mzeekondo
3 Mei, 2018 at 18:09
Jibu
Niwashukuru wote mliochangia pamoja na muandishi ZAMKO kwa kujituma siku zote kuitetea Zanzibar,binafsi siku hizi nimeamua kukaa kimya kirefu huku nikitafakari,sio kazi rahisi kushuhudia nchi yako ikiteketea huku ukijua kuwa huna la kufanya zaidi ya kupiga kelele,na kwa wale wanaoiteketeza si dhani kama kelele hizi huwa zina wanyima usingizi au kuwaotesha ndoto za ajabu ajabu,si kutwa wengine hutokwa na asali nyeupe za midomo kwa utamu wa kutunakamisha bila huruma.
Visiwa vyetu vimechukuliwa kwa kalamu na ulaghai wa alie soma na asie soma,kuto kusoma kwa Karume ndio kiini cha msiba huu,ni kweli mengi alikuja kuyajua na kujuta kabla hata hajauwawa lakini kosa ilikuwa limekwisha fanyika,mimi sina wasi wasi Nyerere alihusika na mauwaji ya mzee Karume, ndio maana alihakikisha Rais wa Zanzibar anakuwa Aboud Jumbe badala ya Seif Bakari ambae ndie alikuwa chaguo la memba wote wa baraza la mapinduzi wa wakati huo,kilicho muogopesha Nyerere ni kuwa hawa watu wengi walikuwa hawakusoma lakini huhitaji au hawakuhitaji elimu kujua kuwa Zanzibar ni nchi.
Kumchagua kwake marhum Aboud Jumbe alijua kuwa huyu kasoma na anaweza kumtumia tena sasa kwa utaalamu zaid,i kwa kuwa ataamini wote ni watu wa Makerere basi wote wana nia jema,Jumbe nae alikuja kugundua kuwa Nyerere hana nia njema, kwa upande wake tena tayari kosa lilikwisha fanyika,alikubali kuunganisha vyama vya siasa na kukiuwa Afro Shirazi, ambacho ndicho kilikuwa mlinzi wa mwisho wa hivi visiwa.
Sasa utagundua haya sio matukio ya kushtukiza tu,ni mipango ya uhakika na ya muda mrefu,bado tuna viongozi kama utapenda kuwaita jina hilo hapa Zanzibar, ambao na wao kila kukicha wana fanya na kugundua makosa ya kila baada ya miaka mitano ya uchaguzi,kwa mfano kumuibia kura maalim Seif kila siku kwa miaka ishirini sasa, hili ni KOSA kubwa linalofanywa na marais wote wa Zanzibar waliotangulia na huyu wa sasa, kwa sababu wao wanadhani wanamkomoa Seif na cuf au wapemba, kumbe wanajikomoa wenyewe kwa ujuha kalulu au upumbavu wao.
Hii misiba tunaipenda sana sisi Wazanzibari wa kulaumiwa sio Magufuli bali ni sisi wenyewe,kama hatujaamua kushughulikiana, basi huu Muungano utadumu kwa kuwa tunatoa ushirikiano wenyewe kwa visingizio vya kibaguzi/chuki nk.hata sisimizi wanatushinda kwa sababu wao wana muungano/ushirikiano unaoeleweka kuliko huu,sisimizi hushirikiana kujenga nyumba ya kila mmoja au familia,sisi tunajenga Tanganyika tangu 1964, huku kwetu bado kuna chimba visima ili tupate maji ya kunywa,hata yale mabomba aliyoyaacha sultan/ muingereza basi yamegoma kutoa maji sio chini ya miaka 30 sasa.
Mimi siutaki muungano huu au mwingine wowote,na kusema hivyo sijafanya kosa lolote kisheria ni haki ya raia japokuwa sina nchi,umepata kuona wapi nchi kuwa na katiba eti Rais huwezi kumshitaki? au uchaguzi wa rais yoyote uwe wa sultan au huu wa kibaraka pia huwezi kuushitaki/kuupinga matokeo yake mahakamani?sasa kwa tuna wafundisha nini vizazi vyetu kuwa haki inapatikana MAHAKAMANI, wakati ikiwa mshitakiwa au washitakiwa wana vyeo basi huko msiende?ni lazima Rais ashitakiwe kwa kosa lolote kama raia mwingine, kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria katika ulimwengu unaoamini HAKI.
Tatizo sisi tunaiishi katika ulimwengu au sayari yetu binafsi.
Source Mzalendo net