pasco,
Ndugu yangu Pasco huyu alieandika makala hio hapo juu ni Muhammed Khelef Ghassany na huyo unaesema aliandika hicho kitabu, "KWAHERI UKOLONI, KWAHERI UHURU", ni Dr. Harith Ghasany.
Vyovyote wiwavyo, kwa maana ya hizo nadharia, la muhimu ni kwamba kwa Wazanzibari sio issue kubwa sana ya kuwafanya waukubali huu unaoitwa "Muungano".
Kwa Wazanzibari walio wengi, huu si Muungano bali ni nchi moja kubwa kuivamia nyengine ndogo. Wanaamini kwamba, matatizo yao yote ya kiuchumi na kijamii, yamesababishwa na huu muungano.
Wanachodai ni kuvunjika kwa muungano huu na sio kuondoa kero, kwani huu Muungano wenyewe ndio kero. Kama zilishindikana kwa miaka 47, hatuwezi kuziondoa leo kwa sababu hakuna political goodwill.
Makala hii inaonyesha ji nsi watawala wetu kujiandaa kwa kila hali kuulinda huu Muungano usio na faida kwa Wazanzibari na Watanganyika ingawa hapana shaka kuna viongozi wa pande zote mbili wanafaidika nao.
Nataka kukuelewesha kwamba makovu hayataweza kuondoka kabisa kabisa lakini rika la leo la Wazanzibari hawashughulishwi na hayo tena ila kupotea kwa Utaifa wao.
Wakati wa mjadala wa huu mswada hivi majuzi, Wazanzibari wa rika zote na political divide zote, walipeleka ujumbe kuwa Muungano kwa hivi ulivyo haukubaliki.
Wanasema uvunjike na kama kuna haja ya kushirikiana na nadhani ipo, basi itokane na misingi ya kuheshimiana.