Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Rev. Kishoka, Zanzibar haitakiwi kwenda kokote,ni sehemu ya Tanzania,kama ilivyo hongkong kwa China,au Catalonia kwa Spain,
Hili sio suala la hisia, kwamba watu waamke asubuhi wajisikie tu, kwamba muungano hauna faida, uvunjwe. No and big no, hii ni nchi moja kama ambavyo Dar inachangia asilimia 80 ya pato lote la Taifa,na wakazi wa dar hawalalamiki,kwamba wajitenge na mikoa mingine,Zenj na mapungufu yake yote,haiendi kokote,
 
Natamani kuishi Tanganyika

Tanganyika ndio ardhi ya baba yangu,

Eeh Mungu nisaidie ndoto hii iwe kweli,
 
Kweli muungano wa tanfanyika na Zanzibar ndio wakujivunia.

Ila huu wa Tanganyika na Zanzibar asilimia kubwa hawaoni umuhimu wala Faida zaidi ya kuongeza mivutano na migogoro.

Muungano ungekua wa kujivunia kusingekua na upande unaotaka kujitoa kwa kuhisi unakandamizwa kila uchao.
 
Zanzibar haitakiwi kwenda kokote,ni sehemu ya TZ,kama ilivyo hongkong kwa China,au Catalonia kwa Spain,
Hili sio suala la hisia,kwamba watu waamke asubuhi wajisikie tu,kwamba muungano hauna faida,uvunjwe,no and big no,hii ni nchi moja,kama ambavyo Dar inachangia asilimia 80 ya pato lote la Taifa,na wakazi wa dar hawalalamiki,kwamba wajitenge na mikoa mingine,Zenj na mapungufu yake yote,haiendi kokote,
😀😀 una hakika hayo unayoyasema!??,Hongkong haijawahi kuwa taifa huru siku zote ilikuwa ni sehemu ya china,waingereza waliikodi Hongkong kwa muda wa miaka 100,1997 mkataba ulipoisha wakairejesha Hongkong kwa wenyewe wachina..

Catalonia haijawahi kuwa nchi huru,imekuwa sehemu ya Spain maisha yote,Kabla hakukuwa na nchi inayoitwa Tanzania kulikuwepo na nchi huru moja iliyoitwa Tanganyika na nyengine Zanzibar,1964 nchi mbili hizi ziliungana kwa mkataba,Zanzibar inaweza kujitoa kwenye mungano kama wanataka,sema wazanzibar bado hawajaamua tu,hao vibaraka CCM Zanzibar wanajidanganya tu...siku ikifika wazanzibari wakiamua basi utakuja kuniambia Mkuu
 
Zanzibar haitakiwi kwenda kokote,ni sehemu ya TZ,kama ilivyo hongkong kwa China,au Catalonia kwa Spain,
Hili sio suala la hisia,kwamba watu waamke asubuhi wajisikie tu,kwamba muungano hauna faida,uvunjwe,no and big no,hii ni nchi moja,kama ambavyo Dar inachangia asilimia 80 ya pato lote la Taifa,na wakazi wa dar hawalalamiki,kwamba wajitenge na mikoa mingine,Zenj na mapungufu yake yote,haiendi kokote,

Zanzibar kufananisha na Dar ni tusi la nguoni.Nchi iliowahi kuwa na kiti UN, ina raisi na wimbo wake wa taifa na bendera.Sijuwi kama vijana wa Dar wanafahamu ukiwa skuli Zanzibar hatuimbi "mungu ibariki Tanzania, bali Unguja na Pemba".
 
Mimi namjibu Pombe Magufuli majibu yangu 3 tuu kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

1. Kama Muungano huu ni wa kipekee na wakuigwa, mbona hakuna Nchi hata moja iliojiunga na Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar?….. Kama MAGU anataka kuangalia Muungano Mzuri wa Kipekee angeanza Kusafiri na Kwenda BRUSEL- Kule angeona Muungano uliokuwa Mzuri na Wakuigwa Duniani nao ni Muungano wa EUROPEAN UNION. ambao Ulianza kwa Nchi 5 tuu za Western Europe yaani UK, SPAIN, FRANCE, GERMAN, ITALY na baadae wakafuata PORTUGAL. Kutoka Miaka hiyo tumeshuhudia hata zile Nchi zilizokuwa na Dictatorship kama Huyu MAGUFULI zimeweza kujivua Magamba yao ya Udictatorship nakujiingiza kwenye Muungano wa Kipekee na wakuigwa Duniani

2. Nini maana ya Muungano wa Kipekee na Wakuigwa? Ni ule Muungano ambao kila Nchi iliojiunga na Muungano huo itakua na

1. Free Movement.

2. Itakua na Nationality yake -Passport, pesa zake na mambo mengine ya ndani na nje ya Nchi Nchi hio yatajishuhulikia wenyewe.

