Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Hayo ni ya mfamaji. Zanzibar will rise again and the Second Zanzibar Republic is coming.

Zanzibar ilikuwapo kabla ya Tanganyika na Zanzibar itakuwepo bila ya Tanzania lakini how about Tanzania without Zanzibar?

Soma historia ya Zanzibar uone na ulinganishe na Tanganyika.

Daini Tanganyika yenu, msijishughulishe na nchi za watu.
 
Does it concern you? Umesikia lini Wapemba na Waunguja wakiuwana kama mnavyofanya nyie huko? Kwani hilo tatizo waliosema UvCCM kuwa Rais hawezi kutoka Kaskazini unalionaje vile?

Kwani cku hzi wapemba na waunguja mnaoleana? Mnazikana? Tangu mkimbilie Shimoni mmekuwa ndugu?
 
Wewe Ngwini hutujui hata kidogo, mmezoea kusikiliza propaganda za CCM sana. Nilichokwambia ni kuwa mlituvuruga kwa maslahi ya viongozi na wala si kwa Watanzania lakini hizo pia zilitokana na fitna zenu.

Tunawaoa hata Wabara na huku tunao kibao.

Jadilini hoja wacheni trivial issues za kuona na kuzikana, kwani maiti gani ulosikia imeliwa na fisi Zanzibar ?

Issue hapa ni Muungano usiofanya kazi kwa maslahi yenu wala yetu.

Daini Tanganyika yenu, ya Zanzibar tuwachieni wenyewe, inawahusu nini na mmetukuta?
 
Wazanzibar watambue mwisho wa muungano ndiyo mwanza wa mwisho wao kiustawi, kwani wengi wao ni wafanyabiashara wanaotegemea soko na bidha za bara.

Kwa hayo wajue soko lao halitakuwa na mazigira yaleyale, itakuwa sawa na kununua na kupeleka bidhaa malawi au uae.

Ndugu zetu wachina na india wanogopewa duniani kwa asilimia kubwa kwa sababu ya wingi wao, hivyo kwa uchache wenu, na uchumi wenu unao tegemea utalii ambao kwa kiasi kikubwa upo kinyume na maadili ya tamaduni zenu; mtakuwa mmejimaliza wenyewe.

Tafuteni njia bora ya kuimarisha muungana wandugu; hayo mnayoyaota ni kujichimbia kaburi wenyewe.
 
angalia bango wakati wa marejeo ya katiba mpya
mwada-wachanwa-430x320.jpg
 
Waleed Waleed,

Mkuu.
Nimesoma michango mingi hapa imejigawa katika makundi mawili.
Yale yanayokatisha tamaa na yenye kuwatisha Wanaotaka uhuru wao.
Na yale yanayosema kuwa matatizo ya wanaodai kujitawala kwa uhuru wanabanwa, wanagawiwa makundi.

Mkuu. Mimi sioni kwa nini tuwakatishe tamaa watu ambao wanaona muungano kuwa ni kero. mwanzoni wametaka Muungano uwe wa haki na usawa. Hilo hawalipati au hawaoni haki kutendeka sasa wanadai umoja ufikie ukomo.Utengano utawapa fursa ya kujiamulia vile watakavyo.

Lakini wale wote wanaotoa vitisho, au tahadhari za athari mbaya baada ya kuvunjika kwa muungano naona wanafanya zaidi siasa chafu. Kama siasa za CCM na viongozi wa CCM. CCM wao husema vyama vya upinzani vitaleta fujo, vitaipoteza amani na utulivu wa nchi. Pia kujisifia kuwa TZ imepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo chini ya uongozi wa CCM......kama wewe ni mmoja wa unaeamini kauli hizi za CCM basi naweza kukubaliana na wewe na mtazamo wako wa kuwa unapovunja muungano basi matokeao yake ni njaa, umasikini, kutokuwa na ajira, ubaguzi, na uduni wa maisha.
Lakini hata kama itakuwa hivyo,itakuwa kuna tofauti gani na maisha ya mwananchi wa TZ kwa sasa? Au haya hayapo leo?

