Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Assume muda ndio huu alafu Muungano unavunjika! Sipati picha Wapemba na Waunguja waliopo Mwanza, Dodoma, Kigamboni, Temeke, Ilala, Kinondoni na sehemu nyingine wanavyotolewa mbio kurudishwa na maboti, mitumbwi na majahazi na Jiwe!

Acha kuwaza upuuzi mkuu.
Wahindi, wakenya wasomali, nk wamejaa kote Tz, kwani mataifa yao yana muungano na Tanganyika??
 
Wahindi na wakenya wamejaa kote Tz, kwani mataifa ya india na kenya yana muungano na Tanganyika??
Kwa hiyo mnategemea kuvunja Muungano alafu muendelee kufaidika na kuishi Bara! Kisha Zanzibar iwe ya kwenu peke yenu? That is selfishness. Btw hiyo itakuwa case nyingine, itabidi mrudi kwanza ili taratibu zengine za kidiplomasia zifuatwe. Na ninavyojua Jiwe (Kama itatokea hii kesi akiwa madarakani) hatorudi mtu. Itakuwa ni ubabe tu.
 
Wazanzibar bila kuchoka wala kukata tamaa wataendelea kuupinga muungano huu hadi pale watakapopata uhuru wao
Uhuru upi tena?Mbona walishapata uhuru kitambo mwanzoni ilikuwa december 1963 toka waingereza ambao ulikuwa uhuru kwa wachache (sultan) na baadae january 1964 ambapo wazalendo walifanya mapinduzi dhidi ya Sultan na serikali ya wachache ya Shamte.
Wazanzibar wako wazi wanasema hawataki tena kutawaliwa na Tanganyika.
Mbona muungano wa 1964 ulikuwa wa nchi mbili kwa makubaliano vipi tena useme wanatawaliwa? Yaan nchi ina Rais, baraza la wawakilishi, wabunge kwenye bunge la muungano,mawaziri,bendera bado useme wanatawaliwa? Labda mniambie maana ya kutawaliwa ni nini?
 
Sultan Jamshid ni Mzanzibar. Dola ya Zanzibar ilijitenga na Oman mwaka 1861 na ndo maana baada ya kupinduliwa hakukimbilia Oman bali Uingereza. Kuna kipindi Rais Salmin Amour alisema anaweza kurudi Zanzibar aishi kama raia.
Umejibu vyema mkuu. Lakini kumbuka vilevile kuwa baada ya dola ya Zanzibar kujitenga na Oman mwaka 1861 ilihama na kuwa chini ya dola ya Uingereza. Bado narudia swali langu la awali. Ni lini Zanzibar ilisimama yenyewe kama dola huru bila kuingiliwa na dola nyingine toka nje?
 
Proved,
Bado hawajapata uhuru wa kweli. Muda wa ukoloni ulishapita. Waacheni wenzenu wapate uhuru, wapumue
 
Bado hawajapata uhuru wa kweli. Muda wa ukoloni ulishapita. Waacheni wenzenu wapate uhuru, wapumue
Uhuru gani tena wewe? Mbona Mzanzibari Mwinyi alikuwa Rais wa pili wa muungano? Wasingekuwa huru wangetupatia raisi wa pili wa JMT? Bado Mawaziri wa muungano, baadhi ya mabalozi wa JMT ni wazanzibar huko kusema wanatawaliwa ni siasa mufilisi za wanaotafuta madaraka kwa kila njia hata kuwagawa raia..
 
Uingereza wanajiondoa Umoja wa Ulaya... Jimbo la Catalunya linajiandaa kujitenga na Spain.Mkoa wa Kiingereza wa Bamenda unajiandaa kujitenga na Cameroon! Wazanzibari wenzangu, huu ndio muda sasa wa kuuvunja huu muungano!!!
Wazanzibar wa CCM wakifika Dodoma wanaufyata alisema Jussa
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Ni miaka 55 imetimia tangu jahazi lililowabeba Watanganyika na Wazanzibar liweke historia ya kung’oa nanga mara baada ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kuzaliwa rasmi mnamo April 26,1964. Hii ilitokana na ujasiri, ushupavu na nia ya dhati waliyokuwa nayo waasisi wa Muungano huu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika) na Abeid Aman Karume (Zanzibar).

Hatua hiyo ilifikiwa kutokana na mtiririko wa kimazingira na mahusiano ambayo yalishabihiana kama sio kufanana kabisa kwa pande zote mbili (Tanganyika na Zanzibar). Zipo sababu za kijiografia, kisayansi, kitamaduni na kihistoria zilizochangia huu muungano wetu.

