Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Ndugu, wanajamii hakuna ubishi kwamba nchi yetu inapitia katika kipindi kigumu sana. ukiachilia mbali matatizo ya kiuchumi na kijamii lakini tatizo la kisiasa ndilo limeonekana kuwa sugu kupita yote. Suala la Katiba mpya hakuna mtu asiyejua kwamba ni dai la watanzania kwa muda mrefu sana.

Serikali ya CCM chini ya Mwinyi kupitia Ripoti ya Jaji Nyalali na Ripoti ya Jaji Kisanga kipindi cha Mkapa suala la Katiba mpya na Muungano yalichambuliwa kwa kina na ushauri ukatolewa mzuri sana. Endapo kama kipindi hicho hawa viongozi wetu wangezingatia maoni na taarifa za Tume zile hakika naamini Tanzania ingekuwa kwenye ramani nyingine na sasa hivi tungekuwa bizzy kushindana na Botswana, Namibia na nchi nyingine kimaendeleo.

Sasa viongozi hawa walikaa kimya, wakafunika kombe mwanaharamu apite sasa hivi jipu linapasuka, wamekaa kimya as if wao si watanzania na hawajui kinachoendelea. Kwanini hawasaidii hata kutoa mawazo tu tutavukaje kwenye matatizo haya? Au ndo tuseme nafsi zao zinawasuta? Mbona Nyerere aliweza kuikosoa Serikali ya kipindi kile na mambo yaliweza kunyoka na kuvuka salama? Kwanini Mwinyi na Mkapa wanakaa kimya?

Mimi nasema endapo Muungano utavunjika wa kwanza kulaumiwa ni Mwinyi na Mkapa. Mimi sioni ustaafu wao unalisaidiaje taifa, maana imebaki kuhudhuria maazimisho ya sikukuu za kitaifa tu. Tena Mwinyi ndo angekuwa wakwanza maana yeye anaushawishi mkubwa Zanzibar na Bara.

Mwinyi na Mkapa nawaombeni sana, hebu jitokezeni mlisaidie taifa ili tuvuke salama katika jambo hili.



PLEASE FANYENI KAMA NYERERE ALIVYOFANYA KIPINDI KILE CHA TANZANIA KUINGIA KWENYE VYAMA VINGI NA UCHAGUZI WA KWANZA WA VYAMA VINGI
 
Wadau naomba mnielimishe umuhimu wa muungano wetu wa tanganyika ma zanzibar, me ni mtanganyika niliye zaliwa baada ya muungano na toka nipate akili timamu ya kujua mbivu na mbichi daima nawasikia wa znz wakiulalamikia muungano huu na inavyo onekana ni sisi wa tanganyika ndio tuna ung'ang'ania

1. Wao wanaserikali yao na hivi karibuni walijitangazia utaifa wao - tumekaa kimya

2. Ishu za znz ni waznz tu ndio wanashiriki ila za bara wa znz wote wanashiriki mfanon bungeni

3. Juzi walichana muswada hakuna aliyezungumza kusikitikia kitendo kile

4. Wanshika mabango ya kuwataka wabunge wao waje kushirikiana nao kudai talaka

5. Kwa idadi ya watu ni wachache sana but wana jeuri kubwa ya kutubwatukia na wote tuka kakaa kimya
 
Nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakiongea mabaya kuhusu Muungano. Bahati mbaya au nzuri watu wengi hawaoni umuhimu wa muungano. Binafsi ninajiuliza, ikiwa muungano utavunjika; watu wa unguja na wapemba walioko bara na wale waTanganyika walioko Zanzibar, watapendelea kwenda upande upi wa uliokuwa muungano? Sipati picha...
Kumbuka wataalamu wa hali ya hewa wanasema kuna siku visiwa vya Unguja na Pemba vitazama, kutokana na kuongezeka kina cha maji ya bahari.
 
Sisi busara mtu alete hoja za kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
 
Muungano wa nini bana acha uvunjike.Kama muungano ungetusaidia kuinua hali yetu ndo tuulilie,lakini umeonekana ni kero,wacha wajitenge tubaki na tanganyika yetu ndo itakua fresh kubanana na hawa mafisadi.
 
