Ndugu zanguni.
Nawaomba niwaulize tu, si kwa shari bali heri.
Hivi huu muungano wa tembo na sisimizi una manufaa kwa nani?
Watanganyika tunautaka wa nini?
Wazanzibari tunajua hawautaki , sasa tatizo ni nini?
Inakuwaje sisimizi ale mlo sawa na Tembo?
Kwa nini kila mtu asichukue taim yake kero ziishe?
Tuna mapori mengi, milima mingi, ardhi kubwa mara alfu kumi ya zanzibar lakini bado tunapoteza muda kuubembeleza huu muungano?
Leo hii mtanganyika haruhusiwi kununua ardhi Zanzibar lakini ruksa mzanzibari kununua tanganyika
Leo hii umeme Tanganyika tunalipa mara dufu ya Zanzibar
Leo hii mimi kama Mtanganyika siwezi tembea kwa amani na uhuru huko visiwani wakati wao wanatembea matumbo mbele huku wakibeua kwetu na kutupigia kelel juu kuwa hawatutaki.
LIWALO NA LIWE
HUU MUUNGANO WA TEMBO NA SISIMIZI UFE.
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA.