Muungano wetu: Ujumbe huu kwenye bango la Timu ya Taifa Zanzibar unamaanisha nini?

Zanzibar huwa wakibeba Mabango kuwa wanahitaji kuwa huru kwa kuukataa muungano huwezi kuona Viongozi wanakuja juu,ila huku Tanganyika Tundu lissu na wenzie wakipiga kelele hawautaki muungano unaona hao hao viongozi ambao walishiriki kwenye mabango ya Zanzibar ya kwamba Wanaleta chokochoko!
 
Ni lazima uwe na akili ya mtu Mwendawazimu ili uweze kuuelewa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 
Masharti ya Mganga wamepewa, yani wanachukia hizo agenda kweli.
 
Kwani kizimkazi imeshindwa kuwasaidia
 
hao jamaa wanajitekenya na kucheka wenyewe, Mchawi wa Zanzibar ni CCM na ndio hao wanaowanyenyekea hao walioshika hilo bango.
 
Zanzibar wachague tuwe nchi moja au tuwe nchi mbili tofauti. Si bado tutakuwa ndugu?
Mbona Kenya tuna undugu?
Tuna undugu upi na Kenya? Maana naona tz na ke ni mafahari wawili hapa afrika mashariki,kuvimbiana wao,kusema wao,yani ni kama simba na Yanga,nieleweshe tafadhari
 
Tuna undugu upi na Kenya? Maana naona tz na ke ni mafahari wawili hapa afrika mashariki,kuvimbiana wao,kusema wao,yani ni kama simba na Yanga,nieleweshe tafadhari
Makabila mengi ya Tanzania yapo Kenya. Ni kawaida kwa ndugu kuvimbiana, hata Simba na Yanga ni ndugu kama ilivyo Orlando na Kaizer ni watu waliowahi kuwa wamoja.
 
Wazanzibar wasipoitumia awamu ya 6 kuondoa dhulma zote walizofanyiwa na machogo, ndio basi tena wasahau milele.
 
Ndio maana hata katika uuzwaji wa Bandari kwa DP world, Zanzibar walikataa huo ujinga, Mzanzibari Samia akaamua kuuza Bandari za Tanganyika kwa wajomba zake... Maana anajua yeye si mtanganyika
Husen kawapa wafaransa bandari ya Unguja.
 
Makabila mengi ya Tanzania yapo Kenya. Ni kawaida kwa ndugu kuvimbiana, hata Simba na Yanga ni ndugu kama ilivyo Orlando na Kaizer ni watu waliowahi kuwa wamoja.
Brother nafahamu mwingiliano wa hayo makabila ila ukweli ni kwamba wakenya wanawadharau watanzania,wanaona ni watu wasio na elimu,akili na watu maskini pia hawapo proud kuwa na ukaribu wa kimahusiano na watanzania,tafiti Hilo swala mkuu
 
Rasmi
Hangaya anauvunja muungano mbele ya macho yetu.

Tuendeleekumshangilia na kumuunga mkono

Huo ujumbe ni maelekezo
 
Lingebebwa na watanganyika basi lisingekubaluka. Kama wao wanataka kuchukukiwa kama nchi kwani i Tanganyika kuiongelea ionekane nongwa
 
Brother nafahamu mwingiliano wa hayo makabila ila ukweli ni kwamba wakenya wanawadharau watanzania,wanaona ni watu wasio na elimu,akili na watu maskini pia hawapo proud kuwa na ukaribu wa kimahusiano na watanzania,tafiti Hilo swala mkuu
Na wapo sahihi kabisa, mimi nikimuona mtu anajifananisha na Kenya namuona ni kama mwehu, wale wana akili kweli wala hawatuonei.

Tuna ardhu ya kutosha kwa kilimo, tuna madini takriban yote, tuna bandari, mbuga za kutosha, gas, mito ya kutosha n.k na bado hatujawafikia kiuchumi, Je hizi rasilimali wangekuwa nazo wao je au hata Kagame?

Tukubali tu kuwa sisi Watanzania CCM wameiua nchi na kutufanya tubaki hapa kwenye shimo la umasikini.
 
Crying for my beloved Tanganyika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…