Muuza duka wangu anatishia kunishtaki

Muuza duka wangu anatishia kunishtaki

Mpe hiyo Hela muachane,ulikosea kumwandikia mkataba.
 
Naomba kama kuna mwenye mfano wa mikataba na wauza duka unaomweka salama mwenye duka atuwekee hapa wengi tufaidike
 
Wanajamvi habarini za asubuhi,

Nilifunga mkataba na muuza duka wangu kwa ajili ya kazi ya duka langu.
Mkataba tuliufunga kwa mtendaji wa kijiji tarehe 7.1.2020.
Mkataba ulikuwa na mashahidi upande wake na mimi.
Pia alidhaminiwa na mtu mmoja mwenye mali zisizohamishika.

Tulikubaliana nitakuwa namlipa tsh 50,000/= kwa mwezi.
Kwa kuwa nina kamgahawa tulikubaliana atakula hotelini kwangu ugali samaki au nyama mara mbili kwa wiki, na siku zingine wali maharage na mbogamboga angepewa kama zitakuwepo.

Pia kwa kuwa alikuwa anatokea wilaya nyingine tulikubaliana nimpe makazi, kitanda na neti na kiwe na umeme ambapo nagharamika mimi.

Makubaliano tulivyoandikishana ilikuwa kwamba nisiporidhika na utendaji wake nina haki ya kumwachisha kazi na niwe nimemlipa malipo yake yote ya 50,000 kwa kila mwezi.

Kwa kuwa utendaji wa kijana umekuwa duni sana na imeshindikana kujirekebisha nimeamua kumwachisha kibarua.

Sasa kijana ananivimbia eti siwezi kumwachisha kazi ghafla bila kumpa mafao ya kuacha kazi na atanishtaki labda nimpe malipo ya miezi mitatu (150,000) ili ajipange kupata kazi sehemu nyingine.

Sheria ya ajira za namna hii inasemaje ndugu wana JamiiForums?
Lukonge
Ulikiwa ni makubaliano, hapo itabidi umlipe jamaa mmalizane kisomi bila kelele.
 
Migogoro mingi ya muajiri na muajiriwa mara nyingi.jamii inakua upande wa muajiriwa kwa kuona kua anaonewa kisa umasikini...huu ni unafki wa wtz wengi kujidai kutetea wanyonge akat mara kibao waajiriwa wanafanya mavitu ya ovyo ukifukuZa jitu linaona limeonewa
 
Migogoro mingi ya muajiri na muajiriwa mara nyingi.jamii inakua upande wa muajiriwa kwa kuona kua anaonewa kisa umasikini...huu ni unafki wa wtz wengi kujidai kutetea wanyonge akat mara kibao waajiriwa wanafanya mavitu ya ovyo ukifukuZa jitu linaona limeonewa
Wivu wivu tu wa watz
 
Asante sana Mr Lukonge kwa nondo zako.
Kwa muktadha huo, je naweza kutumia mkataba upi ili kukidhi mahitaji yangu kulingana na kipato changu,
Vijana wenye uhitaji wa kufanya kazi na mimi ni wengi ila nahitaji kujiweka salama.
Niliwahi kufanya kazi na vijana wengine wawili na walishajitegemea wamefungua biashara zao binafsi na wanafanya vizuri, ni huyu mjanjapori tu ambae aliendekeza anasa ndio sioni future yake. Bahati nzuri huwa nawashauri vizuri namna ya kuwekeza hela zao kny kilimo, imewasaidia sana na wanapiga hatua za haraka.
Namba 2 au 3 zote unaweza kuzigengea mazingira na ukafanya kazi vyema.
 
Sheria inataka umpetaarifa yakumuachisha kazi miez mitatu kabla then umlipe miez yote ilibaki mkataba uixhe. Akikuxhtak nixhida maan pia 50k nichin ya kima chachin chamxhahar
Na wewe ni Mwanaume unaandika KICHOKO hivi,kizazi kimelaaniwa hiki
 
Kweli lakini alikuwa anampa chakula bure na malazi bure.
Waajiriwa wengi hawapewi chakula bure,malazi bure,umeme bure na hata maji bure.
Kwani angekuwa anajilipia chakula,malazi,maji na umeme angekuwa anatumia kiasi gani kwa mwezi.
Kwa hiyo nadhani hakuna kosa kumlipa mtu 50K kwa mwezi huku ukimpa vitu vingine bure (ambavyo alipaswa kulipia)
Point
 
Huo mkataba umekosa sifa haushitakiki mahakamani kwasababu hamkukubaliana ukimfukuza umpe mshahara wa miezi mitatu
 
Mpe hela anayotaka mkuu hata hivyo hiyo 50,000 sio mshahara bhana ni marupurupu ya week
 
Mkataba wowote unapaswa kuwa na kipengele cha kuonesha unaisha lini, na utavunjwaje (ila ya bandari ndio ya milele).

Ungempa hiyo hela kwa kuandikishana na akubali kwamba hatakudai chochote cha ziada. Mkataba ufuatao hakikisha una hivyo vipengele.
 
Soma kwa makini kuhusu mkataba ili umtendee haki kulingana na mkataba.
Nimeona nimlipe tu kadri ya ushauri wa wadau humu, so tushamalizana kwa mtendaji na amekiri kwa maandishi hana cha zaidi tena anachonidai .
 
Huo mkataba umekosa sifa haushitakiki mahakamani kwasababu hamkukubaliana ukimfukuza umpe mshahara wa miezi mitatu
Ukishasema ni mkataba wa ajira, hakikisha unazingatia sheria husika wewe unaetengeneza mkataba.

Kunapotokea tatizo sheria inakwenda kukupitisha kwenye mfumo husika na kuonyeaha matundu yote ili kuwapatieni haki kati yenu.

Hapo ndo kila mmoja atalia kivyake. Ni bira kudunika kombe kwa jinsi ya gharama na muda wako mpaka kugota pwani.
 
Nimeona nimlipe tu kadri ya ushauri wa wadau humu, so tushamalizana kwa mtendaji na amekiri kwa maandishi hana cha zaidi tena anachonidai .
Ni vyema zaidi, pata muda usome Sheria ya ajira na mahusiano mahara pa kazi Tanzania toleo la 2004, itakupa mwangaza wa haya yote. Soma taratibu ili kujua haki za mwajiri na mwajiriwa.
 
Nimeona nimlipe tu kadri ya ushauri wa wadau humu, so tushamalizana kwa mtendaji na amekiri kwa maandishi hana cha zaidi tena anachonidai .
Afadhali umemlipa tupate muda zaidi wa kusoma neno kwa neno kwenye mkataba wa kihuni wa Mwarabu hapo bandari Salama.
Nashangaa sana kutokuona bandari ya Malindi Zanzibar ikihusishwa.
 
Back
Top Bottom