Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano uwepo wake ni kutekelezwa kwa masharti ya Mkataba wa Muungano. Na Mkataba huu wa Muungano wetu ni Mkataba wa kimataifa. Moja ya shuruti kuu la Muungano huu ni kuthibitishwa na Mabunge yiote mawili ya nchi zilizo Ungana yaani Tanganyika na Zanzibar kama haukuthibitishwa na Mabunge yote mawili maanake haupo kwa mujibu wa sheria.

Upo ushahidi kwamba Tanganyika umepelekwa Bungeni na Mwalimu Nyerere. na ukapitishwa. Hapana ushahidi wowote mpaka hivi sasa kwamba Zanzibar nao walifanya hivyo. Kama upo ushahidi wowote naomba jamii itusogezee hapa tuweze kupata ukweli. Kama ikibainika kua haukupelekwa na kupitishwa maana yake nchi ya Zanzibar itakuwa imekaliwa kwa mabavu.

Na ndipo pale Nyerere alipobaini kwamba wananchi 'lazima' watakuja kuuliza siku moja, ndipo alipo sema kwamba "yeyote atakae hoji uhalali wa Muungano ni haini" nadhani Nyerere alikuwa akiijua kwamba Muungano haupo kwa mujibu wa Sheria.
 
Wakuu

Kwa sisi tuliofika pemba na Unguja wala sio siri Wazanzibar hawauhitaji Muungano huu maana hauna faida kwao
Na ukisema leo hii wapige kura hakuna mzanzibar ambae anauhitaji muungano huu tulionao
Naona kwa afya ya Taifa kifanyike kitu ili kunusuru hii hali maana sina imani ya amani yetu miaka ijayo.

Labda tuunde katiba mpya ambapo bara mkuu wa serikali awe waziri mkuu na visiwani mkuu wa serikali awe waziri mkuu wa kutokea huko halafu tuwe na Rais wa Jamhuri ambae atakua kiongozi tu kiprotokali lakini kila nchi iwe na mamlaka kamili bila kuingiliwa na zanzibar iwe na kiti umoja wa mataifa. Na iwe mwanachama wa mashirika ya kimataifa hii naona itasaidia sana.
 
Kama hamuoni faida ya muungano basi tajeni hapa hizo hasara za muungano mlizoona.
 
Arovera,
Nini kifanyike sio jukumu lako, muhimu ni kua Muungano huu hauna Future, nivemya kulitambua mapema ili Kila upande uamue nini cha kufanya
 
Habari wana jukwaa, Binafsi wiki hii ya maazimisho ya mapinduzi Zanzibar kuna maswari mengi nmejiuliza juu ya muungano wetu.

Nikajiuliza kuwa Rais Maghufuli ni amiri jeshi mkuu wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) uwepo wake yeye alitakiw awe mgeni rasimi na apigiwe mizinga, lakn haikuwa hivyo badala ake nikaona Luna amiri jeshi 2 japo anaeteua na kutengua ni mmoja. Huku Tanganyika tunawimbo wetu wa taifa unasema 'mungu ibariki' Zanzibar nao wananchi yao na wimbo wa taifa lao.

Tofauti na kilichomo kwenye katiba kinacho itambua Zanzibar kama serikali na sio nchi. Kasimu majaliwa ni waziri mkuu wa Tanzania (Tanganyika & Zanzibar) lakin hana sauti huko. Bunge lipo la Tanzania, Tanganyika hatuna bunge hata PM. Ndo maana jpm tangu aingie ikulu anashughulika na bara tu na sio Zanzibar maana sio nchi ake yeye kama mgeni huko. Zanzibar wana shirikisho la Mpira na tume yao ya uchaguzi kama nchi huru.