Tuvunje na hakuna wakubeba lawama waache Wanzanzibari wakajifikirie tutarudi hakuna haja ya kuogopa .
Mbona EAC ilivunjika na inarudi taratibu
 
uvunjike tu .picha ninayoipata ni kwamba wale ambao wanaasili yapande fulani watapata shida kwa muda na katranslation kakiaina ila tutafika tu tena salama halafu tutarudiana tena tukiona impact yake.
 
Tupo watu milioni 1 tunalia njaa je tukiungana na watu milioni 43 si ni kujimaliza. Zanzibar hatutaki muungano.
 
Mmeshaona maji ya shingo ndo mnatafuta kafara sasa.......

Hili fuko mmekubali kulibeba wenyewe wakati uwezo hamna, ngoja liwapasukie kinyesi kiwanukie.....nani kimemfia mkononi....!!!
 
MFUKUZI,
Juu ya kweli uliosema lakini unasahau kuwa kulikuwa na Muhusika mkubwa zaidi yule alizuia juhudi za G55 ambazo zilikwishakubaliwa na hata hao kina Mwinyi na Mkapa! Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!
 
Sasa si wakati wa kutafuta mchawi, haitasaidia kitu. Ikiwa Watanganyika hawataki Muungano na ikiwa Wazanzibari hawataki Muungano, maana yake ni kuwa Muungano hautakiwi. Tuuvunje tugawane mbao kila mtu kivyake. Ikiwa baadaye kutakuwa na haja ya kuunga tena, tutaanza kwa "New terms of condition". Tusisahau falsafa ya mshona koti, kwanza lazima akikate kitambaa ndio itoke suti nzuri.
 
Ninapata shida kidogo kama si sana kila ninapofikiri na kuulizwa kuhusu Muungano, kwa nini watawala wabara wanaung'angania ilhali wazanzibari hawautaki?

-Zanzibar ni mtoto aliyedekezwa, tumembeba mgongoni halafu anatupiga makwenzi na kututemea mate akisema Yakhe nishusheee!, mbona wanibeba vibaya weye? kwa mfano mzanzibar (Mr Msoma) aliwahi kuwa katibu mkuu wizara ya mawasiliano na uchukuzi, alipotoka kuwa principal wa Dar Tech, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, ambayo seriously in deal sana na issue za bara kwa sehemu kubwa amepewa mzanzibar vuai nahodha, kamishna wa Magereza anasimamia pia magereza zanzibar? vipi kuhusu Polisi na Uhamiaji? Na kuna wabara wangapi katika nafasi za uongozi visiwani? Wafanya biashara wangapi wazanzibari wako bara na wabara wangapi wako visiwani? Muungano ni kwa faida ya nani kiuchumi na kijamii?

-Jamani Hii kitu inatia hasira na zaidi sana ni kuwa hawaoni tumejitoa kiasi gani kulinda Tanzania at their own benefit. Kwa mfano katika bunge la ECOWAS. Idadi ya wabunge wa ECOWAS ni kwa population ya raia wa nchi. Ndio Maana Nigeria inao wabunge 35 out of about 140 wa nchi zote 15. Haiwezekani rais Mwenye kura sawa na Mbunge wa Ubungo-Mnyika au Mahanga wa Segerea adai haki sawa, pia hata ujumbe katika vyama vya siasa.

-as the fact is ...muungano wetu ilikuwa ni cold war product, mkakati wa mmarekani na mwingereza. Wao waliona tishio la Zanzibar kuwa ya kikomunisti lakini pia kuhofia masheikh wakali. Walipendekeza ichukuliwe na Kenya lakini Kenyatta ...na wenzake wakahofia kuwaunganisha waswahili wa pwani (Mombasa, Malindi , Lamu) na wale wa Zanzibar ingekuwa tishio kwa mshikamano wao wa kikabila. Basi ikabidi wampe Julius japokuwa mjamaa lakini ni afadhali kuliko Cuba ambao waliweka mizizi yao Zenj enzi hizo. Wanaojua che Guevarra mwenyewe alifika Zenj kutoa mafunzo!