Kutokana na sababu za kijiografia na kisayansi inaaminika kabisa kwamba Visiwa vya Zanzibar (Pemba na Unguja) vilikuwa vimeungana na hata kushikamana kwa pamoja pembezoni mwa pwani ya ardhi ya Tanganyika. Hivyo tangu awali tulikuwa ni kitu kimoja, tulio katika ardhi moja na ya pamoja.

Pia kuna historia (isiyo na shaka) ya muingiliano wa kiutamaduni baina ya Wakazi wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hali nzima ya kuoa ama kuolewa ilizidi kushamiri baina yao.

Halikadhalika harakati za kudai ukombozi wa uhuru wetu ili tuweze kujitawala wenyewe kutoka kwa dudu la wakoloni nazo zilichangia kutuunganisha. Inaaminika (na ndiyo ilivyo) ya kuwa asilimia kubwa ya Wazanzibar walishiriki kwenye harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Mwingereza ambapo kutokana na nia, ushupavu na nguvu ya pamoja walifanikiwa kupata Uhuru wa Tanganyika mnamo Desemba 9, 1961.

Lakini pia licha ya asilimia kubwa ya Wazanzibar kushiriki katika mchakato wa Mapinduzi ya Zanzibar lakini pia kulikuwepo na asilimia kubwa ya mchango wa ushiriki kutoka kwa Watanganyika. Hatimaye matunda yake yalionekana ya mapinduzi matukufu yaliyofikia kilele katika uwanja wa Gombani Pemba yaliyofanyika Jamhuri 12, 1964, baada ya kuchoshwa na hila na ghiliba za Waarabu uliotamalaki visiwani humo kwa zaidi ya karne mbili na hatimaye waliwaacha wazalendo watwana katika ardhi yao.

Pia tusisahau lengo na nia ya dhati aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere ya kutaka kuiunganisha Afrika mzima kwa hatua lakini jitihada zake zilianza kuzaa matunda ambayo hayatakaa yatokee tena Afrika kwa kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar.

Mnamo April 22, 1964, Maraisi wa nchi hizi mbili ambazo sasa zinaunda Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (wa Jamhuri ya Tanganyika) na Abeid Amani Karume (wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar ) walitia sahihi Mkataba wa kimataifa wa kuunganisha nchi zao, unaojulikana kama “Hati ya Muungano” (Articles of union) na hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ama United Republic of Tanganyika and Zanzibar (URTZ) ambao ni muungano sahihi kabisa kisheria na unaotambulika Kikatiba.

Siku ya Jumatatu ya tarehe 26 Aprili, 1964 viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee kwa nia ama lengo moja tu la kubadilishana “Hati za Muungano”.

Wananchi wa Tanzania walipiga kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa kwanza kabisa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 1965.

Kama nilivyodokeza kwamba Muungano wa Tanzania ulifikiwa kwa kutiwa sahihi mkataba unaoitwa Hati ya Muungano (Articles of the Union) na wakuu wa nchi hizi mbili, Mwalimu Nyerere (Tanganyika) na Abeid Karume (Zanzibar) Aprili 22,1964 na kuridhiwa na mabunge ya nchi hizo Aprili 25, 1964 na hatimaye kuwa sheria ya Muungano ya (Acts of Union) ya mwaka 1964.

Kimsingi sheria ya Muungano ndiyo iliyoanzisha na ndiyo iliyopewa haki ya chombo cha kikatiba kinachodhibiti katiba zote mbili za Serikali ya Muungano.

Mwanzoni kabisa Hati ya Muungano (Articles of Union) iliyomo ndani ya sheria ya Muungano iliorodhesha na hata kudadavua mambo 11 ya Muungano. Mambo hayo ni kama vile:- Mambo ya nchi za nje, Ulinzi na usalama (lakini si usalama wa Taifa); Polisi, Uraia, uhamiaji, mikopo na biashara za nchi za nje, utumishi katika serikali ya Muungano, kodi ya mapato, usimamizi wa fedha, Bandari, Usafiri wa anga, Posta na simu.

Kwa nia safi na malengo mazuri yanayojitokeza Hati ya Muungano imekuwa ikiboreshwa zaidi kwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele kwa malengo kusudi ya kuleta umoja, mshikamano, amani na utulivu wetu ule ule tulioanza nao awali na halikadhalika maridhiko yanayoendelea kuufanya Muungano huu uendelee kudumu hadi hii kesho.

Ndio maana mtu timamu hatoshangaa sana kuona Hati ya Muungano ikiendelea kuboreshwa kila siku (na itaendelea hivyo) ambapo ilianzia na mambo 11 ambapo hii leo yamefikia takribani 23.