Where is Tanganyika. Back to Tundu lisu's speech about our union. Tubeze mengine yaliyoko kwenye upinzani lakin yenye masilahi na nchi yetu tuyasikilize.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We una umri gani kwanza. Tusijekuwa tunasemezana na vitoto visivyojua hata historia. Unawezaje kuubeza huu Muungano Mtukufu hivi?? Unajua ni nani aliuasisi?? Tuseme, hakujawahi kuwa na mtu mwingine mwenye ufahamu wa hili jambo tangu uasisiwe miaka 58 hadi leo ndo umekuja weye??
Muungano upo na utadumu milele
 
Imekuwa ni jadi na utamaduni kufurahia sikukuu hii na kuwaenzi waasisi wa Muungano wetu Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid Karume kwa matamasha, gwaride na shangwe kebekebe....
Nimeyapenda sana haya maneno maana yamenikumbusha mbali.

''Yakishindwa yote haya mtoto bado hasikii dawa na anaendelea kulia sasa tukimtisha kwa babu mduma. ''

Sasa babu mduma ndo nini kwa siasa zetu?

au Peoples power?
 
Tatizo suala la Elimu tukilitoa kwenye muungano mtaanza kutumia vyeti vya madrasa kwenda universities
Kitu ambacho itakuwa bomu Kwa baadae
Wacha dharau wewe.

Madrasa ni kubwa zidi ya Vyuo vyako vikuu.

Kuhifadhi Qur-an na Hadith za Mtume ,kisha kujuwa Mantiki na Bayana si jambo jepesi.

Ni kubwa kuliko kuvumbua Atomic Bomb
 
Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.

Naawatakia Muungano mwema huku nikisisitiza. Nautakia huu muungano wetu adhimu udumu milele na hivyo kukitokea yoyote anayetaka kuuchokoa muungano, namshauri chokochoko amchokoe pweza, muungano hutauweza kwasababu tutaulinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia muungano mwema.

P
 
Heshima yenu wakuu!

Kuna Watanzania wanampa support Lissu na Maalim Seif kuwa, wakishika hatamu, basi Muungano ndo baas! Tena wanashadadia ile mbaya yani.

Madai yao, tukiachana na ile kwamba (kauli hii itatoa amshaamsha upinzani ushike dola), wanasema kuwa eti Muungano si halali na wananchi hususan Wazenji walibakwa, walishinikizwa na mengineyo.

Hoja yangu: Kama iko hivyo, basi na mfumo wa vyama vingi ufutwe mara moja kwani haikuwa ridhaa ya wananchi. Rejea 80% walosema No! na ile 20% ya Yes!

Cc; Msanii Pascal Mayalla Mohamed Said n.k
 
Kwani ni lazima kuwaza sawa kama binadamu tunatifautiana
 
Kumbuka,Muungano na malidhiano ya pande mbili,siyo Muungano wa kubuluzwa Kama ng'ombe anaenda machinjioni,na kakuambia Muungano utavunjwa?
 
Kwenu wana jukwaa, swali linajieleza. Mara kwa mara nimesikia matamanio ya wazanzibar kuwa na Rais kwa serikali ya muungano.

Thinking critically, will there be any significant difference that will come up by having a big man up there originating from the islands ?
 
Nikiitazama nafasi hiyo ''kimajukumu'' sioni umuhimu wowote wa kiongozi mtajwa kutokea visiwani.

Lakini nikiitazama nafasi hiyo ''kimuungano'' naona ni sawia kabisa kwa mtu wa visiwani kupewa nafasi hiyo japo mara ''moja moja''.
 
Nikiitazama nafasi hiyo ''kimajukumu'' sioni umuhimu wowote wa kiongozi mtajwa kutokea visiwani.

Lakini nikiitazama nafasi hiyo ''kimuungano'' naona ni sawia kabisa kwa mtu wa visiwani kupewa nafasi hiyo japo mara ''moja moja''.
Kama ni hivyo,
Kwanini mnawalazimisha kuungana?
 
Kama ni hivyo,
Kwanini mnawalazimisha kuungana?
Hatujawalazimisha mkuu, kwa ujumla ni kwamba ''wameridhia''.

Swali kwako:
Kwahiyo kama hawautaki muungano (kama usemavyo kuwa ''tunawalazimisha'') ndio tuutumie Urais wa JMT ''kuwabembelezea'' ?
 
Back
Top Bottom