grand millenial
JF-Expert Member
- Jul 29, 2018
- 3,943
- 5,550
Anashindana na genghis khan
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanaangalia picha za mwenye mbegu ndio wananunua🤣🤣🤣Duuh kuwa mwanaume rijali ni lulu aseee ila huku bongo si wangeileta hii kitu au ingekuwa ya wanaume ma HB tu sio 🤔
Mimi sura ya nyani ningekosa soko 😆😆😅😅Wanaangalia picha za mwenye mbegu ndio wananunua🤣🤣🤣
mwamba kama mwamba![]()
Jonathan Jacob Meijer, 41
Kenya. Mwanamuziki wa Uholanzi mwenye makazi yake nchini Kenya, ambaye ni muuzaji mkubwa wa mbegu za kiume, pia mwenye watoto takriban watoto 550 duniani kote anakabiliwa na mashtaka ya kuongeza athari kwenye mahusiano.
Jonathan Jacob Meijer, 41, ameshtakiwa kwa madai ya kuongeza hatari ya uhusiano wa kingono kati ya ndugu wa damu.
Kwa mujibu wa gazeti la ‘New York Post’ wameeleza kuwa Meijer, anauza mbegu za kiume katika kliniki 13, zikiwemo 11 za Uholanzi, ambapo aliwekewa vikwazo mwaka 2017 kwa kuwa na watoto 102.
Kulingana na sheria za Uholanzi, wafadhili wa mbegu za kiume hawaruhusiwi kuzaa zaidi ya watoto 25 au kuwapa mimba zaidi ya wanawake 12 ili kuzuia kuzaliana, uhusiano wa ujamaa au matatizo ya kisaikolojia kwa watoto wanaogundua kuwa wana ndugu na dada wengi.
Lakini licha ya vikwazo hivyo, Meijer anandelea kutoa mbegu zake nje ya Uholanzi, ikiwa ni pamoja na Denmark na Ukraine.
Haya ni kulingana na Wakfu wa Uholanzi wa DonorKind, ambao umemshataki mwanamziki huyo. Kundi hilo linadai kuwa mfadhili huyo wa mbegu za kiume amekuwa akidanganya kuhusu idadi ya watoto aliowazaa.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanamke Mholanzi ambaye ni mmoja wa waliomzalia Meijer watoto mwaka wa 2018.
Mwanamke huyo, aliyetambuliwa kwa jina la Eva, alipofanya mahojiano na gazeti la ‘The Times’ kutoka jijini London amesema anajutia sana kumchagua Meijer kama mfadhili wake na asingelimzaliwa angelijua tayari alikuwa amezaa zaidi ya watoto 100.
"Ninapofikiria namna matokeo ambayo yanaweza kuathiri mtoto wangu ninaumwa na tumbo langu. Kwenda mahakamani ndiyo njia pekee ya kumlinda mtoto wangu,” amesema Eva.
Wanawake waliozaa na Meijer sasa wanataka mahakama kumkomesha akome kufadhili mbegu zake na zilizohifadhiwa zote ziharibiwe.
MWANANCHI