Mengineyo ama baadhi ya yale yalioongezeka ni kama vile;- Noti; Elimu ya juu,; Maliasili na mafuta (mafuta) yasiyochujwa, bidhaa za mafuta na gesi asilia , ya mwaka 1968; Baraza la Mitihani ya Taifa; utafiti; utabiri wa hali ya hewa; Takwimu,; Mahakama ya Rufaa ya juu ya mwaka 1979; pamoja na uandikishwaji wa vyama vya kisiasa .

Tusisahau mwaka 1965 iliundwa katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The Interim Constitution of The United Republic of Tanzania) mpaka kufikia mwaka 1977 ndipo ilipoundwa katiba ya kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo inaendesha nchi hadi sasa.

Kukuru kakara za Wazanzibari zinatookana na madai yao ya kuwa Tanganyika(Bara) imeimeza Zanzibar (Visiwani) katika masuala mazima yahusuyo Muungano. Ikumbukwe Ubaguzi wa dhana ya Tanganyika umeimeza Zanzibar si ya kweli na hii imebainishwa katika katiba ya Muungano kuwa kuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Haya ni mapenzi ya dhati waliyoonyesha kwa Wazanzibari kwa kuwaruhusu wawe na serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ikumbukwe Serikali ya Muungano inaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaongozwa na Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar na chombo chao cha kutunga sheria kinaitwa Baraza la Wawakilishi.

Ndugu zangu hali ya kupuuzia na hata kuuchezea Muungano wetu ni hatari sana tena ni dhambi iliyotukuka. Mathalani Wazanzibari wakiamua kujiengua kwenye huu Muungano ili wawe kivyao vyao,hawatabaki salama. Mwalimu Nyerere alishawahi kusema ya kuwa “wakifika kwenye hatua hiyo watagundua kuwa ndani yao kuna Wazanzibari na Wazanzibara”. Nao wataamua kuwafukuza wale wa Wazanzibara, lakini hiyo haitakuwa mwisho. Punde si punde watajigundua kuwa nao (Wazanzibari) wamegawanyika kwani kuna Wapemba na Waunguja, na wakifikia hapo pia hawatakuwa salama ni lazima machafuko yatatokea.

Daima Wazanzibari watambue ya kuwa dhambi ya kutokutamalaki kwa dhana ya Unguja na Pemba unatoka na kufunikwa na kivuli cha mwamvuli cha Muungano. Hivyo umoja, mshikamano, amani na utulivu wao unategemea sana uwepo wa nguzo hii imara ya Muungano huu tulionao.

Vivyo hivyo kwa watu wa Bara (Tanganyika) ni rahisi kwao kutafunwa na dhambi ile ile ya ubaguzi watakayo ianzisha nje ya uwepo wa Muungano ni rahisi sana kwa ukabila, udini, ukanda na hata U-rangi kutamalaki ndani ya jamii wakishafikia hapo, hawatabaki salama kwani watachafuana tu.

Muungano huu tulionao unawafanya wale wageni, mataifa ya nje na watu wote wenye hila, donge, roho ya korosho kuogopa kutugusa na kutuvuruga kutokana na kuwepo kwa nguvu kubwa ya umoja, ushirikiano na mshikamano baina yetu.

Muungano huu wetu unatupatia fursa kubwa ya uhuru wa kusafiri kwa pande zote iwe ni bara ama ni visiwani. Leo hii ni rahisi sana kwa mtu wa bara kwenda Visiwani na hata wale wa Visiwani kuja Bara kwa uhuru zaidi kwani Uhuru huo wa uwepo wa nafasi hiyo umeshalipiwa na huu Muungano wetu tulionao.

Kutokana na uwepo wa uhuru wa kusafiri usio na mipaka baina yetu, pia Muungano wetu tulionao unazidi kutuongezea fursa na nafasi zaidi ya uwanja mpana wa ufanyaji biashara. Hali hii imesababisha uwepo wa mzunguko mkubwa wa pesa ndani yetu kwani si jambo la ajabu kuona pesa zikitoka Visiwani (Zanzibar) kuja Bara (Tanganyika) kupitia mabadilishano ya bidhaa kama vile nafaka, kahawa, matunda, vipuri vya magari na kadhalika.

Pia si jambo geni tena kwa sasa kuona pesa zikivuka Bahari na kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya ufanyaji ama ununuzi wa biashara kama vile Magari, nazi, Karafuu, Tende na kadhalika.

