doriani
Member
- Nov 24, 2019
- 42
- 38
Muungano uwepo wake ni kutekelezwa kwa masharti ya Mkataba wa Muungano. Na Mkataba huu wa Muungano wetu ni Mkataba wa kimataifa. Moja ya shuruti kuu la Muungano huu ni kuthibitishwa na Mabunge yiote mawili ya nchi zilizo Ungana yaani Tanganyika na Zanzibar kama haukuthibitishwa na Mabunge yote mawili maanake haupo kwa mujibu wa sheria.
Upo ushahidi kwamba Tanganyika umepelekwa Bungeni na Mwalimu Nyerere. na ukapitishwa. Hapana ushahidi wowote mpaka hivi sasa kwamba Zanzibar nao walifanya hivyo. Kama upo ushahidi wowote naomba jamii itusogezee hapa tuweze kupata ukweli. Kama ikibainika kua haukupelekwa na kupitishwa maana yake nchi ya Zanzibar itakuwa imekaliwa kwa mabavu.
Na ndipo pale Nyerere alipobaini kwamba wananchi 'lazima' watakuja kuuliza siku moja, ndipo alipo sema kwamba "yeyote atakae hoji uhalali wa Muungano ni haini" nadhani Nyerere alikuwa akiijua kwamba Muungano haupo kwa mujibu wa Sheria.