3. Kiti chake kule UN- yaani Muungano wa Kuigwa ni ule uliokuwa umejifungakwa kiuchumi, Ulinzi na Usalama- kwakupashana habari na kusaidiana pale nchi moja inapokua iko katika hatari yaani( Alliance).. Zanzibar na Tanganyika Wana Muungano huu?

4. Magufuli naona maneno yake anayoyasema, anayasema kwa WAFU wa Madaraka ambao ni Wazanzibari Wa CCM na wengi wao wana Asili ya ya Tanganyika. Na kama ni Wazanzibari halisi ambao bado watakua wako CCM akina SHAKA, Haji Omari Heri na kundi jengine basi Watakuwa ni Watu Wasio na Elimu ya Dini wala Duniani. Hapo CCM wapo kwa kushiba matumbo yao na Familia zao. Lakini kwa Mzanzibari mwenye akili hawezi kusema kwamba Muungano wa Tanganyika ni Waina yake na ni wakuigwa Duniani.. Labda awe Mbumbumbu kama Hao akina Sheni, Vuai, Shaka, Kombo nk. Hapo nitamtyoa
Mzalendo net.
 
1 + 1 = 1

Zanzibar + Tanzania = Tanzania

Muungano na udumu milele
 
mzeekondo
3 Mei, 2018 at 18:09
Jibu
Niwashukuru wote mliochangia pamoja na muandishi ZAMKO kwa kujituma siku zote kuitetea Zanzibar,binafsi siku hizi nimeamua kukaa kimya kirefu huku nikitafakari,sio kazi rahisi kushuhudia nchi yako ikiteketea huku ukijua kuwa huna la kufanya zaidi ya kupiga kelele,na kwa wale wanaoiteketeza si dhani kama kelele hizi huwa zina wanyima usingizi au kuwaotesha ndoto za ajabu ajabu,si kutwa wengine hutokwa na asali nyeupe za midomo kwa utamu wa kutunakamisha bila huruma.

Visiwa vyetu vimechukuliwa kwa kalamu na ulaghai wa alie soma na asie soma,kuto kusoma kwa Karume ndio kiini cha msiba huu,ni kweli mengi alikuja kuyajua na kujuta kabla hata hajauwawa lakini kosa ilikuwa limekwisha fanyika,mimi sina wasi wasi Nyerere alihusika na mauwaji ya mzee Karume, ndio maana alihakikisha Rais wa Zanzibar anakuwa Aboud Jumbe badala ya Seif Bakari ambae ndie alikuwa chaguo la memba wote wa baraza la mapinduzi wa wakati huo,kilicho muogopesha Nyerere ni kuwa hawa watu wengi walikuwa hawakusoma lakini huhitaji au hawakuhitaji elimu kujua kuwa Zanzibar ni nchi.

Kumchagua kwake marhum Aboud Jumbe alijua kuwa huyu kasoma na anaweza kumtumia tena sasa kwa utaalamu zaid,i kwa kuwa ataamini wote ni watu wa Makerere basi wote wana nia jema,Jumbe nae alikuja kugundua kuwa Nyerere hana nia njema, kwa upande wake tena tayari kosa lilikwisha fanyika,alikubali kuunganisha vyama vya siasa na kukiuwa Afro Shirazi, ambacho ndicho kilikuwa mlinzi wa mwisho wa hivi visiwa.

Sasa utagundua haya sio matukio ya kushtukiza tu,ni mipango ya uhakika na ya muda mrefu,bado tuna viongozi kama utapenda kuwaita jina hilo hapa Zanzibar, ambao na wao kila kukicha wana fanya na kugundua makosa ya kila baada ya miaka mitano ya uchaguzi,kwa mfano kumuibia kura maalim Seif kila siku kwa miaka ishirini sasa, hili ni KOSA kubwa linalofanywa na marais wote wa Zanzibar waliotangulia na huyu wa sasa, kwa sababu wao wanadhani wanamkomoa Seif na cuf au wapemba, kumbe wanajikomoa wenyewe kwa ujuha kalulu au upumbavu wao.

