Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtwange barua tatu za onyo yaani hakikisha kila kasoro unayoikuta mnaijadili na kumwandikia barua ya onyo.Wanajamvi habarini za asubuhi,
Nilifunga mkataba na muuza duka wangu kwa ajili ya kazi ya duka langu.
Mkataba tuliufunga kwa mtendaji wa kijiji tarehe 7.1.2020.
Mkataba ulikuwa na mashahidi upande wake na mimi.
Pia alidhaminiwa na mtu mmoja mwenye mali zisizohamishika.
Tulikubaliana nitakuwa namlipa tsh 50,000/= kwa mwezi.
Kwa kuwa nina kamgahawa tulikubaliana atakula hotelini kwangu ugali samaki au nyama mara mbili kwa wiki, na siku zingine wali maharage na mbogamboga angepewa kama zitakuwepo.
Pia kwa kuwa alikuwa anatokea wilaya nyingine tulikubaliana nimpe makazi, kitanda na neti na kiwe na umeme ambapo nagharamika mimi.
Makubaliano tulivyoandikishana ilikuwa kwamba nisiporidhika na utendaji wake nina haki ya kumwachisha kazi na niwe nimemlipa malipo yake yote ya 50,000 kwa kila mwezi.
Kwa kuwa utendaji wa kijana umekuwa duni sana na imeshindikana kujirekebisha nimeamua kumwachisha kibarua.
Sasa kijana ananivimbia eti siwezi kumwachisha kazi ghafla bila kumpa mafao ya kuacha kazi na atanishtaki labda nimpe malipo ya miezi mitatu (150,000) ili ajipange kupata kazi sehemu nyingine.
Sheria ya ajira za namna hii inasemaje ndugu wana JamiiForums?
Lukonge
Mmejua hasara anayoingia au ni vile huyo goi goi anataka kuchuma vya bure?aise yaani hukupaswa kubishana nae , kimya kimya mpatie hiyo laki na nusu muachana, ukiendelea kuzungusha halafu wakaja wajanja wakamshtua imekula kwako. mahakani utaingiliwa zaidi Hadi hutaamini .
yaani unamfungisha mkataba wa ajira wa elfu 50 kwa mwezi , hapo ulijichanganya Sana .
Ndiyo ni ndogo,,,yaani kama huyo dogo anapata mtu was kumsimamia mbona jamaa atatoa pesa nyingi[emoji16]Kwanza mbna kadai ndogo, ilibidi 1M Kabisaa.
Unaweza kujipanga kumpiga tukio, na yeye akakupiga bonge la tukio.Mtwange barua tatu za onyo yaani hakikisha kila kasoro unayoikuta mnaijadili na kumwandikia barua ya onyo.
Ikifika ya nne unaambatanisha barua ya kumtimua maana maonyo yamezidi.
Wewe vumilia mwezi mmoja kisha hayo yote yafanyike ndani ya mwezi. Hakikisha unapeleka nakala kwa mtendaji kila barua.
Anafanya makusudi kukutia hasara
Ameshaonesha ni poyoyo anapokea maelekezo ya wajinga.Unaweza kujipanga kumpiga tukio, na yeye akakupiga bonge la tukio.
Sheria nadhani inakataza kutoa mkataba wa chini ya mwaka mmoja. Vinginevyo toa mkataba wa specific task.(KAZI maalum.)Fanyia kazi huu ushauri haraka sana na wakati mwingine toa mkataba wa muda mfupi
Kweli lakini alikuwa anampa chakula bure na malazi bure.Sheria inataka umpetaarifa yakumuachisha kazi miez mitatu kabla then umlipe miez yote ilibaki mkataba uixhe. Akikuxhtak nixhida maan pia 50k nichin ya kima chachin chamxhahar
Ni sheria gani inayosimamia mikataba ya ajira Tanzania?Lukonge
Nakuomba hapa ushauri na wadau wengine:
Biashara yangu ni ndogo tu, inanipa kafaida kidogo upande wa mpesa, upande mwingine nachaji simu na betri, nauza visimu vya button na spare zake ie cover, chaja betri, memory card, usb cable nk, mtaji hauzidi m.3, hata mapato nalipa laki na leseni 20k, ni vibanda vya nje ya mji.
Makusanyo ya faida ya mauzo na mpesa kwa mwezi ni wastani wa laki tano baada ya kulipia frame, ulinzi na umeme.
Hiyo laki tano sasa ndio nilipie chakula cha kibarua 3000@siku=90k, pango lake 15k, umeme 5k, malipo yake 50k, sawa 170,000 kwa mwezi.
Nabaki na 339,000/=
Mimi pia ni paid slave somewhere, next time nafanyaje kitaalamu kuepuka kusumbuana na hawa vibarua wa kuuza vibanda vyetu hivi ambavyo hata havikui sababu ya majukumu na management?
Sasa hiyo alfu hamsini unayomlipa ni ya vocha tu au mshahara?
Napendekeza kijana akushtaki tu maana unapenda kubembea kwenye migongo ya wasio nacho
Kibarua ni miezi sita tu kisheria na kama alimpa mkataba hakua kibarua tangu mwanzo , akimpeleka mahakamani jamaa amekwishaKima cha wapi Mkuu?
Hiyo laki mbili unafikiri mchezo😂😂
Nenda Huko viwandani uone Watanzania wakihenyeka,
Mabadiliko ya sheria za juzi kima cha Chini ukikisikia utaishia kucheka tuu. Ni masikitiko makubwa.
Hiyo laki 2 unayoisema haipo Mkuu.
Huyo jamaa mwenye Duka hakuwahi kuajiri Mfanyakazi. Aliajiri kibarua. Maana ndio mishahara Yao hiyo
Asante sana Mr Lukonge kwa nondo zako.Ni sheria gani inayosimamia mikataba ya ajira Tanzania?
Kwa ujumla Sheria ya Mikataba inasimamia aina zote za mikataba Tanzania. Lakini kwa mikataba mahususi kuna sheria mahususi inayosimamia mikataba hiyo.
Kwa mfano: Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi inaelezea mikataba ya ajira. Kwa maana hiyo ni sawa kusema Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Mikataba zote zinasimamia mikataba ya ajira.
Kuna aina ngapi za mikataba?
Kuna aina kuu tatu (3) za mikataba ambazo unaweza kuajiriwa nayo, nazo ni:
1: Mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa
Kama jina linavyojieleza, kwa aina hii ya mkataba kipindi cha ajira hakiainishwi. Mara nyingine huitwa mkataba wa kudumu.
2: Mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa.
Hii ni aina ya mkataba ambao umetaja kipindi cha muda. Chini ya mkataba huu kama kipindi kilichotajwa kikimalizika basi mkataba utakua umefikia mwisho. Mkataba wa kipindi cha muda uliotajwa unaweza kua kwa kipindi cha mwezi, miezi mitatu, mwaka mmoja, miaka miwili nakadhalika.
3: Mkataba wa kazi maalumu
Hii ni aina ya mkataba ambapo mtu huajiriwa kufanya kazi maalumu. Pindi kazi inapoisha na mkataba hufikia mwisho. Kwa mfano, mtu anaweza kuajiriwa kushusha kreti za soda kutoka kwenye gari na pindi kazi ile inapoisha na mkataba hufikia mwisho