Je kuuvunja muungano ni hasara kuliko kuurekebisha? na ni kwa nini watawala (hasa wa bara) wanasita kuurekebisha au kuuvunja?
 
Wakati wa muungano ilikuwa still watu wapende hizi wananingiliana kwa visa,na passport mkononi,lakini kuna mpumbavu mmoja mbunge wa uzi nafikiri yule aloanguka juzi katika bunge ndio alotuondelea control border ,,na hii ndio tatizo moja limetuathiri hapa zanzbar tumeingiliwa hadi wamalawi,na wakongo,wanaishi kinyume na sheria na wamepewa card za ccm ili wa support chama,pia tuna ogopa kupoteaza utaifa wetu wazanzbari kutokana,sisi tuko wachache iweje tuungane na watu milioni 43,wakati sie milioni 1 tu,

Ndi maana tunalilia tuvunje muungano,mzanzibari amekuwa hana haki katika nchi yake,hapewi nafasi ya kupiga kura,wala kazi,wageni ndio wanaopewa kazi,,ubaguzi mtupu,,tumechokaView attachment 27159
 
watu watapewa uhuru wa kuchagua wanapenda kuwa wapi. walio bara wanaweza baki bara na wa VC1 watabaki VC1
 
<br />
<br />
Hivi umoja gani unao ujua wewe ukawa na nguvu hapa nchini?huwahurumii ndugu zako wanao geuzwa mashoga huko visiwani?yakheeeeee wee vipi!
Mnayaona haya ya uzawa wa sasa? Halafu muwalazimishe kwa jambo wasililolipenda!
 
Inategemea na sheria za nchi,ikiwa baba ni mzenji basi unahaki ya kuenda kwa baba,kama mama mzenji mama yako anaweza kukuombea ukawa ni mzanzibari,lakini tutaweka sheria ambazo hazitoleta athari kwa wale waliochanganya damu mbili ya visiwani na bara,ila kuna haki utazikosa ikiwa sio mzaliwa hasa hapa zanzbar,kama kugombea urais,

Lakini nitawaambia kitu kimoja,udugu utakuwepo pale pale,utengano ni nchi tu,tufahamu hilo,mie muungano ukivunjika nakuja bara kuna mtoto mmoja nimeshaposa singida wa kiarabu nasubiri amalize shule tu nije kuowa.
Wewe ni mmoja wapo wa walio laumu sana waTanganyika katika huu muungano.
Sasa mnaipata picha kuwa to hell with muungano, undugu ni mtu yule mnayepatana , wazanzibari warudi kwao na waTanganyika warudi kwao vile vile.
Unchosema na bibi wa Singida ni double standards kwa vile kuna waarabu vile vile kwenu, kaoe kwenu.
Muda si muda hapa Tanganyika itakuwa kama Uganda au Kenya kwenu mje huku kwa visa au immigration control.
 
Inategemea na sheria za nchi,ikiwa baba ni mzenji basi unahaki ya kuenda kwa baba,kama mama mzenji mama yako anaweza kukuombea ukawa ni mzanzibari,lakini tutaweka sheria ambazo hazitoleta athari kwa wale waliochanganya damu mbili ya visiwani na bara,ila kuna haki utazikosa ikiwa sio mzaliwa hasa hapa zanzbar,kama kugombea urais,

Lakini nitawaambia kitu kimoja,udugu utakuwepo pale pale,utengano ni nchi tu,tufahamu hilo,mie muungano ukivunjika nakuja bara kuna mtoto mmoja nimeshaposa singida wa kiarabu nasubiri amalize shule tu nije kuowa.

tutawafukuza wapemba wanaofanya biashara za rejareja, kama alivyopania Nyarandu kwa wa china , hapo Namanga patakuwa kwetu watanganyika
 
Back
Top Bottom