Hii misiba tunaipenda sana sisi Wazanzibari wa kulaumiwa sio Magufuli bali ni sisi wenyewe,kama hatujaamua kushughulikiana, basi huu Muungano utadumu kwa kuwa tunatoa ushirikiano wenyewe kwa visingizio vya kibaguzi/chuki nk.hata sisimizi wanatushinda kwa sababu wao wana muungano/ushirikiano unaoeleweka kuliko huu,sisimizi hushirikiana kujenga nyumba ya kila mmoja au familia,sisi tunajenga Tanganyika tangu 1964, huku kwetu bado kuna chimba visima ili tupate maji ya kunywa,hata yale mabomba aliyoyaacha sultan/ muingereza basi yamegoma kutoa maji sio chini ya miaka 30 sasa.

Mimi siutaki muungano huu au mwingine wowote,na kusema hivyo sijafanya kosa lolote kisheria ni haki ya raia japokuwa sina nchi,umepata kuona wapi nchi kuwa na katiba eti Rais huwezi kumshitaki? au uchaguzi wa rais yoyote uwe wa sultan au huu wa kibaraka pia huwezi kuushitaki/kuupinga matokeo yake mahakamani?sasa kwa tuna wafundisha nini vizazi vyetu kuwa haki inapatikana MAHAKAMANI, wakati ikiwa mshitakiwa au washitakiwa wana vyeo basi huko msiende?ni lazima Rais ashitakiwe kwa kosa lolote kama raia mwingine, kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria katika ulimwengu unaoamini HAKI.

Tatizo sisi tunaiishi katika ulimwengu au sayari yetu binafsi.
Source Mzalendo net
 
muungano huu wa kulazimisha tununue sukari ya upande mmoja,tutumie Zantel huku? tuangalie jamani tusilazimishane kutumia bidhaa za huko! !chonde chonde
 
Hilo ulilolitaja ni dudu kubwa sana kwa hao wenzako kupambana nalo....wangejaribu angalau kwa Jecha, pengine leo ningeweza kufikiria andiko lako
 
Uingereza wanajiondoa Umoja wa Ulaya... Jimbo la Catalunya linajiandaa kujitenga na Spain... Mkoa wa Kiingereza wa Bamenda unajiandaa kujitenga na Cameroon! Wazanzibari wenzangu, huu ndio muda sasa wa kuuvunja huu muungano!!!
Hakika.........naungana nawe mia fil mia
 
Assume muda ndio huu alafu Muungano unavunjika! Sipati picha Wapemba na Waunguja waliopo Mwanza, Dodoma, Kigamboni, Temeke, Ilala, Kinondoni na sehemu nyingine wanavyotolewa mbio kurudishwa na maboti, mitumbwi na majahazi na Jiwe!

Acha kuwaza upuuzi mkuu.
Eritrea au Sudan Kusini walipojitenga hao waliokuwa kwenye miji tofauti na kwao walipatwa na nini? Acha kuogopa kisichoonekana
 
Mtoa mada naomba uniambie ni lini Zanzibar iliwahi kusimama yenyewe kama dola huru katika historia. Ukishaniambia tutaweza kujadili Zanzibar kujitoa katika muungano..
 
Mtoa mada naomba uniambie ni lini Zanzibar iliwahi kusimama yenyewe kama dola huru katika historia. Ukishaniambia tutaweza kujadili Zanzibar kujitoa katika muungano..
Uhuru wa Zanzibar12 December 1963(baada ya majadiliona ya kina na mapana) hadi uvamizi. Sisemi mimi sauti ya historia.
 
Uingereza wanajiondoa Umoja wa Ulaya... Jimbo la Catalunya linajiandaa kujitenga na Spain... Mkoa wa Kiingereza wa Bamenda unajiandaa kujitenga na Cameroon! Wazanzibari wenzangu, huu ndio muda sasa wa kuuvunja huu muungano!!!
Lianzishe tuu ila utawaponza wenzio laiti ungejua bora ukae tuu kimya
 
Back
Top Bottom