Muungano huu unatuzidishia fursa ya mianya ya uwanja mpana tena usio na kikomo wa ufanyaji biashara, Muungano huu hautubagui ama kutojulisha au kuwa na upendeleo wa upatikanaji wa Elimu bora, huduma za kijamii bora, Muungano hautugawi wala kuwa na upendeleo bali umejaa uwiano sahihi wa upatikanaji wa mabo yote ya msingi yaliyomo ndani ya “Hati ya Muungano” (Articles of union). Muungano huu ni nguzo imara katika muktadha mzima wa nyanja za kimaisha yetu.

Ni ukweli uliodhahiri kuwa haitakaa itokee Muungano kama huu (wa Tanganyika na Zanzibar) hapa Barani Afrika umoja ushirikiano, ushikamano, amani na utulivu ni sehemu mojawapo ya manufaa ya Muungano huu.

Njia mojawapo ya kuwaenzi vyema waasisi wetu ni kwa kuudumisha Muungano wetu ambao ni urithi wa aina yake waliotuachia. Watanzania yatupasa tuenzi Muungano wetu kwa kuulinda na kuudumisha kwa vitendo kwani ni nguzo na fahari ya kipekee na ya aina yake Barani Afrika.
 
Katika muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar kuna mambo mengi yenye matatizo ndani yake

Mambo ambayo ni kikwazo kikubwa sana kwa Zanzibar

Ukweli ni kwamba muungano huu una matatizo mengi na kero ni nyingi

Na kero zenyewe zinaweza kutatulika lakini watu wanaojiita viongozi hawataki kutatua kero hizo

Na hawataki kuzitatua kwa makusudi kwa sababu ya maslahi yao binafsi

Na utakuta yale mambo madogo madogo wao hawana haja nayo na wanataka yale mambo makubwa ili Zanzibar ibaki kua hivyo hivyo duni na izibitiwe isiinuke milele

Kwa mfano hapa nitataja baadhi ya mambo makubwa machache ambayo yameingizwa kwenye muungano ili kusudi Zanzibar ithibitiwe na sio kwa maendeleo

1. Mambo ya fedha na bank kuu muungano
2. Mambo ya elimu ya juu na vyuo vikuu muungano
3. Mambo ya ulinzi na usalama wa nchi muungano
4. Mambo ya bahari kuu muungano
5. Mambo ya kodi na ushuru muungano
6. Mambo ya usafirishaji safari za anga na safari za majini muungano nk.
7. Uhamiaji

Kwenye mambo ya elimu ya msingi hayo hawana haja nayo maana hayo hayaleti athari yoyote na mambo mengine ovyo ovyo hayo chukueni mtajuana wenyewe huko

Na ndio maana ukaona Zanzibar kambi za jeshi ni nyingi sana na askari ni wengi kulingana na ukubwa wa nchi yenyewe kuliko hata tanganyika

Nchi ni ndogo lakini kambi za jeshi na askari ni wengi tena wa kigeni na hiyo sio kwa sababu ya ulinzi hapana ila ni kwa sababu ya kuwachunga wa Zanzibar ili wasilete madhara katika muungano huu usio eleweka

Habari hizi ni kubwa sana na tukiziongelea hatuwezi kuzimaliza na kwa bahati mbaya baadhi ya watu mkiongea habari kama hizi wao hubabaisha na kutia pamba masikioni

Na mwisho utawasikia wao wanasifia sifia tu mambo yasiokua na maana yoyote

Lakini yote kwa yote muungano huu hauna nia njema na mstakabali mzuri kwa Zanzibar na unawaumiza wa Zanzibar

Na katika hili tumepoteza nguvu zote
Nguvu za ulinzi
Nguvu za uchumi
Nguvu za dola na ustaarabu pia

Na sio vibaya kua na muungano lakini uwe ni muungano wenye haki na usawa na kutoa hadhi kamili kwa kila muhusika.
 
Huu si Muungano vp utaanza kuita kwa jina hilo huu ni uloloni wa mtu mweusi mwenye roho mbaya dhidi ya Taifa nyonge lisilo na nguvu ya kujikomboa ktk utunwa huu wa MITANGANYIKA
 
Kwanza wapemba na waunguja bado hamjaungana nyoyo zenu vizuri,ndo mtaweza kurekebisha muungano nyinyi,wkt muungano wenu unanyufa kibao.
 
Mimi kwenye ishu zoote za muungano ile ya kununua gar zanzibar ukileta bara unalipia miushuru kibao ndio nnapochoka.
 
Kwanza wapemba na waunguja bado hamjaungana nyoyo zenu vizuri,ndo mtaweza kurekebisha muungano nyinyi,wkt muungano wenu unanyufa kibao.
Wqpemba na waunguja wanaongea lugha MOJA ttzo lipo kwa WAZANZIBARA waliopo Zanzibar ndio wanaotuvurugaa
 
Back
Top Bottom