Waleed Waleed,
Mkuu.
Nimesoma michango mingi hapa imejigawa katika makundi mawili.
Yale yanayokatisha tamaa na yenye kuwatisha Wanaotaka uhuru wao.
Na yale yanayosema kuwa matatizo ya wanaodai kujitawala kwa uhuru wanabanwa, wanagawiwa makundi.
Mkuu. Mimi sioni kwa nini tuwakatishe tamaa watu ambao wanaona muungano kuwa ni kero. mwanzoni wametaka Muungano uwe wa haki na usawa. Hilo hawalipati au hawaoni haki kutendeka sasa wanadai umoja ufikie ukomo.Utengano utawapa fursa ya kujiamulia vile watakavyo.
Lakini wale wote wanaotoa vitisho, au tahadhari za athari mbaya baada ya kuvunjika kwa muungano naona wanafanya zaidi siasa chafu. Kama siasa za CCM na viongozi wa CCM. CCM wao husema vyama vya upinzani vitaleta fujo, vitaipoteza amani na utulivu wa nchi. Pia kujisifia kuwa TZ imepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo chini ya uongozi wa CCM......kama wewe ni mmoja wa unaeamini kauli hizi za CCM basi naweza kukubaliana na wewe na mtazamo wako wa kuwa unapovunja muungano basi matokeao yake ni njaa, umasikini, kutokuwa na ajira, ubaguzi, na uduni wa maisha.
Lakini hata kama itakuwa hivyo,itakuwa kuna tofauti gani na maisha ya mwananchi wa TZ kwa sasa? Au haya hayapo leo?
Jana nilitoa mchango wangu na nilisema huu Muungano unaonekana una faida sana kwa watu wachache na hasa kwa viongozi wa serikali ya Muungano.
Kuna member alisema tunawabeba sana Zanzibar kwa kuwapa 4.5 % ya misaada inayokuja kwa jina la TZ na hasa ukilinganisha na idadi ya watu wake. pia alisema vipi Muungano,serikali ya TZ inakuwa wadhamini kwa mikopo ambayo Zanzibar wanachukua,,,je wakikataa kulipa,au wakishindwa kulipa nani atalipa deni lao?
Nilipochangia nilisema kwa bahati mbaya tunautizama muungano katika mtazamo potofu. Muungano moja ya matarajio yake ni kuleta hali bora, tija, faida, mshikamano,mapenzi na udugu. Sasa kama huu wa kwetu hauleti haya una maana gani? je kuna ulazima wa kuwepo?
Tuutizame muungano huu kama biashara ya benki. unapoweka akiba benki na benki ikakupa riba ya 4.5%. Je benki huwa inapata asilimia ngapi kabla ya kukumegea hii 4.5%? Je kuna anayetaka kuendelea na biashara yenye kumtia hasara?
Mbona tulipoona EAC ya mwanzo haina tija kwetu, tulijitoa/tuliivunja?
Ni wazi kuwa huu Muungano kwa vile tunaung'anga'ania una faida na wanaojua faida hiyo hawataki kutupa ukweli.
Kwenye bishara kuna mapato na matumizi. Nani kati yetu anajua mapato na matumizi ya Muungano? Naweza kusema hakuna hata mmoja kati yetu. Bila ya kujua kimahesabu, nini kinaingia kutokana na shughuli za muungano na nini kinatumika basi tutabaki katika ushabiki zaidi kuliko uhalisi wa mambo.
Kwa nini kila kitu ni siri za serikali hapa TZ?......nafikiri moja ya sababu ni kuficha ukweli.na kuwaacha wananchi wajenge hoja butu na kujenga chuki.
Lakini siku tutakapotengana kila mtu atabeba msalaba wake. Anaetoa 4.5% hatatoa hiyo 4.5% na atabaki na 100% na yule ambaye hana leo akipata atapata 100% na sio 4.5%. Hii ni win-win situation.
Hatutahitaji kutoa udhamini.Kila nchi itajidhamini kivyake....hii pia ni win-win situation.
Lakini la faida zaidi ni kwa wananchi kujua wanakabiliana na nani..nani wa kumuuliza masuali na nani atoe majibu. Wananchi tulio "Tanzania bara" aka Tanganyika tunalalamika kuwa hatuna vyombo vya Tanganyika na kwa hiyo viongozi wanaoendesha shughuli za Tanganyika wamejificha ndani ya muungano huku wakitugawia umaskini, hasira zetu tunazielekeza kwa wazanzibari.
Wananchi wa Zanzibar wanapotaka majibu kutoka kwa viongozi wao,wao wanapata jibu kuwa muungano unaibana serikali ya Zanzibar. Wananchi wanabaki kuuchukia muungano lakini viongozi wao pia wanajificha nyuma ya Muungano kama sababu ya Uduni wa huduma na ustawi mbovu wa jamii.
Muungano ukivunjika hii sababu haitakuwepo tena kwa viongozi wote, watanzania bara na wazanzibar.
Katika hoja ya biashara na uchumi wa nchi ndogo. Jisomee hapa unaweza kuona huu wingi wa watu au udogo wa sehemu si tatizo. Tatizo lipo kwenye how you
manage the business!
Huu muungano wetu na muundo wake una utata mkubwa na ni moja ya sababu kuwa hatupigi hatua za maendeleo vile inavyopasa. Na kama hatuchukui hatua kusawazisha kasoro zilizopo ni kuwa tunakaribisha maafa siku za usoni. Tumeona wazanzibari walivyokosa imani na muungano kupitia tume ya Sitta wakati wa kukusanya maoni juu ya muswada wa "katiba mpya".
Muungano ukivunjika tutapata Tanganyika yetu na taaasisi zake.
The Mauritius economic miracle - Opinion - Al Jazeera English
BBC News - Mauritius country profile
Mauritius Economy