Jana nilitoa mchango wangu na nilisema huu Muungano unaonekana una faida sana kwa watu wachache na hasa kwa viongozi wa serikali ya Muungano.
Kuna member alisema tunawabeba sana Zanzibar kwa kuwapa 4.5 % ya misaada inayokuja kwa jina la TZ na hasa ukilinganisha na idadi ya watu wake. pia alisema vipi Muungano,serikali ya TZ inakuwa wadhamini kwa mikopo ambayo Zanzibar wanachukua,,,je wakikataa kulipa,au wakishindwa kulipa nani atalipa deni lao?

Nilipochangia nilisema kwa bahati mbaya tunautizama muungano katika mtazamo potofu. Muungano moja ya matarajio yake ni kuleta hali bora, tija, faida, mshikamano,mapenzi na udugu. Sasa kama huu wa kwetu hauleti haya una maana gani? je kuna ulazima wa kuwepo?

Tuutizame muungano huu kama biashara ya benki. unapoweka akiba benki na benki ikakupa riba ya 4.5%. Je benki huwa inapata asilimia ngapi kabla ya kukumegea hii 4.5%? Je kuna anayetaka kuendelea na biashara yenye kumtia hasara?
Mbona tulipoona EAC ya mwanzo haina tija kwetu, tulijitoa/tuliivunja?

Ni wazi kuwa huu Muungano kwa vile tunaung'anga'ania una faida na wanaojua faida hiyo hawataki kutupa ukweli.

Kwenye bishara kuna mapato na matumizi. Nani kati yetu anajua mapato na matumizi ya Muungano? Naweza kusema hakuna hata mmoja kati yetu. Bila ya kujua kimahesabu, nini kinaingia kutokana na shughuli za muungano na nini kinatumika basi tutabaki katika ushabiki zaidi kuliko uhalisi wa mambo.

Kwa nini kila kitu ni siri za serikali hapa TZ?......nafikiri moja ya sababu ni kuficha ukweli.na kuwaacha wananchi wajenge hoja butu na kujenga chuki.

Lakini siku tutakapotengana kila mtu atabeba msalaba wake. Anaetoa 4.5% hatatoa hiyo 4.5% na atabaki na 100% na yule ambaye hana leo akipata atapata 100% na sio 4.5%. Hii ni win-win situation.
Hatutahitaji kutoa udhamini.Kila nchi itajidhamini kivyake....hii pia ni win-win situation.

Lakini la faida zaidi ni kwa wananchi kujua wanakabiliana na nani..nani wa kumuuliza masuali na nani atoe majibu. Wananchi tulio "Tanzania bara" aka Tanganyika tunalalamika kuwa hatuna vyombo vya Tanganyika na kwa hiyo viongozi wanaoendesha shughuli za Tanganyika wamejificha ndani ya muungano huku wakitugawia umaskini, hasira zetu tunazielekeza kwa wazanzibari.

Wananchi wa Zanzibar wanapotaka majibu kutoka kwa viongozi wao,wao wanapata jibu kuwa muungano unaibana serikali ya Zanzibar. Wananchi wanabaki kuuchukia muungano lakini viongozi wao pia wanajificha nyuma ya Muungano kama sababu ya Uduni wa huduma na ustawi mbovu wa jamii.
Muungano ukivunjika hii sababu haitakuwepo tena kwa viongozi wote, watanzania bara na wazanzibar.

Katika hoja ya biashara na uchumi wa nchi ndogo. Jisomee hapa unaweza kuona huu wingi wa watu au udogo wa sehemu si tatizo. Tatizo lipo kwenye how you manage the business!
Huu muungano wetu na muundo wake una utata mkubwa na ni moja ya sababu kuwa hatupigi hatua za maendeleo vile inavyopasa. Na kama hatuchukui hatua kusawazisha kasoro zilizopo ni kuwa tunakaribisha maafa siku za usoni. Tumeona wazanzibari walivyokosa imani na muungano kupitia tume ya Sitta wakati wa kukusanya maoni juu ya muswada wa "katiba mpya".

