RingaRinga
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,047
- 521
Wanajamvi habarini za asubuhi,
Nilifunga mkataba na muuza duka wangu kwa ajili ya kazi ya duka langu.
Mkataba tuliufunga kwa mtendaji wa kijiji tarehe 7.1.2020.
Mkataba ulikuwa na mashahidi upande wake na mimi.
Pia alidhaminiwa na mtu mmoja mwenye mali zisizohamishika.
Tulikubaliana nitakuwa namlipa tsh 50,000/= kwa mwezi.
Kwa kuwa nina kamgahawa tulikubaliana atakula hotelini kwangu ugali samaki au nyama mara mbili kwa wiki, na siku zingine wali maharage na mbogamboga angepewa kama zitakuwepo.
Pia kwa kuwa alikuwa anatokea wilaya nyingine tulikubaliana nimpe makazi, kitanda na neti na kiwe na umeme ambapo nagharamika mimi.
Makubaliano tulivyoandikishana ilikuwa kwamba nisiporidhika na utendaji wake nina haki ya kumwachisha kazi na niwe nimemlipa malipo yake yote ya 50,000 kwa kila mwezi.
Kwa kuwa utendaji wa kijana umekuwa duni sana na imeshindikana kujirekebisha nimeamua kumwachisha kibarua.
Sasa kijana ananivimbia eti siwezi kumwachisha kazi ghafla bila kumpa mafao ya kuacha kazi na atanishtaki labda nimpe malipo ya miezi mitatu (150,000) ili ajipange kupata kazi sehemu nyingine.
Sheria ya ajira za namna hii inasemaje ndugu wana JamiiForums?
Lukonge