiana na jambo lisilohusu muungano, kwa mfano sheria ambayo haifanyi kazi Zanzibar, kwanini wasikae majumbani kwao na kutakiwa kuhudhuria pale masuala ya muungano yanapojadiliwa!
Ilipohojiwa kwa nini wazanzibari wanaajiriwa na kupewa fursa katika vyombo ambavyo si vya muungano, kama jeshi la kujenga taifa (JKT) wakati wasukuma na wafipa hawawezi kupata ajira katika jeshi kama hilo upande wa pili wa muungano (JKU), serikali ilijibu kwamba, JKU ni ya Zanzibar kama lilivyo baraza la mapinduzi na kwamba wazazibari wanaajiriwa JKT na kuwa na haki ya kumiliki ardhi Kariakoo na hata Kigoma kwa kuwa ni Watanzania!
Kama hivyo ndivyo, nionavyo mimi na kwa mantiki ya majibu ya serikali kuhusu fursa wanazopewa wazanzibar katika pande zote mbili za muungano kwa kuwa ni watanzania - bila kujali kama wenzano hawapati fursa adimu kama hizo visiwani, basi hata pale maamuzi au hatua zinapochuliwa na uongozi wa taifa (Tanzania) wachukulie kwamba wamewakilishwa sawa na wenzao wa Tanganyika maana wanaofanya maamuzi hayo ni viongozi wa atanzania na wala si wa watanganyika pekee.