MFUKUZI
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 933
- 700
Ndugu, wanajamii hakuna ubishi kwamba nchi yetu inapitia katika kipindi kigumu sana. ukiachilia mbali matatizo ya kiuchumi na kijamii lakini tatizo la kisiasa ndilo limeonekana kuwa sugu kupita yote. Suala la Katiba mpya hakuna mtu asiyejua kwamba ni dai la watanzania kwa muda mrefu sana.
Serikali ya CCM chini ya Mwinyi kupitia Ripoti ya Jaji Nyalali na Ripoti ya Jaji Kisanga kipindi cha Mkapa suala la Katiba mpya na Muungano yalichambuliwa kwa kina na ushauri ukatolewa mzuri sana. Endapo kama kipindi hicho hawa viongozi wetu wangezingatia maoni na taarifa za Tume zile hakika naamini Tanzania ingekuwa kwenye ramani nyingine na sasa hivi tungekuwa bizzy kushindana na Botswana, Namibia na nchi nyingine kimaendeleo.
Sasa viongozi hawa walikaa kimya, wakafunika kombe mwanaharamu apite sasa hivi jipu linapasuka, wamekaa kimya as if wao si watanzania na hawajui kinachoendelea. Kwanini hawasaidii hata kutoa mawazo tu tutavukaje kwenye matatizo haya? Au ndo tuseme nafsi zao zinawasuta? Mbona Nyerere aliweza kuikosoa Serikali ya kipindi kile na mambo yaliweza kunyoka na kuvuka salama? Kwanini Mwinyi na Mkapa wanakaa kimya?
Mimi nasema endapo Muungano utavunjika wa kwanza kulaumiwa ni Mwinyi na Mkapa. Mimi sioni ustaafu wao unalisaidiaje taifa, maana imebaki kuhudhuria maazimisho ya sikukuu za kitaifa tu. Tena Mwinyi ndo angekuwa wakwanza maana yeye anaushawishi mkubwa Zanzibar na Bara.
Mwinyi na Mkapa nawaombeni sana, hebu jitokezeni mlisaidie taifa ili tuvuke salama katika jambo hili.
PLEASE FANYENI KAMA NYERERE ALIVYOFANYA KIPINDI KILE CHA TANZANIA KUINGIA KWENYE VYAMA VINGI NA UCHAGUZI WA KWANZA WA VYAMA VINGI