Muungano ukivunjika tutapata Tanganyika yetu na taaasisi zake.

The Mauritius economic miracle - Opinion - Al Jazeera English

BBC News - Mauritius country profile

Mauritius Economy
 
Makaimati
Haya! Mtoto akililia wembe na apewe ila wakumbuke kuwa azma ikitimia wale wapemba na wamakunduchi walio bara lazima na wafungashe virago warejee kwao wakabanane hukohuko watuachie ardhi yetu.
 
Waleed Waleed,

Mimi nawashangaa kushupalia ya Zanzibar wakati mna issues zenu kibao hamjazipatia solutions.

Wazanzibari mkiwafukuza, watarudi kwao na watapokewa. Sisi hatuwafukuzi maana wataendelea kutulimia mashamba yetu maana kweli ardhi yetu ni ndogo hayafiki matrekata.
 
Punda haelemewi na mizigo yake.

Leave Zanzibar to Zanzibaris please
 
Juu ya mstari Nonda, haya ya Wazanzibari watafukuzwa, watakosa nyama na upuuzi kama huo si ajenda yetu kwa sasa.

Zanzibar for Zanzibaris
 
Chifunanga unauliza jibu?

At least sio hivi ulivyo maana huu si Muungano bali uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar
 
Nonda,

..yale masuala 11 original ya muungano yanaibana Zanzibar kuliko hayo mengine yaliyoongezwa.

..yale ya mwanzo ndiyo msingi unaopelekea kuwepo kwa hayo ya nyongeza.

..ndiyo maana mara zote nawasihi wa-Zanzibar wajiondoshe tu kwenye muungano. Tanganyika tutajipanga baada ya wao kuondoka.

..Zanzibar tayari wana serikali yao. hakuna sababu ya kusubiri ruhusa toka kwa wa-Tanganyika.

..hata Tanzania tulipojitoa kwenye EAC mwaka 1977 hatukusubiri ruhusa toka kwa Wakenya au Waganda.

NB:

..utaratibu wa serikali ya muungano kuidhamini Zanzibar ktk kuchukua mikopo ndiyo unawapa kiburi SMZ kukataa kulipa madeni yao kwa taasisi za Tanganyika kama Tanesco.
 
JokaKuu,

Kama Muungano huu ungekuwa kama wa EAC iliokuwepo au iliopo, Wazanzibari wasingetaka kujitoa kwenye huu "Muungano" mnaoung'angania.

Kujiondoa tutajindoa wala usiwe na shaka mjomba wala usipate presha.

Kuhusu deni la TANESCO ni suala la makubaliano na sio kiburi. Hivyo huko kwenu baba mwenye nyumba anaweza tu kupandisha kodi bila ya utaratibu? TANESCO haiwezi tu kuipandishia bei tu kiholela.

Zanzibar haitolipa hilo deni, what can you do about it?

Kuvunja Muungano?

Nawashangaa sana.
 
Ndoa ya muungano ivunjwe tu maana Wazanzibari wanaona kama Bara inanufaika sana na ndoa hii wakati katika hali halisi wao ndio wanaonufaika.
 
Ndg zangu huo ndiyo ukweli na mimi siku zote nimekuwa nikitafakari sana maneno ya Hayati Mwl. Nyerere linapokuja suala la Muungano. Hivi sasa kuna vuguvugu la chini la wazanzibar kujitenga na Tanganyika. Lakini ikitokea muungano ukavunjika, huo ndiyo utakuwa mwisho wa Zanzibar. Lazima chokochoko zitaanza kati ya wapemba na waunguja. Sijui kama akina 'yakhe' wanatambua hilo.
Acha kuongea pumba...Zanzibar kama nchi ilidumu kwa miaka isiyopungua 800. Na hilo la Upemba na Uunguja limetokea Tanganyika. Zanzibar ilikua nchi kabla ya Tanganyika . Mwaka 1800s tayari Marekani walikua na ubalozi Zanzibar. Mimi naona hofu ya watanganyika ni Maendeleo ya Zanzibar. Wanahofia kuachwa nyuma kimaendeleo. Time will tell, as new generations demand change.
 
Tuvunje na hakuna wakubeba lawama waache wanzanzibari wakajifikirie tutarudi hakuna haja ya kuogopa .
Mbona eac ilivunjika na inarudi taratibu

Zanzibar haitokataa kuungana kwa misingi ya kuheshimiana.

Huu si Muungano jamani, ni nchi moja kubwa kukalia nchi nyengine ndogo.
 
Nikionacho ni kutokuwezekana kuvunjika kwa Muungano ,kwani CCM wataulinda kwa bei yeyote ile. Yaani matatizo na hizi ziitwazo kero za Muungano ni danadana wanazopigwa WaTanzania wote kwa ujumla.

Hebu nipe jibu ikiwa Muungano utavunjika leo ,unafikiria ni nini kitatokea ,tuchukulie Zanzibar itatulia na kwa vile wao lao ni moja (CCM ,CUF na vyama vinginevyo) kwamba Muungano unamatatizo kama hayawezi kutatuliwa bora uvunjike (Sawa umevunjika) ,Upande huu wa Tanganyika ,je kutakuwa shwari ? Naomba jibu.

Ninaposema hasara kwa CCM ni kwamba mara Muungano utakapovunjika ,serikali iliyopo madarakani itapoteza uhalali wake au sivyo ? Wabunge wote watapoteza uhalali wao kwani Bunge la Muungano litakuwa nalo halina uhalali kwani muungano haupo tena.

Serikali yote inaundwa na CCM wabunge wengi wanatoka CCM ,Muungano ukivunjika CCM wanapoteza kila kitu au sivyo,je tunaweza kukubali kuwa wabunge wa Muungano wawe ndio wabunge wa Tanganyika ?? Sidhani kama vyama vyengine watalikubali hilo ? Je Lipi likubalike ?
CCM haitokubali kula hasara ,kwani kurudi kwa Tanganyika na kufa kwa Muungano ,itabidi kuitishwe uchaguzi upya wa Tanganyika na ndio utakuwa mwisho wa mafisadi.Na Chama kipya kitaitawala Tanganyika.
 
Mkuu Mwiba i do conqur with you...huu ni ukweli kabisa na naamini ni mfupa mwingine kwa JK

Niliwahi kuandika kwenye post moja hapa na bado naamini niko sahihi kuwa hali inavyoendelea katika mjadala wa katiba ni wazi kabisa ndugu zetu wazanzibar wangependa kuwa na "sovereign state" itakayojitegema........

Kikwazo cha kwanza kwa wazanzibar itakuwa ni CCM ambayo haitakubali kupoteza hodhi ya serikali ya Mapinduzi (kama walivyokubali kishingo upande kete ya kushiriki serikali ya umoja ili kuendlea kuwa na hodhi katika hali yoyote) na "busara" iatatumika japo kwa namna ninavyowafahamu wazanzibar sio kama sisi wa upande wa Tanganyika, wakinuia jambo wamenuia.......

Hapa pia wazanzibar wenyewe watakuwa kwenye paradox, should they give Muungano kwa expense ya CCM au kinyume chake?

Na hapa ndipo utagundua kuwa huu ni mfupa mwingine kwa Mzee wa Kuvua Mgamba...sasa hili sijui litakuwa ni hamba au ni fupa kabisa

Ninachoamini JK hataki kuyasikia haya na he cant afford yatokee mikononi mwake na ndio maana akaweka kipngele kwenye mapendekezo yake ya mabadiliko ya katiba inayotaka ku-sanctivy na kutokuugusa wala kuuzungumzia muungano kwenye makusanyo ya maoni wala mapenekezo yenyewe ya katiba
 
Back
Top Bottom